TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 20.11.2014.
- WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI PAMOJA NA MICHE YA BHANGI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA NYAKATI TOFAUTI WAKIWA NA BHANGI PAMOJA NA MICHE YA BHANGI.
KATIKA MSAKO WA KWANZA,
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KATSON IYISEGA (68) MKAZI WA KIJIJI
CHA ISWAGO ALIKAMATWA AKIWA AMEOTESHA MICHE YA BHANGI 12 KATIKA SHAMBA
LAKE LA MAHINDI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
19.11.2014 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISWAGO,
KATA YA SANTILYA, TARAFA YA ISANGATI, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA
NI MUUZAJI WA BHANGI NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
AIDHA KATIKA MSAKO WA PILI,
MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BRYSON
SANGA (28) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI
KETE 15 SAWA NA UZITO WA GRAM 75.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
19.11.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA NSALAGA –
UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI, TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII
KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA ULIMAJI WA BHANGI ILI
WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment