Sehemu
ya Wanyama kazi katika Shamba Kubwa la Uzalishaji wa ngo'mbe wa nyama
katika Gereza Ubena lililopo Mkoani Pwani. Shamba hilo lina takribani
jumla ya ngo'mbe zaidi ya 1500. Uzalishaji wa ngo'mbe umekuwa
ukiongezeka kwa mafanikio makubwa kila Mwaka hivi karibuni kutokana na
juhudi kubwa zinazofanywa na Uongozi wa Jeshi la Magereza katika
kuyahudumia mashamba hayo Nchini.
Lango
Kuu la kuingilia Gereza la Mifugo Ubena lililopo Mkoani Pwani ambalo
linashughulika zaidi na Uzalishaji wa Mifugo. Wafungwa katika Gereza
hilo wanapata elimu ya Ufugaji bora unaozingatia Kanuni za Ufugaji wa
Kisasa ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa jukumu la Urekebishaji kwa
Wafungwa.
Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Uzalishaji wa Mifugo Gereza la Mifugo Ubena, Mkoani Pwani.
Kundi
la ngo'mbe wa maziwa katika Shamba la Mifugo la Mtego wa Simba lililopo
Mkoani Morogoro. Shamba hili la Mifugo ni Maalum kwa Uzalishaji wa
Ngo'mbe wa maziwa kama inavyoonekana katika picha na Gereza hilo
lilianzishwa rasmi mwaka 1944.
No comments:
Post a Comment