Mkuu
wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Beno Hunja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa
Habari(hawapo pichani) walipotembelea Ofsini kwake Desemba 17, 2014
kujionea ujenzi unaoendelea wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji. Mradi
huo unajengwa kwa kutumia fedha za ndani na utagharimu kiasi cha Milioni
2.8 hadi kukamilika kwake hivyo kukamilika kwa mradi huo kutalifanya
Jeshi la Magereza kuzalisha mazao ya chakula kwa wingi kuliko hivi sasa. Waandishi
wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali vya Daily News, Tanzania Daima,
Habari Leo na Michuzi Blogu wakifanya mahojiano na Mkuu wa Gereza
Idete(hayupo pichani) walipofanya ziara yao ya kikazi Desemba 17, 2014
kujionea ujenzi wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji. Mkuu wa Gereza Idete, Beno Hunja akiwaongoza Waandishi wa Habari kutembelea eneo kunakojengwa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Sehemu ya Mbanio na chanzo Kikuu cha kupokelea maji yatakayotumika katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete Mfereji ambao tayari umekamilika kujengwa katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Gereza Idete, Mkoani Morogoro. Wafungwa
wa Gereza Idete wakilima shamba kwa kutumia trekta kama inavyoonekana
katika picha. Wafungwa hao wamepatiwa ujuzi wa kulima na trekta wakiwa
gerezani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu mbalimbali za
Urekebishaji zinazofanywa na Jeshi la Magereza hapa nchini. Kwa wastani
Wafungwa hao hulima hekari 10 kwa siku
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment