TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, April 27, 2012

FRANCIS CHEKA NA MADA MAUGO WAPIMA UZITO TAYARI KWA MPAMBANO WAO


WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wamewapima uzito   na bondia  Mada Maugo  na  Na Francis Cheka wote wamekutwa na kilogramu 76.5 ambapo mpambano wao utafanyika Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.
“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D.

Thursday, April 26, 2012

Benki ya NBC yaandaa mkutano wa masuala ya kuchumi

Maofisa wa ABSA Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya Afrika Kusini wakiwa katika  mkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital jijini Dar es Salaam jana jioni. Katikati ni Ridle Markus, Jeff Gable (kushoto), Pius Tibarazwa (wa pili kushoto) wa NBC Tanzania na Michael Keenan (kulia) wa ABSA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kulia) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo wa makampuni katika mkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya Afrika Kusini jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kushoto) akimsikiliza mmoja wa maofisa wa  ABSA Capital ambayo ni sehemu ya benki ya ABSA ya Afrika Kusini, Jeff Gable,  katika mkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital kwa wateja wa makampuni wa NBC, jijini Dar es Salaam jana jioni. Wa pili kushoto ni Mohamed Sayed wa ABSA Capital na Mkuu wa Idara ya Fedha na Masoko wa NBC, Pius Tibarazwa.
Mkuu wa Idara ya Fedhana Masoko wa  Benki ya NBC Tanzania, Pius Tibarazwa (kushoto) akizungumza na mmoja wa maofisa wa ABSA Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya Afrika Kusini, Jeff Gable katika mkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA
Capital kwa wateja wa makampuni wa NBC, jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (katikati)akisalimiana na baadhi ya wateja wa makampuni wa benki hiyo katikamkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya Afrika Kusini jijini Dar
es Salaam jana jioni.

CHEKA AMUWEKA KIPOLO KASEBA KUKUTANA SIKU YA SABASABA


 Bondia Japhet Kaseba  katikati akisaini mkataba kabla ya pambano lake na bondia Francis Cheka.
Bondia  Francis Cheka kushoto akisaini mkataba kabla ya pambano lake na bondia  Japhet Kaseba.
Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  amesaini mkataba wa kupigana na  bingwa wa kick Boxing. Japhet  Kaseba   katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Cheka amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mchezo wa masumbwi na mabondia wengi wanamtaka   kupigana  na yeye.
Najua mabondia wa hapa bongo kila mtu anataka kucheza na mimi tu wanajua mimi ndio nalipa kwa soko la bongo na nitahakikisha kila anaekuja mbele yangu namtandika kifupi Tanzania akuna bondia mwenye uwezo zaidi yangu alisema Cheka.
Kaseba nilimpiga kwa K.O tareha 3 October 2009 nilimpinga anataka tena wembe kwa ngua ngumi ni sehemu ya maisha yangu siwezi kukataa na mimi ndio napata ridhiki yangu humu hivyo nitahakikisha anaekuja mbele yangu namtwanga tu bila huruma nitaanza na Mada Maugo 28 April na huyo namuweka kama kipolo

Nae Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi
Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae;

MOHAMED MTONGA: HAKUTATOKEA UBADHIRIFU TENA WIZARA YA FEDHA


NA MWANDISHI WETU
 
WIZARA ya Fedha nchini imesema baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu  wa Serikali (CAG), kubaini matumizi mabovu ya mishahara hewa na mikataba mibovu, wizara hiyo haitarajii  kujitokeza tena kwa ubadhirifu huo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Mohamed Mtonga wakati akifufunga semina ya siku nne ya maodita wa ndani jijini Dar es Salaam leo.
Alisema lengo la semina kwa washiriki hao ili kuwa ni kuwajengea uwezo ambao utawasaidia katika kazi zao haswa  kudundua maeneo hatarishi ya upotevu wa fedha.
Mtonga alibainisha kuwa mafunzo hayo yawasaidia kubaini matumizi yasiyo ya kawaida kwa haraka kwa kuwa wizara imeanzisha mfumo mpya kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa njia ya kompyuta.
Alisema teknolojia hiyo ya kisasa ambayo inauwezo wa kugundua makosa hayo haraka katika maeneo mbalimbali, hivi sasa inatumiaka katika nchi ya Kenya ambapo imefanikiwa kwa kiwango cha juu.
Mtonga alisema kutokana na mafanikio ya nchi hiyo, Tanzania imeamua kuwapeleka maodita wake wanne (4), kwenda kujifunza teknolojia hiyo ambapo itaanza kutumika hivi karibuni hapa nchini.
Aidha, alisema Wizara ya Fedha imetoa muongozo unaowataka kila Katibu Mkuu wa Wizara kufanya uchunguzi katika kubaini maeneo hatarishi katika ofisi zao kitendo kitakacho wasaidia kugundua haraka  ubadhirifu wa mishahara hewa na mikataba bandia kwa kutumia teknolojia hiyo.
Cheo hicho cha Mkaguzi Mkuu wa Ndani kimeanzishwa kisheria hivi karibuni kwa ajili ya kuboresha na kuongeza nguvu katika kazi za ukaguzi wa fedha ambapo hapo awali hakikuwepo. 

  POLISI WAPIGWA FAINI MIL 1/- KILA MMOJA


 
 
Kamati ya Ligi ya TFF imewafungia mechi tatu na kuwapiga faini y ash. milioni mmoja kila mmoja wachezaji tisa wa timu ya Polisi Dodoma baada ya kumpiga mwamuzi Martin Saanya kwenye mechi dhidi ya Azam iliyochezwa Aprili 14 mwaka huu mjini Dodoma.
Wachezaji hao walioadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 25(g)(iii) ni Noel Msekwa, Frank Sindato, Abdallah Matila, Bantu Admin, Salmin Kisi, Madope Mwingira, Sihaba Mkude, Kaliyasa Mashaka na Ibrahim Massawe.
Iwapo wachezaji hao watahama Polisi na kujiunga na timu nyingine, watahama na adhabu zao.
Vilevile timu ya Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri. Pia timu hiyo imepewa barua ya onyo kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi yao na Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MTIBWA SUGAR YAPOTEZA MECHI DHIDI YA AZAM


Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemuondoa mwamuzi Rashid Msangi wa Dodoma kwenye orodha ya waamuzi kwa kuvuruga mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa Aprili 23 mwaka huu.
Pia waliokuwa waamuzi wasaidizi wa mechi hiyo; Samuel Mpenzu na Abdallah Uhako wote kutoka Arusha nao wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Vilevile Kamati imeipa Azam ushindi wa mabao 3-0 kwa mujibu wa Ibara ya 31 ya Kanuni za Nidhamu za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Kwa mujibu wa kanuni hiyo, timu itakayohesabika kupoteza mechi (Mtibwa Sugar) itakuwa imefungwa mabao 3-0.
Kwa mujibu wa Kanuni ya Ligi Kuu ya Vodacom kifungu cha 22(3-6) Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000, imepoteza mapato yote ya mchezo huo na inatakiwa kulipa faini hiyo kabla ya mechi inayofuata.
Nao makamishna watatu; Abdallah Mitole wa Dar es Salaam, William Chibura (Musoma) na Omari Mawela (Mwanza) wameondolewa kwenye orodha ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kushindwa kufika kwenye mechi walizopangiwa kusimamia bila taarifa.
Makamishna hao wametakiwa kutoa maelezo ya maandishi wakieleza sababu za kutofika kwenye mechi. Mechi walizokuwa wamepangia ni Coastal Union vs Ruvu Shooting (Mitole), Kagera Sugar vs Yanga (Chibura) na Kagera Sugar vs African Lyon (Mawela).
Nayo Moro United imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya wachezaji wake kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadirishia (dressing rooms) wakati wa mechi namba 171 kati yao na Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 8(16).
Pingamizi la Villa Squad dhidi ya African Lyon kuwa wakati wa mechi yao ilitumia wachezaji wawili (Mohamed Samata na Benedict Jacob) ambao mikataba yao imemalizika limetupwa kwa vile wana leseni halali za kucheza ligi.
Pia mwamuzi wa mechi namba 160 kati ya Moro United na Oljoro JKT, Nathaniel Lazaro wa Kilimanjaro amefungiwa miezi sita na kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa kutozingatia kutunza muda kwa mujibu wa kanuni ya 26(1)(f).
Vilevile Kamishna wa mechi ya Moro United na Oljoro JKT, Ali Mkomwa wa Pwani na Said Mnonga wa Mtwara aliyekuwa mwamuzi msaidizi mechi kati ya Villa Squad na Coastal Union wameandikiwa barua za onyo wakitakiwa kuwa makini kwenye michezo wanayosimamia.

MECHI YA TWIGA STARS, ZIMBABWE YAFUTWA

 
Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) na Zimbabwe iliyokuwa ichezwe keshokutwa (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imefutwa.
Uamuzi huo umefanywa na Chama cha Mpira wa Miguu Zimbabwe (ZIFA) ambayo sasa imeamua kucheza mechi ya kirafiki na Zambia. Mechi hiyo itachezwa Aprili 28 mwaka huu jijini Harare.
Twiga Stars inaendelea na mazoezi chini ya kocha wake Charles Boniface Mkwasa katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) iliyoko Ruvu mkoani Pwani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na jitihada za kuitafutia mechi za kirafiki Twiga Stars kabla ya kucheza mechi ya mashindano dhidi ya Ethiopia ambayo itafanyika Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa.

HARAIKI YA WANAFUNZI YAPAMBA SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANZANIA.

(NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO)
DAR ES SALAAM
Haraiki ya  wanafunzi wapatao  1,727 kutoka shule za msingi mbalimbali Tanzania bara na visiwani  wameipamba vizuri sherehe ya maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika  leo katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kati ya wanafunzi hao, ni wanafunzi 727 ambapo 500 wanatoka Tanzania bara, 200 Tanzania visiwani na 27 ni mahodari wa kucheza sarakasi ambao waliingia uwanjani na kutengeneza maumbo mbalimbali pamoja na kuimba wimbo maalumu uitwao Uamuzi wa Busara.
Maumbo yaliyotengenezwa na haraiki hiyo ni pomoja na bendera ya taifa, herufi zenye  umbo la miaka 48 ya Muungano, na maumbo ambayo ndani yake walicheza salakasi na ngoma za asili za ndalandala kutoka Tanzania bara na chaso kutoka Zanzibar.
Maumbo mengine ni pamoja na madini ya Tanzanaiti ambayo hayapatikani sehemu yoyote duniani zaidi ya Tanzania na maumbo ya mazao ya uchumi ya katani na pamba yanayolimwa Tanzania bara na karafuu Tanzania visiwani.
Haraiki hiyo imeandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na wakufunzi wake ni Kilema Athuman Kambangwa akisaidiwa na Mwalimu Grace Ernest Kabohora kutoka shule ya msingi Wailesi katika manispaa ya Temeke.
Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa ni Rasi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kauli mbiu ni “Shiriki kikamilifu katika Sensa na mchakato wa Mabadiriko ya Katiba”.(Mwandishi Shaaban Mpalule)

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WANANCHI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2012 katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akiingia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuongoza maadhimisho ya mika 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo asubuhi (Picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipowasili katika uwanja wa Uhuru kuongoza sherehe za Muungano zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo (Picha na Freddy Maro)
Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2012 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo leo.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo leo.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo leo.
Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha alaiki, wakionyesha manjonjo ya michezo na maumbo mbalimbali wakati wa sherehe hizo leo.
 
Kikundi cha Sanaa cha JKT Oljoro, kikionyesha umahiri wake wa kuimba na kucheza 'Kiduku' wakati wa sherehe hizo.

ANGALIA PICHA ZA MAADHIMISHO YA MUUNGANO


 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais na amiri jeshi mkuu akikagua gwaride leo asubuhi.(Picha kutoka IKULU)