TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, November 20, 2014

KINANA AHUTUBIA WANA LIWALE MKOANI LINDI


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu za ajira badala ya kuwa za kudumu ziwe za mikataba kwani itasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.
 Wananchi wa Liwale wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia kuwa wapinzani kwenye mikoa hiyo hawajai hata kiganjani hivyo wananchi wasipoteze muda kwa wapinzani.
 Vijana hawakuwa nyuma kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa michezo Liwale mkoani Lindi.
 Wananchi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipokuwa akihutubia wananchi hao kwenye uwanja michezo wa wilaya. Mbunge wa Jimbo la Liwale (CCM) Faith Mitambo akihutubia wananchi wa Liwale kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo vya wilaya ambapo alitoa taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akishiriki uvunaji wa korosho wilayani Liwale mkoa wa Lindi.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchanganya zege wakati wa ujenzi wa sehemu za kuchotea maji katika kijiji cha Mpigamiti wilayani Liwale mkoa wa Lindi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji kama ishara ya kuzindua huduma za maji kwa wakazi wa kijiji cha Mpigamiti, mradi huo utahudumia vijiji vingine viwili vya Namakololo na Mitawa ambapo wakazi zaidi ya 6000 watafaidika na mradi huo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi.Hadija Sheweji  mkazi wa kijiji cha Mpigamiti mara baada ya kukagua mradi wa maji.
Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mangirikiti wilayani Liwale mkoa wa Lindi.
 Wananchi wa kata ya Mangirikiti wakifurahia ushiriki wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ujenzi wa ofisi ya chama ya kata ya Mangirikiti ,wilayani Liwale mkoa wa Lindi.

NACTE INTER COLLEGE TANZANIA- DAR ES SALAAM BONANZA- JUMAMOSI HII 22/11/20149 (DIT)


PRESS  RELEASE
(Taarifa kwa Vyombo vya Habari)
Ndugu,  Waandishi wa Habari,
Siku ya jumamosi tarehe 22/11/2014 itakuwa ni siku ya Ufunguzi wa Michezo ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, utakaofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Dar es salaam Institute of Teckinology (DIT) kuanzia saa mbili (2:00) asubuhi  mpaka saa kumi na mbili (12:00) jioni.
 itafanyika kila mwaka kwa kushirikisha vyuo mbali mbali  vya elimu ya kati  hapa nchini Tanzania na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na wasichana
Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd,yenye makao makuu yake Mwenge  jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ndiyo itakayokuwa ikisimamia taratibu zote za michezo hiyo wakati wote wa mashindano.
Kwa upande wa mkoa wa dare s salaam vyuo vilivyopo katika orodha ni 105 hivyo kulingana na bajeti kuwa kubwa, kama imeweka utaratibu wa kushiriki wenye michuano hiyo ya NACTE ambapo ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES SALAAM.
Siku ya jumamosi itakuwa ni sehemu ya kwanza( Season one) ambapo vyuo vilivyotaarifiwa kuhusika katika kuwania nafasi hizo mbili za juu ni pamoja na Wenyeji D.I.T, majirani zao C.B.E na wakongwe wa Michezo Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM).
Vyuo vingine ni Dar es salaam City College(DACICO) na majirani zao chuo cha Mlimani Profesional, na Royal, na Timu Mwalikwa katika Season hiyo ni Timu ya 100.5 TIMES FM Radio, kwa kuwa katiba ya michuano hiyo inaruhusu kuhusisha timu mbili waalikwa ambao watatokana na vyombo vya habari ama chombo cha habari, hivyo 100.5 Times Fm, wakiwa pia ni kati ya wadhamini wakuu wa matangazo ya radio,  wamepata fulsa ya kushiriki hatua hii ya kwanza (Season one).
Michezo itakayohusishwa hiyo siku ya ufunguzi ni pamoja na Mpira wa Miguu, Netball, Basketball, na Voleyball na washindi wa kwanza watazawadiwa Kombe wakati washindi wa pili watapata Mpira Mmoja kutoka kwa Wadhamini Wakuu Kampuni ya Simu za Mkononi VODACOM .
Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji  kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha,  na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.
Mgeni Rasmi  katika Bonanza hilo ni Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na mgeni mwalikwa atakayekabidhi zawadi kwa washindi ni mkurugenzi mtendaji wa 100.5 -TIMES RADIO, Bw. Leule Nyaulawa.
Aidha nichukue fulsa hii kuwaomba ndugu zetu wandishi kuhamasisha Makampuni na wadau kujitokeza kudhamini michuano hii ambayo maleng yake ni kuendeleza vipaji na kuibua vijana watakaokuwa viongozi, pamoja na kuwajengea mazingira ya kushiriki mara kwa mara katika michezo kwani Micheo uleta udugu, Upendano, mshikamano, amani, Afya na pia kijana anayeshiriki mazoezi upata muda wa kutumia akili kutafakali mambo ya Maendelezo zaidi.
  Imetolewa na -Katibu Mkuu Miss Demokrasia Tanzania- HALIMA BAKARI

WAZIRI MKUU PINDA AKIWA BUNGENI MJINI DODOMA

PG4A0561
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akiteta na Mbunge wa Urambo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 20, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A0532
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Baadhi ya wabuge na Mawaziri, Bungeni mjini Dodoma Novemba 20, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SDL SASA KUANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 6, RAMBIRAMBI MSIBA WA MUNYUKU, KARASHANI

Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu huu iliyokuwa ianze kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu kwa mechi kumi katika viwanja vitano tofauti imesogezwa mbele hadi Desemba 6 mwaka huu.
 Mechi hizo zimesogezwa ili kutoa fursa ya kukamilisha maandalizi mbalimbali ya ligi hiyo inayoshirikisha timu 24 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
 Mikoa yenye timu katika ligi hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Katavi, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora.
 MASHINDANO YA TAIFA YA U12 YASOGEZWA
Mashindano ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 yanayoshirikisha kombaini za mikoa yote ya Tanzania yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 30 mwaka huu hadi Januari 5 mwakani.
 Awali mashindano hayo yalipangwa kuanza Desemba 6 mwaka huu, lakini yamelazimika kuyasogeza ili kutoa fursa ya kukamilika kwa matengenezo ya viwanja vitatu ambayo vitatumika.
 Kila timu ya mkoa inatakiwa kuwa na ujumbe wa watu 16, wakiwemo wachezaji 14 na makocha wawili katika mashindano hayo ya timu yenye wachezaji saba (7 aside).
 Timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu tayari kwa ajili ya uhakiki wa umri na taratibu nyingine za mashindano. Timu zote zitafikia katika shule ya Alliance (Alliance Schools).
 Wachezaji wanaotakiwa kushiriki mashindano hayo ni wenye umri chini ya miaka 12, hivyo ni wale waliozaliwa kuanzia Januari 2003 na kuendelea.
 RAMBIRAMBI MSIBA WA MUNYUKU, KARASHANI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko vifo vya waandishi wa habari Innocent Munyuku na Baraka Karashani vilivyotokea jana (Novemba 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
 Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu, na tasnia ya habari nchini kwa ujumla kutokana na mchango mkubwa waliotoa katika ustawi wa mpira wa miguu nchini kupitia kalamu zao.
 Munyuku alikuwa mmoja wa waandishi waanzilishi wa gazeti la Mwanaspoti wakati Karashani kwa nyakati tofauti alifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo kampuni ya New Habari 1996 akiripoti habari za mpira wa miguu.
 Tunatoa pole kwa familia za marehemu, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), na kampuni ya New Habari 1996 na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
 Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.
 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MKUTANO WA CCM MABALOZI WILAYA DIMANI

IMG_1623
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi  CCM katika viwanja vya Ofisi ya Mkoa Amani leo alipofika kuzungumza na  Mabalozi na wenyeviti wa maskani katika mfululizo wa ziara zake za mikutano ya kuimarisha Chama katika Mikoa ya Unguja,[Picha na Ikulu.]IMG_1643
IMG_1688
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wanachi na Wanachama wa CCM katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Dimani katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katikaMikoaya Unguja, [Picha na Ikulu.]

Halmashauri ya Mji Handeni lawamani

Na Mwandishi Wetu, Handeni
MKUTANO wa kwanza wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation uliyofanyika juzi Novemba 19, katika kijiji cha Misima, wilayani Handeni, mkoani Tanga na kuwakutanisha wananchi wote umeibua kero nyingi za wananchi, ikiwamo ya kijiji chao kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji bila ridhaa yao.
Mmoja wa wakazi na wananchi wa kijiji cha Misima, akilalamikia eneo lao kuingia kwenye Halmashauri ya Mji kinyume cha sheria ya utawala bora, ikiwa ni pamoja na kutoshirikishwa kwa lolote na viongozi wa juu.
Taasisi hiyo ilianzishwa mapema mwaka huu na kuzinduliwa Mei 8 jijini Dar es Salaam, ilifanya mkutano mkubwa wa hadhara Misima, ambapo umati wa wanchi ulihudhuria, huku kero nyingi zikiwasilishwa na kudhihirisha changamoto za utawala bora zinazoathiri maendeleo ya Tanzania.
 
Wakizungumza kwa uchungu mkubwa, mwananchi wa Misima aliyejitambulisha kwa jina la Mhina Ally, alisema viongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na madiwani waliamua kuingiza kijiji chao katika Halmashauri ya Mji bila ya kuwashirikisha, ikiwamo kubandika tangazo la pingamizi kwa siku 90 katika maeneo yao kama sheria inavyotaka.
 
Alisema kutoka Handeni Mjini hadi katika eneo lao ni kilomita 16 zilizozunguukwa na mapori yanayowafanya wananchi wajihusishe na kilimo kwa asilimia 99, hivyo kuingizwa kwenye sheria za mji ni kusababisha ugumu wa maisha.
 
“Inashangaza mno kusikia Tanzania kuna utawala bora wakati viongozi wachache wanaweza kufanya watakavyo; hali inayoweza kuleta mapigano makubwa, endapo wananchi tutasimama kidete kudai haki zetu zinazokandamizwa na viongozi kila siku,” alisema.
 
Ally alifika mbali zaidi kwa kusema walisikia tangazo redioni la kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji, huku tangazo la pingamizi likishindwa kuwekwa kijijini kwao kwa hofu ya kupingwa na wananchi wao.
“Viongozi wa serikali ya kijiji waliamua kutoliweka tangazo la pingamizi kijijini kwetu kwasababu wanajua fika tusingekubali, hivyo inashangaza malalamiko yetu kufumbiwa macho na serikali inayoitwa sikivu, licha ya kuzunguuka sehemu nyinyi, kama kwa Mkuu wa wilaya na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa Tanga, alipokaimu DC Halima Dendego, ambaye sasa amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,” aliongeza.
 
Naye Naye Idd Kisege alisema kuwa ili kuona viongozi wanaogopa kufika Misima, hata namba kwenye nyumba zao hakuna ingawa wanatangaza uchaguzi kwa sheria za mji katika kijiji chao, jambo lisiloweza kuvumiliwa na kila mpenda maendeleo ya Misima.
 
“Watu wa Misima tunaambiwa sisi ni watata, wakorofi tunapodai haki zetu, ili waendelee kutuburuza, ndio maana kwenye ziara ya Mheshimiwa Rais, Profesa Jakaya Mrisho Kikwete waliniburuza Polisi kwasababu ya kuonyesha bango kwa mheshimiwa ili kuona kero zetu,” alisema Kisege.
Naye Mkomwa Athuman alisema kuwa Misima haipo tayari kutumikia sheria za Mji kwakuwa ni mapema mno kwao, hivyo wanaomba serikali, ikiwamo ofisi ya Waziri kulifuatilia suala hilo kwa kina.
 
“Mzozo huu umeshakuwa mkubwa na kuondoa ushirikiano kabisa kwa viongozi na wananchi wa hapa Misima, hivyo tayari malalamiko yetu yamefikishwa Ofisi ya Waziri Mkuu kulishtakia suala hilo kwasababu sheria ya kuingia kwenye Mamlaka ya Mji Handeni haijafuatwa na imeanzishwa na watu wachache ili kuzima uozo wa ardhi waliyoufanya kwenye kijiji chetu,” alisema.
 
Katika kila mwananchi aliyezungumza kwenye mkutano huo alionyesha kuguswa na kero hiyo ya mji, huku wakisema kutoka Handeni Mjini hadi Misima ni mbali pamoja na viongozi kushindwa kufuata sheria za utawala bora.
Awali, mkutano huo ulioanza saa tisa alasiri ulifunguliwa na mtoa mada wa kwanza, Kambi Mbwana, ambaye ndiye Msemaji Mkuu wa taasisi hiyo, aliyejikita sababu na dhamira kuu ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo.
Mbwana alisema kuwa sababu kubwa ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha utawala bora, ikiwa ni njia moja wapo ya kuwafanya Watanzania wote wajiletee maendeleo kwa kushirikiana baina yao na viongozi wote.
 
Akizungumzia utawala bora, Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Adam Malinda, alisema kwamba matatizo mengi katika jamii yamekuwa yakichangiwa na viongozi wasiojua nini maana ya utawala bora.
 
“Utawala bora ni somo muhimu na lazima lipigiwe kelele na watu wote, maana malalamiko mengi ya watu wa Misima yamesababishwa na tatizo hilo, ndio maana unaona kero zimepamba moto,” alisema.
 
Malinda aliwataka viongozi wa juu, wakiwamo wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kuzungumza na wananchi wa Misima ili kutatua mtafaruku huo kwa ajili ya kuwafanya wananchi waendelee na shughuli za kujiletea maendeleo, sambamba na serikali kuwafanyia kazi watendaji wabovu.
Kuhusiana na mzozo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, alikaririwa akisema kuwa utaratibu ulifuatwa, ikiwamo kutoka kwa siku 60 za pingamizi, ingawa wananchi hao walishindwa kupita njia hiyto kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.

Zaidi ya wakazi 700 wa Kerege wamenufaika na huduma ya matibabu ya bure kutoka klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay

Timu ya madakitari wakitoa huduma ya uchunguzi ya meno kwa mkazi wa kerege 10
Wananchi wa kijiji cha kerege wamenufaika na huduma ya bure ya matibabu inayotolewa na klabu ya Rotary ya Oster Bay ya jijini Dar es Salaam kila mwaka katika shule ya msingi ya Kerege-Bagamoyo.
Akizungumza na wanahabari waliofika kujionea aina ya huduma za matibau zinazotolewa na klabu hiyo, Dk. Shukuru kawambwa,mbuge wa bagamoyo , Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi akiwa kama mgeni rasimi amesema kuwa amefurahishwa na kitendo hicho cha wanachama wa Rotary klabu na kuwataka wananchi wa Kerege wajitokeze kwa wingi siku nyingine kwani huduma hiyo ni bure.
“Ningependa kuwashukuru wanachama wa Rotary kwa msaada huu wa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi wa kerege na niwakuigwa katika jamii. Na pia ninawaomba wanakijiji wa kerege mjitokeze kwa wingi kwani huduma hii ni ya bure, unapima afya yako, unapata ushauri kutoka kwa madakitari bingwa mia moja”, Alisema Dk.Shukuru.
Naye Bwana Thomas Scherer ambeye ni raisi wa klabu hiyo amesema kuwa anajiskia furaha kuona wanachama wa klabu hiyo wakiwa na moyo wakijitolea kwa ajiri ya jamii inayowazunguka.
rotary-kerege-10
“Tuna furaha na tunajivunia ya kwamba kwa kupitia juhudi za pamoja za jamii, wanachama wa klabu za Rotary nchini na nje ya nchi, serikali za mitaa na taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali, jumuiya ya matabibu na sekta binafsi; tumeweza kuandaa Kambi hii ya matibabu kwa mara ya nne,” alisema Thomas Scherer, Rais wa mwaka 2014-2015 wa Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay
Kambi ya Matibabu, sehemu mojawapo ya Miradi ya Afya ya Jamii, ambayo hufanyika kila mwaka toka ilipozinduliwa mwaka 2011 katika kitongoji cha Chanika jijini Dar es Salaam ambapo takribani wananchi 600 walijitokeza kupima malaria, VVU, kisukari, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, macho na viashiria vya magonjwa sugu.
Pia Dawa za bure na miwani zilitolewa kwa watu waliokutwa na matatizo ya afya na macho. Mwaka 2012 tulitoa huduma kwa watu zaidi ya 700, na kutoa huduma kwa idadi kama hiyo katika mwaka 2013. Mwaka huu, inatarajiwa kuwa idadi hiyo hiyo ya watu watakaowahi kufika watasajiliwa ili kupata matibabu bure.

WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 20.11.2014.
  • WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI PAMOJA NA MICHE YA BHANGI.
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA NYAKATI TOFAUTI WAKIWA NA BHANGI PAMOJA NA MICHE YA BHANGI.
 KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KATSON IYISEGA (68) MKAZI WA KIJIJI CHA ISWAGO ALIKAMATWA AKIWA AMEOTESHA MICHE YA BHANGI 12 KATIKA SHAMBA LAKE LA MAHINDI.
 MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.11.2014 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISWAGO, KATA YA SANTILYA, TARAFA YA ISANGATI, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BHANGI NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 AIDHA KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BRYSON SANGA (28) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 15 SAWA NA UZITO WA GRAM 75.
 MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.11.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA NSALAGA – UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA ULIMAJI WA BHANGI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
          Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

TEWUTA YATOA MWITO KAMPUNI YA BHART AIRTEL KUJIONDOA UBIA KATIKA KAMPUNI YA SIMU YA TANZANIA (TTCL)

  Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Junus Ndaro. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Junus Ndaro (wa tatu kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,wakati akitoa  wito wa kujiondoa ubia kwa Kampuni ya Bhart Airtel katika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Kutoka kulia ni Mfanyakazi wa Tewuta, Rashid Rajab, Mwanasheria Beatrice Monyo, Mwenyekiti Taifa wa Tewuta, Pius Makuke, Mwanasheria, Leila Farijalah na Ofisa wa Masijala, Ericla Frank.
 Mwenyekiti Taifa wa Tewuta, Pius Makuke (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Na Dotto Mwaibale
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wameitaka Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Bhart Airtel kujitoa ubia ndani ya TTCL.
Mwito huo umetolewa na  Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (Tewuta), Junus Ndaro kwa niaba ya wenzake wakati akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi. Alisema ni mara nyingi wamekuwa wakiitaka kampuni hiyo kuondoka ndani ya TTCL bila  mafanikio jambo ambalo ni kuifanya TTCL ishindwe kujiendesha. Alisema tangu Bhart Airtel ipewe mkataba wa ubia ndani ya TTCL wa umiliki wa wa hisa asilimia 35 imeshindwa kuwekeza na kuiboresha kampuni hiyo kama walivyokubaliana hivyo kusababisha TTCL kujiendesha kwa hasara. “Kitendo cha Bhart Airtel kuendelea kumiliki hisa zake hizo katika Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL) ni sawa na kitendo cha kuihujumu TTCL, na  kuwa toka mwaka 2012 Celtel walitoa taarifa ya awali ya kujiondoa ndani ya TTCL, na kuanzisha majadiliano ya uvunjaji wa mkataba baina ya pande zote mbili” alisema Ndaro Ndaro aliongeza kuwa hadi sasa majadiliano hayo yamekuwa yakicheleweshwa na mwenye hisa ndogo pasipo kuwepo kwa sababu za msingi, kitendo hiki ni sawa na hujuma, mmiliki mdogo mwenye hisa anatambua kuwa TTCL haiwezi kupata mtaji mahali popote pasipo idhini yake. Alisema Tewuta inapongeza juhudi zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa serikali kwa kuwaunga mkono kufuatilia jambo hilo na kuhakikisha wabia hao wanaondolewa ndani ya TTCL. Ndaro ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kuungana katika jitihada za kuwaondoa wabia hao Bhart Airtel ambao wanaihujuma Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

Uzinduzi wa Acha hizo leo

index
UZINDUZI wa albamu ya Mwanamuziki Tarsis Masela,  iitwayo ‘Acha Hizo’unafanyika kesho
kwenye ukumbi wa Ten Lounge, zamani ulikuwa unaitwa Bunisiness Park, uliopo Victoria
Dar es Salaam.
Katika uzindu huo bendi ya Mashujaa, Akudo Impack na Jahazi Modern Taarab,zitasindikiza usiku huo maalum wa Tarsis Masela.
Akizungumza Dar es Salaam jana Masela, alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huoyamekamilika, huku akiwataka wapenzi wajitokeze kwa wingi kuangalia uzinduzi wakeutakavyofana.
Masela ambaye ni Rais wa bendi ya Akudo Impact, anazindua albamu yake hiyo yenyenyimbo saba, ambayo ni ya kwanza kuzindua na kuikamilisha.
Alisema kuwa kila mshabiki atakayekuja atapata burudani safi kutoka kwake na hata bendizinazomsindikiza.
Katika uzinduzi huo viingilio vitakuwa viwili ambavyo ni shilingi 30,000 kwa viti vya maalum na sh.10,000 kwa kawaida.
Katika albamu hiyo kuna nyimbo saba ambazo ni Tabia Mbaya ambayo amemshirikishaMzee Yusuf‘Mfalme’  Chaguo Langu, Nimevumilia Lady Jay Dee, nyingine ni VidoleVitatu, Penzi Langu Limezidi Asali, Mwiko na Tusiachane.
Onesho hilo limedhaminiwa na RJ Company, Jambo Leo na Clouds Radio.

TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YAKAGUA MADARAJA LUHEKEI MKOANI RUVUMA

SONY DSCMeneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma, Mhandisi Abraham Kissimbo akizungumza na timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake. SONY DSCKiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijinea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60. SONY DSCKiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijinea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60. SONY DSCTimu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na  mwenyeji wao Mhandisi Lusage Mulenzi katika kibao cha ufunguzi rasmi wa Darala la Luhekei C. Daraja hili lina urefu wa mita 60, lilifunguliwa rasmi tarehe 18 Julai, 2014 na Mheshimiwa Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI

Mkwaja FC mabingwa wapya Mwidau CUP 2014

Mabigwa wa Mwidau CUF 2014, Timu ya Mkwaja FC wakishangilia ushindi baada ya kukabidhiwa kombe. unnamed1Mdhamini wa Kombe la Mwidau CUF, Amina Mwidau akiwa na wabunge wenzake, Yussuf Salim (Chambani) na Khatib Said Haji (Konde) unnamed2
Mbunge Amina Mwidau akikabidhi kombe ya ushindi kwa kapteni wa timu ya Mkwaja FC, Salim Rashid akiwa pamoja na wabunge wenzake. unnamed3Kombe la likiwa mezani huku mchezo wa fainali ukiendelea. Na mpigapicha Wetu
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu,Pangani
Timu ya soka ya Mkwaja FC imetwaa ubingwa wa kombe la Mwidau CUP mwaka 2014 baada ya kuifunga timu ya soka ya Kiman’ga kwa mabao 4-2 katika mtanange uliipigwa kwenye Uwanja wa Mwera wilayani Pangani.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni wakuvutanikuvute katika kipindi cha kwanza lakini timu ya Kiman’ga ilionyesha kuzidiwa uwezo kwa kuweza kuruhusu mvua ya magoli katika dakika za awali toka mpira kuanza.
Mchezaji wa Mkwaja FC Masoud Ticha ndio alionekana kinara katika mchezo baada ya kuifungia timu yake mabao matatu katika dakika za 8 na 38 kabla ya kwenda mapumziko . 
 Hata hivyo kipindi cha pili Kiman’ga ilionyesha makucha baada ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya 49 baada ya mchezaji wake frank kufanikiwa kufunga golo hilo baada ya kumhada mlinda mlango wa Mkwaja.
Goli la pili la timu hiyo lilipatikana katika dakika 70 hali iliyoleta matumaini kwa mashabiki wa timu hiyo kuamini kwamba wataweza kurudisha magoli yote lakini shauku yao ilikwisha baada ya dk 80 Mkwaja FC kufunga bao la nne.
Akikabishi zawadi kwa washindi hao Mbunge wa viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF), kwa timu ya Mkwaja FC walijinyakulia kitita cha fedha taslimu Sh 500,000, kikombe kikubwa, medali za dhahabu, seti mbili za jezi pamoja na mpira.
Huku mshindi wa pili ambae ni Kimang’a alipata Sh 200,000,kikombe kidogo, medali ya shaba, seti moja ya jezi pamoja na mpira huku timu 40 zilizoshiriki zikipatiwa mpira na 16 zikipatiwa jezi seti moja moja.
Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa mchezo huo Mwidau, alisema kuwa atahakikisha anakuza vipaji vya soka  katika wilaya hiyo kwa kuwashirikisha kwenye mashindano mbalimbali hapa nchini.
Katika mchezo huo wa fainali ulidhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji pamoja na Mbunge wa Chambani, Yussuf Salim wote kutoka CUF.

WAKULIMA WA SHAYIRI MONDULI WAELEZEA MAFANIKIO YA UFADHILI WA TBL

Pichani ni baadhi ya nyumba za Mkulima wa Shayiri, Barrick Kivuyo zikionekana baada ya kuwa amezifanyia ukarabati ikiwa ni pamoja na kuweka umeme wa jua (Solar)
 Mkulima wa Shayiri akionesha moja ya Ghala lake (Stoo) kwa ajili ya kuhifadhia zana mbalimbali za kilimo ikiwamo utunzaji wa pembejeo, ambapo jengo hilo amelijenga kutokana na fedha za Shayiri.
Baadhi ya Wanawake wanaojishughulisha na kilimo cha Shayiri wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa wa  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha anayesimamia wakulima katika eneo hilo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha.
Mkulima wa Shayiri wilayani Monduli Meporoo Losulu akionesha Trekta zake mbili ambazo amezinunua kutokana na kilimo cha Shayiri, pichani nyingine akizungumza kuelezea mafanikio yake.