Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Mecki Sadiki akifungua mkutano wa
Wajumbe wa Baodi ya Barabara ya Mkoa wea Dar es salaam leo. Kushoto ni
Katibu Tawala wa mkoa Bi.Theresia Mmbando na Naibu Waziri wa Kazi
Mh.Makongoro Mahanga (kulia).
(PICHA NA ARON MSIGWA -MAELEZO)
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema(kushoto) na mkuu wa wilaya ya
Ilala Bw. Raymond Mushi wakifuatilia mkutano wa wajumbe wa Bodi ya
barabara ya mkoa wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaam Meneja
wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam Muhandisi J. Nyamukama akiteta jambo
na baadhi ya wahandisi wa ofisi yake leo jijini Dar es salaam wakati wa
kikao cha Bodi ya Barabara ya mkoa wa Dar es salaam.
Mbunge wa Ubungo Mh. John Myika akichangia kuhusu hali ya usafi na uimarishaji wa miundombinu katika jiji la Dar es salaam.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya mkoa wa Dar es salaam Mh. Idd Azzan
Mh. akichangia kuhusu hali ya usafi na uimarishaji wa miundombinu katika
jiji la Dar es salaam.
……………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki amewataka
wahandisi wanaosimamia ujenzi wa miradi ya barabara katika jiji la Dar
es salaam kuhakikisha kuwa wanawasimamia ipasavyo wakandarasi wanaojenga
miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa viwango na muda uliopangwa na
kuwaondolea wananchi adha ya usafiri inayotokana na ubovu wa barabara.
Aidha,amezitaka Mamlaka zinazohusika na utoaji wa vibali vya
ujenzi katika maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es salaam
kuwachukulia hatua za kisheria wananchi wanaovunja sheria kwa kujenga
majengo na kuta katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuziba mifereji ya maji
na kubomoa kingo za mito hali inayosababisha mafuriko katika makazi ya
watu wakati wa msimu wa mvua.
Akifungua kikao cha kwanza cha wajumbe wa Bodi ya Barabara ya
Mkoa wa Dar es salaam kilichofanyika leo jijini Dar es salaam kujadili
na kutathmini utekelezaji wa miradi ya barabara kwa mwaka 2014/2015 Bw.
Sadiki amesema kuwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam yamekuwa
yakikumbwa na mafuriko kutokana na ujenzi holela katika mikondo ya maji,
uharibifu wa kingo za mito, na uzibaji wa mifereji unaofanywa na baadhi
ya watu kwa kujenga kuta jambo linalosababisha uharibifu wa miundombinu
kutokana na mafuriko wakati wa mvua.
Amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto za miundombinu ya
barabara katika jiji la Dar es salaam, zaidi ya shilingi bilioni 88
zimependekezwa kuidhinishwa katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 kwa lengo
la kufanya ukarabati wa kawaida, matengenezo ya barabara za zamani na
mpya kwa kiwango cha lami na ujenzi madaraja mapya na yale
yaliyoharibiwa wakati wa msimu uliopita wa mvua.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo wakizungumza kwa
nyakati tofauti wameipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha
miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu wa mvua uliopita maeneo
mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, ujenzi wa barabara ya Uhuru,Daraja
la Kinyerezi, Ujenzi wa kituo cha mabasi eneo la Machinga Complex,
utekelezaji wa mradi wa barabara ya Shingofeni, Barabara ya Mombasa
–Moshi bar na ujenzi wa barabara ya Ulongoni A kuelekea Kilimani.
Wamesema kuwa juhudi za usafi wa mito, madaraja na mifereji
katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam lazima iwe shirikishi
ili mafanikio ya kuliweka jiji katika hali ya usafi na usalama wakati wa
msimu wa mvua yaweze kuonekana na kuwaondolea usumbufu wananchi.
Aidha, wamezitaka mamlaka zinazohusika katika manispaa za za
Ilala, Temeke na Kinondoni kuanisha maeneo yote hatarishi katika
halmashauri zao ambayo wananchi wamevamia mito kwa kujenga na kuharibu
kingo za mito waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment