SHEREHE za miaka kumi ya kuanzishwa kwa Mtandao wa WAsanii Tanzania (SHIWATA)zilizokuwa zifanyike Desemba 25, jijini Dar es Salaam zimeahirishwa.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim
Taalib alisema jana kuwa kuahirishwa kwa sherehe hizo kumetokana na
wanachama wengi ambao walitakiwa kukabidhiwa nyumba zao kuwa katika
sherehe za Krismas nje ya mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kuahirishwa huko
kumesababisha pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga Veterani
lililokuwa lichezwe Desemba 25 kwenye uwanja wa Azam, Charambe mpaka
litakapotangazwa tena.
Mwenyekiti Taalib alisema sababu nyingine ya kuahirishwa kwa
sherehe hizo ni kutokana na maombi ya mgeni rasmi ambaye hakumtaja kuwa
yuko nje ya nchi kikazi ambaye aliomba ahudhurie tamasha hilo la
kihistoria.
Nyumba ambazo zitakabidhiwa ni 38 ambazo zimejengwa na
kukamilika ambako wanachama hao walichangia ujenzi kwa kutoa fedha
kidogo kidogo kupitia benki na kuchangua aina ya nyumba anayoitaka
kutokana na kiasi alizochangia.
Ili kuwapatia makazi ya bei nadfuu wanachama wake SHIWATA
inajenga nyumba za sh. 631,000, sh. 1,500,000, sh. 3,800,000 na sh.
6,400,000 ambazo mwanachama anagaiwa kila mwezi Juni na Desemba kila
mwaka..
Alisema katika makabidhiano hayo
wamiliki wa nyumba hizo pia watakabidhiwa vyeti maalum vya kumaliki
nyumba zao katika sherehe kubwa itakayofanyika kijiji cha Mwanzega,
Mkuranga. Mpaka sasa SHIWATA ina wanachama 8,000.
No comments:
Post a Comment