Kikosi cha Timu ya Mtanda
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga (Kushoto) Akiwa na Mgeni Rasmi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, R.P.C Renatha Mzinga, wakati wa Uzinduzi wa Michuano ya Kombe la R.P.C CUP LINDI 2016, kwenye Uwanja wa Ilulu Mkoa wa Lindi tarehe 28/7/2016. Fainali ya Michuano ni 25/8/2016 katika Uwanja huo.(Picha Zote na Fungwa Kilonzo)
Mkurugenzi wa Mashujaa Fm Radio, na Mratibu wa Michezo ya R.P.C CUP LINDI 2016, Shaaban Mpalule, akiwagawia Mashabiki Furana mbali mbali za G.S.M na T-Mark Tanzania, wakati wa Uzinduzi huo.

Mmoja wa Mashabiki akivalia Furana ya G.S.M
===================================
-R.P.C RENATAHA MZINGA AZINDUA KWA MBWEMBWE.
-DC LINDI AIPONGEZA KAMPUNI YA GSM
-MASHABIKI WATAKA GSM IFANYE MICHEZO HIYO KILA MWAKA.
Na: Mwandishi wa Miss Demokrasia Tanzania.
Kampuni
ya GSM Tanzania, wauzaji wa Pikipiki za GSM na Magodoro ya kisasa ya GSM, leo jumatano
28/7/2016 imekamilisha uzinduzi wa Michuano ya Kombe la R.P C Cup LINDI 2016, ambayo
lengo lake ni kuwaweka Vijana karibu na Jeshi la Polisi pamoja na kuwapa Elimu
mbali mbali Madereva kuhusiana na Usalama barabarani ususani vijana waendesha
Bodaboda na ilianza 13/7/2016 kwenye Uwanja wa Ilulu.
katika
uzinduzi huo GSM ambao ni wadhamini wa Jumla katika michezo hiyo kwa Upande wa
Jeshi la Polisi katika mikoa ya Lindi, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na
Dodoma, ilipongezwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga
kwa kuweza kujitokeza kusaidia mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa
mkiwango kisichoridhisha ikiwa ni pamoja na kukosekana na vifaa vya michezo
pamoja na furana kwa Wageni mbali mbali.
Aidha wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo Kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi, Afande R.P.C Renatha Mzinga, alisema kuwa wanaishikuru Kampuni GSM kwa mwaka huu kujitokeza kusaidia michezo hiyo ambayo hata hivyo bado kuna upungufu wa vifaa mbali mbali vya michezo ikiwemo mipira ya kuchezea.
"Mashindano ya Mwaka huu ni Mazuri na yameonyesha kuwa tofauti na miaka ya nyuma, pengine ni kwa kuwa yamejitokeza makampuni kama hawa GSM, Halotel na BIG BON, kwa kweli kunachangamoto nyingi sana kwenye hii michezo, na hata timu za mwaka huu zimeonekana kujiandaa vizuri kwa ajili ya kuwania zawadi siku ya Fainali, Niwapongeze wadhamini wote waliojitokeza kusaidia kwa namna moja na nyingine, kile kidogo walichotupatia kwetu ni kikubwa sana, kwa maana kimeonekana kuleta utofauti na miaka ya nyuma, hivyo nichukue fulsa hii kuwaomba hawa wadhamini kuweza kukumbuka kutusaidia kwenye hii hatua ya mwisho ambapo inaonekana vifaa bado havijatimia kama hii Mipira, Sare za Waamuzi na Zawadi zingine kwa ajili ya Timu, pamoja na kwamba tumepata vikombe lakini tunatakiwa pia kuwapa zawadi zingine ili kuonyesha tofauti ya mwaka huu na miaka ya nyuma, niwashukuru GSM kwani hawa wamejitokeza hatua za mwisho mwsiho lakini wametuwezesha leo kupendeza uwanjani, mashabiki wamevalia na watu mbali mbali furana zao, kwa kweli ninawapongeza sana, wasiishie mwaka huu tu bali wayachukue na kuyafanya mashindano kuwa ni ya kwao kila mwaka" alisema R.P.C Renatha Mzinga.

Aidha
michuano hiyo imezidi kushika kasi na kufikia jumla ya michezo 27 ambayo tayari
imechezwa katika kuwania kinyang’anyoro cha ubingwa mwaka huu.
Wachezaji wa timu mbali mbali
wamezidi kuonyesha uwezo mkubwa katika michuano hiyo ambayo inashirikisha
jumla ya timu 18 kutoka kata zote za Mkoa wa Lindi.
Katika hatua hii michezo ambayo
imechezwa na matokeo ni kama ifuatvyo, Mtanda A imefanikiwa kuifunga Mitandi
kwa 1-0, Matopeni 1-0 Wailes, Mnazi mmoja 2-0 Mbanja, Nachingwe 0-0 Msinjaili,
Rahaleo 2-1 Mtanda B, Rasibula 2-1 Tandangongoro, Mingoyo3-0 Chikonji, Mtandi
5-1 Kitumbikwela, Makonde 5-0 Mikumbi, Polisi 1-1 Matopeni, Mnazi Mmoja 4-1
Mtanda A, Msinjaili 8-0 Wailes, Mtanda(B) 2-1 Mbanja, Rahaleo 2-0 Chikonji,
Rasibula 2-0 Nachingwea, Mikumbi 2-0 Tandangongoro.
MIchezo mingine ni Mingoyo
0-Kitumbikwela. Makonde 1-0 Polisi, Mitandi 1-1 Mnazi Mmoja, MAtopeni 3-0
Msinjahili, Mtanda(A)1-1 Mbanja, Wailes 2-5 Nachingwea, Kitumbikwela 3-4
Chikonji, Polisi 0-1 Mikumbi, Mnazi MMoja 0-0 Mingoyo, Msinjahili 0-3 Makonde,
Mitandi 2-0 Mbaja, MAtopeni 2-2 Nachingwea, na Mtanda 2-3 Raha Leo.
Michezo hiyo inaendelea tena kesho(leo) ambapo Wailes wataikaribisha timu ya Tandangomgoro katika mchezo wa kwanza na mchezo wa pili Mtanda (B) wataikaribisha Kitumbikwela kwenye mchezo wa pili majira ya saa kumi jioni.

mashindano yameendelea kuwa kuvutio
kikubwa kwa wakazi wa mkoa wa lindi kutokana na wenyeji kujitokeza
kuzishangilia timu za kata zao ambazo zinawania uchampioni huo wa kombe la
R.P.C Renatha Mzinga.
Zawadi ambazo mpaka sasa zimetolewa na GSM ni pamoja na Filimbi, Stopwatch, Soksi, Mabegi, Kofia, Sare na Viatu kwa ajili ya Waamzuzi, pamoja na zawadi ya Soksi kwa Wachezaji ambao wanafanikiwa kufunga magoli matatu katika mechi moja, ambapo badala ya kuondoka na mpira umewekwa utaratibu wa kuwazawadia Soksi kila anapotokea mchezaji amefunga mabao matatu.
Kiasi cha Shilingi Milioni Mbili tayari Kimetumika Mpaka sasa kutoka Kampuni ya GSM ambazo zimetumika kulipa Posho za Waandishi wa Habari wanaoendelea kuripoti matukio hayo kila siku na zingine zimesaidia kununua vifaa hivyo kwa ajili ya Waamuzi na zawadi za kila siku kwa wachezaji.
katika kiasi hicho kutoka GSM pia kimesaidia kununua Filimbi na Stop Watch kwa ajili ya Makocha wa Timu zote zinazoshiriki ligi hiyo ya R.P.C CUP LINDI mwaka huu.
katika hatua nyingine kampuni ya T-Mark Tanzania ambao pia ni miongoni mwa wawezeshaji wadogo wameweza kusaidia Furana za kwa ajili ya Vikundi vya Uhamasishaji.

Kilele cha Michuano hiyo ni tarehe 25 ya mwezi wa nane ambayo itakuwa siku ya kilele cha siku ya Polisi Day.