Mwimbaji
wa muziki wa injili Tumaini Njole akizungumza na waandishi wa habari
katika ofisi za kampuni ya Msama Promotion ambayo inaandaa Tamasha la
Pasaka litakalofanyika sikukuu ya Krismas tarehe 25/12/2014 mkoani
Mbeya wakati alipozungumzia maadalizi ya tamasha hilo na jinsi
alivyojipanga kukonga mioyo ya mashabiki wa nyimbo za injili mkoani
Mbeya , Tamasha hilo linatarajiwa kuanza muda wa Saa nane mchana
viingilio vikiwa ni shilingi 5000 kwa watu wazima na watoto shilingi
2000, Katika tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu
Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye na waimbaji wengine watakaotumbuiza ni
Faraja Ntaboba, Upendo Nkone, Upendo Kirahilo, Rose Muhando, Bony
Mwaiteje Edson Mwasabwite, Ambwene Mwasongwe na wengine wengi, Pia
matamasha mengine yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa tarehe 26/12/2014
na Songea tarehe 28/12/2014, Katika Picha kushoto ni Mwimbaji Joshua
Mlelwa. Mwimbaji
wa muziki wa Injili Edson Mwasabwite akifafanua jambo wakati wa mkutano
huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam , Kushoto ni mwimbaji Joshua
Mlelwa na katikati ni Mwimbaji Tumaini Njole Mwimbaji Joshua Mlelwa
akielezea maandalizi yake wakati wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika
mkoani Mbeya wakati wa Sikukuu ya Krismas kulia ni Mwimbaji Tumaini
Njole.
No comments:
Post a Comment