Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu anayemaliza muda wake, Salvatory Rweyemamu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ,Kushoto ni Mwandishi wa habari Msaidizi wa Ikulu, Premy Kibanga. Picha na Ikulu
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu amemaliza mkataba wake na kuondoka huku akiwashukuru watendaji kwa muda wote aliokuwa nao wakimsaidia Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete. Kuondoka kwake kunampa fursa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kuunda safu mpya ya Kurugenzi ya Mawasiliano. Salva aliteuliwa, kwa mara ya kwanza, na Rais Kikwete kushika wadhifa huo Septemba 17, 2007 na alimaliza mkataba wake Septemba 11, 2015 lakini aliongezewa hadi Novemba 10. Baada ya Dk Magufuli kuapishwa Novemba 5, Rais Kikwete aliondoka siku iliyofuata kurudi nyumbani kwao Msoga, Chalinze, na kwa kuwa Salva amemaliza pia muda wa nyongeza ameondoka na kurudia majukumu yake ya awali. Kabla ya kuteuliwa kusimamia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Salva alikuwa mmoja wa wamiliki na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Habari Corporation (sasa New Habari Corporation). |
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, November 11, 2015
Mkurugenzi wa habari Ikulu afungasha virago
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment