wacheza dakika 45 tu, wadhihirisha hakuna bifu kati yao
by
SAID MDOE
Mafahari hao wawili wakiwa wameteka gumzo la mechi hiyo kwa wiki nzima, wakatoka uwanjani bila kugusa nyavu – hakukuwa na mbabe kati yao kwa maana ya mchezaji mmoja mmoja.
Ronaldo na Messi wote wawili walitolewa mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza na hivyo hakuna aliyehusika kwa namna yoyote na bao la dakika za majeruhi la Raphael Guerreiro aliyeipatia Ureno goli pekee lililofanya mchezo huo wa aina yake umalizeke kwa matokeo ya 1-0.
Nyota
hao ambao kwa sasa ndio wachezaji bora zaidi duniani wakizechezea timu
pinzani chini Hispania (Barcelona na Real Madrid), wakaonyesha kuwa
hawana bifu lolote na mara nyingi walionekana kutaniania na kucheka kila
walipokutana uwanjani.
Hata wakati wakiwa njiani kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kuelekea dimbani kuanza mchezo, Ronaldo ambaye ni nahodha wa Ureno, alimfuata Messi ambaye nae pia ni nahodha wa Argenitina na kumkumbatia huku wote wawili nyuso zao zikipambwa na tabasamu.
Ronaldo aliyekuwa kama anacheza kwenye uwanja wa nyumbani (nyumbani kwa Manchester United) akapokewa na mabango mengi yaliyomwambia “Karibu nyumbani”.
Wote wawili walipata alama 7 kati ya 10 katika ubora wa viwango vya uchezaji katika mchezo huo.
Argentina: Guzman
6, Roncaglia 5.5, Biglia 6, Demichelis 5.5, Ansaldi 6 (Silva 71, 5.5),
Mascherano 7, Otamendi 5.5, Pastore 6.5 (Pererya 73, 5), Di Maria 6
(Tevez 61, 5), Higuain 5.5 (Lamela 61, 5), Messi 7 (Gaitan 45, 6)Booked: Ansaldi.Portugal::
Beto 6.5, Bosingwa 6, Bruno Alves 6, Pepe 5.5 (Fonte 45, 6), Tiago
Gomes 5.5 (Guerreiro, 6); Nani 5, Moutinho 6, Danny 5.5 (Eder 45, 5.5),
Tiago 6 (Carvalho, 77) , Andre Gomes 5.5 (Silva 68, 5.5), Ronaldo 7 (Quaresma 45, 6).
No comments:
Post a Comment