Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi
Katika kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof,Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari nchini Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imefanikiwa kujenga vyumba 17 vya maabara kwa shule zake sita za Sekondari kwa gharama ya shilingi 568.6 milioni.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa maabara kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima aliyekuwa Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha wilaya , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’ah katika taarifa yake ilieleza kuwa ujenzi umekamilika kwa asilimia 90 na kazi zilizobakia ni kuweka miundo mbinu ya vifaa vya maabara tu, kazi ambayo inatarajia kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba 2014, na kazi zinaendelea za ukamilishaji.
Chang’ah alieleza kuwa ujenzi wa Maabara hizo ulianza mwezi Januari 14 mwaka 2014 na ulitarajia kukamilika ifikapo Novemba 28 mwaka huu,ambapo kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huu ilikwa kiasi cha shilingi 686.3 milioni hadi kutolewa kwa taarifa hiyo kiasi cha shilingi 568.6 milioni zimetumika kwa ajili ya ujenzi huo ambao umekamilika sawa na asilimia 90.
Akifafanua zaidi alieleza kuwa baadaya kupewa maagizo ya ujenzi wa maabara kwa shule za Sekondari kama menejimenti walikaa na kujadili namna ya ukamilishaji wa ujenzi huu, ambapo walitenga kiasi cha shilingi milioni 686,310,179 kwa ajili ya kujenga vyumba 17,ambapo hadi kufikia walipofikia wametumia kiasi cha shilingi milioni 568,633,685 ndizo zimetumika.
Mkurugenzi huyo akaeleza kuwa baada ya kukaa na kujadiliana na menejimenti walichakata na kuona namna ya kufanya ambapo waliomba kuhamisha fedha kutoka kwenye baadhi ya miradi ili kuipeleka kwenye Maabara ambapo Menejimenti ilipitisha fedha na kupeleka kwenye Kamati ya Fedha na Mipango ili kuweza kupewa ridhaa na Baraka.
Kamati ya fedha ilipitisha na kupeleka kwenye Baraza la Madiwani na Madiwani wakatoa Baraka fedha hizo kutumika kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maabara hivyo matumizi ya fedha hizo zilipata baraza za baraza la madiwani ambapo aliwashukuru madiwanikwa moyo wao wa uzalendo kuruhusu kutumiwa kwa fedha hizo vinginevyo wangekataa kupitia au kuridhia fedha hizo hali ingekuwa tete kupata fedha za kujengea hawajui ingetoka wapi.
Mkurugenzi aliendalea kueleza kuwa walipoanza ujenzi walitumia Wakandarasi ili waweze kujenga maabara,hivyo Halmashauri iliingia Mkataba naWakandarasi ili kujenga Maabara lakini mwenendo wa Wakandarasi ulikuwa wa kusuasua,hivyo ikabidi Halmashauri ikaamua kuvunja Mkataba na kuwatumia Mafundi wa kienyeji ambao walisimamiwa na watalaam wa Halmashauri kupitia kitengo cha ujenzi.
Kwa uwatumia Mafundi hao wa Kienyeji ujenzi ulienda kwa kasi hadi hapo walipofikia,ambapo mafundi wa kienyeji wameonesha kuwa wakitumiwa vizuri wana uwezo mzuri jambo la msingi ni usimamizi wa karibu na ufuatiliaji kisha kuelekezwa wama fanya Vizuri tofauti na wakandarasi ambao wanachelewesja kazi, na kama “tuendelea kuwategemea wakandarasi Maabara tusingefikia hapa tulipofikia’Alisema Mkurugenzi..
Aidha Mkurugenzi huyo alizitaja shule za Sekondari zilizojengwa Maabara kuwa ni Mwese,Karema,Ikola, Mpandandogo,Ilandamilumba na Kabungu ambazo zote zimejengwa vyumba vya maabara ya sayans na shule za Kata za Wananchii.
Pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba hivyo vya Maabara zipo changamoto kadhaa zilizojitokeza katika utekelezaji wa ujenzi huo ,baadhi ya changamoto hizo ni kukosekana kwa nguvu za wananchi katika kuchangia miradi hiyo ambapo katika maeneo mengi suala la kuchangia nguvu za wananchi limekuwa ni changamoto kubwa.
Baadhi ya miradi mingi inayotekelezwa na Halmashauri ilibidi isimame kutokana na kuhamishwa kwa fedha kupelekwa kwa ajili ya ujenzi wa maabara.
Changamoto nyingine ni kuwa pamoja na kukamilika kwa maboma bado kuna suala la miundombinu ya ndani na vifaa vya maabara na bajeti bado inabana ,kubwa zaidi ni namna gani ya kuweza kukamilisha vifaa vilivyobakia.
Ambapo ukiwaambia wananchi kuchangia elimu katika mkoa huu bado ina kuwa suala ngumu tofauti na maeneo mengine hasa mikoa ya Kaskazini wananchi wanamwamko kuchangia elimu huku nitofauti ,
Hata hivyo aliomba wadau mbalimbali wajitokeze kuchangia chochote walichonacho ili kufanikisha suala hilo la ukamilishaji wa miundo mbinu ya maabar kwa kuwatumia viongozi wa ngazi mbalimbali katika mkoa wajaribu kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza katika uchangiaji wa wa maabara.
Naye Mkurugenzi wa Mji wa Mpanda Seleman Lukanga hadi kufikia Novemba 16 mwaka huu jumla ya maabara kumi zimikalika na nyingiene ziko katika hatu ya ukamilishaji.
Lukanga amezitaja shule za Sekondari za Kasimba kuwa maabara tau zimejenga mbili zimekamilika na moja imekamilika nyingine mbili zinaendelea kujengwa.
Shule ya Nsemlwa mabaara tatu ambazo ziko katika hatua ya kupauwa,,Kashaulili maabara tatu zinajengwa,Mwangaza moja iko katika hatua ya kupauwa na nyingine zinaendelea vizuri,Misunkumilo Sekondarizimejengwa mbili moja iko katika hatua ya ukamilishaji,Rungwa Sekondari mbili zimekamilika moja iko katika hatua ya ukamilishaji, Shanwe moja imekamilika na nyingine iko katika ya ukamilishaji.
Hata hivyo pamoja na ukamilishaji huo kwa baadhi ya maabara zipo changamoto kadhaa ambazo zinakabili ujenzi wa maabara hizo,ni wakandarasi kutokukamilisha kazi zao kwa wakati,mwamko mdogo kwa wananchi kuhusu uchangiaji wa shughuli za maendelo.
Changamoto nyingine ni upatikaji wa fedha,michango ya wananchi imekuwa ikisuasua,pamoja na usimamizi katika maeneo mbalimbali kwenye Halmashauri uko chini.
Akashauri ushirikishwa wa wadau mbalimbali washirikishwe has kwa viongozi kwa nafasi walizonazo hasa wakuu wa Wilaya na Mikoa kwa kupata ushirikiano wa karibu ili wananchi washawishiwe kuchangia.
No comments:
Post a Comment