PRESS RELEASE
(Taarifa kwa Vyombo vya Habari)
Ndugu, Waandishi wa Habari,
Siku ya jumamosi tarehe 22/11/2014
itakuwa ni siku ya Ufunguzi wa Michezo ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA,
utakaofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Dar es salaam Institute of
Teckinology (DIT) kuanzia saa mbili (2:00) asubuhi mpaka saa kumi na
mbili (12:00) jioni.
itafanyika kila mwaka kwa
kushirikisha vyuo mbali mbali vya elimu ya kati hapa nchini Tanzania
na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za
Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa
wavulana na wasichana
Kampuni ya Miss Demokrasia
Tanzania & Entertainment C.o Ltd,yenye makao makuu yake Mwenge
jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ndiyo
itakayokuwa ikisimamia taratibu zote za michezo hiyo wakati wote wa
mashindano.
Kwa upande wa mkoa wa dare s
salaam vyuo vilivyopo katika orodha ni 105 hivyo kulingana na bajeti
kuwa kubwa, kama imeweka utaratibu wa kushiriki wenye michuano hiyo ya
NACTE ambapo ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya
mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA
ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER
COLLEGE DAR ES SALAAM.
Siku ya jumamosi itakuwa ni sehemu
ya kwanza( Season one) ambapo vyuo vilivyotaarifiwa kuhusika katika
kuwania nafasi hizo mbili za juu ni pamoja na Wenyeji D.I.T, majirani
zao C.B.E na wakongwe wa Michezo Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM).
Vyuo vingine ni Dar es salaam City
College(DACICO) na majirani zao chuo cha Mlimani Profesional, na Royal,
na Timu Mwalikwa katika Season hiyo ni Timu ya 100.5 TIMES FM Radio,
kwa kuwa katiba ya michuano hiyo inaruhusu kuhusisha timu mbili waalikwa
ambao watatokana na vyombo vya habari ama chombo cha habari, hivyo
100.5 Times Fm, wakiwa pia ni kati ya wadhamini wakuu wa matangazo ya
radio, wamepata fulsa ya kushiriki hatua hii ya kwanza (Season one).
Michezo itakayohusishwa hiyo siku
ya ufunguzi ni pamoja na Mpira wa Miguu, Netball, Basketball, na
Voleyball na washindi wa kwanza watazawadiwa Kombe wakati washindi wa
pili watapata Mpira Mmoja kutoka kwa Wadhamini Wakuu Kampuni ya Simu za
Mkononi VODACOM .
Ukiachilia mbali michezo hiyo,
michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni
DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji kwa viongozi
wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri
Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha, na Spika , watakaokuwa wakichuana
katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na
changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo
mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.
Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo
ni Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na
mgeni mwalikwa atakayekabidhi zawadi kwa washindi ni mkurugenzi mtendaji
wa 100.5 -TIMES RADIO, Bw. Leule Nyaulawa.
Aidha nichukue fulsa hii kuwaomba
ndugu zetu wandishi kuhamasisha Makampuni na wadau kujitokeza kudhamini
michuano hii ambayo maleng yake ni kuendeleza vipaji na kuibua vijana
watakaokuwa viongozi, pamoja na kuwajengea mazingira ya kushiriki mara
kwa mara katika michezo kwani Micheo uleta udugu, Upendano, mshikamano,
amani, Afya na pia kijana anayeshiriki mazoezi upata muda wa kutumia
akili kutafakali mambo ya Maendelezo zaidi.
Imetolewa na -Katibu Mkuu Miss Demokrasia Tanzania- HALIMA BAKARI
No comments:
Post a Comment