TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, December 20, 2013
NANI MTANI JEMBE!! KIVUMBI JUMAMOSI OKWI ATUA YANGA KUWAKABILI SIMBA
Okwi katikati baada ya kuwasili JNIA akiwa na Katabaro kulia na Bin Kleb kushoto jioni hii na chini akionyesha jezi namba 25.
Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
HABARI
ya mjini kwa muda huu ni kwamba; mshambuliaji mpya wa Yanga, Emmanuel
Anord Okwi amewasili alasiri ya leo uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam tayari kwa kuanza kazi ya kuitumia
klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Okwi
ametia miguu Tanzania saa 9:30 kwa ndege na kulakiwa na viongozi wa
Yanga ambao walikuwa na uchuku wa kupokea jembe lao la kazi.
Waandishi
wa habari walikuwa na uchu wa kusikia kauli ya Okwi na ndipo muda
ukafika baada ya nyota huyo kutoka nje ya uwanja wa JNIA ambapo alisema
amekuja Yanga kufanya kazi.
Alipoulizwa
sakata lake la usajili, Okwi alifungua mdomo wake kwa mara nyingine na
kusema; “Mimi nimekuja kufanya kazi, hayo mengine hayanihusu, zipo
mamlaka zinazohusika na zitajua la kufanya”.
Cha kufurahisha Okwi amewasili akiwa tayari ameshavalia jezi ya Yanga, namba 25 mgongoni.
Akizungumza
uwanjani hapo, mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga, Abdallah
Ahmed Bin Kleb amesema Okwi anakwenda moja kwa moja katika hoteli ya
Protea kuungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kesho
kutwa ya Nani Mtani Jmebe dhidi ya Simba sc, uwanja wa Taifa.
Wakati Okwi akiwa amewasili, taarifa iliyopatikana kutoka mtandano wa MTNFootball.com
mchana wa leo imeeleza kuwa kaimu mkurugenzi wa mashindano wa
shirikisho la soka nchini Uganda FUFA, Decolas Kiiza amethibitisha kuwa
FIFA wamemruhusu Okwi kujiunga na Yanga.
“Ndiyo tuliandika barua FIFA na walisema mchezaji yuko huru kuuzwa”. Kiiza aliuambia mtandao wa MTNFootball.com.
Mapema
wiki hii Mkurugenzi mkuu wa FUFA, Edgar Watson alisema wameiandika FIFA
barua kuhitaji maelezo zaidi juu ya suala la Okwi.
Okwi
aliuzwa na Simba katika klabu ya Etoile Du sahel ya Tunisia januari
mwaka huu kwa kitita cha dola 300, 000 za kimarekani, lakini hakudumu
katika klabu hiyo kwa madai ya kutolipwa haki zake na kuamua kurejea
kwao Uganda.
Okwi
baada ya kurejea kwao Uganda alikaa miezi sita bila kucheza na ndipo
shirikisho la kandanda la Uganda (FUFA) likasimama kidete kumpigania
aruhusiwe kureja nyumbani na kujiunga na Sport Club Villa ya Uganda
`Majogoo wa Kampala` ili kulinda kiwango chake.
Kwa
usajili wa Okwi, Yanga imetimiza wachezaji watano wa kigeni kwa maana ya
washambuliaji Didier Kavumbagu, Khamis Friday Kiiza, beki Mbuyu Twite,
kiungo Haruna Niyonzima.
Sakata la Okwi lilifikishwa FIFA na mpaka sasa Etoile Du Sahel hawajailipa Simba Sc fedha za mauzo ya mchezaji huyo.
Mchezaji
huyo mwenye akili kubwa ya mpira na kasi alikuwa na kikosi cha timu ya
Taifa ya Uganda katika michuano ya CECAFA Chellenge jijini Nairobi na
kuonesha kiwango cha juu na sasa ametua Jangwani.
Yanga
wamefanya usajili huo kwa lengo la kuimarisha kikosi chao kabla ya
kuanza kampeni za ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.
Mpaka sasa wametangaza kumsajili Juma Kaseja, Hassan Dilunga na leo hii Okwi imetia nanga katika rada zao.
MAMA SALMA APOKEWA KWA SHANGWE BAADA YA KURUDI NA TUZO YA UONGOZI KUTOKA DUBAI
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akiwasili kwenye ofisi yake iliyoko karibu na Ikulu mara
baada ya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu
alikopokea tuzo ya uongozi huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuja
kumpokea tarehe 19.12.2013
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea maua kutoka kwa Mwenyekiti wa wake
wa viongozi, Mke wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa
William Lukuvi na Mwakilishi kutoka ofisi ya WAMA, mara baada ya
kuwasili ofisini hapoakitokea Dubai kupokea Tuzo ya uongozi itolewayo na
Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA akiangalia ngoma za utamaduni mara baada
ya kuwasili kwenye viwanja vya Ofisi za WAMA, ambako mamia ya wananchi
walikusanyika kwa ajili ya kumpongeza baada ya kurudi na Tuzo ya uongozi
aliyopokea huko Dubai tarehe 18.12.2013.
Baadhi
ya wananchi walioshiriki mapokezi ya Mama Salma wanaonekana
wakimsikiliza wakati alipokuwa akiwahutubia katika viwanja vya WAMA
tarehe 19.12.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi waliofika kumpokea
aliporejea kutoka Dubai tarehe 19.12.2013. Mama Salma alienda huko
kupokea Tuzo ya uongozi ulitukuka kutokana na kazi anazofanya kupitia
Taasisi yake kwa ajili ya elimu kwa wanaotoka katika mazingira magumu,
afya ya mama na mtoto pamoja na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akiongea jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Raymond Mushi wakati wa
shamrashamra za kumpokea Mama Salma baada bya kuwasili nchini akitokea
Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu kupokea TUZO ya uongozi uliotukuka.
Tuzo hiyo hutolewa na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi,
(CELD).
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza na wananchi waliofika kumpokea kwenye ofisi za WAMA tarehe 19.12.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI
RAIS DKT. KIKWETE AENDA MAREKANI KUFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatano, Desemba 18, 2013, kwenda
Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Kwa
mujibu wa ratiba ya shughuli za uchunguzi wa afya yake na kwa kutilia
maanani siku za kusafiri kwenda Marekani na kurudi nchini, Rais Kikwete
anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki ijayo, Desemba 26, 2013.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2013
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2013
IDDY MNYEKE AMPANIA COSMAS CHEKA DESEMBA 31
Bondia Iddy Mnyeke akipambana na Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam mabondia hawo watapanda ulingoni kuwakabili wapinzani wao ambapo Mnyeke atacheza na Cosmas Cheka na King class mawe atazidunda na Mohamed Kashinde desemba 31 katika ukumbi wa msasani klabu kulia ni kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli ‘Masta’ Picha na BLOG YA SUPER D |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Iddy Mnyeke yupo katika
mazoezi mazito akijiandaa na mpambano wake na Cosmas Cheka utakaofanyika
desemba 31 katika ukumbi wa msasani klabu jijini ar es salaam
akizungumzia mpambano huo mnyeke
amesema cheka ni mtoto mdogo sana anazani anaweza kusafiria nyota ya
kaka yake ajue ameingia anga nyingine hivyo ata kiona cha mchema kuni
kwa mimi sio kama mabondia aliewai kuwashinda
Mnyeke ambaye anafanya mazoezi
katika kambi ya ilala jijini Dar es salaam ameongeza kwa kusema siku
hiyo watu waje kwa wingi wangalie anavyo mchakaza na kuongeza kuwa waje
yeye na kaka yake ili apate msaada wakati atakapo mwangusha chini kwa
ngumi kali misri ya nondo
ambazo zitakazo msambalatisha raundi za awari kwani yeye ni cha mtoto kwake
Katika
mchezo huo kutakuwa na michezo mingine ambapo bondia Ibrahimu Class
‘King Class Mawe’ ataoneshana ubabe na Mohamed Kashinde,Antony Mathias
akizipiga na Fadhili Majiha katika mchezo mwingine ni kati ya Fransic
Miyeyusho wa Tanzania akizichapa na David Chalanga kutoka Kenya
Katika
mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo
wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali
kama vile
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS IKULU NA UTAWALA BORA ZANZIBAR AWEKA JIWE LA MSINGI LA KITENGO KIPYA CHA UTIBABU WA UTI WA MGONGO NA UBONGO
Jengo jipya la kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo linalojengwa kwa mashirikiano ya Serekali ya Spen na ya Zanzibar.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mhe. Mwinyi Haji Makame
(wakatikati) akiongozana na viongozi mbalimbali kuweka jiwe la msingi la
kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo katika kuadhimisha
miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, sherehe hiyo imefanyi Mnazi mmoja
Hospitali Mjini Zanzibar.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATUNUKU SHAHADA ZA UZAMILI KWA WAHITIMU TAASISI YA NELSON MANDELA ARUSHA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Bilal ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia
ya Nelson Mandela iliyopo Arusha, akiwa kwenye maandamano ya wahitimu wa
shahada ya uzamili kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo
iliyofanyika leo Disemba 19-2013.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akihutubia kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika
leo Disemba 19-2013.
Makamu
Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela
iliyopo Arusha akimkabidhi zawadi maalum Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambae pia ni Mkuu
wa Taasisi hiyo kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika
leo Disemba 19-2013.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Bilal , akimtunuku Clarence Msafiri mhitimu wa shahada ya uzamili
kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba
19-2013.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Bilal ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya
Nelson Mandela iliyopo Arusha, katikati akiwa katika picha ya pamoja na
wahitimu wa shahada ya Uzamili kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi
hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.
(Picha na OMR
Subscribe to:
Posts (Atom)