Mhakama
moja ya kijeshi nchini Nigeria imewahukumu kifo askari 54 kwa kukataa
kupigana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram.
Wanajeshi
hao ambao walipatikana na kosa la uasi,walituhumiwa kukataa kuikomboa
miji mitatu iliyokuwa imetekwa na Boko Haram mwezi Agosti.
Wakili wa wanajeshi hao 54 alisema kuwa watawauwa kwa kupigwa risasi huku wengine watano wakiachiliwa huru.
Wanajeshi wamelalamika kuwa hawapewi silaha na mabomu ya kutosha kupigana na Boko Harm.
Kundi
hilo limekuwa likipigana tangu mwaka 2009 na linalenga kujenga nchi
inayoongozwa na sheria za Kiislamu kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Zaidi
ya watu 2000 wameuwawa katika mashambulizi yaliyolaumiwa kufanywa na
kundi hilo kufikia sasa mwaka huu na maelfu zaidi ya watu wamelazimishwa
kuhama makwao kutokana na vita vinavyoendelea.
Koti hiyo ya kijeshi ilianza mwezi Oktoba na ilifanywa kwa siri.Viongozi wa kijeshi hawakupatikana kuzungumzia swala hilo.
Wakili
anayewawakilisha,Femi Falana,alisema kuwa wanajeshi hao wote
walituhumiwa ''kupanga njama ya kuasi dhidi ya mamlaka ya kikosi cha
Divisheni ya 7 cha jeshi ya Nigeria.''
Wanajeshi wote walikataa mashtaka na hukumu hiyo inasubiri idhini ya maafisa wa ngazi za juu.
Katika
kisa sawia mwezi Septemba,wanajeshi 12 walihukumiwa kifo kwa makosa ya
uasi na jaribio la kumuua afisa wa jeshi katika mji wa
kaskazini-mashariki wa Maiduguri.
No comments:
Post a Comment