Okwi katikati baada ya kuwasili JNIA akiwa na Katabaro kulia na Bin Kleb kushoto jioni hii na chini akionyesha jezi namba 25.
Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
HABARI
ya mjini kwa muda huu ni kwamba; mshambuliaji mpya wa Yanga, Emmanuel
Anord Okwi amewasili alasiri ya leo uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam tayari kwa kuanza kazi ya kuitumia
klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Okwi
ametia miguu Tanzania saa 9:30 kwa ndege na kulakiwa na viongozi wa
Yanga ambao walikuwa na uchuku wa kupokea jembe lao la kazi.
Waandishi
wa habari walikuwa na uchu wa kusikia kauli ya Okwi na ndipo muda
ukafika baada ya nyota huyo kutoka nje ya uwanja wa JNIA ambapo alisema
amekuja Yanga kufanya kazi.
Alipoulizwa
sakata lake la usajili, Okwi alifungua mdomo wake kwa mara nyingine na
kusema; “Mimi nimekuja kufanya kazi, hayo mengine hayanihusu, zipo
mamlaka zinazohusika na zitajua la kufanya”.
Cha kufurahisha Okwi amewasili akiwa tayari ameshavalia jezi ya Yanga, namba 25 mgongoni.
Akizungumza
uwanjani hapo, mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga, Abdallah
Ahmed Bin Kleb amesema Okwi anakwenda moja kwa moja katika hoteli ya
Protea kuungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kesho
kutwa ya Nani Mtani Jmebe dhidi ya Simba sc, uwanja wa Taifa.
Wakati Okwi akiwa amewasili, taarifa iliyopatikana kutoka mtandano wa MTNFootball.com
mchana wa leo imeeleza kuwa kaimu mkurugenzi wa mashindano wa
shirikisho la soka nchini Uganda FUFA, Decolas Kiiza amethibitisha kuwa
FIFA wamemruhusu Okwi kujiunga na Yanga.
“Ndiyo tuliandika barua FIFA na walisema mchezaji yuko huru kuuzwa”. Kiiza aliuambia mtandao wa MTNFootball.com.
Mapema
wiki hii Mkurugenzi mkuu wa FUFA, Edgar Watson alisema wameiandika FIFA
barua kuhitaji maelezo zaidi juu ya suala la Okwi.
Okwi
aliuzwa na Simba katika klabu ya Etoile Du sahel ya Tunisia januari
mwaka huu kwa kitita cha dola 300, 000 za kimarekani, lakini hakudumu
katika klabu hiyo kwa madai ya kutolipwa haki zake na kuamua kurejea
kwao Uganda.
Okwi
baada ya kurejea kwao Uganda alikaa miezi sita bila kucheza na ndipo
shirikisho la kandanda la Uganda (FUFA) likasimama kidete kumpigania
aruhusiwe kureja nyumbani na kujiunga na Sport Club Villa ya Uganda
`Majogoo wa Kampala` ili kulinda kiwango chake.
Kwa
usajili wa Okwi, Yanga imetimiza wachezaji watano wa kigeni kwa maana ya
washambuliaji Didier Kavumbagu, Khamis Friday Kiiza, beki Mbuyu Twite,
kiungo Haruna Niyonzima.
Sakata la Okwi lilifikishwa FIFA na mpaka sasa Etoile Du Sahel hawajailipa Simba Sc fedha za mauzo ya mchezaji huyo.
Mchezaji
huyo mwenye akili kubwa ya mpira na kasi alikuwa na kikosi cha timu ya
Taifa ya Uganda katika michuano ya CECAFA Chellenge jijini Nairobi na
kuonesha kiwango cha juu na sasa ametua Jangwani.
Yanga
wamefanya usajili huo kwa lengo la kuimarisha kikosi chao kabla ya
kuanza kampeni za ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.
Mpaka sasa wametangaza kumsajili Juma Kaseja, Hassan Dilunga na leo hii Okwi imetia nanga katika rada zao.
No comments:
Post a Comment