Idadi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uspika na Unaibu Spika katika Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) linalotarajiwa kuanza wiki ijayo, inazidi kuongezeka na hapa ni majina 21 ya ambao wameshachukua fomu hizo, kadiri ya taarifa ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib.
- Aliyekuwa Naibu Spika katika Bunge la 10 na Mbunge mteule wa Kongwa, Job Ndugai
- Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Tulia Arkson
- Aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi
- Aliyewahi kuwa Spika na Waziri, Samuel Sitta
- Mbunge mteule wa Chato, Dk Medard Kalemani
- Diwani wa Goba jijini Dar es Salaam, Mwakalika Watson
- Julius Pawatila
- Agnes Makune
- Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Ali Hassan Mwinyi
- Naibu Waziri, Ritha Mlaki
- Mhitimu wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 28, Veraikunda Urio
- Aliyekuwa Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes
- Aliywania nafasi ya Urais wa JMT kupitia CCM, Dk Kalokola Muzzamil.
- Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi
- Aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo
- Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu
- Mbunge wa zamani wa Afrika Mashariki, George Nangale
- Simon Rubugu
- Banda Sonoko
- Leonce Mulenda
- Mbunge mteule wa Kasulu Mjini Daniel Nswanzungwanko
- Mbunge mteule wa Ilala Mussa Hassan Zungu
No comments:
Post a Comment