Mji mkuu wa Qatar Doha, utakuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya riadha mwaka 2019 baada ya kuzipiku Barcelona na mji wa Eugene nchini Marekani zilizotaka kuandaa mashindano hayo.
Imependekezwa kuwa mashindano hayo yafanyike kati ya tahere 28 Septemba hadi tarehe sita Oktoba mwaka huo ili kuondokana na msimu wa jua kali.
Maafisa wakuu nchini Qatar, wanadai kuwa nyuzi joto zitakuwa zimeshuka ikilinganishwa na mwezi Mei ambapo Doha itaandaa mashindano ya Diamond League.
Doha ilitaka kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya mwaka 2017 lakini London ikaipiku.
Mji huo pia unajiandaa kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.
Mashindano ya riadha ya mwaka 2015, yatafanyika mjini Beijing kuanzia tarehe 22-30 Agosti wakati mashindano ya mwaka 2017 yatafanyika mwezi Agosti.
"tumekuwa na ndoto ya kuandaa mashindano haya kwa muda mrefu , '' alisema afisa mkuu wa Doha, Dahlan al Hamad.
Uwanja wa kimataifa wa Khalifa ambao utakuwa kitovu cha dimba la dunia mwaka 2022, ndiko mashindano hayo yatafanyika.
No comments:
Post a Comment