TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 31, 2013

LULU KUTOKA RUMANDE CCM yajitosa sakata la gesi *Kinana adai wananchi Mtwara wana hoja *Nape asisitiza rasilimali kunufaisha wote *53 wafikishwa kortini, Nchimbi atoa agizo Mpina alipuka utoroshaji tril. 11.6/- *Aitupia lawama serikali, apeleka hoja bungeni CHUPA DC Korogwe ategwa kwa magogo Kisandu amtega Zitto Bulembo amshukia Bujugo UKAMATAJI Uchumi umekua kwa asilimia 6.7-Mgimwa BoT yataka Katiba Mpya iwabane wanasiasa wasiingilie utendaji VITAFUNWA Wazee waliopigana Vita ya Dunia wailaumu Serikali Bilioni 8/- zatengwa kwa ajili ya mradi wa UMATA Wenyeviti waitaka Serikali kuzitambua kazi zao kikatiba MAKABURI Polisi Pwani yawashikilia wahamiaji haramu watano Wakulima wa kahawa watuhumiana K'njaro TRA yatakiwa kutafuta mbinu mpya ya ukusanyaji kodi JK kuzindua mkutano wa TNBC WAKIPONGEZANA PFT yaitaka jamii kufahamu umuhimu wa VICOBA Haki za binadamu waombwa kuingilia mgogoro wa mirathi Maktaba sekondari ya Baobab kugharimu mil. 800

Posted: 29 Jan 2013 02:27 AM PST
Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu'  akiongozwa na askari magereza, wakati akitoka Mahabusu ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam jana, baada ya taratibu za dhamana kutokamilika. Msanii huyo anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii wa filamu, marehemu Steven Kanumba. (Picha na Charles Lucas)
Posted: 29 Jan 2013 02:24 AM PST

Na Waandishi Wetu, Mtwara na Dar
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Abdulrahman Kinana, amesema wananchi mkoani Mtwara wana hoja ya msingi kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam, hivyo wanahitaji majibu sahihi ya kuwaridhisha.
Bw. Kinana aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye  kipindi cha 'Power Breakfast', kinachorushwa na Redio Clouds akiwa mkoani Kigoma alikwenda kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM.
Alisema wananchi hao wana hoja ambayo hivi sasa imerukiwa na wanasiasa wakidhani wanaikomoa CCM wakati wanaoumia ni wananchi.
“Hoja ya wananchi ya Mtwara ni ya msingi japo imerukiwa na wahuni na kuanza kuchoma magari ya watu, wana Mtwara
wanahitaji majibu ya kile wanachokihoji,” alisema.
Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, alisema msimamo wa chama hicho ni rasilimali zote za nchi kunufaisha Watanzania wote.
“Mimi ni mtu wa Kusini, kama ningezuiwa nisitoke ndani ya Mkoa wangu hata shule nisingesoma...naiomba Serikali iwachukulia hatua bila huruma watu wote waliohusika na uchomaji moto magari na kuharibi mali,” alisema Bw. Nnauye.
Wakati huo huo, miili ya watu wanne waliouawa na polisi kwa kupigwa risasi wilayani Masasi, imezikwa juzi katika makaburi
ya Masasi Mbovu, Nyasa na Upanga kati ya saa nne asubuhi
na 10 alasiri.
Maiti mbili kati ya hizo, moja imetambuliwa kwa jina la Jofrey Banabas na nyingine imefahamika kwa jina la Imrani.
Wakizungumza na waandishi wa habari, ndugu wa marehemu Simonje, walilaani kitendo cha polisi kutumia risasi za moto
kutuliza ghasia na kusababisha mauaji.
“Inakuwaje askari aliyepata mafunzo wanapambana na raia wasio
na silaha kwa kutumia risasi za moto, wao walipaswa kutumia
mbinu za kukabiliana nao si vinginevyo,” walisema.
Miili ya marehemu hao imekutwa na matundu ya risasi  tumboni, kifuani, kitovuni, mgongoni na maeneo mengine ya mwili.
Katika vurugu hizo, watu 13 akiwemo polisi mmoja aitwaye Hosea Kibona, wameumizwa vibaya sehemu mbalimbali ya miili yao na kulazwa Hospitali ya Mission ya Ndanda.
Kati ya majeruhi hao, 12 bado wamelazwa hospitalini hapo wakiendelea na matibabu wanne kati yao wapo mahututi na
mmoja aliyeumia bega la kushoto alitibiwa na kuruhusiwa.
Waziri Pinda
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, jana aliwasili mkoani humo kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali pamoja na wawakilishi wa wananchi ili kutafuta suluhu ya mgogoro
huo akiwa katika ziara ya siku mbili kuanzia jana.
Katika ziara hiyo, Bw. Pinda alichukua maoni ya viongozi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na wafanyabiashara ambao wengi wao walitaka Serikali isitishe uamuzi wa kusafirisha gesi kutoka mkoani humo kwenda jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi wa wananchi walidai kuwa, hawaoni umuhimu wa Serikali kusafirisha gesi hiyo kwenda Dar es Salaam hivyo ni
bora itafute uratatibu mwingine.
Baadhi yao waliiomba Serikali kumwondoa Mkuu wa Mkoa huo kwa madai ya kushindwa kusimamia suala hilo kikamilifu na
kutetea gesi hiyo isisafirishwe.
Taarifa iliyotufikia wakati tukienda mtamboni, inadai kuna tetesi kuwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli wanatarajia kuwasili mkoani humo leo ili kuongeza nguvu ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Watumishi Mtwara
Watumishi wa idara mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, jana walijikuta wakisota nje baada ya ofisi zao kuteketezwa kwa moto kutokana na vurugu zilizotokea hivi karibuni.
Baadhi ya watumishi hao walionekana wakichambua mabaki ya nyaraka ambazo ziliungua moto.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake, Ofisa Elimu Taaluma wa Shule za Msingi, wilayani humo, Garama Kinderu alisema wamelazimika kukaa nje baada ya ofisi yao kuchomwa
moto na vijana waliokuwa wakiandama kupinga mwendesha
pikipiki 'bodaboda, kukamatwa na polisi.
Alisema idara ya elimu imeathirika kwa kupoteza kumbukumbu
za walimu, wanafunzi na taarifa za maendeleo ya elimu baada
ya kuungua kwa kompyuta zilizokuwa zikitunza kumbukumbu.
Watuhumiwa 53
Katika hatua nyingine, watuhumiwa 53 wanaodaiwa kuhusika na vurugu zilizotokea wilayani humo, jana wamefikishwa kwenye mahakama ya Wilaya na kusomewa mashitaka yao likiwemo
la kula njama, kutenda kosa la kuchoma moto majengo ya halmashauri ya wilaya na uharibifu wa mali.
Wakisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Elizabert Nyembele, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Bw. Daniel Samuel, alidai kwa nyakati tofauti watuhumiwa walitenda kosa la kuchoma moto majengo na uharibu mali.
Alidai washtakiwa waliichoma moto Ofisi ya CCM Wilaya, Mahakama ya Mwanzo Lisekese, Ofisi ya Idara ya Elimu, Msingi
na Sekondari, Maliasili na Wanyama pori, magari ya halmashauri,
nyumba za raia na viongozi ikiwemo ya mbunge wa Masasi,  Mariamu Kasembe na Anna Abdallah.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Februari 11 mwaka huu na watuhumiwa wamerudishwa rumande baada ya upande wa Serikali kupeleka pingamizi la washtakiwa kupewa dhamana.
Ziara ya Dkt. Nchimbi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, jana alifanya ziara ya kukagua majengo ambayo yameteketea kwa moto kutokana na vurugu hizo.
Katika ziara hiyo, Dkt. Nchimbi aliongozana na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Bw. Paul Chagonja pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mngulu.
Dkt. Nchimbi aliliagiza jeshi hilo wilayani humo kuhakikisha kuwa, wote waliohusika katika uharibifu huo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
“Tukio hili limenisikitisha sana kwani ni la aina yake kutokea hapa nchini, uharibifu wa mali umekuwa mkubwa pamoja na nyaraka za Serikali hivyo kusababisha hasara kwa Taifa,” alisema.
“Hatuwezi kuacha vitendo hivi vinaendelea kuharibu amani, mali za watu na Serikali, naliagiza Jeshi la Polisi wilayani hapa kuusaka mtandao unaofanya vitendo hivi,” alisema Dkt. Nchimbi.
Hasara ya mali
Katika vurugu hizo, magari, majengo ya watu binafsi na taasisi za Serikali, yaliharibiwa vibaya kwa kuchomwa moto ambapo hadi
sasa, hasara iliyotokana na uharibifu huo bado haijafahamika.
Vurugu hizo zinazodaiwa kufanywa na vijana wenye umri chini ya miaka 40 kwa madai ya kuchoshwa na tabia ya baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kunyanyasa wananchi hasa vijana wakiwemo waendesha pikipiki za abiria wilayani Masasi.
Majengo nane yaliharibiwa katika vurugu hizo na magari 11 zikiwemo nyumba tatu za kuishi zinazomilikiwa na Bi. Mariamu Kasembe, Bi. Anna Abdallah na polisi wa Usalama Barabarani
aliyefahamika kwa jina la Mussa Kero.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Maria Nzuri, ameitaka jamii kutojihusisha na masuala ya vurugu ili kudumisha amani iliyopo nchini na kama wana madai, watumie njia zinazokubalika kudai
haki zao badala ya kufanya vurugu na kuharibu mali.
Upatikanaji mahitaji
Kutokana na vurugu kubwa zilizotokea juzi wilayani humo, baada ya kundi la waendesha pikipiki za kubeba abiria 'bodaboda', kufanya maandamano wakipinga kukamatwa na polisi, kutozwa faini zisizo lingana na makosa halisi, hali hiyo imesababisha upatikanaji wa huduma za msingi kuwa mgumu.
Wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi walisema hali ya upatikanaji mahitaji ya msingi ni ngumu kutoikana na maduka pamoja na vipanda vinavyotoa huduma kufungwa siku mbili mfululizo tangu kutokea vurugu hizo.
“Tumekuwa tukihangaika kutafuta bidhaa mbalimbali bila mafanikio hivyo kusababisha ugumu wa maisha,” alisema Bw. Mohamed Rajanu na kuongeza kuwa, bidhaa zisizopatikana kirahisi ni
vocha za simu, mchele, sukari, ngano, mafuta ya kupikia.
Imeandikwa na Reuben Kagaruki, Said Hauni, Cornel Anthony na Hamisi Nassir.
Posted: 29 Jan 2013 02:23 AM PST

Na Benedict Kaguo

MBUNGE wa Kisesa, mkoani Simiyu, Bw. Luhaga Mpina (CCM), amefichua mpango wa Serikali kuwalinda viongozi walioficha fedha katika benki zilizopo nje na kusababisha umaskini kwa Watanzania.
Alisema kitendo cha kuondolewa kipengele kinachozungumzia  utoroshaji fedha zaidi ya sh. trilioni 11.6, kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliopitishwa na Bunge, inaonesha Serikali haina nia ya kurejesha fedha zilizofichwa na wajanja.
Bw. Mpina aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, kutokana na hali hiyo amedhamiria kuwasilisha hoja binafsi katika Mkutano wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma ili Serikali iwaeleza Watanzania kwanini kipengele hicho kimeondolewa.
“Kwa kutumia kifungu cha 55 cha kanuni za Bunge toleo la 2007, tayari nimepeleka barua kwa Spika kumweleza kuwa, kipengele kilichokuwa kwenye mpango huo hakijawahi kuondolewa na
Bunge... lakini Serikali imekifuta wakati Watanzania wanataka
mjadala huo uendelee ili fedha hizo zirejeshwe,” alisema.
Aliongeza kuwa, kwa kutambua unyeti wa suala hilo barua yake ameipeleka kwa Spika Januari 23 mwaka huu, kutaka hoja hiyo ijadiliwe bungeni ili kujua sababu ya kufutwa kipengele hicho.
Alisema Bunge la Aprili 2011, lilipitisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano na kipengele hicho kilikuwepo kikizungumzia suala la utoroshaji fedha nje hivyo ni jambo la kushangaza kuona mwaka 2012, wakati akisoma mpango huo bungeni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wassira, kipengele hicho kilikuwa kimeondolewa.
Bw. Mpina alisema tatizo la ufisadi haliwezi kumalizika kama Serikali haioneshi nia ya dhati ya kupambana na vitendo hivyo ambavyo vinawaumiza wananchi masikini nchini.
“Bunge litahoji kwa nini kipengele cha utoroshaji fedha nje ya nchi kiliondolewa wakati Serikali inasema ina dhamira ya kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa nchini,” alisema Bw. Mpina
Hata hivyo, katika Bunge la Bajeti 2012/2013, Bw. Mpina aliikataa bajeti ya Serikali kwa sababu ya kutoweka fedha za kutosha katika shughuli za maendeleo huku akifichua utoroshaji wa sh. trilioni 11.6 uliofanywa kuanzia mwaka 1979 hadi 2008. 
Posted: 29 Jan 2013 02:21 AM PST

Mkazi wa jiji ambaye (hakutaja jina), akiwa amebeba chupa tupu za maji zilizotumika kwa lengo la kuziuza, kama alivyokutwa na mpigapicha wetu.  Pamoja na kujipatia kipato kwa kazi hiyo pia uokotaji wa chupa hizo kunaliweka jiji safi. (Picha na Prona Mumwi)
Posted: 29 Jan 2013 02:19 AM PST

Na Yusuph Mussa, Korogwe

MSAFARA wa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Bw. Mrisho Gambo, juzi uliwekeza magogo barabarani na kusababisha taharuki kubwa kwa watu waliokuwa katika msarafa huo.
Magogo hayo yaliwekwa kwenye Kitongoji cha Kwemshai- Miembeni, wakati Bw. Gambo na msafara wake wakitoka Kijiji
cha Kizara, Kata ya Kizara, Tarafa ya Magoma, kukagua
maendeleo ya zahanati ya kata hiyo.
Msafara huo ulikuwa ukienda Kijiji cha Bombo-Majimoto, kuzungumza na Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Kizara
ukiwa na magari manne.
Katika msafara huo, alikuwepo Mbunge wa Korogwe Vijijini,
Bw. Stephen Ngonyani, Kamati ya Ulinzi na Usalama ambao
wote walihofia kutekwa na majambazi.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walishuka na kwenda kutoa magogo hayo ambapo baadaye ilibainika kuwa, vijana walioweka magogo hayo walikuwa wanataka kupewa fedha
na viongozi waliokuwa katika msafara huo.
Pamoja na vijana hao kudai wao hawakuhusika kuweka magogo hayo, tisa walikamatwa wakiwemo waliokuwa wakinywa pombe
ya kienyeji 'boha',  chini ya Mwembe na kupakiwa katika gari la
Bw. Gambo, lenye namba STK 3837, gari la Ofisa Usalama wa
Taifa, wilayani humo T 775 BFP na gari la Halmashauri ya
Wilaya SM 3842.
Baadhi ya vijana hao walimtaja mwenzao Bw. Juma Mgosi ambaye alifanikiwa kukimbia na kudai ndiye aliyeweka magogo hayo.
Hata hivyo, vijana hao waliongozana na msafara huo hadi Kijiji cha Bombo-Majimoto ambapo kulikuwa na mkutano wa hadhara na kuachiwa saa moja usiku wakati msafara ukiondoka kurudi mjini Korogwe baada ya Bw. Nyonyani kumuomba Bw. Gambo awaachie.
Baadhi ya vijana hao walijikojolea katika magari waliyopatika ambapo Bw. Ngonyani alidai kuwa, vijana hao aliwazoesha
vibaya kwani kila anakopita barabara hiyo huwapa fedha
lakini njia waliyotumia siku hiyo kuweka magogo si sahihi.
“Nimeambiwa wale vijana walikuwa wanataka pesa ndio maana waliweka magogo wakati msafara ukipita lakini njia waliyotumia
haikuwa sahihi walifanya makosa,” alisema Bw. Ngonyani.
Posted: 29 Jan 2013 02:18 AM PST

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Uhusiano na Uenezi Taifa, Kitendo cha Vijana wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. Deogratius Kisandu, amesema Tanzania imekosa vijana wazalendo ndio sababu ya kushindwa kutekeleza wanachokisema.
Bw. Kisandu aliyasema hayo katika taarifa yake aliyoitoa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), kushindwa kuwataja vigogo walioweka mabilioni ya fedha nchini Uswisi.
Alisema kitendo cha Bw. Kabwe kushindwa kuwataka vigogo hao ni kuwahujumu Watanzania ambao walitegemea angewataja ili kuonesha uzalendo badala yake suala hilo ameiachia Serikali.
“Serikali haiwezi kuwataja vigogo husika, Bw, Kabwe alipaswa kuonesha uzalendo wa kuwataka kama kweli ana uhakika, hakuna haja ya kusubiri upelelezi au kuundwa kamati wakati tayari alishasema majina yao anayo,” alisema Bw. Kisandu.
Aliongeza kuwa, umefika wakati wa Wanasiasa waache kuwahadaa wananchi bali wawe wawazi na wenye uchungu na Taifa lao hasa ukizingatia kuwa, walimu wanalia mishara midogo na wajasiliamali kukosa mikopo ya mabilioni ya Rais Jakaya Kikwete.
Alisema Mtwara wanalia njaa hivyo kugomea gesi isitoke nje ya Mkoa huo wakati kuna fedha nyingi ambazo zingeweza kuokoa
maisha ya Watanzania.
“Serikali haihitaji kuunda kamati wala tume bali wahusika watajwe moja kwa moja...kama Bw. Kabwe atashindwa kuwataja mimi nipo taayari kuwataja Februari mwaka huu kama atanipa majina hayo.
“Wakati wa kuogopana umekwisha, hivi sasa tunajenga Taifa na kama atashindwa kufanya hivyo ni bora avuliwe ubunge maana hajawatendea haki Watanzania..hatuhitaji viongozi ambao wanashindwa kutekeleza walichokisema,” alisema.
Posted: 29 Jan 2013 02:18 AM PST

Na Gladness Mboma

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Bw. Abdallah Bulembo, amemtaka Diwani wa Kata ya Magomeni Dar es Salaam, anayeendesha Chuo cha Kilimo cha Kaole, kilichopo Bagamoyo, mkoani Pwani, Bw. Julian Bujugo, kukikabidhi chuo hicho kwa jumuiya hiyo kabla hajachukuliwa hatua za kisheria.
Bw. Bulembo alitoa agizo hilo wakati akijibu maswali ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), wilayani humo, Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Jumuiya ya Wanawake (UWT) na Mabaraza ya Wazazi kwenye kikao cha ndani.
Wajumbe hao walitaka kufahamu hatima ya chuo hicho kurudi mikononi mwa jumuiya hiyo ambapo Bw. Bulembo alisema,
uamuzi wa jumuia hiyo kumuondoa Bw. Bujugo katika chuo
hicho uko pale pale kwani hana haki kisheria ya kuendelea
kuwepo eneo hilo na kufanya ujenzi kiholela.
“Bujugo aliingia hapa kijanja, mikataba yake ni feki, haina baraka za Baraza Kuu la Wadhamini la Wazazi, lakini kibaya zaidi anaendelea na ujenzi bila kuwa na kibali kutoka wazazi au halmashauli hili ni kosa lingine.
“Kabla sijachukua hatua nyingine za kisheria, nakuagiza Ofisa
Ardhi uliopo hapa, usimamishe mara moja ujenzi unaoendelea, lazima Kaole iendelee kuwa ya Wazazi kama ilivyokuwa awali maana ina historia kubwa kwa wakazi wa Bagamoyo, chama na Serikali,” alisema Bw. Bulembo.
Bw. Bujugo anadaiwa kukabidhiwa shule ya sekondari na Ufundi Kaole ili kuiendesha kama Meneja wa shule lakini alikiuka makubaliano na kuigeuza shule hiyo kuwa Chuo cha Kilimo.
“Nawahakikishia kipimo changu cha uongozi katika jumuiya
hii, mtakiona katika suala hili ili jumuiya ipate haki yake kwa kurudishiwa shule yake ambayo hivi sasa ni chuo.
“Tukiwa mjini Dodoma wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akifunga mkutano wetu wa uchaguzi, alidai kukerwa na hali ilivyo sasa katika shule hii yenye historia
kubwa katika nchi yetu.
“Leo hii majengo ya kihistoria yamevunjwa jambo ambalo si kwamba limemkera Rais wetu pekee, hata wananchi ndani na
nje ya Bagamoyo,” alisema Bw. Bulembo.
Kwa upande wake Mjumbe wa NEC, wilayani humo Bw. Ridhiwani Kikwete, alisema hakubaliani na mikataba iliyopo kati ya wazazi na Bw. Bujugo.
“Nakushukuru sana Mwenyekiti kwa kuliona hili, lakini niwaulize ndugu zangu ni kweli tunashindwa kuchukua hatua hadi mgeni aje ndipo tuseme matatizo yetu,” alihoji Bw. Kikwete.
Alisema yeye kitaaluma ni Mwanasheria na haelewi kitu kuhusu mkataba huo ambapo Bw. Bujugo hawezi kuliendeleza eneo hilo
bila kibali hivyo alimuunga mkono Bw. Bulembo na kusisitiza
kuwa, Wilaya hiyo ina maatatizo kwa Maofisa wa Ardhi ambao
wamekuwa wakifanya kazi kinyume na maadili.
Aliongeza kuwa, baadhi ya watendahi wameifanya wilaya hiyo kama 'shamba la bibi', kwa ajili ya kufanikisha mipango yao ya kudhulumu ardhi za wananchi na kuwaacha wakitaabika kutafuta
haki zao na wengine kupelekwa mahakamani kwa kudai haki.
Awali wananchi hao waliulalamikia uongozi wa halmashauri hiyo kutokana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wake hususan Idara ya Ardhi kuuza ardhi ya wananchi bila ridhaa yao.
Kwa upande wake, Bujugo alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alisema hawezi kuzungumza lolote ila anaamini chuo hicho anakiendesha kisheria na ana mikataba yote inayomruhusu
kuwepo eneo hilo.
Posted: 29 Jan 2013 02:16 AM PST

Askari wa Jiji akifungua mnyororo katika gurudumu la gari lenye na za kibalozi T 25 CD 123, kama alivyokutwa Posta Mtaa wa Samora, Dar es Salaam jana. Ukamataji wa magari ya kibalozi unahitaji utaratibu maalumu. (Picha na Asia Mbwana)
Posted: 29 Jan 2013 02:14 AM PST
Na Eliasa Ally, Iringa

WAZIRI wa Fedha na Uchumi Dkt.william Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Kalenga katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini amesema kuwa hali ya uchumi hapa nchini inaendelea kuimarika ambapo kwa sasa uchumi ndani ya nchi umekua hadi kufikia asilimia 6.8 hali ambayo inaleta matumaini makubwa kwa wananchi na serikali yao.
Hayo aliyasema jana alipokuwa akizungumza na wananchi katika uwanja wa Mwembetogwa wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Philipo Mangula alipokuwa amekuja mkoani Iringa na kuzungumza na wananchi wa mkoa wa Iringa ambapo alisema kuwa kuna ongezeko kubwa linaloonesha uchumi wa nchi kwa sasa unakua kwa kasi tofauti na hapo awali ambapo uchumi ulikuwa unalalamikiwa.
Dkt.Mgimwa alisema kuwa serikali ya CCM inaendelea kuhakikisha kuwa uchumi ndani ya nchi unaendelea kukua kwa kasi na kuwawezesha wananchi pamoja na serikali yao kupata maendeleo sitahiki katika kufanya biashara, kuuza mazao na kwa upande wa serikali kuhakikisha wanakusanya kodi kufikia malengo ambayo yamewewekwa na serikali inayosimamiwa na CCM.
"Kwa sasa maendeleo yanapiga hatua kubwa kiuchumi, takwimu za sasa zinaonesha kuwa uchumi wetu ndani ya nchi umekua kwa asilimia 6.8, hii ni hatua kubwa sasa hivyo katika kila hatua ambayo tunapiga tutahakikisha tunawarifu ninyi wananchi ili mweze kufahamu bayana hali yetu ya kukua kwa uchumi wa ndani", alisema Dkt. Mgimwa.
Aidha, alisema kuwa kutokana na uchumi wa ndani ya nchi kuendelea kuimarika na kukua kwa kasi, wafanyabiashara, wakulima na wajasiliamali wataendelea kukuza mitaji yao ambapo aliwataka kila mwananchi aendelee kuhakikisha kuwa anajiajiri na siyo anakaa
vijiweni na kutaka serikali ndiyo imletee maisha bora huku akiwa amekaa na hawataki kufanya kazi ambazo zitawaingizia vipato.
Aliongeza kuwa maisha bora kwa wananchi yanakuja baada ya wao wenyewe
kujishughulisha, kufanya kazi, kuzalisha shughuli za kiuchumi na kuhakikisha kuwa katika mitaji yao waliyonayo wanendelea kukuza vipato na kushirikiana na serikali katika kufanya kazi za kuajiriwa na kujiajiri mtu binafsi hususani katika shughuli za ujasiliamali.
Posted: 28 Jan 2013 10:09 PM PST
Anneth Kagenda na Rehema Maigala

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imependekeza kuwekwa kipengele cha sheria ambacho kitawabana wanasiasa kutoingilia kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na benki hiyo.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndullu, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa maoni ya Katiba Mpya kwa tume inayoratibu mchakato huo.
Alisema BoT ina jukumu la kutoa huduma nyeti za kiuchumi kwa wananchi wake hivyo haitakiwi kuingiliwa na mambo ya kisiasa.
“Utendaji kazi wa BoT usiingiliwe na siasa kwani ina mambo muhimu ya kufanya ili kukuza uchumi katika Taifa letu hivyo
ipewe uhuru wa kufanyakazi,” alisema.
Aliongeza kuwa, pia kuwepo na sheria mama kwenye Bunge za kuikinga BoT kufanya mambo yake yenyewe bila kuingiliwa ambapo kwa kufanya hivyo kutaboresha utendaji kazi wake.
Akijibu maswali ya waandishi likiwemo la watu kuficha fedha nje ya nchi, Prof. Ndullu alisema historia inaonesha kuwa, watu waliokuwa na fedha nyingi walikuwa wakipeleka fedha zao
nje ya nchi tofauti na sasa ambapo watu wachache wanaiba
fedha na kwenda kuzificha nje.
“Hvi sasa watu wanaiamini nchi yao na fedha nyingi wanazihifadhi nchini...kwa mfano, fedha ya haraka ninayoweza kusema iko nchini ni dola za Marekani bilioni 2.2 hatujahesabu na zingine zilizopo nje hivyo ninachoweza kusema ni kwamba, watu wamewekeza sana kwenye nchi yao na wameiamini,” alisema Prof. Ndullu.
Akizungumzia suala la kutakatisha fedha, Prof. Ndullu alisema ni vigumu kulizungumzia lakini anaamini kama Katiba Mpya itaweka sheria anazozisema, zitaweza kuainisha jambo hilo.
Posted: 28 Jan 2013 10:03 PM PST

Baadhi ya wanawake wachuuzi wa vitafunwa wakisubiri wateja kando ya Barabara ya Msimbazi Karikoo, Dar es Salaam jana. Uuzaji wa vyakula katika mazingira yasiyo rasmi kunaweza kuhatarisha afya ya walaji. (Picha na Peter Twite)
Posted: 28 Jan 2013 09:58 PM PST

Na Darlin Said

CHAMA cha Wazee Waliopigana Vita vya Pili ya Dunia hapa nchini (TCL) wameilaumu serikali kwa kuwatelekeza na kuwaacha wakihujumiwa mali zao.
Akizungumza na gazeti hili Katibu Mkuu wa (TCL), Sylvester Lubala alisema tangu chama chao kiundwe mwaka 1996 kimekuwa na misukosuko pamoja na kukosa ushirikiano kutoka serikalini hasa utetezi wa maslahi yao.
Alisema, kutokana na hali hiyo imesababisha kukosa ruzuku zao zinazotumwa kutoka 'Royal Common Wealth Ex-service League' (RCEL) kutokana na Serikali kutotilia mkazo wowote katika kushughulikia kuhusu pesa zao badala yake zinaliwa na wajanja wachache.
Mbali na hilo, Lubala alivitaja vitu walivyodhulumiwa ni pamoja na kuchang'anywa kwa ofisi yao iliyopo maeneo ya Fire Kariakoo.
Posted: 28 Jan 2013 09:55 PM PST

Na Grace Ndossa

JUMLA ya sh. bilioni nane zimetengwa kwa ajili ya kuendesha mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA) ambao utaanzia katika Mkoa wa Dodoma na jumla ya watu milioni moja watafaidika na mradi huo.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Usafi na Mazingira Prof.Anna Tibaijuka alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Prof. Tibaijuka alisema mradi huo unalenga kuhakikisha usafi wa mazingira unafanyika kikamilifu na upatikaniaji wa maji unakuwewpo katika vijiji hivyo ambao umefadhiliwa na Shirika la Kimataifa lisilokuwa la kiserikali la Plan Intertional.
Alisema kuwa, mradi huo wa usafi utaenda sambamba na upatikaji wa maji utafanyika katika mikoa mitatu ambayo mkoa wa kwanza utaanzia Mkoa wa Dodoma na utafanyika kwa muda wa miaka mitano.
"Mradi wa maji ambayo utakuwa unaendelea hapa nchini utasaidia kupunguza tatizo la maji katika Mkoa wa Dodoma na wananchi wanaweza kuweka mazingira kuwa safi,"alisema Prof.Tibaijuka.
Naye Mkurugenzi wa Plan International kwa upande wa Tanzania, David Muthungu alisema mradi huo umeshaanza kufanyika na wanaendelea kutafuta wadau ambao watasaidia katika mradi huo ili waweze kufikia mikoa yote.
Pia alisema kuwa, kazi yao kubwa ni kusimamia  mradi katika maeneo yaliyoanishwa kwa kujenga visima maeneo ambayo hayana maji na kutoa elimu jinsi ya kutumia maji ili waweze kuweka mazingira safi.
Muthungu alisema, watafanya tathimni katika mradi huo baada ya kukamilika na kutoa ripoti jinsi mradi huo unavyoendelea.
Hata hivyo alisema kuwa, mradi huo unahitaji uwezo mkubwa katika kuhakikisha unafanyika kwa usahihi ili waweze kumaliza kwa muda uliotakiwa.
Posted: 28 Jan 2013 09:52 PM PST

Na Rose Itono

UMOJA wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Dar es Salaam (UWESEMIDA)umeitaka Serikali kuzitambua kazi zao kikatiba kama viongozi wengine kulingana na majukumu yao kikazi.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa UWESEMIDA, Othman Mohamed wakati wa mkutano wao mkuu uliokuwa ukijadili mambo mbalimbali ikiwemo kupitisha rasimu yao kikatiba ili iweze kusajiliwa na kutambulika kikatiba.
Alisema kuwa, kumejengeka tabia ya baadhi ya viongozi wengine kuona kuwa wenyeviti wa serikali za mitaa hawana kazi yeyote kitu ambacho ni ukiukwaji wa taratibu.
Alisema, wenyeviti wa mitaa siku zote ndiyo watendaji wakuu ambao hufanya kazi za kimaendeleo kwa kushirikiana na jamii katika mitaa lakini wamekuwa wakidharaulika.
Mwenyekiti huyo alisema, kulingana na hali hiyo waliamua kuanzisha umoja wao ili kuweza kupashana habari kuhusu fursa mbalimbali zinaweza kutumiwa na wananchi katika kujiletea maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Oysterbay, Peter Mushi alisema kuwa kutokana na hali halisi ya utendaji kazi katika mitaa maofisa watendaji wamekuwa wakijiona ni waungu watu na kuwadharau wenyeviti wa mitaa.
Alisema, hali hiyo inatokana na jinsi serikali inavyowachukulia wenyeviti na kuwaona kuwa ni watu ambao hawana kazi huku wakisahau kuwa kila kitu kinachohusu maendeleo hakiwezi kufanyika ndani ya mtaa pasipo kushirikisha wenyeviti.
Katibu wa UWESEDA, Hassan Kingalu alisema hali hiyo inajidhihirisha na ukweli kuwa serikali haitambui uwepo wa wenyeviti kikatiba mpaka kufikia kutotambua mihuri inayowekwa na wenyeviti katika mitaa.
"Zamani kazi ya mwenyekiti wa mtaa ilikuwa ni pamoja na kuweka mihuri kwa wananchi katika mtaa wake pale linapotokea aidha tatizo au sababu nyingine, lakini sasa hivi wamekuwa hawatambuliki mpaka kuwe na mhuri wa Ofisa Mtendaji,"alisema.
Aliongeza kuwa, hali hiyo inapaswa kutokuwepo na kuwataka maofisa watendaji na wenyeviti kufanya kazi kwa pamoja.
Posted: 28 Jan 2013 09:47 PM PST

Baadhi ya watoto wakiwa wamepumuzika juu ya kaburi ya Mburahati, Dar es Salaam jana, Siku hizi imekuwa kawaida kwa watoto na watu wazima kufanya vijiwe na kucheza juu ya makaburi  tofauti na zamani walijenga heshima na kuogopa vifo. (Picha na Prona Mumwi)
Posted: 28 Jan 2013 09:45 PM PST

Na John Gagarini, Kibaha

JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia wahamiaji haramu watano wa nchi ya Ethiopia na Somalia kwa kuingia nchini bila kibali.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ulrich Matei alisema raia hao walikamatwa wakati wa msako wa kukamata wahamiaji haramu.
Kamanda Matei alisema kuwa, wahamiaji haramu hao walikamatwa Januari 23, mwaka huu huko Kitongoji cha Kibosha Kijiji cha Mapinga wilayani Bagamoyo.
“Wahamiaji haramu hao walikamatwa wakiwa wanasafirishwa kwenye gari namba T 371 BTL aina ya Noah,” alisema Kamanda Matei.
Alisema kuwa, gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Bw.Evarist Mbilinyi (25) dereva wa Mwananyamala Jijini Dar es Salaam akisaidiwa na Omary Karim (28) fundi magari mkazi wa Magomeni Makuti wakielekea Ethiopia kupitia Bagamoyo.
Aliwataja wahamiaji hao kuwa ni Itemegen Wolde (20) mwanafunzi, Beyene Dutano (25), Aduel Ashebo (24) na Detene Bore (25) kutoka nchini Ethiopia na Abdirsa Abdilim (20) ambaye ni raia wa nchi ya Somali.
Posted: 28 Jan 2013 09:40 PM PST

Na Gift Mongi

MRAJISI Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoani Kilimanjaro, Kasya Kasya amedaiwa kukikingia kifua Chama Kikuu cha Ushirika mkoani humo (KNCU) ikiwemo kulihujumu zao la kahawa.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa Oktoba 24, mwaka jana kutoka Chama cha Msingi Marangu Mashariki ambayo mwandishi wa habari hizi ana nakala yake
ilitaka mrajisi huyo kukiruhusu chama hicho kukopa sh. milioni 10 katika Benki ya KCB kwa ajili ya kununulia pembejeo lakini hawakuruhusiwa.
Barua hiyo iliyoandikwa na Mwenyekiti wa chama hicho cha msingi, Charles Lyimo kuomba kukopeshwa kiasi hicho cha fedha ilieleza kuwa KNCU haina fedha kwa ajili ya kuwasaidia wakuliam kununulia pembejeo.
"Madeni tunayodai KNCU ni masawazisho ya bei ya kahawa sh. 500 kwa kila kilo kwa msimu 2011/2012 ambayo ni kilo 40,241. Ambapo hapa ni zaidi ya milioni 20,"ilieleza sehemu ya barua hiyo.
Pia maelezo katika inaendelea kufafanua kuwa, kutokana na ukata unaoikumba KNCU wameshindwa kulipwa mabaki yao hivyo kukosa fedha kwa ajili ya kununulia pembejeo za kuendeleza zao hilo la kahawa.
Hata hivyo wakulima hao kupitia barua yao hiyo walikiri kuwa KNCU ina duka la pembejeo ambalo haliwakopeshi wakulima na badala yake huwauzia bei ghali.
Aidha, kutokana na hali hiyo Mrajisi Msaidizi huyo inadaiwa alikikataza chama hicho kukopa fedha kwa madai kuwa deni limefika kikomo wakati KNCU ina madeni lakini bado wanaruhusiwa kukopa.
Barua ya Mrajisi Msaidizi yenye kumbukumbu namba BD 54/247/04/K ya Desemba 31, 2012 imetaka chama hicho cha msingi kuhudumiwa na KNCU kwa kuwapatia mahitaji yote ikiwemo pembejeo katika duka la chama hicho.
"Mrajisi huyo akijua fika kuwa KNCU ina madeni alikitaka chama cha msingi kihudumiwe na KNCU mahitaji yake yote, ingawa tayari KNCU ilishindwa kulipa mabaki ya wakulima hao.
"Je hakuna madeni yoyote mnayodaiwa na KNCU (1984)LTD? Tafadhali kuweni wawazi kwani wao ndio wenye mamlaka ya kuwahudumia," iliongeza sehemu ya barua hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi, Mrajisi huyo alidai hana lengo la kuitetea KNCU na badala yake mahesabu yake ndio yatakayojieleza na si vinginevyo.
"Ndugu naomba unielewe KNCU sina njama nao hata kidogo ila mimi ninachokijua mahesabu yao ndio yatakayojieleza kaka," alidai Mrajisi huyo.
Katika mkutano mkuu maalumu ulioitishwa mapema Januari mwaka huu, uliolenga kujadili kushuka kwa zao la kahawa Mkoa wa Kilimanjaro uliahidi kulipa mabaki ya wakulima ifikapo tarehe 15 mwezi huu jambo ambalo hadi hivi sasa halijatekelezeka.
Posted: 28 Jan 2013 09:39 PM PST

Na Mariam Mziwanda

NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi Bi.Saada Mkuya ameitaka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kutafuta mbinu mpya za ukusanyaji wa kodi ili kuliongezea taifa mapato.
Bi.Mkuya aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mahafali ya tano ya Chuo cha Uhasibu (TIA) na kusisitiza haja ya mamlaka hiyo kutumia taasisi zake katika kutoa elimu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa kila ngazi ya jamii.
"Tunaitaka TRA waendelee kuimarisha chuo na kuhakikisha kila mwanachuoni anayehitimu anakua balozi katika familia na jamii kwa kueneza elimu ya kulipa kodi na umuhimu wake ili kila mwananchi ajue kuwa ni wajibu wake kwa maslai ya taifa,"alisema.
Alisisitiza wahitimu hao kutumia taaluma hiyo kwa kuwa wabunifu wa somo la maadili na kuwa waaminifu katika kazi zao ili taifa liweze kufikia malengo kwani ongezeko la wataalamu wa kodi ni changamoto kwa Serikali kutokana na mahitaji yaliyopo kwani umuhimu wa walipa kodi kupatiwa huduma ni mkubwa.
Aliutaka uongozi wa chuo hicho kudumisha ushirikiano na vyuo vya Bara la Afrika ili kuendeleza matunda ya vijana kuajiliwa katika nchi mbalimbali huku akiwataka kupanua wigo wa elimu na kuweza kuwafikia nchi nyingi duniani sambamba na kutekeleza mkakati wa uboreshaji wa eneo jipya la ujenzi wa chuo huko Kibaha na mikoani.
Aliitaka TRA kutokuridhika na kiwango cha ukusanyaji wa kodi cha  Sh.trilioni 8 kwa mapato ya ndani kwa mwaka ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo ya kuondokana na bajeti ya utegemezi kwa wahisani na kuitaka mamlaka hiyo kushirikiana na Serikali katika kuchukua hatua kwa kuhakikisha inaondoa malalamiko ya wananchi ya kuwepo maafisa walipa kodi wasio waadilifu.
Naye Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho Pro. Palamagamba Kabudi alieleza kuwa kati ya wahitimu 435 waliotunukiwa cheti miongoni mwao wanawake ni 137 na 298 wanaume ambapo wafanyakazi 33 ni kutoka TRA na nane wakiwa ni maofisa forodha kutoka Botswana. 
Alisema jumla ya wahitimu 186 walitunukiwa cheti cha uwakala wa forodha cha Afrika Mashariki,98 cheti cha usimamizi wa forodha  na kodi huku 88 kati yao wakipatiwa stashahada ya usimamizi wa forodha na kodi na wengine 63 wakipatiwa stashahada ya uzamili katika kodi.
Alisema kuwa chuo hicho kinajivunia uanzishwaji wa kozi ya stashahada ya uzamili inayoitwa master of arts in Revenue law and Administration kwa ushirikiano na chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Chuo Kikuu cha Munster huko Ujerumani.
Posted: 28 Jan 2013 09:37 PM PST
Na Heri Shaaban

RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuzindua mkutano wa biashara wa Kitaifa Machi mwaka huu, utakaohusu semina elekezi kuhusiana na majadiliano ya ushirikiano kwa wote.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na mtaalam wa mazingira ya kufanya biashara kutoka Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Willy Magehema wakati wa kufungua mafunzo ya siku moja yalioandaliwa na baraza hilo.
Alisema kuwa mkutano huo una lengo la kuwainua Watanzania wenye kipato cha chini wawe na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Madhumuni ya mkutano huo wa majadiliano kuwapa elimu viongozi wa kuanzia ngazi ya mtaa hadi Taifa,kwa kushirikisha Jeshi la Polisi ili elimu hiyo iweze kuwafikia kwa kuwa wanashirikiana na wananchi  katika utendaji wa kazi zao.
Pia alisema kuwa lengo kuu kuwapa nyenzo watendaji hao katika kusimamia majukumu yao ambapo mwenye nafasi ndogo kiutendaji awe na uwezo mkubwa kwa ajili ya kukuza uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Temeke Sofia Mgema aliwataka Watendaji wote nchini kusimama na kuangalia uzalendo na kuweka siasa pembeni ili malengo yaliokusudiwa yanatekelezwa kwa manufaa ya Taifa.
Aliwataka Watanzaia kujituma kwa uzalendo katika nyanja za sayansi na teknolojia na kuibua miradi mbalimbali ya ubunifu.
Naye Kamishina wa Kanda Maalum Dar es Salaam Sulemani Kova alisema kuwa bila usalama akutakuwa na uwekezaji mzuri,jeshi la polisi litakikisha linaimalisha ushirikiano ili polisi na raia wawe kitu kimoja katika kukuza uchumi.
Posted: 28 Jan 2013 09:36 PM PST
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto), akipongezana na mmoja wa wanachama wa chama hicho katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Bi. Fatma Bakari  wakati wa mkutano wa kumbukumbu ya Miaka 12 ya mauaji ya wanachama wa chama hicho yaliyotokea Zanzibar. (Picha na Peter Twite)
Posted: 28 Jan 2013 09:31 PM PST

Na Rose Itono

SHIRIKA la Kupambana na Umasikini (PFT) limeitaka jamii kufahamu kuwa VICOBA ni silaa kubwa katika kupambana na umasikini.
Akizungumza Dar es Salaam juzi katika hafla ya uzinduzi wa VICOBA katika kikundi cha Vibukiyo B, Mkurugenzi Mtendaji wa PFT Bw.Issa Mohamed alisema,ili kuweza kukuza uchumi ni wajibu wa jamii kukaa katika vikundi na kubuni miradi ili kuweza kujipatia kipato.
Alisema kuwa,kwa kufanya hivyo kutawezesha jamii kupitia vikundi kupata mikopo ya pamoja na kuweza kupambana na umasikini.
Mkurugenzi alizitaka taasisi zinazojihusisha na utoaji mikopo yakiwemo mabenki mbalimbali yaliyopo nchini kubadilisha sera zao ili ziweze kuendana na matakwa ya wanavikundi.
"Kumekuwa na masharti makubwa katika kupata mikopo hali inayofanya wanavikundi hasa wanawake kushindwa kutumia fursa hizo kupata mikopo',alisema.
Alisema kuwa,mabenki mengi yamekuwa yakitoa masharti magumu ambayo yamewafanya wanavikundi kushindwa kukopa na kusababisha hali ya umasikini kuendelea kuwepo.
"Vikundi hivi vinategemea taasisi za fedha hivyo mkiweka mashati magumu mnawanyima fursa ya kukuza uchumi",alisisitiza.
Hata hivyo Meneja Mwendeshaji Mwandamizi wa Benki wa wanawake Bi. Magreth Msengi aliwataka wanavikundi kuitumia Benki hiyo ili kuweza kukopa na kukuza mitaji yao.
Alisisitiza kuwataka wanavikundi kuwa waaminifu pale wanapopatiwa mikopo ili kuweza kupata fursa za kupata mikopo mikubwa zaidi na kuinua uchumi wao.
Alisema kuna baadhi ya wanavikundi wamekuwa si waaminifu na kusababisha wenzao kupata kazi ya kuwalipia madeni pale wanapowakimbia.
Alisema Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo mbalimbali kwa jamii bila kujali jinsia yeyote kwa faida ya nchi.
Posted: 28 Jan 2013 09:30 PM PST


Na Mariamu Mziwanda

FAMILIA ya marehemu Juma Maulid wameiomba wanasheria za haki za binadamu iwasaidie kupata mirathi ya marehemu baba yao pamoja na Serikali kutokana na baadhi ya ndugu wa familia kuzikumbatia mali hizo kwa miaka mitatu na kusababisha watoto kuishi maisha ya shida na kushindwa kwenda shule.
Akizungumza jana Dar es Salaam kwa masikitiko kwa niaba ya watoto wa marehemu Seif Juma (18),mkazi wa Kijitonyama alisema kutokufunguliwa kwa mirathi hiyo kumesababisha mali za baba yao kutumiwa vibaya na baadhi ya ndugu na kuwaona watoto wa marehemu hawana haki ya kuishi katika nyumba aliyoacha marehemu.
"Tunaomba mirathi ifunguliwe tukabidhiwe mali zetu na sisi tukaishi na mama yetu anayeishi Mbagala kwani maisha tunayoishi hapa ni ya shida ambapo chakula tunafadhiliwa na majirani huku tukilazimishwa kuandika mkataba wa kuruhusu uuzwaji wa gari lililoachwa na baba yetu," alidai kijana huyo.
Aliongeza anawaomba wanasheria wa haki za binadamu na asasi nyingine za kiraia ziwasaidie ili waweze kupata haki zao ikiwa ni pamoja na kulipiwa ada ili waende shule kwani tangu shule zifunguliwe wiki mbili zilizopita hakuna dalili ya kurudi shule.
Juma alisema baba yao aliacha nyumba, magari na yadi ya kuhifadhia magari ambayo ipo Kijitonyama na hulipiwa kodi kiasi cha Dola za Kimarekani 1,000 kwa mwezi lakini ndugu yake na baba yake wa karibu amekuwa akizitumia fedha hizo kwa kuwasomesha watoto wake huku wao akiwaacha na kusaidiwa chakula na sabuni na majirani.
Alisema dada yake wa kwanza aitwaye Mariam amemaliza kidato cha nne mwaka jana na hivi sasa yupo chuo anasomeshwa na mama yake hivyo ni vyema mirathi ikafunguliwa na akapewa kazi ya kusimamia.
"Nimechoka namuomba Mungu na wahisani wanisaidie kutetea haki yetu kwani juzi kulitokea kutoelewana na huyo shangazi yake baada ya kudai ada na sabuni ya kufulia ambapo alianza kunishambulia pamoja na familia yake kisha kwenda kunipeleka kituo cha Polisi Kijitonyama  ambapo nilifunguliwa kesi ya kutumia lugha ya matusi yenye namba RB/ KJN/RB/649/13 na nilikaa mahabusu hadi mama yangu mzazi alipokuja kuniwekea zamana, "alidai.
Kituo cha Polisi Kijitonyama kilikiri kufunguliwa kwa jalada hilo dhidi ya mtoto huyo ambapo ilidaiwa kuwa anatuhumiwa kutumia lugha ya matusi dhidi ya watoto wa shangazi yake.
Naye mama mzazi wa watoto hao Husna Yauo aliiomba serikali imsaidie ili watoto wake waweze kupata haki zao za msingi kwani marehemu amecha mali ambazi zinaweza kuwasomesha watoto ambapo wapo watano na wote hawanufaiki na mali ya marehemu baba huyo.
Wakati huohuo, Abdul Maganga  Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Kijitonyama alisema, wanafahamu kwa undani mali zilizoachwa na baba wa watoto hao lakini wamechoshwa na migogoro ndani ya familia hiyo kwani wamesuluhisha vya kutosha na uroho wa mali wa ndugu wa marehemu wanasababisha watoto hao kuishi maisha ya shida huku mtaa huo wakisubiri mahakama itende haki ili watoto waendelea na masomo
Naye Mjumbe wa shina Omary Bilali alisema amesuluhisha migogoro ya watoto hao kwa muda mrefu lakini kwa kifupi watoto hao wanateseka na wanatakiwa kupewa haki zao.

Posted: 28 Jan 2013 09:29 PM PST

Na Rehema Maigala

SHULE ya sekondari ya Baobab iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani inajenga maktaba ya kisasa itakayoghalimu sh.milioni 800 ili kukidhi haja ya wanafunzi wao
Akizungumza katika mahafali ya saba ya kidato cha sita,mwishoni mwa wiki meneja wa shule hiyo Sophia Swai alisema kuwa,wameamua kujenga maktaba hiyo ili kukidhi haja ya wanafunzi na vilevile kuongeza idadi kubwa ya ufulu kwa wanafunzi.
Alisema kuwa shule yao ni ya wasichana hivyo wanahaja kubwa ya kufaulisha watoto wa kike kwa kuwa ukimwelimisha mtoto wa kike umeimalisha jamii nzima
"Tunajenga maktaba hii na tunatarajia kuongeza vitabu 2000 kila mwanzo wa mwaka kufuatana na mahitaji na ongezeko la wanafunzi "alisema Swai.
Aliongeza kuwa tayari shule hiyo imepata mkopo wa sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo na kwa gharama iliyobaki wanatafuta msaada au mikopo nafuu kutoka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali.
Alisema kuwa kwa sasa hivi shule ina maktaba yenye vitabu 11400 vya kiada na ziada ambavyo kwa wanafunzi tulionao vinatosheleza.
Vilevile alisema kuwa shule ina maabara nne ya fizikia, kemia, baolojia na maabara zote vina vifaa vya kutosha kuwawesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo ili kuongeza ufahamu wao katika masomo ya sayansi.
Naye,MKurugenzi wa shule hiyo Alphan Swai alisema kuwa,sera ya shule yake ni ni kumuelimisha mtoto wa kike ambaye atajitegemea katika maisha yake kifikra,kiuchumi na kijamii katika hali ya sasa ilivyo.
Alisema kuwa shule yake inasajili wanafunzi wenye alama za kuanzia asilimia 30 katika somo la hisabati na 50 katika masomo ya lugha na maarifa.
Aliongeza kuwa jumla ya wanafunzi 140 wa kidato cha sita wanatarajiwa kufanya mitihani ya kumaliza kidato cha sita Februali mwaka huu.
Habari zote kwa Mujibu wa Mtandao wa Gazeti la Majira.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KANDA WA MASHAURIANO WA BARAZA LA VIJANA WA JUMUIYA YA MADOLA.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mkutano  wa  Mashauriano wa Kanda wa  Baraza la Vijana wa Jumuiya ya Madola uliofunguliwa leo Januari 29, 2013 katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bila, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bila, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bila, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bila, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo, wanaowakilisha makundi mbalimbali ya vijana.



Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, akizungumza wakati wa Mkutano  wa  Mashauriano wa Kanda wa  Baraza la Vijana wa Jumuiya ya Madola uliofunguliwa leo Januari 29, 2013 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam.


:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo, wanaowakilisha makundi mbalimbali ya vijana.






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Maendelea ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel, baada ya kufungua mkutano wa  Mashauriano wa Kanda wa  Baraza la Vijana wa Jumuiya ya Madola uliofunguliwa leo Januari 29, 2013 katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel, wakati wa ufunguzi wa Mkutano  wa Mashauriano wa Kanda wa  Baraza la Vijana wa Jumuiya ya Madola uliofunguliwa leo Januari 29, 2013 katika Hoteli ya White Sands  jijini Dar es Salaam. Picha Zote
 na OMR