Na Mwandishi Wetu, Handeni
MKUTANO
wa kwanza wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation uliyofanyika juzi
Novemba 19, katika kijiji cha Misima, wilayani Handeni, mkoani Tanga na
kuwakutanisha wananchi wote umeibua kero nyingi za wananchi, ikiwamo ya
kijiji chao kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji bila ridhaa yao.
Mmoja
wa wakazi na wananchi wa kijiji cha Misima, akilalamikia eneo lao
kuingia kwenye Halmashauri ya Mji kinyume cha sheria ya utawala bora,
ikiwa ni pamoja na kutoshirikishwa kwa lolote na viongozi wa juu.
Taasisi
hiyo ilianzishwa mapema mwaka huu na kuzinduliwa Mei 8 jijini Dar es
Salaam, ilifanya mkutano mkubwa wa hadhara Misima, ambapo umati wa
wanchi ulihudhuria, huku kero nyingi zikiwasilishwa na kudhihirisha
changamoto za utawala bora zinazoathiri maendeleo ya Tanzania.
Wakizungumza
kwa uchungu mkubwa, mwananchi wa Misima aliyejitambulisha kwa jina la
Mhina Ally, alisema viongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na madiwani
waliamua kuingiza kijiji chao katika Halmashauri ya Mji bila ya
kuwashirikisha, ikiwamo kubandika tangazo la pingamizi kwa siku 90
katika maeneo yao kama sheria inavyotaka.
Alisema
kutoka Handeni Mjini hadi katika eneo lao ni kilomita 16
zilizozunguukwa na mapori yanayowafanya wananchi wajihusishe na kilimo
kwa asilimia 99, hivyo kuingizwa kwenye sheria za mji ni kusababisha
ugumu wa maisha.
“Inashangaza
mno kusikia Tanzania kuna utawala bora wakati viongozi wachache
wanaweza kufanya watakavyo; hali inayoweza kuleta mapigano makubwa,
endapo wananchi tutasimama kidete kudai haki zetu zinazokandamizwa na
viongozi kila siku,” alisema.
Ally
alifika mbali zaidi kwa kusema walisikia tangazo redioni la kuingizwa
kwenye Halmashauri ya Mji, huku tangazo la pingamizi likishindwa kuwekwa
kijijini kwao kwa hofu ya kupingwa na wananchi wao.
“Viongozi
wa serikali ya kijiji waliamua kutoliweka tangazo la pingamizi kijijini
kwetu kwasababu wanajua fika tusingekubali, hivyo inashangaza
malalamiko yetu kufumbiwa macho na serikali inayoitwa sikivu, licha ya
kuzunguuka sehemu nyinyi, kama kwa Mkuu wa wilaya na Mkuu wa Mkoa wa
Mkoa Tanga, alipokaimu DC Halima Dendego, ambaye sasa amekuwa Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara,” aliongeza.
Naye
Naye Idd Kisege alisema kuwa ili kuona viongozi wanaogopa kufika
Misima, hata namba kwenye nyumba zao hakuna ingawa wanatangaza uchaguzi
kwa sheria za mji katika kijiji chao, jambo lisiloweza kuvumiliwa na
kila mpenda maendeleo ya Misima.
“Watu
wa Misima tunaambiwa sisi ni watata, wakorofi tunapodai haki zetu, ili
waendelee kutuburuza, ndio maana kwenye ziara ya Mheshimiwa Rais,
Profesa Jakaya Mrisho Kikwete waliniburuza Polisi kwasababu ya kuonyesha
bango kwa mheshimiwa ili kuona kero zetu,” alisema Kisege.
Naye
Mkomwa Athuman alisema kuwa Misima haipo tayari kutumikia sheria za Mji
kwakuwa ni mapema mno kwao, hivyo wanaomba serikali, ikiwamo ofisi ya
Waziri kulifuatilia suala hilo kwa kina.
“Mzozo
huu umeshakuwa mkubwa na kuondoa ushirikiano kabisa kwa viongozi na
wananchi wa hapa Misima, hivyo tayari malalamiko yetu yamefikishwa Ofisi
ya Waziri Mkuu kulishtakia suala hilo kwasababu sheria ya kuingia
kwenye Mamlaka ya Mji Handeni haijafuatwa na imeanzishwa na watu
wachache ili kuzima uozo wa ardhi waliyoufanya kwenye kijiji chetu,”
alisema.
Katika
kila mwananchi aliyezungumza kwenye mkutano huo alionyesha kuguswa na
kero hiyo ya mji, huku wakisema kutoka Handeni Mjini hadi Misima ni
mbali pamoja na viongozi kushindwa kufuata sheria za utawala bora.
Awali,
mkutano huo ulioanza saa tisa alasiri ulifunguliwa na mtoa mada wa
kwanza, Kambi Mbwana, ambaye ndiye Msemaji Mkuu wa taasisi hiyo,
aliyejikita sababu na dhamira kuu ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo.
Mbwana
alisema kuwa sababu kubwa ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutoa elimu
ya uraia na kuhamasisha utawala bora, ikiwa ni njia moja wapo ya
kuwafanya Watanzania wote wajiletee maendeleo kwa kushirikiana baina yao
na viongozi wote.
Akizungumzia
utawala bora, Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Adam Malinda, alisema
kwamba matatizo mengi katika jamii yamekuwa yakichangiwa na viongozi
wasiojua nini maana ya utawala bora.
“Utawala
bora ni somo muhimu na lazima lipigiwe kelele na watu wote, maana
malalamiko mengi ya watu wa Misima yamesababishwa na tatizo hilo, ndio
maana unaona kero zimepamba moto,” alisema.
Malinda
aliwataka viongozi wa juu, wakiwamo wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
kuzungumza na wananchi wa Misima ili kutatua mtafaruku huo kwa ajili ya
kuwafanya wananchi waendelee na shughuli za kujiletea maendeleo,
sambamba na serikali kuwafanyia kazi watendaji wabovu.
Kuhusiana
na mzozo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas
Mzinga, alikaririwa akisema kuwa utaratibu ulifuatwa, ikiwamo kutoka
kwa siku 60 za pingamizi, ingawa wananchi hao walishindwa kupita njia
hiyto kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.
No comments:
Post a Comment