Ujumbe
wa wataalamu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA) unatembelea Bandari
ya Singapore (PSA) ili kubadilishana utaalamu wa namna ha kuongeza
ufanisi na kuimarisha Ulinzi na usalama wa Bandari kwa kutumia Mitambo
ya kisasa na Teknolojia ya Habari na mawasiliano (ICT) , Ujumbe wa TPA
unaongozwa na Ndg. Phares Magesa , Mkurugenzi wa ICT wa TPA, pia wamo
wahandisi wa majengo, wataalamu wa Ulinzi na wataalamu wa TEHAMA. Ziara
hii ni muendelezo wa ushirikiano wa PSA na TPA ikiwa ni sehemu ya
makubaliano yaliyotiwa sahihi kati ya TPA na PSA wakati wa ziara ya Mhe.
Rais Kikwete alipotembelea nchini Singapore mwaka jana.Mkuu
wa msafara wa TPA Ndg. Magesa akipokea zawadi toka Makamu wa Rais
Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore ( PSA) anayeshugulikia
biashara Ndg. Vignes kulia
Mkuu wa msafara Ndg. Magesa akisalimiana na Makamu wa Rais Msaidizi wa PSA anayeshugulikia ICT Ndg. Andrew Gill wakati akiwakaribisha makao makuu wa PSA Ujumbe wa TPA ukiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa PSA makao makuu ya PSA
Ujumbe wa TPA ukiwa kwenye chakula Cha pamoja na Ujumbe PSA

No comments:
Post a Comment