January 18, 2013
Mh.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiimba wimbo wa mshikamano kabla ya kuanza
mkutano mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Serekali za mitaa Talgwu jana
amabao una fanyika mjini Dodoma kushoto kwa waziri mkuu ni Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa( Tamisemi) Mh Hawa Ghasia na
kulia kwa waziri mkuu ni mwenyekiti wa (Talgwu) Edna Mwaigomole pamoja
naviongozi wengine Picha na Chris Mfinanga
Mh.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua Tovuti ya chama cha wafanyakazi wa
wa serekali za mitaa kulia kwa waziri mkuu anaye shuhudia uzinduzi huo
ni Mwenyekiti wa chama hicho Bibi Edna Mwaigomole na aliye vaa tai ni
mtalamu wa kompyuta uzinduzi ume fanyika leo mjini Dodoma Picha na Chris
Mfinanga
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mjini Dodoma baada ya kuuzindua.
Mh.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwasili kufungua mkutano mkuu wa Baraza la
wafanyakazi wa serekali za mitaa Talgwu kushoto kwa waziri mkuu ni
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa (Tamisemi) Mh Hawa
Ghasia na kulia ni Mwenyekiti wa Talgwu Edna Mwaigomole mkutano huo
unafanyika mkoani Dodoma Picha na Chris Mfinanga
WASANII WA FILAMU BONGO KUCHEZA FILAMU NIGERIA NA DRC CONGO
Mkurugenzi wa Mad Mad
Entertainment, Yasmin Razak (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kampuni yake kuingia mikataba na
wasanii wa filamu wa Tanzania watakaokwenda Nigeria na Jmahuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kutengeza filamu. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa
Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba.
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.
“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.
Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalie namna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.
Msanii wa filamu, Steve Nyerere
(kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano hupo.Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la
Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba.
……………………………………………………………….
KAMPUNI ya Mad Mad Entertainment
iliyopo jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program maalum ya
kupeleka wasanii wa filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la kukuza
sanaa hiyo hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo
Yasmin Razak alisema ameamua kufanya kazi na wasanii hao ili kuleta
mabadiliko na kuwakwamua kiuchumi wasanii wa filamu hapa nchini.
“Kwa muda mrefu niliokaa London
sioni kama sanaa hii ina maendeleo, nikafikiria kitu gani nifanye ili
kukuza tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza
filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha Sh. 50 milioni pamoja na
malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na
asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini.
“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria
wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata
Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia
katika mchakato huo,”alisema Razak.Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.
“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.
Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalie namna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.
Rais Kikwete apokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Msumbiji na Indonesia
Balozi
mpya wa Msumbiji nchini Tanzania Dkt.Vicente Mebunia Veloso na Balozi
Mpya wa Indonesia nchini(4395) Mhe.Zakaria Anshar wakiwasilisha hati zao
za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es
Salaam leo(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Indonesia ikulu jijini Dar es Salaam.
DK SHEIN KUONGOZA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA
January 17, 2013
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuongoza Mkutano
wa saba wa Baraza la Biashara Zanzibar utakaofanyika Jumamosi Januari
19 katika ukumbi wa Salama Hoteli Bwawani mjini Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa Vyombo vya
habari huko Gulioni katika Jengo la ZSTC Katibu Mtendaji wa Baraza hilo
Ali Haji Vuai alisema mkutano huo wa saba utazikutanisha Sekta za Umma
na Sekta Binafsi, ambao utajadili mada mbili muhimu ambazo ni Maendeleo
ya uwekezaji katika viwanda na Ubiya unaohitajika katika viwanda vya
Zanzibar.
Amesema wameamua kuzungumzia
masuala hayo kutokana na Sekta ya Viwanda Zanzibar kuwa nyuma sana jambo
ambalo pia huchangia ukosefu wa Ajira kwa vijana na mapato kwa
maendeleo ya Zanzibar.
Ameongeza kuwa Zanzibar ina fursa
nzuri ya kuanzisha viwanda vipya na kuvifufua vile vilivyokuwepo awali
jambo ambalo litachochea kasi ya maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa
Zanzibar.
Vuai amefahamisha kuwa Viwanda
vilivyokufa Zanzibar vilitokana na sababu mbalimbali na kwamba Mkutano
huo utakuwa ni sehemu muafaka ya kuelezea chanzo cha kufa viwanda hivyo
na kubuni mipango mipya ya kufufua sekta hiyo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete afunga kongamano la Ulimwengu la afya ya uzazi mjini Arusha
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete
akifunga kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi la siku 3 Katika
ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC mjini Arusha leo, Kongamano hilo
lilewashirikisha wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi wapatao 800
kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni, (Picha na Mwanakombo Jumaa-
MAELEZO).
Baadhi
ya wataalamu wa kongamano la ulimwengu la afya ya uzazi wakimsikiliza
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete
(hayupo pichani wakati wa kufunga kongamano Jan,17,2013 mjini Arusha,
ambapo wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi zaidi ya 800 kutoka ndani
na nje ya nchi wamehudhuria, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
Baadhi
ya wataalamu wa kongamano la ulimwengu la afya ya uzazi wakimsikiliza
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete
(hayupo pichani wakati wa kufunga kongamano Jan,17,2013 mjini Arusha,
ambapo wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi zaidi ya 800 kutoka ndani
na nje ya nchi wamehudhuria, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa kmataifa wa AICC Arusha leo.
Mke
wa Rais na Mwenyikiti wa Taasisisi ya WAMA ,Mama salma Kikwete (alievaa
kitnge) akiogozana na watendaji wakuu wakielekea katika eneo la kupigia
picha ya pamoja
Picha ya pamoja na watendaji wakuu wa kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi.
Mama Salma Kikwete akifurahia ngoma ya msanja ya kikundi cha akina mama huko Arusha
WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUJICHULIA SHERIA MIKONONI
Mahmoud Ahmad Arusha
…………………………………………..
Wananchi wenye hasira kali hapa nchini wametakiwa kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuwapiga ama kuwachoma moto watu wanaodaiwa kuwa ni wezi bila ya kujua kama madai wanaotuhumiwa nayo ni ya kweli au la na wengine kujikuta wakipoteza maisha bila ya kuwa na hatia na kutakiwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na usalama.
Kauli hiyo imetolewa na wananchi mbali mbali wakati wakiongea
na waandishi wa habari kwenye matukio mawili tofauti yaliyotoke kwenye
sehemu mbili tofauti kwenye kituo kikuu cha mabasi na kituo kidogo cha
vifodi jijini hapa jana.Wananchi wenye hasira kali hapa nchini wametakiwa kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuwapiga ama kuwachoma moto watu wanaodaiwa kuwa ni wezi bila ya kujua kama madai wanaotuhumiwa nayo ni ya kweli au la na wengine kujikuta wakipoteza maisha bila ya kuwa na hatia na kutakiwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na usalama.
Katika tukio la kwanza kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 37 mkazi wa jijini hapa mwenye ugonjwa wa akili alipata mkong’oto wa kufa mtu baada ya kupiga gari la mtu lililokuwa kwenye stand hiyo na kumwaga vyakula na karanga za wafanyabiashara ndogo ndogo na vijana stand hapo kumpa mkong’oto huo.
Vijana hao huku wakimpa mkong’oto kijana huyo walikuwa wakimwambia kuwa wanampa dawa ya sigareti kubwa kwani dawa yake wanayo wao kijana huyo aliendelea kupatiwa mkong’oto nhadi askari wa jeshi la polisi aliyekuwa doria stand hapo kumuokoa na kumfikisha kwenye vyombo vya usalama kumuokoa na kipigo hicho kutoka kwa vijana wasio na chembe hata ya huruma kwa mgonjwa huyo.
Katika tukio la pili kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 17 mkazi wa jiji hili alipata mkong’oto wa paka mwizi hadi kushindwa kujua uelekeo wake wa kwenda baada ya kudai kuiba vitu kwenye duka moja stand ndogo ya vifodi
Waandishi walipohoji kwa mwenye duka hilo ni vitu gani vimeibiwa kwenye duka hilo alishindwa kuthibitisha kuwa alIIbiwa nini dukani humo huku mgambo wa jiji wakiangali bila ya kuchukuwa hatua yeyote.
Taarifa zinadai kuwa wananchi mbali mbali wamekuwa wakipatiwa mkong’oto bila ya kuwa na hatia ya makosa wanayotuhumiwa na kuwataka wananchi mbali mbali kutokujichukulia sheria mikononi
Alipohojiwa kamanda wa polisi
mkoani hapa Liberatus Sabas kuhusiana na wananchi kujichukulia sheria
mkononi alisema matukio mengi ya kujichukulia sheria mkononi ni tatizo
hapa nchini huku akiwataka watanzania kujenga mazoea ya kujichunguza
kabla ya kujichukulia sheria mkononi.
WAZIRI MWANRI AWACHACHAMALIA WANAOPIGA MIMBA WANAFUNZI
Na Kibada Kibada wa Fullshangwe-Katavi
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya
waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Agrey
Mwanri amewaagiza viongozi na Watendaji wa serikali kuhakikisha
wanakomesha suala la mimba mashuleni.
Waziri Mwanri alitoa agizo hilo
(leo) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kijiji cha Kilida Kata ya Mamba wilayani Mlele
Mkoani Katavi katika ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za
maendeleo na kuona jinsi gani Halmashauri zinasimamia fedha za serikali
zinazoletwa kwenye halmashauri kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika
kutekeleza miradi na kupeana mikakati jinsi ya kusimamia fedha hizo ili
zifznye kazi iliyokusudiwa.
Amesema ni wajibu wa viongozi
kuhakikisha suala la mimba linakomeshwa kabisa mashuleni na haitoshi
kila mara viongozi kuripoti tu, suala la mimba mashuleni bila hatua
kuchukuliwa kwa wale wahusika wanaofanya vitendo hivyo vya kuwapa mimba
watoto wa kike.
“Haitakiwi kuripoti tu,pia
inatakiwa kueleza ni hatua gani zimechukuliwa kuhakikisha hao wanofanya
vitendo hivyo wamechukuliwa hatua zipi za kisheria ili kukomesha
vitendo hivyo”alisema kwa kufoka Mwaniri.
Aliagiza kufuatia kusomewa
taarifa ya Mkoa kuhusu maendeleo ya Mkoa iliyosomwa na Kaimu Katibu
Tawala wa Mkoa wa Katavi Lauten Kanoni ikieleza hali ya elimu na jinsi
suala la mimba kwa watoto wa kike linavyo shughulikiwa
Aidha katika taarifa hiyo
ilieleza hali ilivyo kwa sasa ilieleza kuwa mimba kwa mkoa wa katavi
zimepungua kutoka wasichana waliopata ujauzito mwaka 2011 (63) na
mwaka 2012 mimba zilipungua kufikia (61) sawa na asilimia tano
.taarifa ambayo haikueleza namna wanavyolishughulikia tatizo la mimba na
kueleza wangapi walichukuliwa hatua za kisheria kulingana na makosa
hayo.
Na ni mikakati gani inafanywa
kuhakikisha wanakomesha kabisa suala la mimba mashuleni kwa wanafunzi
wengi wanapatiwa mimba na wazazi na jamii inaangali badala yake
wanamalizana kwa kupeana zawadi huko huko majumbani hali hiyo inayofanya
kuendelea kila mwaka.
“Juhudi kubwa inatakiwa kufanyika
ili kuhakikisha wale wote wanaohusika wanachukuliwa hatua kali za
kisheria kukomesha suala hili kwa kushirikiana wote viongozi wananchi,
serikali, jamii, wazazi, walimu na wanafunzi kwa nafsi yao kukomesha
suala la mimba kwa watoto wa kike mashuleni”alimaliza Mwanri.
Push Mobile, Channel Ten kutoa zawadi ya gari Valentine Day
Meneja
Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo
wakati wa uzinduzi wa shindano la kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu
ya wapendanao ‘ Valentine Day’ iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Kampuni
ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel
Ten na Redio Magic FM. Kushoto ni AFISA Masoko na Mauzo wa AMG, Prosper
Vedasto
………………………………………………………………….
KAMPUNI ya Push Media Mobile
itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya shs milioni 8 kwa
mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanoa
“Valentine Day” ikayoa adhimishwa Februari 14.
Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.
Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.
Rugambo alisema kuwa wameamua
kutoa zawadi kubwa hiyo ili kuwafanya wapendanao wegi kushiriki na
kupata nafasi ya kushinda. Alisema kuwa ili kuingia katika droo ya
shindano hilo, unatakiwa kutuma neno “Penzi” kwenda namba 15678 na
kujibu maswali mbali mbali yahusiyo masuala ya mapenzi na siku ya
Valentine.
“Hii ni promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile vile kuwazawadia wadau waokwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kujisha kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya shs milioni 1.5, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya shs 500,000 na Home theatre ya thamani ya shs 400,000 na Ipad.
Kwa mujibu wa Rugambo, lengo lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao kuwa kubwa kama nyingine kwani mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku.
Alisema kuwa mipango yao ni kuwekeza katika sikukuu hiyo ambayo jamii imeanza kuitilia mkazo japo si siku ya mapumziko kama sikukuu nyingine. Alisema kuwa kwa mwaka huu, wameweka bajeti ya shs milioni 30 ili kufanikisha zaoezi hilo.
“Hii ni promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile vile kuwazawadia wadau waokwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kujisha kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya shs milioni 1.5, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya shs 500,000 na Home theatre ya thamani ya shs 400,000 na Ipad.
Kwa mujibu wa Rugambo, lengo lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao kuwa kubwa kama nyingine kwani mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku.
Alisema kuwa mipango yao ni kuwekeza katika sikukuu hiyo ambayo jamii imeanza kuitilia mkazo japo si siku ya mapumziko kama sikukuu nyingine. Alisema kuwa kwa mwaka huu, wameweka bajeti ya shs milioni 30 ili kufanikisha zaoezi hilo.
MAKAMO MWENYEIKI CCM ZANZIBAR DK. SHEIN, AZUNGUMZA NA VIONGOZI OFISI KUU YA CCM KISIWANDUI
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisisitiza jambo alipokua akizungumza na Viongozi wa Tawi la
CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali
mbali za Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Mjini Zanzibar jana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya
kusalimiana na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisisitiza jambo alipokua akizungumza na Viongozi wa Tawi la
CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali
mbali za Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Mjini Zanzibar jana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya
kusalimiana na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(wapili kulia) akizungumza na Viongozi wa Tawi la CCM Afissi
Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali mbali za
Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
Zanzibar jana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana
na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(wapili kulia) akizungumza na Viongozi wa Tawi la CCM Afissi
Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali mbali za
Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
Zanzibar jana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana
na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali MohamedShein,akizungumza na Viongozi wa Tawi la CCM
Afissi Kuu ya CCMKisiwandui,wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbali mbali
za Chama hichokatika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
Zanzibarjana,Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimana
naViongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha
Mapinduzi,(CCM)(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali
Vuai,na (kushoto)Mwenyekiti wa Tawi Nadra Juma Mohamed.[Picha na
Ramadhan
Othman,Ikulu.]
36 WACHUKUA FOMU TFF, 18 WAREJESHA
Wakati kesho ndiyo mwisho wa
kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania
(TPL Board) waombaji 36 wameshachukua na 18 tayari wamesharejesha.
Idadi hiyo ni kufikia leo
mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF
inasisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa email wanatakiwa kuzituma
kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa email ya tfftz@yahoo.com na si kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.
Waombaji wanne walioongezeka
katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na Rukwa, Eliud
Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na Pwani), na Omari
Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha kamili ya waombaji ni
Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais) wakati
waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura, Ramadhan
Nassib na Wallace Karia.
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati
ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita),
Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara
na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu
(Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na
Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy
Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James
Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi na Zafarani Damoder
(Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na
Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki (Morogoro na
Pwani), Elias Mwanjala na Eliud Mvella (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed
(Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih
Dauda (Dar es Salaam).
Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu
(TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji
amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya
kuwania umakamu mwenyekiti.
ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA
Mwenyekiti
wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa
vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.
Foleni
ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa
vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa
kuanza Januari 20 mwaka huu.
Baadhi
ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la
Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo
wa soka jimboni kwake. (Picha zote na Nathaniel Limu).
……………………………………………………….
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa
mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9
vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua
vumbi januari 20 mwaka huu.
Vifaa
hivyo ni pamoja na jezi pea 854,mipira 122,soksi pea 854 na cloves za
magolikipa 61.Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi
ngazi ya kitongoji katika jimbo la Singida mjini.Baada ya ligi
hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.
Akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la
Singida mjini, Hamisi Nguli amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa
misaada mikubwa mbalimbali katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza
wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.
“Dewji
toka awe mbunge wa jimbo la Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi
na vijana. Amewasaidia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza
kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa ajili ya vijana wa bodaboda
watakaojiunga katika vikundi”,alisema.
Awali
msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni
mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza
kimaisha.
MKE WA RAIS NA MWENYEKITI WA TAASISI YA WAMA AFUNGA MKUTANO WA MAMA NA MTOTO LEO JAN 17,2013-ARUSHA
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya Dkt.Seif Rashid
(mwenye miwani) wakielekea kupanda ndege katika Uwanja wa ndege wa
kimataifa wa- JK- Nyerere jijini Dar es Salaam 16-jan 2013 kuelekea
Arusha kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya na Mtoto jan.
17,2013. Mkutano huo unawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje
ya nchi. (picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama
Salma Kikwete (mwenye kilemba) akisalimiana na wafanyakazi wa ndani ya
ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini
Dar es Salaam Jan 16,2013 wakati akielekea kufunga mkutano wa Masuala ya
Afya na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Mkutano huo
anawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi, (kulia) ni
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid. (Picha na Mwanakombo Jumaa-
MAELEZO).
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
Salma Kikwete(kulia) akiangalia vikundi vya sanaa ya ngoma mbalimbali
za utamaduni alipowasili katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha
Kilimnjaro (KIA) jan 16.2013 kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya
Afya ya Mama na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Aliengozana nae
wapili ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Arusha (UWT) Flora
Zelote (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Kikundi
cha kinamama cha ngoma ya Msanja kikitumbuiza katika mapokezi ya Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
salma Kikwete (hayupo pichani) kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa
Kilimanjaro (KIA ) Jan 16,2013.(Picha na Mwanakombo Jumaa wa
MAELEZO).
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Wanawake(WAMA) kulia, Mama Salma
Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa Arusha Magesa Mulongo (kushoto)
wakati alipowasil katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA)
Jan 16,2013.- Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John
Mongela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Jan
16,2013. –Picha na Mwnakombo Jumaa- MAELEZO.
………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Kauli mbiu ya kongamano la
ulimwengu la Afya ya uzazi linaloendelea jijini Arusha imepewa msisitizo
na kuwa hakuna mama atakayekufa wakati akileta kiumbe duniani na pia
Afya ya mama na mtoto ipewe kipaumbele.
Kauli hiyo imeendelea kutolewa na
Mke wa Rais mama Salma Kikwete wakati akiwasilisha na kuzungumza na
washiriki wa kongamano hilo jijini hapa na kuwataka watafiti na
wataalamu hao kuja na majibu yatakayosaidia kupunguza vifo vya
wakinamama wakati wa kujifungua.
Mama kikwete alisema kuwa takwimu
zinaonyesha kupungua kwa kiasi kidogo tatizo la kujifungua na kupoteza
maisha hapa nchini na kuwataka wataalamu humu nchini kuchukuwa uzoefu
walioupata kuchangia kupunguza vifo vya wamama wakati wa kujifungua
sanjari na watoto huku wajawazito zaidi ya 459 hufa kila mwaka wakati
wakijifungua.
“Asilimia 90% ya nchi
zilizoendelea wanaweza kupunguza ama kuokoa maisha ya kinamama na watoto
huku hapa nchini wakiandaa mpango endelevu wa kuokoa maisha ya
wamamawajawazito wakati wa kijifungua na kutoa rai kuwa wamama wasife
kwa magonjwa ambayo yanaweza kupatiwa tiba”alisema mama Salma.
Mama Salma alisema kuwa suala la
afya ya uzazi liwe mpango endelevu kwa serekali na asasi mbali mbali na
kuitaka serekali kulipa kipaumbele suala la afya ya mama na mtoto licha
ya majukumu mbali mbali iliyonayo.
Nae naibu waziri wa Afya na
maendeleo ya jamii hapa nchini Seif Raishid alisema kuwa serekali
kupitia wizara hiyo wameweka kipaumbele suala la mama afya ya uzazi na
kuwa hakuna mama atakaeyekufa wakati akiwa analeta kiumbe duniani
sanjari na watoto na wamejipanga kuongeza wigo wa kuwafikia wakinamama
kwa kuongeza zahanati kuwa karibu na usafiri sanjari na huduma muhimu.
Rashid akwataka watanzania
walioshiriki kongamano hilo kutoa uzoefu walioupata kutatua tatizo la
afya ya mama na watoto ilikupunguza vifo ambvyo vinawezekana kuepukika
kutokana na kukosa eidha huduma muhimu wakati wakujifungua.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
afya dkt dumilia chalamila alisema kuwa mkutano huo umewashirikisha
zaidi ya wataalam na watoa maamuzi zaidi ya 800 kutoka mataifa mbali
mbali ulimwenguni wakichangia uzoefu katika kulipatia ufumbuzi suala la
afya ya uzazi.
TANZANIA YAANZA RASMI KUTUMIA MFUMO WA KIMATAIFA WA UKAGUZI
NA GLADNESS MUSHI -ARUSHA
Tanzania imeanza kutumia rasmi mfumo wa kimataifa katika masuala ya ukaguzi wa ndani ambapomfumo huo utaweza kupunguza Viashiria mbalimbali vya ubadilifu wa fedha za umma
Hayo yamebinishwa leo na mkaguzi
mkuu wa ndani hapa Nchini Bw Mohamed Mtonga wakati akifungua mafunzo
kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika kanda ya kaskazini
Mohamed alisema kuwa mpango huo
wa ukaguzi kwa mfumo wa Kimataifa umeanza kutumika rasmi hapa nchini
July Mosi ambapo utaweza kutoa na kuonesha viashiria mbalimbali ambavyo
vinakwamisha shuguli za ukaguzi ndani ya Serikali kuu pamoja na
Serikali za Mitaa.
Alisema kuwa kupitia mfumo huo
mpya wa kimataifa wa ukaguzi wa ndani utaweza kuboresha na kuwafanya
wakaguzi wa ndani kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi tofauti na mfumo
uliokuwa hapo awali ambao ulikua hautoi fursa kwa wakaguzi wa ndani
Alifafanua kuwa hapo awali
wakaguzi wa ndani walikuwa wanashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana
na viashiria vya vitu mbalimbali kama vile rushwa na uhusiano baina ya
mkaguzi na mkaguliwa hali ambayo ilikuwa chanzo cha kukwamisha malengo
mbalimbali ya ukaguzi hapa nchini ingawaje ndani ya mfumo wa ukaguzi
kimataifa suala hilo halipo kabisa.
SHIRIKA LABUNI MBINU MPYA YA KUWAFUATILIA MAMA WAJAWAZITO KWA SIMU ILI KUPUNGUZA VIFO NYAKATI ZA KUJIFUNGUA
Na Gladness Mushi -Arusha
SHIRIKA la Jhpiego la jijini
Dar es saalam limefanikiwa kubuni aina mpya ya mradi ujulikao kama
Maisha ambapo mradi huo utaweza kutumia simu za mkononi kwa ajili ya
kufuatilia afya za mama wajawazito kwa malengo ya kupunguza vifo vya
wajawazito
Akiongea na
“Fullshangweblog”mjini hapa mapemajana Meneja mradi wa shirika hilo Dkt
Dunstan Bishanga alisema kuwa mradi huo wa maisha umeanza kutekelezwa
kwa mkoa wa Morogoro
Dkt Bishanga aliongeza
kuwa mradi huo una malengo ya kuhakikisha kuwa inapunguza vifo vya mama
wajawazito hapa nnchini lakini njia pekee ya kuwakutanisha wahudumu wa
afya pamoja na wajawazito ni simu za mkononi hasa kwa kuwapa wajawazito taarifa mbalimbali
Pia alisema kuwa Mradi huo ambao
kwa sasa umeanza kutumika katika Mkoa wa Morogoro lakini wanaendelea
kufanya tathimini mbalimbali za kuhakikisha kuwa unasambaa nchi nzima
kwani una uwezo mkubwa sana wa kuokoa maisha ya mama wajawazito
Hataivyo aliongeza kuwa mara
baada ya mkoa wa Morogoro kunufaika na mradi huo wataweza kwenda mikoani
ikiwa ni pamoja na kuongeza zaidi ubunifu zaidi ili kuimarisha zaidi
afya ya mama kwa manufaa ya Nchi nzima kwani vifo hivyo vinasababisha
sana Umaskini katika jamii.
Awali alisema kuwa suala la mama
wajawazito ni suala ambalo linatakiwa kuchukuliwa tahadhari kubwa sana
ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu sahihi za afya kutoka kwa wataalamu
hivyo nao wazazi wa kiume wana nafasi kubwa sana ya kufanya hivyo
Miss Demokrasia Tanzania- INAKUPA POLE SANA BW. ERASTO MAPUNDA KWA KUMPOTEZA MKE WAKO MPENDWA
Marehemu Judith Chikaka Mapunda enzi za uhai wake.
Mwili wa Judith Chikaka ukiwa umelazwa ndani ya Jeneza Pamoja na mwili wa marehemu Mtoto wake mchanga.
Marehemu Judith Chikaka
alifariki siku ya Jumapili ya tarehe 13/01/2012 katika Hospitali ya
Mwananyamala wakati alipofikishwa hapo kwa ajili ya kujifungua, kwa
bahati mbaya na mapenzi yake muumba alifariki kabla ya kujifungua.
Mume wa Marehemu Judith, Bwana Erasto Mapunda akiwa amembeba mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mkewe.
Baba mzazi wa marehemu Judith, Mzee Chikaka
Mama mzazi wa marehemu Mama Chikaka sakiwana majonzi makubwa baada ya kumpoteza mtoto wake kipenzi
Padre kutoka Parokia ya
Kigamboni akiendesha Ibada ya misa takatifu ya kumwombea Judith alale
kwa amani. Ibada hiyo ilifanyika nyumbani kwa Marehemu Judith maeneo ya
Kigamboni Kibada.
Baadhi ya viongozi wa CCM Temeke wakitoa rambi rambi zao.
Spika wa Bunge la wanafunzi wa chuo cha Ardhi akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bwana S. Nyambui akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanachama na chama chao kwa ujumla.
Mume wa marehemu Judith akiweka Shada la maua katika nyumba ya milele ya mkewe
Kushoto ni mwakilishi wa Familia
ya marehemu akipokea rambi rambi kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa
marehemu kutoka wizara ya Ardhi
Mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi upande wa michezo akitoa salamu zake kwa niaba ya wanamichezo wenzake.
Hii ndio nyuma ya milele ya marehemu Judith Chikaka Mapunda.
Marehemu Judith alizikwa jana katika makaburi ya Kibada maeneo ya Kigamboni, ameacha Mume na Mtoto mmoja.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEME MAHALI PEMA PEPONI.
AMIN.
SOKO LA BUGURUNI WAMUOMBA RAIS JAKAYA KIKWETE KUTEKELEZA AHADI YA KUJENGO SOKO
WAFANYABIASHARA
wa soko la Buguruni lililoko wilayani Ilala jijini Dar es Salaam
wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi yake kwa vitendo kwa
kuwajengea soko jipya wafanyabiashara hao kinyume chake watasitisha
kulipa ushuru.
Akizunguza na Mwandishi wa habari hizi kwa
niaba ya wenzake jijini, mmoja wa wafanyabiashara hao, Maulu Mali
alisema hawaamini kama serikali haina fedha za kujenga soko hilo.
Alisema wamefikia hatua hiyo
baada ya viongozi mbambali akiwemo Rais kushindwa kutekeleza ahadi zao
za kujenga soko hilo ambapo kwa uchakavu wa soko hilo inawafanya
washindwe kufanyabiasha zao kwa mafanikio.
Mali alisema hadi sasa wamechoka
kudanganywa hivyo ni vema wakasitisha kulipa ushuru hadi hapo
watakapohakikishiwa vingine tena kwa vitendo wala si kwa maneno.
Alisema hali ni mbaya katika
soko hilo haswa katika kipindi hiki cha mvua, bidhaa za wafanyabiashara
hao zinaharibika kutokana na kuvujiwa.
Alisema ndani ya soko hilo hivi
sasa kumejaa maji yaliyochanganyika na uchafu, baada ya mifereji kuziba
hali inayohatarisha afya zao na maradhi ya mlipuko.
Alipoulizwa Ofisa Masoko wa
wilaya hiyo, Athuman Mbelwa, kuhusu tatizo linalowakabili
wafanyabiashara hao, Mbelwa alikiri kuwa soko hilo liko katika hali
mbaya likifanana na kiota cha ndege.
BONDIA IDDY MNYEKE AJIFUA KUMKABILI SADIKI MOMBA FEBRUARI 14
Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA AU NA RAIS WA BENIN MHE BONI YAYI
Rais
Jakaya Mrisho akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa
Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam jana Januari 16, 2013
Rais
Jakaya Mrisho akimuaga Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa
Benin Mhe Boni Yayi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jana Januari 16, 2013
Rais
Jakaya Mrisho akimuaga Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa
Benin Mhe Boni Yayi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jana Januari 16, 2013
Rais
Jakaya Mrisho na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin
Mhe Boni Yayi wakiongea katika mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es
salaam leo Januari 16, 2013
Rais
Jakaya Mrisho akiandika jambo akiangaliwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
(AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam leo
Januari 16, 2013
MZEE MKAPA NA MZEE MSUYA WATOA MAONI
Rais
Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akifurahia jambo na Wajumbe wa Tume na
Sekretarieti ya Tume Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam
jana(Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo
Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika
uandishi wa Katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba na
kulia ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu Mwenyekiti wa
Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume Bw. Assaa
Rashid.
PICHA NAKATIBA TUME YA KATIBA
Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya jana (Jumatano,
Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji
Joseph Warioba.
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana
mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo
(Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo
Mstaafu jana jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika
uandishi wa Katiba Mpya.
Rais
Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na
Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu
jana (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na
uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
Rais
Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na
Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu
jana (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na
uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
MAOFISA WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL ARUSHA
Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es
Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda
cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri (wa pili kushoto), walipotembelea
Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa
ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho
mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es
Salaam, wakiangalia eneo ambapo maji yaliyotumika kiwandani yanachujwa
tayari kwa matumizi mengine, walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa ziara ya siku moja kujionea
shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Usalama,
wakitembelea mwishoni mwa wiki Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), cha Arusha, walipofanya ziara ya siku moja kujionea
shughuli mbalimbali za kiwanda hicho.
Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Usalama,
wakitembelea mwishoni mwa wiki Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), cha Arusha, walipofanya ziara ya siku moja kujionea
shughuli mbalimbali za kiwanda hicho.
Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es
Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda
cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri (wa pili kushoto), walipotembelea
Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa
ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho
mwishoni mwa wiki.
RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AZINDUA AWAMU YA KWANZA YA JENGO JIPYA LA HOSPITALI YA SHREE HINDU MANDAL JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasha mshumaa kama ishara ya uzinduzi wa
Awamu ya Kwanza ya jengo jipya na Awamu ya pili ya Hospitali ya Shree
Hindu Mandal ya jijini Dar es salaam leo katika Mtaa wa Nyanza, ambapo
huduma hiyo itapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali jijini na
kuongeza wigo wa utoaji huduma n kuongeza vitanda vya kulaza wagonjwa,
Hospitali ya Shree Hindu Mandalilianzishwa mwaka 1931 ikianza na
Zahanati anayeshuhudiatukio hilowa pili katikati ni Mwenyekiti wa
hospitali hiyo Bw Ramesh Patel.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa hoapitali hiyo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo leo.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi akimkaribisha Rais Jakaya
Kikwete ili kuzungumza na wafanyakazi wa hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal Bw. Ramesh Patel akielezea historia ya hospitali hiyo.
Rais
Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili
hospitalini hapo kwa ajili ya kuizindua, kushoto ni Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na Kulia ni Bw. Ramesh Patel
Mwenyekiti wa Hospitali hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi akizungumza na Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na Kulia ni Bw. Ramesh Patel
Mwenyekiti wa Hospitali hiyo.
Baadhi ya madaktari na wauguzi wakisubiri kuwasili kwa Rais Jakaya Kikwete
Baadhi ya madaktari na wauguzi wakisubiri kuwasili kwa Rais Jakaya Kikwete
Baadhi ya wauguzi na wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi , Madaktari ,
Wauguzi pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya Shree Hindu Mandal mara
baada ya kuzindua rasmi leo
Waziri Simba akabidhi vyerehani kwa wajane
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akimsikiliza
Gavana wa Lions Ukanda wa Uganda na Tanzania, Joseph Kiwanuka, wakati
alipomtembelea leo ofisini kwake akiwa na ujumbe wa watu watano.
Waziri
Simba akiangalia baadhi ya vyerehani viwili viliyotolewa na Lions kwa
ajili ya kuwasaidia wanawake wajane. Vyerehani hivyo ni kati ya 100
vitakavyotolewa na Lions kuwawezesha wanawake kujikimu kimaisha.
Waziri
Simba akimkabidhi mmoja wa wafaidi wa vyerehani vilivyotolewa na Lions
Bi. Jane Fuiko wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi zilizofanyika leo
ofisini kwa Waziri.
Gavana Kiwanuka akimkabidhi cherehani Waziri Simba kabla ya kumkabidhi mfaidika wa pili wa vyerehani hiyo Bi. Mariam Mohamed.
………………………………………………………………
Usu-Emma Sindila na Sakina Mfinanga
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba amekabidhi
msaada wa vyerehani viwili kati ya 100 vilivyotolewa kwa wanawake
wajane wa Mkoa wa Dar es Salaam ofisini kwake leo kutoka Taasisi ya
Lions Club,
Akizungumza
kwenye hafla fupi ya kukabidhi vyerehani hivyo, Gavana wa Lions Ukanda
wa Tanzania na Uganda, Ndg. Joseph Kiwanuka, amesema taasisi yao
imekuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii hasa wanawake na watoto,
kuboresha huduma za maji kwa kuchimba visima ambavyo huwasaidia wananchi
hasa wanaokaa sehemu zenye shida ya maji.
Amesema
Lions imekuwa ikisaidia watoto wenye matatizo ya moyo kuwapeleka nchini
India kwa ajili ya matibabu,kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu kwa kuwapeleka shule hasa zile za awali na wameanzisha
mkakati wa kuwaelimisha wanafunzi mashuleni kuhusu utumiaji wa madawa ya
kulevya ili watoto wasijihusishe na vitendo hivyo.
Kwa
upande wake Waziri Simba ameishukuru taasisi ya Lions kwa misaada
mbalimbali ambayo wamekuwa wakiisaidia jamii na zaidi kwa msaada huo wa
vyerehani kwa wajane kwa kuwa utawawezesha kujikwamua kimaisha wao
wenyewe, watoto na familia zao.
Aidha,
Waziri Simba amewapongeza Lions kwa kazi kubwa wanayofanya kupitia
mradi wao wa kuelimisha wanafunzi juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za
kulevya na kuongeza kuwa Serikali inafanya jitihada kuhakikisha kila
kata inakuwa na shule ili kusaidia kupunguza wimbi la watoto wasiojua
kusoma na kuandika.
UJUMBE KUTOKA JIJI LA MWANZA WATEMBELEA MANISPAA YA ILALA KUJIFUNZA MBINU ZA UKUSANYAJI MAPATO
Mstaiki
meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula na ujumbe wa kamati yake ya
fedha wametembelea halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa maagizo ya
Mhe.Waziri Mkuu kuja kujionea mbinu za kisasa za kukusanya mapato.
Mstaiki
Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa amewakaribisha
na kuwaeleza jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa akiueleza
ugeni huo kutoka jiji la Mwanza mambo mbalimbali jinsi walivyoweza na
wanavyoendelea kukusanya mapato.
Mtahiki
Meya wa Ilala Mhe Jerry Silaa akiwa na ugeni huo kutoka jiji la Mwanza
katika kikao kilichozungumzia mbinu za ukusanyaji wa mapato.
MFANYAKAZI WA NDANI AJINYONGA TABATA MARAKUDA
Mwili
wa mwanadada ambaehatukulipata jina lake mara moja unkichukuliwa na
Polisibaada ya kujinyonga katika eneo la Tabata Barakuda jijini Dar es
salaam bado haijafahamika ni chanzo cha kujinyongwa kwake,taarifa zaidi
zinasema msichana huyo alikuwa akifanya kazi za ndani (House Girl) Picha
kwa hisani ya www.tzdadaz.blogspot.com.
Hapa
mwili ukitolewa na Polisi katika chumba alichojinyongea katika eneo la
Tabata Barakuda jijini Dar es salaam bado haijafahamika ni chanzo cha
kujinyongwa kwake
SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTEKELEZA MPANGO WA MIRADI WA AFYA YA MAMA
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi
……………………………………………………………………….
Na Gladness Mushi -Arusha
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
SERIKALI kwa kushirikiana
na wadau inaendelea kutekeleza mpango wa miradi ya miaka mitano wa
kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga wakati wa kujifungua na walio
chini ya miaka mitano ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma ya mama na mtoto na kuokoa maisha yao.
Hayo yameelezwa na Daktari bingwa
wa akina mama na watoto wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ,Dk Koheleth
Winani, kwenye kikao cha pamoja na baadhi ya wakuu wa mashirika
mbalimbali wanaohudhuria mkutano mkuu wa kimataifa wa afya ya mama na
mtoto, wanaoshirikiana na serikali kutekeleza mpango huo wa kupunguza
vifo vya mama na watoto nchini walipokuwa wakitoa ufafanuzi wa maswala
mbalimbali kwa wanahabari.
Dakta Winani, amesema 75% ya
watanzania wanaishi vijini ambako hawapati huduma zilizo bora wakati wa
kujifungua kutokana na umbali na maeneo mengine kutopitika hasa wakati
wa maska kutokana na miundo mbinu duni na kusababisha wajawazito
kujifungulia majumbani au wengine kupoteza maisha wakati wakipelekwa
kwenye Hospital , Vituo vya afya na Zahanati..
Amesema kuwa mpango huo unalenga
kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito na watoto 500 mwaka 2000 hadi
kufikia 19 ifikapo mwaka 2015 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo
ya Milenium, na kusisitiza kuwa ushirikiano kati ya serikali na wadau
hao ni muhimu kwa kuwa serikali peke yake haiwezi kutekeleza mpango huo
kwa ufanisi.
Kwa upande wake daktari Dustan
Bishanga, ambae ni mkurugenzi wa mradi wa Maisha unaofadhiliwa na
,shirika la misaada la Kimarekani, USAID , kwa kipindi cha miaka mitano
kuanzia mwaka 2008 kwa thamani ya Dola milioni 40 umeboresha huduma ya
afya ya mama na mtoto mchanga.
Dakta Bishanga, amesema mradi
umetengeneza mwongozo unaotumika na wadau wengine kutekeleza mradi hiyo
,pia mradi huo unatengeneza mitaala ya kufundishia watoa huduma kwa
kushirikiana na wizara ya afya ili kutoa mafunzo na uratibu wake katika
vituo tofauti tofauti vipatavyo 250 nchini kote Tanzania bara na
Zanzibar lengo ni kuboresha huduma ya mama na mtoto mchanga na kuokoa
maisha
HABARI ZA UA MIGUU TFFCHAGUZI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA W
WATATU WACHUKUA FOMU ZA URAIS TFF
Wadau watatu wa mpira wa miguu
wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitosa katika uchaguzi huo
utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30.
Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa
wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile
zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua leo (Januari 16 mwaka
huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne
Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA),
Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.
Mwengine aliyechukua leo ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias
Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha
Kanda ya Iringa na Mbeya.
Orodha kamili ya wadau
waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal
Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan
Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais).
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati
ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita),
Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara
na Mwanza).
SERIKALI KUFUATILIA MAENDELEO YA MIRADI INAYOZINDULIWA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU
Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza kwa wajumbe
wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kuhusu
serikali kufuatiliaji maendeleo ya miradi inayozinduliwa wakati wa mbio
za Mwenge mjini Zanzbar.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ali Nassoro Lufunga akizungumza na viongozi na
waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu
maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013.Mkoa wa shinyanga
ulikuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa mwaka 2012.
…………………………………………….
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Zanzibar.
Serikali inaandaa utaratibu wa
kufuatilia maendeleo ya miradi yote inayozinduliwa wakati wa mbio za
Mwenge wa Uhuru ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakua endelevu na
kuwanufaisha wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Zanzibar na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel wakati akitoa tathmini ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2012 na
maendeleo ya miradi iliyozinduliwa wakati wa mbio hizo kwenye mkutano wa
viongozi na waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Amesema serikali ina wajibu wa
kufuatilia kwa karibu miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2012
katika Halmashauri za wilaya, manispaa na Miji ili kuhakikisha kuwa
gharama kubwa iliyotumika wakati wa uanzishaji na ujenzi wa miradi hiyo
inawanufaisha wananchi kutoka kizazi kimoja hadi kingine ili kutunza
hadhi na heshima ya Mwenge wa Uhuru.
Amesema mbio za Mwenge wa uhuru
zimezindua miradi mingi nchini yenye thamani ya mabilioni ya fedha na
kuongeza kuwa si dhamira ya serikali kuona kuwa mwenge wa uhuru
unatumika tu kuzindua miradi ya maendeleo bali kuhakikisha uendelevu wa
miradi hiyo.