TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, November 13, 2015

WANACCM WALIOCHUKUA FOMU KUWANIA USPIKA WA BUNGE

Idadi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uspika na Unaibu Spika katika Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) linalotarajiwa kuanza wiki ijayo, inazidi kuongezeka na hapa ni majina 21 ya ambao wameshachukua fomu hizo, kadiri ya taarifa ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib.

STARS KAMILI KUWAVAA MBWEHA WA JANGWANI

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Algeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mkwasa amesema wamejiandaa kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo, wanajua Algeria ni miongoni mwa timu bora Afrika, lakini hilo halitawazuia kuibuka na ushindi.

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO AFANYA ZIARA BASATA,TBC NA TSN.


 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(wa kwanza kushoto) akiangalia mitambo ya kurushia matangazo ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) wakati alipofanya ziara ya kikazi katika minara ya shirika hilo leo hii  Kisarawe.Profesa Elisante amefanya ziara katika Taasisi tatu zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Baraza la Sanaa Tanzabia (BASATA),Tanzania Standard Newspapers(TSN) na Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) lengo likiwa ni kufahamiana na wafanyakazi,kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kujua changamoto zinazowakabili ikiwa ni kutimiza kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya awamu ya Tano.Anaefuatia ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw.Clement Mshana.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiangalia tofauti ya santuri ya  zamani na flashi ya kisasa  zinavyozidiana ukubwa kwa umbo alipotembelea maktaba mojawapo katika ofisi za shirika la utangazaji Tanzania (TBC) alipofanya ziara kuongea na menejimenti ya shirika ilo leo jijini Dar es Salaam.Santuri zilitumika kipinda shirika hilo likiitwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (waliosimama watatu kulia) akiwa katika mojawapo ya studio za kurushia matangazo ya shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wwakati alipotembelea shirika ilo leo kuongea na menejimenti yake pamoja na kuona utendaji wake.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (aliyekaa mwenye miwani) akipata maelekezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mtumishi wa Standard News Papers(TSN) leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi na kuangalia utendaji wa kazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(wa pili kulia) akiangalia moja ya kazi za vijana wanojifunza kutengeneza batiki na kuweka chapa alipotembelea ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) leo hii jijini Dar es Salaam.

Wednesday, November 11, 2015

LIGI KUU ZANZIBAR YAANZA ‘KICHAKANI’, MAFUNZO WACHEZEA KICHAPO CHA JKU

Na Salum Vuai, ZANZIBAR

KUFUATIA uwanja wa Amaan kuzuiwa kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya soka Zanzibar bila kuelezwa sababu za msingi, ligi hiyo iliyochelewa imelazimika kuanza jana katika uwanja wa kijiji cha Bweleo umbali wa takriban maili 15 kutoka mjini Zanzibar.
Kwa kuwa uwanja huo si rasmi na hauna uzio wala huduma muhimu ikiwemo vyoo, waandaaji wa ligi hiyo, kamati ya muda ya ZFA wamejikuta wakipata hasara kwani hakuna kiingilio cha fedha kilichowekwa kwa watazamaji.
Na katika mchezo wa ufunguzi jana, JKU makamu bingwa msimu uliopita, waliilaza Mafunzo mabao 2-1.
Kamisaa wa mchezo Ramadhani Ibada Kibo, akiwaongoza waamuzi wa mpambano huo kurudi uwanjani kuanza kipindi cha pili, baada ya kupumzika katika kichaka pembezoni mwa uwanja.  

Mafunzo ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo na wawakilishi wa Zanzibar kweli Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, wakati JKU watashiriki Kombe la Shirikisho.

TOTO AFRICANS WAAMUA ‘KUTEMBEZA BAKULI’ KWA WANACHAMA WAKE

Na Philipo Chimi, MWANZA
KLABU Toto Africans ya Mwanza imeandaa mkutano maalum kwa wanachama wake kwa ajili ya kufanya harambee kuchangia timu hiyo iweze kushiriki vyema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 Mwenyekiti wa klabu hiyo, Godwine Aiko amesema kwamba wameandaa mkutano huo kufuatia hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili timu.
Amesema timu inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka ili kunusuru mwendo wake mbovu katika Ligi Kuu.
“Tumeandaa mkutano huo ambao utafanyika siku ya Novemba 22 kwa ajili ya kufanya mipango kuona namna gani timu inapata fedha,” amesema na kuongeza. 

Ratiba ya Kombe la Challenge 2015 kama ilivyotolewa na CECAFA



MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Ramadhani Mgunda ameteuliwa kuwa Msaidizi namba moja wa Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden' katika kikosi cha timu ya Tanzania Bara, 'Kilimanjaro Stars' kitakachoshiriki michuano ya CECAFA Chellenge baadaye mwezi huu mjini Addis Ababa, Ethiopia.

DK. KIMEI AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA SIHA SANGO

KAMERA YETU NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

VYOMBO HABARI VIMECHANGIA KUFANYA UCHAGUZI KUWA WAZI NA HAKI NA HURU –NEC

KIINGILIO CHA KUITIZAMA MECHI KATI YA STARS NA ALGERIA 5000

THANKSGIVING HOUSTON, TX PARTY - 2 More weeks

‘Marufuku kutumia ramani ya Tanzania isiyo sahihi’

Bunge jipya, mzigo zaidi

JESHI LA POLISI LAANZA KUTOA ELIMU KWA ABIRIA NA MADEREVA ILI KUKABILIANA NA AJALI KATIKA KIPINDI CHA MWISHO WA MWAKA

Mkurugenzi wa habari Ikulu afungasha virago

Dk. Shein, Maalim Seif wateta Ikulu Z'bar. NA MWINYI SADALLAH

VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UBAKAJI WATOTOTO WILAYA YA TEMEKE VYAONGEZEKA

JIJI LA MBEYA LAJIPANGA KUKUSANYA KODI KATIKA MRADI WA SOKO JIPYA LA MWANJELWA

KAIMU MKURUGENZI MPYA AANZA KAZI, AKUTANA NA WATENDAJI MUHIMBILI

World Bank Group: Evaluation Officer, Washington DC

JOB OPPORTUNITY

The Independent Evaluation Group (IEG) is the organizational unit in the World Bank Group (WBG) providing evaluation and feedback on the development effectiveness of Bank Group activities in client countries.
They are currently recruiting 3 Evaluation Officers (GF) VIEW HERE under two streams i.e.:

  • Human Development: social protection, health and nutrition, and/or education. (1 position) 
  • Sustainable Development: sustainable development, including Infrastructure (water, transport), environment, agriculture. (2 positions) Under the direction of the Unit Manager, the Evaluation Officer will contribute directly to IEG evaluations. This work will include conducting project-level validations and evaluations (at least 50% of the annual work program will be dedicated to this), contributing to larger thematic, sectoral and corporate evaluations, overseeing contributions from consultants, contributing to budget and team oversight, and commenting on the work of others. 

SERIKALI IMEOMBWA KUINGILIA KATI SAKATA LA FAMILIA YA JUMA ISANGU, ARUMERU


 Mkazi wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Juma Isangu akiwa na mkewe Janet Tinai pamoja na mwanao, Issa Juma (katikati) wakiangalia nyaraka mbalimbali nje ya nyumba yao mara baada ya kufukuzwa na kisha kuvunjiwa nyumba yao wilayani humo na kampuni ya Majembe Auction Mart kwa amri ya mahakama.
Mkazi wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Janet Tinai akilalamika mbele ya waandishi wa habari akiwa na baadhi ya vyombo vyake  mara baada ya kuhamishwa kwa amri ya mahakama na kampuni ya Majembe Auction Mart.

NIKO TAYARI KUKAMATWA, MAALIM SEIF

  Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

By Hassan Ali, Mwananchi, Mwananchi Zanzibar. 

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema yuko tayari kukamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka, kama kitendo chake cha kujitangazia ushindi ni kosa.

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII JIJINI MONTREAL, CANADA YAFANA

JASIRI WA WANASHERIA WASAIDIA KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI WA JINSIA SOKO LA TABATA MUSLIM JIJINI DAR ES SALAAM Posted:

 Katibu wa soko la Tabata Muslim lililopo Manispaa ya Ilala, John Nombo (kushoto),  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG), kutoa mafunzo ya kupinga ukatili huo katika masoko sita ya Manispaa hiyo. Kulia ni Mwezeshaji wa Sheria wa Soko hilo, Aisha Juma na  Saada Ngunde.

Tuesday, November 10, 2015

WIZARA YA AFYA, WHO WAENDESHA SEMINA KUHUSU UGONJWA WA KIPINDUPINDU HOTELI YA NEW AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
 Ofisa Habari wa Wizara ya Afyaaaa na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kulia), akibadilishana mawazo na mwenzake katika semina hiyo.

BODI YA MIKOPO YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII


BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016

BODI  ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuutaarifu umma kuwa kuna taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016. Taarifa hizo si za kweli na hivyo Bodi inauomba umma kuzipuuza.

KAMPUNI YA TTCL YAWASAIDIA WATOTO VIFAA VYA MASOMO KITUO CHA AWALI LUKEMA VINGUNGUTI



Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services baadhi ya vibao maalumu kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi wa darasa la awali.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services baadhi ya maboksi ya chaki kwa ajili ya kufundishia watoto wa darasa la awali ikiwa ni sehemu ya msaada kukisaidia kituo hicho. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi. Kulia pembeni ni Ofisa Uhusiano wa TTCL Amanda 

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI DKT. KIJO-BISIMBA NA KUKAGUA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akimjulia hali Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt. Helen Kijo-Bisimba aliyelazwa katika Hospitali ya Agha Khan mara baada ya kupata ajali mbaya ya gari katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jana.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli katikati akitoka kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika Taasisi ya Mifupa MOI kujionea halihalisi ya utoaji huduma kwa wagonjwa katika taasisi hiyo.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATANGAZA MFUMUKO WA BEI WA MWEZI OKTOBA, 2015

Na Veronica Kazimoto
09/11/2015
Dar es Salaam.

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 mwezi Septemba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo amesema kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei kumesababishwa na kupanda kwa bei za bidhaa na huduma zingine za kijamii ikiwemo chakula na nishati.

“Kupanda kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2015 kumechangiwa na ongezeko la bei za vyakula kama vile Mchele ambao umeongezeka bei kwa asilimia 0.8, unga wa muhogo umeongezeka hadi asilimia 0.7, nyama kwa asilimia 0.8, samaki kwa asilimia 5.5, ndizi za kupika asilimia 0.7 na choroko kwa asilimia 0.9”, amesema Kwesigabo.

Bidhaa zisizokuwa za vyakula kama vile vitambaa kwa ajili ya nguo za kike zimepanda kwa asilimia 1.6, viatu vya kiume asilimia 1.1, mkaa asilimia 1.4 na gharama za kupata ushauri kwa daktari pia zimepanda hadi kufikia asilimia 1.4.

Kwa upande Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.1 ambao ni ongezeko sawa na mwezi Septemba, 2015. Fahirisi za bei pia zimeongezeka kutoka 159.04 hadi kufikia 159.17 kwa mwezi Oktoba, 2015.

“Fahirisi za bei za vyakula vya nyumbani na migahawani iliongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 10.0 kutoka asilimia 9.4 kwa mwezi Septemba, 2015 ambapo bidhaa zisizokuwa za vyakula zimepungua kidogo kutoka asilimia 1.9 hadi asilimia 1.7 kwa mwezi Oktoba, 2015,” amefafanua Kwesigabo.

Kwesigabo amesema kuwa Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa mwezi Oktoba, 2015 umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 2.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwezi Septemba, 2015.

Mwisho. 

 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akizungumza na waandishi wa habari  leo Jijini Dar es Salaam Kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 ambao umepanda hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwezi Septemba, 2015.