Serikali
imewashauri wahitimu kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea ajira kutoka
serikalini kwani inatambua ukosefu wa ajira nchini.
Hayo yamesemwa
leo jijini Dar ea Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Uratibu na Bunge Mhe. Willium Lukuvi alipokuwa akifungua kongamano la
mafunzo kwa wajasiliamali wadogo wadogo.
Amesema kuwa
vijana wanatakiwa kuweka mkazo katika suala la ujasiriamali na
kujihusisha na mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali ili kuwa na fursa
mbalimbali kiuchumi.
“Mtazamo chanya,
kujitambua, kuwa wabunifu na kusema inawezekana vinachangia kuzidisha
maendeleo binafsi hivyo kila kijana afikirie kuwa anaweza” aliongeza
Waziri Lukuvi.
Mbali na hayo
Waziri Lukuvi alisema kuwa vijana hawana mitaji ya kujiendeleza lakini
taasisi za kifedha zinauwezo wa kuwakopesha iwapo watakua na
vitambulisho vya Taifa na anwani za makazi hivyo kupelekea vijana
kujiajiri.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa wajiri nchini Bw. Almasi Maige amewaasa wahitimu kuwa na
mawazo chanya na kufikiria zaidi kuhusu kujiajiri na si kusubiri
kuajiriwa.
“Hakuna ujasiriamali rahisi, inatakiwa kujitoa haswa kwa watu ama vijana wenye nguvu kama ninyi” aliongeza Maige.
Hivyo kuwashauri
vijana kuwa wabunifu na kuanzisha shughuli zitakazosaidia kuongeza
kipato na si kutegemea kukopi kutoka sehemu nyingine.
Kongamano hilo
lililoandaliwa na kampuni ya Gilgal nchini yenye kauli mbiu isemayo
“wajasiriamali wadogo fursa zilizowazi” lenye lengo la kubadili fikra
kwa vijana walio vyuoni kutumia fursa zilizopo
No comments:
Post a Comment