Wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo Mheshimiwa Naibu Waziri aliwasihi wadau mbalimbali wa maendeleo ya Jinsia kutekeleza kwa vitendo kauli Mbiu Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayosema “Maisha Yangu,Haki Yangu, Piga Vita Ndoa za Utotoni”
Alieleza kuwa Suala la ndoa za utotoni na ukeketaji linatia dosari kubwa katika harakati za kumkomboa mtoto wa kike kwa vile taifa linahitaji mchango wa kila mwananchi ili kufikia malengo yake ya kujiletea maendeleo sambamba na utekelezaji wa Malengo ya Mpango wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini( MKUKUTA), Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Malengo ya Milenia, hivyo ndoa za utotoni na ukeketaji zinapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote na jamii yote.
Aidha, akiwa Mkoani Mara, Mheshimiwa Dkt.Pindi Chana (Mb.) alitembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare, Musoma.
No comments:
Post a Comment