MRATIBU
wa mtandao wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji kijinsia Jeshi la
Polisi Makao Makuu, Hasina Ramadhan Toufik ameitaka jamii kutoa ushahidi
mahakamani kwa watu wanaotuhumiwa kubaka ili kukomesha matukio hayo.
Akizungumza
katika maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia katika
Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongo Chekundu mjini hapa, Toufiki
alisema wagonjwa wa akili wamekuwa walengwa wa matukio ya ubakaji.
Alisema
ubakaji kwa watu wenye matatizo ya akili, haukubaliki na kuitaka jamii
kuwa tayari kuwafichua watu wa aina hiyo kwa kutoa ushahidi mahakamani.
“Walemavu
wenye matatizo ya akili, wanakabiliwa na tishio la ubakaji huku wakiwa
walengwa wakubwa kwa sababu ushahidi wao haukubaliki mahakamani,â€
alisema.
Aidha,
alisema moja ya kikwazo kikubwa ambacho kinahitaji kufanyiwa
marekebisho ni Sheria ya Ushahidi ya mwaka 1917, ambayo haitambui
ushahidi wa mtu mwenye matatizo ya akili mahakamani.
Alisema
wabakaji wengi wanatumia mwanya huo wa kufanya vitendo vya uhalifu,
wakijua wazi kwamba hakuna ushahidi utakaokubalika mahakamani kwa mtu
aliyebakwa ambaye ni mgonjwa wa akili.
“Sheria
hii inakabiliwa na mapungufu mengi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ili
kuona kwamba watuhumiwa wa makosa ya ubakaji, wanachukuliwa hatua za
kisheria na kukomesha vitendo hivyo moja kwa moja,†alisema.
Mkuu
wa Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongo Chekundu mjini hapa, Vuai
Kombo Haji alilipongeza Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsia kwa
kujitolea na kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Alikiri
kuwa wagonjwa wa akili katika hospitali ya Kidongo Chekundu,
wanakabiliwa na tishio kubwa la vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia
ikiwemo kubakwa.
Mtandao
wa Polisi wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijiinsia
ukiwajumuisha zaidi ya polisi 30, walikuwa katika zoezi la kufanya usafi
katika eneo la hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo Chekundu.
Chanzo:Habari Leo
No comments:
Post a Comment