Timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ikishuka kutoka kwenye tanki la kuhifadhia maji ya Mradi wa Maji wa Ruhuiko
Kanisani utakaohudumia zaidi ya wakazi 3000 wa kitongoji ya Kijiji cha Ruhuiko
Kanisani na maeneo ya jirani.
Timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ikishuhudia kazi ya utandazi wa mabomba ya maji ya Mradi wa Maji wa Ruhuiko
Kanisani. Hadi kukamilika kwake mradi huo utatumia zaidi ya shilingi milioni
480.
Msanifu
wa Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani Bw. Elezear Ndunguru (Kulia) akitoa
maelekezo kuhusu maendeleo ya mradi huo. Mradi huu unafadhiliwa kwa pamoja kati
ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia na unagharimu zaidi ya shilingi
milioni 480 za Kitanzania.
Kiongozi
wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri (Mwenye koti jekundu) akihoji masuala mbalimbali kuhusu
utekelezaji wa miradi ya maji kwenye manispaa ya Songea.
Msanifu
wa Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani Bw. Elezear Ndunguru (Kulia) akisisitiza
jambo wakati akizungumza na kiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri (Kushoto).
Anayewasikiliza ni Mratibu wa zoezi hilo Bw. Senya Tuni.
Kiongozi
wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akihimiza juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu
ya maji wakati walipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi 10 ya maji katika
manispaa ya Songea. Wanaomsikiliza ni Msanifu wa Mradi wa Maji wa Ruhuiko
Kanisani Bw. Elezear Ndunguru (Kulia) na Mratibu wa ukaguzi huo Bw. Senya Tuni
(katikati).
Na
Saidi Mkabakuli
Serikali
imetoa wito kwa taasisi za umma kusimamia kwa umakini miundombinu ya miradi ya maji
pindi inapokamilika ili kuweza kuwapatia wananchi huduma ya maji ya uhakika
mara miradi hiyo inapokabidhiwa kwa kamati za usimamizi wa maji.
Wito
huo umetolewa na kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati timu hiyo ilipokuwa
ikifanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya maji ya utekelezaji wa program ya
maji na usafi wa mazingira katika vijiji 10 vya manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma.
Bibi
Mwanri ambaye pia ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia Huduma
za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu, alisema kuwa kwa miaka mingi kumekuwepo
na ubadhirifu wa miundombinu ya miradi mingi ya maji hali inayorudisha nyuma
juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wanafikiwa na maji safi na
salama kote nchini.
“Kumekuwa
na tabia mbaya ya ubadhirifu wa miundombinu hii, msikubali waiharibu ama kuiba
vifaa vya ujenzi wa miradi yote 10 maana kama munavyoona serikali na wafadhili
wamejitolea ili kuhakikisha munafikiwa na huduma hii muhimu,” alisema.
Akizungumza
wakati timu hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ilipotembelea na kukagua Mradi
wa Maji wa Ruhuiko Kanisani utakaohudumia zaidi ya wakazi 3000 wa kitongoji ya
Kijiji cha Ruhuiko Kanisani na maeneo ya jirani, Msanifu wa mradi huo, Bw.
Elezear Ndunguru alisema kuwa mpaka sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia
asilimia 55.
“Kasi
ya utekelezaji wa mradi huu ni ya kuridhisha kwani mpaka sasa tumeweza kujenga
vituo 12 vya kuchotea maji kati ya 15, kinachongojwa kwa sasa ni kukamilika kwa
tanki la kuhifadhia maji,” alisema.
Msanifu
huyo ameongeza kuwa hadi kukamilikwa miradi yote 10 jumla ya shilingi bilioni
2.77 zitatumika na kuweza kuwahudumia zaidi ya wakazi 9000 wa vijiji
vitakavyopitiwa na miradi hiyo.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo, lengo kuu kwa upande wa maji ni kuongezeka
kwa upatikanaji wa maji safi na salama ni mojawapo ya maeneo yanayotiliwa mkazo
ili kuweza kuongeza kasi ya maendeleo na kupunguza umaskini miongoni mwa
Watanzania.
No comments:
Post a Comment