TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, November 18, 2014

Samsung Galaxy note 4 launch

Image 10
Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Tanzania, akielezea sifa za simu aina ya  Samsung Galaxy Note 4 kwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa simu hiyo Profesa Patrick J Makungu  katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na tekinolojia katika uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.
Image 1
Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Tanzania akiwahutubia wageni waalikwa katika uzinduzi rasmi wa simu ya Samsung Galaxy Note 4 uliofanyika katika ukumbi wa  Terrace, Slip wayImage 4
Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Tanzania akizindua rasmi simu ya Samsung Galaxy Note 4.
Image 9
Mwanamuziki Vanessa Mdee akiwaburudisha wageni waalikwa katika uzinduzi rasmi wa simu ya Samsung Galaxy Note 4 uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.

AZAM YAMNASA STRAIKA WA MALI

MATAJIRI Azam FC wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumnasa straika Mmali wa El Merreikh, Mohamed Traore ambaye anatarajiwa kutua nchini mwishoni mwa mwezi huu kwa mazungumzo ya mwisho, pia klabu hiyo imetangaza dau analouzwa Muivory Coast wao, Kipre Tchetche ni Sh336 milioni.
Traore atawasili nchini baada ya kumaliza mechi yake ya Jumatano ijayo ambayo atakuwa akiichezea timu yake ya Taifa ya Mali itakayocheza na Algeria kuwania kufuzu fainali za Kombe  la Mataifa ya Afrika na atakuwa mchezaji wa pili kutoka El Merreikh baada ya Muivory Coast Pascal Wawa aliyepewa mkataba wa miaka miwili.
Azam inamsajili Traore ambaye atakuwa mchezaji wa tano wa kigeni baada ya Tchetche, Wawa, Muivory Coast Kipre Bolou, Mrundi Didier Kavumbagu na Mhaiti Leonel  Saint-Preux baada ya kumtupia virago Mmali, Ismail Diara.
Na ili kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni wanaohitajika Ligi Kuu Bara, inaweza kumuuza Tchetche ambaye anatakiwa na klabu mbalimbali kutoka Malaysia na Sri- Lanka kwa makubaliano ya kulipwa kiasi hicho cha pesa au Leonel.
Akimzungumzia Tchetche kigogo mmoja wa Azam alisema: “Kuhusu Tchetche yuko sokoni lakini wanaomhitaji wafahamu dau lake ni Dola 200,000.”
 Katika hatua nyingine, Azam itaanza maandalizi yake leo Jumatatu na wachezaji wote wataanza mazoezi Uwanja wa Chamazi isipokuwa wale waliokuwa na timu zao za Taifa.
Mmoja wa maafisa wa El Merreikh ameliambia Mwanaspoti kuwa, klabu yake ilikubaliana na Wawa  kuvunja mkataba wake uliobakiza miaka miwili na aondoke kama mchezaji huru kwani mwenyewe aliomba kuondoka.
“Wawa tulikubaliana naye aondoke baada ya kutuomba kwani amecheza kwetu kwa miaka mitano na kuitumikia klabu asilimia 96, sasa mtu mliyeishi naye vizuri akiomba kitu lazima mumsikilize hivyo ameondoka kama mchezaji huru.
“Lakini katika kuondoka kwake ametuachia kasheshe hapa kwani mashabiki wamekasirika, hawaelewi kilichotokea lakini hatukuwa na jinsi kwani Wawa alituambia hata kama akibaki hana uhakika na uwezo wake utakavyokuwa,” alisema kiongozi huyo.
 Source: Mwanaspoti
Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushilikiana na Shirika la kisukari kimataifa la  International Diabetes Federation (IDF) walianzisha Siku ya Kisukari Duniani mnamo mwaka 1991 ili kuadhimisha kuzaliwa kwa mwanasayansi Frederick Banting ambaye kwa kushirikiana na Charles Best aligundua tiba muhimu kwa wagonjwa wa kisukari  ya insulin mnamo mwaka 1922.
Novemba 14 Kila mwaka mashirika ya kiserikali, mashirika binafsi, wagonjwa wakisukari na wadau mbalimbali hukutana ili kuadhimisha siku hii duniani kote. Siku hiyo huadhimishwa kwa kaulimbiu mbalimbali, kampeni na pia hutoa nafasi kwa wagonjwa wa kisukari na wasio wagonjwa kufanya vipimo na mashauriano na wataalamu na madaktari wa ugonjwa wa kisukari.  Mwaka huu kauli mbiuni Go Blue for Breakfast kauli mbiu hiyo inasisitiza ulaji wa afya wa kifungua kinywa.
Kisukari ni ugonjwa wenye matibabu ya muda mrefu unaosababishwa na hitilafu kwenye mmeng’enyo wa chakula ndani ya mwili wa binadamu unaoambatana na kiasi cha juu cha sukari kwenye mzunguko wa damu. Hali kadhalika, hutokana kongosho kutengeneza kiasi kidogo cha insulini au seli za mwili kushindwa kufanyia kazi insulin inayotegenezwa na kongosho.
Mathalan, kuna aina mbili za ugonjwa wa kisukari ikiwemo aina ya kwanza ya kisukari ambayo husababishwa na mwili kushindwa kutengeneza insulin yakutosha ambayo chanzo chake hakiko bayana. Aina ya pili ya kisukari yenyewe husababishwa na seli za mwili kushindwa kufanyia kazi insulin inayotengenezwa mwilini ambayo chanzo chake kikubwa ni ukosefu wa mazoezi ya mwili na kuwa na uzito kupindukia.
Kauli mbiu ya mwaka huu inatilia mkazo umuhimu kupata chakula bora hususan katika kifunguwa kinywa ili kuepuka aina ya pili ya kisukari na matatizo yanatokanayo na aina hiyo ya kisukari.  Jambo ambalo litasaidia jamii kuweka uzito waokatika kiasi kinachotakiwa nakuweka kiasi chao cha sukari mwilini katika kiwango salama pia.

TAMASHA LA KUONESHA VIPAJI BAINA YA WANAFUNZI WA SHULE ZA ST MARY’S INTERNATIONAL ZA DAR ES SALAAM LAFANA

001
Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s, mama Getrude Lwakatare akizungumza na wanafunzi wa Shule za St Mary’s International za Dar es Salaam wakati akizundua tamasha la kuonyesha vipaji vya wanafunzi wa Shule za St Mary’s International za Dar es Salaam lililofanyika Novemba 15, 2014 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. 
002
Mwalimu wa Shule ya St Mary’s International, Eric Sendi akiwaasa wanafunzi waandelee kuonyesha vipaji vyao.mm
003 
Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s, mama Getrude Lwakatare (kushoto), akikabidhiwa baadhi ya Peni na Meneja Masoko wa Kampuni ya SILAFRICA, Salman Pathan kama mchango wake kwaajiliya shule za St Mary’s International.
006
Wanafunzi kutoka shule za St Mary’s International za Dar es Salaam wakiwa kwenye tamasha hilo.
 007
Wanafunzi kutoka shule za St Mary’s International za Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa tamasha la kuonyesha vipaji.
Tamasha Hilo lililoshirikisha Shule za Mbagala, Tabata na Mbezi Junior lililenga kuonyesha vipaji vya wanafunzi katika sanaa ya kucheza, kuimba na sarakasi.
Akizungumza wakati wa kuzindua tamasha Hilo,Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s, Mheshimiwa Mama Getrude Lwakatare, Alisema ukuzaji wa vipaji Ni sehemu muhimu ya Shule za St Mary’s International.
‘Leo Ni Siku muhimu kwetu sisi kama St Mary’s Kwani pamoja na elimu bora tunayoitoa, Lakini pia tunasisitiza umuhimu wa vipaji Kwa wanafunzi wetu ‘ Alisema Mheshimiwa Mama Lwakatare.
Tamasha Hilo Ambalo limeandaliwa Kwa kushirikiana na Tanzania House of Talent, limedhaminiwa na Simtank ambao wametoa peni pamoja na tenki moja.

TAmasha kubwa la SHIWATA laja

Na Mwandishi Wetu
 MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) imeandaa tamasha kubwa la kuadhimisha miaka kumi (10) kutoka uanzishwe mwaka 2004 kwa michezo mbalimbali ukiwemo mpambano wa maveterani wa watani wa jadi  Simba na Yanga litakalofanyika kilele cha sherehe hizo uwanja wa Karume,Dar es Salaam Desemba 25,(Krismasi) mwaka huu.
 Mwenyekiti wa SHIWATA,  Cassim Taalib alisema katika wiki ya maadhimisho hayo, Desemba 24 sherehe hizo zitatanguliwa na ugawaji wa nyumba 38 zilizojengwa na wanachama wa SHIWATA kwa njia ya kuchangiana na kufikisha idadi ya jumla ya nyumba 104 ambazo mpaka sasa zimekwisha jengwa katika kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga chenye ekari 300 kwa ajili ya makazi.
 Alisema ili kuwavutia wenye nyumba hizo wahamie kijijini, SHIWATA imetoa eneo maalumu kwa ajili ya kulima bustani ya mboga mboga na mazao ambayo si ya kudumu ili wajikimu wao wenyewe na familia zinazowazunguka.
 Alisema SHIWATA unaomiliki shamba la ekari 500 katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga unasimamia usafishaji wa shamba hilo kutumia mtambo wa kisasa (bulldozer) lililokodishwa kutoka Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kwa gharama ya sh. mil. 22 kwa siku 20 kukamilisha kazi hiyo.
 Alisema Bulldozer hilo limefikisha siku kumi sasa kutoka kazi ya kusafisha shamba hilo na kung’oa visiki  ianze, wanachama 90 waliomilikishwa sehemu ya shamba kwa lengo la kulima mazao yanayostawi eneo hilo, wameanza kuchangia gharama za kusafisha shamba hilo.
 Mwenyekiti huyo alisema mazao yanayostawi eneo hilo ni mpunga, mahindi, mbaazi, viazi vitamu, ndizi, kunde, korosho, mtama na matunda kama embe, machungwa, matikiti maji na mafenesi.
 Alisema pia kuwa sherehe za maadhimisho hayo zitawakutanisha wakongwe wa soka wa Simba na Yanga ambao ni wanachama wa SHIWATA wamekubali kushiriki mpambano huo.
 Kwa upande wa Yanga, mchezaji wa zamani wa Klabu hiyo, Mtwa Kiwhelo na Athumani Juma Chama kwa upande wa Simba wanawawakilisha wenzao katika maandalizi ya awali ya mchezo huo.
 SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 kutoka fani mbalimbali za sanaa za maigizo, mpira wa miguu, mpira wa wavu, netiboli, waigizai wa filamu, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, vijana na waandishi wa Habari kila kundi litapewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao siku hiyo.

Nishati na Madini watakiwa kuboresha tathmini ya mapendekezo ya miradi

Picha Na 1
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu  Lusius Mwenda kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya jinsi  ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki  mjini Bagamoyo. Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara  ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)  na Kampuni ya Uendelezaji  wa Jotoardhi (TDGC)
Picha Na 2
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini hotuba  ya ufungaji wa mafunzo hayo iliyokuwa inatolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu  Lusius Mwenda (hayupo pichani)
Picha Na 3
Afisa Rasilimali watu kutoka Idara ya Utawala Judith Ntyangiri akipokea  cheti cha   ushiriki mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mwishoni mwa wiki Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Lusius Mwenda, alifunga  awamu ya kwanza ya mafunzo ya jinsi  ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki  mjini Bagamoyo.
 Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara  ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)  na Kampuni ya Uendelezaji  wa Jotoardhi (TDGC). Pamoja  na kufunga mafunzo hayo, alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa washiriki na kuwataka kuboresha tathmini ya mapendekezo ya miradi ( project proposals)
Ninawasilisha kwenu habari pamoja na picha za matukio ambazo zimeambatishwa pamoja na email hii.  Pia captions zimeambatishwa

MTOTO WA MIAKA 02 AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI RUNGWE.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 17.11.2014.
  • MTOTO WA MIAKA 02 AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI RUNGWE.
  • WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
  • WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI.
 KATIKA TUKIO LA KWANZA:
 MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 02 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ANITA BOAZ MKAZI WA KIJIJI CHA MPANDAPANDA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.730 CKD AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE HAMPHREY MWALENGO.
 AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 16.11.2014 MAJIRA YA SAA 17:45 JIONI HUKO KATIKA SHULE YA SEKONDARI KIPOKE TUKUYU, BARABARA KUU YA TUKUYU/MBEYA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO MARA BAADA YA AJALI, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
 TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SUZANA JORAM (34)  NA 2. PODENSIANA ANDREA (32) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA UPENDO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 15.
 WATUHUMIWA HAO KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 16.11.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAPIKAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI, WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JOSHUA FRANSIS (22) 2. ISSA JUMA (22) 3. EMANUEL MWIGOSO (24) WOTE WAKAZI WA UYOLE JIJINI MBEYA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI KETE SITA [06] SAWA NA UZITO WA GRAM 30.
 WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 16.11.2014 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI] PAMOJA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
                                             Imetolewa na kusainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MISA YA SHUKRANI YA KUTIMIZA MIAKA SABA YA MAMA AURELIA KOBULUNGO MUGANDA TANGU ALIPOITWA NA MWENYEZI MUNGU ILIYOFANYIKA NYUMBANI KWA MTOTO WAKE FR.JAMES RUGEMALIRA MAKONGO JUU JIJINI DAR ES SALAAM


Mama Aurelia Kobulungo Muganda enzi za uhai wake
 Kaburi la Mama Aurelia linavyoonekana
 Altare iliyoandaliwa kwa ajili ya misa takatifu ya shukrani kwa ajili ya Mama Aurelia
Fr Mukandara akibariki maji yaliyochanganywa na chumvi ambayo yalitumika kubariki kaburi. (Imeandaliwa na www.habari za jamii.com)
Padri Mukandara akibariki kaburi
Ni wakati wa kuanza ibada takatifu ya misa ya shukrani. Wanafamilia wakielekea kwenye ukumbi maalumu.
Bwana na Bibi Fr. James Rugemalira wakiwaongoza mapadre kuelekea kwenye misa takatifu
Paroko wa Kanisa Katoliki Makongo Juu Joseph Masenge akisisitiza jambo wakati wa misa hiyo
Jopo la mapadre walioshiriki katika misa hiyo takatifu
Wanakwaya kutoka kanisa la Makongo Juu wakitumbuiza katika misa hiyo
Wanafamilia kutoka kushoto Everine Rugemalira, Joe Mgaya na Jerome Rugemalira wakifuatilia kwa karibu ibaada ya misa hiyo
Wageni mbalimbali wakitafakari matendo makuu ya Mungu kwenye ibadaa hiyo
Waalikwa mbalimbali wakiwa kwenye ibaada hiyo





Wanafamilia wakiwa kwenye ibaada hiyo

Mmm ni upendo ulioje unapoona kusanyiko kubwa kama hili


Mdau Joyce (katikati) hakupenda kukosa ibaada hiyo takatifu
Paroko Masenge akipokea vipaji mbalimbali kutoka kwa watukuu wa Bibi Aurelia. (Imeandaliwa na www.habari za jamii.com) 

JAJI MKUU AMJULIA HALI RAIS KIKWETE MAREKANI

1
: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake
waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika
hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore,Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako  Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein Katanga.
3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu Mhe Mohamed
Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16,
2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland.  Jaji Mkuu yuko  Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. 5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani  Dkt. Sweetbert Mkama ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014 6
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Meja Jenerali Adolph
Mutta ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande
Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili
Novemba 16, 2014 7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Mtendaji Mkuu wa
Mahakama Mhe Hussein Katanga. ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014 8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Msajili wa Mahakama Kuu
ya Tanzania Mhe Ignass Kitusi  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara
wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda
kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014 9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Balozi wa Tanzania
nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyesindikiza   msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014 10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji wa Mahakama Ya
Rufani Tanzania Mhe Ibrahim Juma  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa
msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman
walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili
Novemba 16, 2014
11
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali
Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako  Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama.

MAMIA WAMZIKA MDAU NASELI JOSHUA DORIYE

 Mwili wa marehemu Naseli Joshua Doriye ukitolewa nyumbani kwao Africana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ibada ya mazishi.
 Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Nasali.
Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es salaam, Prof. Joshua Doriye ambaye ni mzazi wa Naseli akiwa na mkewe wakati wa ibada ya mazishi nyumbani kwake Africana.
Ibada ikiendelea nyumbani kwa marehemu Naseli Joshua Doriye Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
 Picha ya marehemu Naseli enzi za uhai wake.
 Baadhi ya waombolezaji.
 Waombolezaji.
Wanafamilia wakiimba nyimbo za kumsifu mungu.
Ni huzuni ilitawala wakati wa ibada ya kuaga mwili.
Ndugu jamaa na marafiki wakitoa hesima za mwisho.
Wanafamilia.
Familia.
Mwakilishi wa familia kutoka Mburu akitoa salamu za rambirambi.
Ndugu, jirani, marafiki wakitoa heshima za mwisho.
Zoezi la kuga mwili likiendelea
Mdau Abdalah Natepe akitoa heshima za mwisho.
Baadhi ya wanafunzi alioasoma nao marehemu Naseli wakitoa heshima za nmwisho.
Ndugu na marafiki wakitoa heshima za mwisho.
Wanafamilia wakitoa heshima za mwisho. 
Wanafamilia wakitoa heshima za mwisho.
Wanafamilia wakiwa na huzuni kwa kuondokewa na Naseli Doriye.
Ibada ya ikiendelea.
Marafiki wa marehemu Naseli wakipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu kutoa heshima za mwisho.
 Wazazi wa Naseli wakitoa hesima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu, Naseli Doriye.
 Wadogo zake Naseli wakitoa heshima za mwisho.
 Tutakukumbuka kaka yetu mpendwa.
 Waida mdogo wa marehemu akitoa heshima za mwisho.
 Marafiki waliosoma na Naseli.
 Wanafunzi waliosoma na Naseli wakiwasili nyumbani kwa marehemu.
 Baadhi
ya marafiki waliosoma pamoja na mdau Naseli Joshua Doriye wakiwa katika
picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa ibada ya mazishi.
 Waombolezaji
 Baadhi ya waombolezaji wakipata chakula.

DEVOTA KASANDA MDACHI-TANZANIA’S MOST POWERFUL BUSINESS WOMAN

unnamed unnamed2 unnamed1 
By Ayoub Mzee Meet Devota Kasanda Mdachi the Tanzania Tourist Board ‘s Marketing Director, the first woman to hold this position in Tanzania. She is billed as Tanzania’s most powerful business woman by Newdeal Africa – based in London. It’s been a ground breaking year for her in business .Within a short time since her appointment Tanzania’s fortunes have doubled as far as Tourism is concerned in Tanzania Ms. Mdachi will be based in the TTB head office in Dar es Salaam, Tanzania. More CEOs, more industries, more power, more challenges. That’s the story of Fortune’s 2014 ranking of the 50 Most Powerful Women in ­Business, which features an all-time record of 24 large-company CEOs in its pages. Our women are leading—and in many cases pushing through difficult tran She has been art of the team that has seen Sunderland AFC (SAFC) an English premiership club officially strengthen its links with the African continent, after cementing its partnership with Tanzania.She also oversaw the ground breaking deal between Tanzania Tourism and Stoke City English premiership club.This made Tanzania the first African coutry to dela with the English premiership. Why the English Premiership? It is the world favourite game. In England, almost 75% of 16 to 50 years old are interested in football, football provides an excellent , entertaining and exciting backdrop to showcase a product and football is played by over 265 million people and still growing. By this Tanzania will get brand awareness, brand visibility, trust and credibility, web traffic, promotional assets, talent rights, shirt sponsorship, broadcast to 211 countries worldwide with 2.85 billion cumulative audience for all English games in over 500 million homes alone.And why Tourism? Tourism is a key factor in the upward growth of the Tanzanian economy and the partnership uses the global reach of the Barclays Premier League to promote the country as a premier tourist destination. Premier League football is watched in over 200 countries, with accumulative audience of a phenomenal 4.2 billion, making it the most watched sporting league in the world. As of now, Sunderland FC has already developed close links with Tanzania, through providing technical and practical support to the development of a football academy project, the first of its kind in the country. The project will see thousands of youngsters benefit from a joined up approach combing football, education and community engagement, harnessing the knowledge and expertise of Sunderland AFC and its own successful academy. Lazaro S. Nyalandu, MP, Tanzania’s Minister of Natural Resources and Tourism, is quoted as said: “Tanzania Tourist Board is proud to be associated with Sunderland AFC. We believe that the partnership enhances the Board’s efforts in promoting Tanzania to the world and will also help to attract investments and develop sports tourism in Tanzania.” Did you know that there is now a Tanzania Tourism app which is designed for both iPhone and iPad?.Please Kindly follow the link: https://itunes.apple.com/us/app/tanzania-tourism-guide/id530460453?mt=8. This version is optimised for iPhone5. Now this is a universal compact app. Supports iPhone5/ iPhone/ iPad/ iPod. When contacted on how she does it, she smiled and said “It all a big team’s work and support of Governemnt”

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AHUTUBIA KILWA MASOKO

1 
4 
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali walikokuwa wakihutubia.
6
Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungala Maarufu kama Bwege akiwa na wanachama wenzake   wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Kilwa Masoko leo.
7
Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungala Maarufu kama Bwege akifurahia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Kilwa Masoko leo.
8
9
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega akimpongeza Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
10
Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano huo.
11
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa  Ndugu Abdalah Ulega akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
12
Kikundi cha muziki kikitumbuiza katika mkutano huo.
13
Wananchi wakiserebuka na muziki katika mkutano huo.
02
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha mtambo wa kutengeneza barabara wakati akishiriki katika ujenzi wa mmradi wa barabara ya Kwa Mkocho inayoelekea Kilwa Kivinje wilayani Kilwa.
01 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda kwenye Mtambo wa kutengeneza barabara tayari kwa kushiriki ujenzi wa barabara hiyo.
03
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi.
04
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa na Mkuu wa wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega wakati alipokuwa akiendesha mtambo wa kutengeneza barabara aliposhiriki katika ujenzi wa mradi wa barabara ya Kwa Mkocho inayoelekea Kilwa Kivinje.
05
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye mtambo wa kutengeneza barabara ya Kwa Mkocho mara baada ya kushiriki ujenzi huo, kushoto anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega.
2
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya  chanzo cha maji wakati alipokagua  shamba la kilimo cha uwagiliaji  Mavuji kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega.
1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua chanzo cha maji wakati alitembelea kilimo cha Umwagiliaji kata ya Mavuji.
3 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa shamba la umwagiliaji kata ya Mavuji.
4  5 
Mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Said Mtanda akisalimia wananchi Nangurukuru.
6
Mbunge wa jimbo la Mtama, Mlezi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kilwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa Mh Bernard Membe akisalimia wananchi Nangurukuru.
8 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu ABdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kabla ya kushiriki ujenzi wa nyumba ya daktari katika zahanati ya Nangurukuru
13
Mradi wa shambi la kuvuna chumvi Miima wilayani Kilwa
14
Baadhi ya wananchi wakisafisha chumvi katika mradi wa kuvuna chumvi Miima Kilwa.
16
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli za uvunaji wa Chumvu katika shamba la Miina wilayani Kilwa.

FREEMAN MBOWE AHUTUBIA MANG’ULA MKOANI MOROGORO

VIONGOZI WA UKAWA LYAMGUNGWE WADAI KUVUTIWA NA UTENDAJI WA MBUNGE MGIMWA KALENGA WAJIUNGA CCM

Mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa kulia akipokea kadi ya Chadema  kutoka kwa mmoja kati ya  viongozi wa Chadema   kata ya Lyamgungwe  aliyehamia CCM
Mbunge Mgimwa  akikagua miradi ya maendeleo  jimboni kwake
Wananchi  wa Lyamgungwe  wakiwa  wameongozana na mbunge wake  kwenda kutembelea  miradi ya maendeleo
Kada  wa Chadema  kulia akipongezwa na mbunge Mgimwa baada ya  kujiunga na CCM
Mbunge Mgimwa akizungumza na  wananchi  wake baada ya  kupokea  wana chama wa ChademaNa MatukiodaimaBlog
VIONGOZI
watatu  wa vyama  vinavyounda katiba ya  wananchi (UKAWA) kata ya
Lyamgungwe  jimbo la kalenga  wamempongeza mbunge wa  jimbo la hilo
Godfrey Mgimwa   kwa  kutekeleza ahadi  mbali mbali  zilizoachwa na
marehemu mbunge aliyepita Dr  Wiliam Mgimwa kwa  muda mfupi na kuwa
katika  kuonyesha  umoja  wao wameamua  kuunganisha  nguvu zao  kwa
mbunge huyo kwa kuhama Chadema na  kujiunga na CCM.
 
Akizungumza
kwa niaba ya  wanachama  wenzao zaidi ya 20 ambao  walikuwa nyuma  yao
kabla ya   kujiengua  Chadema na  kujinga na CCM   walisema kuwa  sababu
ya  kujiunga na upinzani  ilitokana na makundi  ndani ya CCM na
upendeleo wa uteuzi wa wagombea  mbali mbali pamoja na wabunge
waliotangulia  kuonyesha kutumia ubunge kulea  familia  zao badala ya
kuleta maendeleo  katika jimbo  hilo jambo ambalo mbunge Mgimwa amekuwa
wa  tofauti  na  wabunge wengine kwa kuonyesha  kuwajali  zaidi  wapiga
kura  wake .
 
Bw
Mapinduzi Kalolo  ambae  alikuwa ni    viongozi  wenzake  wengine
waliorudi CCM ni  pamoja na katibu kata ,mwenyekiti na wajumbe na  kuwa
kujiunga kwao  Chadema  ni baada ya mambo  ndani ya CCM kutokwenda
vizuri  ila kwa  sasa  mbunge  wao  ameendelea  kuwaunganisha
wananchi  wote  bila  kujali itikadi zao  za  vyama .
 
Pia
alisema  walipotoka CCM kwenda  Chadema  walikuwa  wameahidiwa mambo
mengi na viongozi wa Chadema jimbo  hilo la Kalenga  ila baada  ya
kujiunga utekelezaji wa ahadi  walizotoa  ikiwemo ya  kufungua ofisi
ilionekana na ngumu na kuwa  chama  hicho hata  kuwajali kilishindwa na
hivyo kuishia  kuonekana si chochote katika kata  hiyo  zaidi ya
kutumika kama karai na Chadema.
 
“Kujiunga
na  Chadema  kweli  tulikuwa  tumepotea  ila  kwa  sasa  tumeona  ni
vema  kurudi  kwa  baba na mama  CCM baaba  ya maisha ya  kuishi kama
mwana mpotevu  kutushinda …… hivyo tunakuhakikishia  mheshimiwa
mbunge Mgimwa  wewe  ndio  umetushawishi  kuhama  Chadema na kujiunga na
CCM kutokana na kuonyesha mfano katika kutekeleza ahadi  zao kwa
wananchi …..kalenga hatujapata  kuwa na mbunge ambae  amefanya mambo
makubwa kama wewe  ndani ya  miezi minne …haya  uliyofanya  wewe
wabunge wengine  walikuwa  wakishindwa  kuyafanya kwa  kipindi  cha
miaka 5  ya  ubunge “
 
Hata
hivyo  Kalolo  alisema  kuwa  ni matumaini makubwa  kwao  kuwa  kazi
iliyofanywa na mbunge Mgimwa kwa  kipindi  kifupi  cha miezi  minne
ama  cha mwaka  mmoja wa utawala  wake ni imani  tosha kwao kwa
kuendelea  kumchagua  zaidi kwa  miaka mingine 10  mbele  ili
kuliwezesha  jimbo  hilo  kuwa la mfano zaidi.
 
HIvyo
alikitaka   CCM kuacha tabia ya  viongozi  wake wa  wilaya  kuwaruhusu
baadhi ya  wana CCM kuzunguka  kuwavuruga wapiga  kura  kwa  kubeza
jitihada  zinazofanywa na mbunge  Mgimwa na kuwa kufanya  hivyo ni
kukaribisha upinzani katika   jimbo  hilo.
 
Kalolo
alisema  iwapo  viongozi wa CCM ngazi ya  wilaya na mkoa  watashikamana
na mbunge  Mgimwa upo  uwezekano  wa upinzani kufutwa kabisa katika
jimbo  hilo ambalo halijapata  kuwa na historia ya  kuongozwa na
upinzani .
 
 
kwa
upande  wake  aliyekuwa  mwenyekiti  wa  jimbo  la  kalenga kupitia
Chadema  Dr  Salum Kalolo  alisema  kuwa  kuondoka kwa   viongozi hao
Chadema na  kujiunga  na CCM kutokana na utendaji wa  mbunge  huyo
Mgimwa hawajakosea kwani kwa  mtazamo  wake  kazi inayofanywa na mbunge
huyo jimboni inapaswa  kuungwa mkono na  kila mwananchi bila kujali
itikadi ya chama chake.
 

Wengi  walijua kuwa  kutokana na ujana  wake  mambo ya maendeleo
yasingeweza  kusonga mbele  ila mimi  si CCM mimi ni Chadema kutoka
sakafu ya  moyo  wangu  ninampongeza munge Mgimwa  amekuwa mbunge wa
mfano katika  kutuletea maendeleo Kalenga “
 
Zipo
changamoto  mbali mbali ambazo iwapo  atapewa  muda  wake wa kipindi
japo  kimoja cha miaka 5  kuanzia mwakani 2015  tungependa atusaidie
kutatua  ni pamoja na adha  ya maji na uboreshaji wa  shule za msingi
ambazo nyingi  hazipo katika hali nzuri .
 
Hata
hivyo mbunge  Mgimwa alisema malengo  yake ni  kuweka rekodi  nzuri ya
ubunge katika  jimbo  hilo la Kalenga na kulifanya kuwa  jimbo lenye
maendeleo makubwa  ikiwa ni pamoja  na kuona ndoto  yake ya kuanzisha
benki ya  wananchi wa Kalenga  inaanzishwa  ili  kusaidia  kuwakopesha
wakulima mitaji .
 
Kuhusu
suala la maji alisema  tayari katika baadhi ya maeneo ameanza
kutekeleza ahadi ya  maji  safi pamoja na kupeleka  umeme katika kata ya
Mgama na Magulilwa ili  kuchochea kasi ya maendeleo japo  maombi  yake
kwa  wananchi ni  kuendelea  kumwombea  zaidi  ili ndoto  yake ya kuleta
maendeleo ifanikiwe zaidi

MAHAFALI YA 49 CHUO CHA CBE YAFANA, SERIKALI YATOA ANGALIZO KWA MAKAMPUNI YANAYOAJILI WAFANYAKAZI WENGI KUTOKA NJE YA NCHI.

1 
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam waliohitimu masomo yao kwa mwaka 2014. Takribani wahitimu 3459 wametunukiwa Astashahada, Shahada na Stashahada za fani mbalimbali.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 49 ya Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam akiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi rasmi wa mahafali hayo jijini Dar es salaam. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Mathew Luhanga (katikati) na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema. 
 5 
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza na wahitimu 3459 wa fani mbalimbali wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam waliohitimu masomo yao mwaka 2014. 6Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)Prof. Mathew Luhanga akizungumza na wahitimu hao. 8 
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda akisoma tamko la kuwatunuku wahitimu 3495 wa fani mbalimbali wa chuo cha CBE wakati wa mahafali ya 49 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KATA YA CHUMO WILAYANI KILWA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kata ya Chumo Wilayani Kilwa mkoa wa Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza sughuli za maendeleo zinazotekelezwa na serikali kwa pamoja na wananchi huku akihimiza huai wa chama, Katibu Mkuu Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Lindi na Mtwara akiongozana na Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi Mh. Bernald Membe.  2 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi  na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika kata ya Chumo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Chumo. 5 
Nape akisisitiza jambo katika mkutano huo 7 
Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi na Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi Mh. Bernald Membe akishuka jukwaani mara baada ya kuwasalimia wananchi wa kata ya Chumo. 8Wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano huo. 9Wananchi wakipunga mikono juu kuashiria kukubali hotuba iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani. 14 
Umati wa wananchi ukiserebuka na muziki kabla ya kuanza kwa mkutano huo. 10Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Maimuna Mtanda akizungumza na wananchi katika mkutano huo. 16 
Mafundi wakiendelea na Ujenzi wa ofisi ya jimbo kwenye Kata ya Chumo wilayani Kilwa mkoani Lindi. 19 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Tingi  20 
Kikundi Cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Tingi wilayani Kilwa mkoani Lindi.

MBOWE MKOANI MOROGORO

MAKAMU WA RAIS DK.MOHAMMED GHARIB BILAL AFUNGUA MKUTANO WA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA DAR ES SALAAM WA KUJADILI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU WA 2015

Makamu wa Rais na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitoa hutuba kwa viongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakiingia ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya mkutano. (Imeandaliwa na www. habari za jamii.com)
Viongozi mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa wakimkaribisha mgeni rasmi wa mkutano huo, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Garib Bilal (hayupo pichani)
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba “Gadafi” akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akihutubia kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dk. Bilal.
Makamu wa Rais ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mpinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Mohamed Gharib Bilal (katikati), akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam leo, kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu 2015. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonah Kaluwa (katikati), akifurahia jambo na viongozi wenzake katika mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanaccm wakiwa wamefurika ukumbi wa Karimjee 
katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanaccm wakiwa katika mkutano huo.
 
Dotto Mwaibale
 
MAKAMU wa Rais ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mpinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Mohamed Gharib Bilal ametoa mwito kwa viongozi na wanachama wa chama hicho kuacha misuguano na mifarakano ili kukiepusha chama hicho na mipasuko isiyo ya lazima.
 
Dk. Bilal alitoa mwito huo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akiwahutubia katika mkutano uliowakutananisha viongozi mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa kujadili uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015.
 
Alisema CCM ni chama pekee hapa nchini ambacho kinafanya shughuli zake kidemokrasia na ndio maana kinaendelea kushika dola na kukubalika na wananchi.
 
Dk.Bilal alisema  katika kipindi hiki cha mchakato wa kuwapata viongozi kuelekea katika chaguzi mbalimbali kunakuwa na changamoto za hapa na pale hivyo wenye dhamana ya kuwateua wagombea wanapaswa kutenda haki kwa kumteua yule aliyepigiwa kura kwa wingi badala ya kufanya ndivyo sivyo.
 
“Chama Cha  Mapinduzi ndio chama chenye dira na sera zinazotambulika hivyo viongozi wake wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha hakuna makundi yanayoweza kuwagawa wanachama” alisema Bilal
Alisema  viongozi wa chama hicho  wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika chaguzi zote kwani uwezo wa kufanya hivyo upo kwa kuwa chama hicho kimejipanga vizuri kuanzia ngazi ya shina na kina maadili.
 
Bilal aliongeza kuwa kila uchaguzi unapofanyika watu na vyama vingine wanaangalia CCM imemsimamisha nani hivyo ni vizuri wakati wa uteuzi wa viongozi wanapaswa kuwa makini kwa kumchagua aliyebora.
 
Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema wamejifunza mengi katika chaguzi zilizopita ambapo walipoteza maeneo kadhaa kwa kuchuliwa na vyama v, kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kupata mgingine kutokana na makosa hayo.
 
Alisema hivi sasa mwanachama yeyote atakaye shinda kura za maoni ndiye atakayekuwa mgombea katika eneo husika labda tu awe amepita kwa rushwa na mambo mengine ambayo yatathibishwa.
 
Madabida alisema kwamba katika mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi za serikali za mitaa kulikuwa na changamoto za hapa na pale ambazo watahakikisha zinafanyiwa kazi ili mambo yaende sawa.(Imeandaliwa na www. habari za jamii.com)
 

Friends Rangers wanashuka katika Uwanja wa Karume kesho

images
Mwandishi Wetu
VINARA wa Ligi Daraja la kwanza katika kundi A, timu ya
Friends Rangers, leo wanashuka katika Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam, kuvaana na timu ya Kimondo, katika mchezo
wa Ligi Daraja la Kwanza.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Asha Kigundula, amewataka wapenzi wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo, kuwapa hamasa wachezaji wao. Kigundula alisema kuwa wana amini mchezo huo utakuwa mgumu, lakini kujitokeza kwa wapenzi wengi kutawafanya wachezaji wao wawe na hamasa kubwa na kuweza kupata ushindi katika mchezo huo.
Alisema kuwa kikosi chao tayari kipo kambini kujiandaa na mchezo huo, ambao ni muhimu kushinda, ili kiweze kupigania nafasi ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Kigundula alisema kuwa kushinda kwao katika mchezo wao uliopita dhidi ya Majimaji, kumeisaidia timu yao kuzidi kupaa na kukaa juu ya msimamo wa kundi lao.
Alisema kushinda kwao katika mchezo huo ni juhudi binafsi za wachezaji, viongozi na wapenzi wa timu hiyo kwa sababu walikuwepo na kuwapa ushirikiano mwanzo.
Katika mchezo wa huo uliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Friends Rangers iliwapa kichapo cha mabao 2-1 timu ya Majimaji ya Songea.
Kwa matokeo hayo Friends Rangers wanaongoza kundi kwa pointi 19 huku maji maji ambao ndio walikuwa wakiongoza ligi hiyo katika kundi hilo wakishushwa na kubakia na pointi zao 18.

No comments:

Post a Comment