TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, September 19, 2014

WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WATAALAM WA UTAFITI WA HALI YA UMASIKINI WA KAYA TANZANIA.

 Naibu Waziri wa Fedha –Sera, Mhe. Mwigulu Nchemba akifungua mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera akiwakaribisha washiriki wa mafunzo ya wiki 3 ya utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya mwaka 2014/15 mkoani Morogoro.
 Washiriki wa mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, wasimamizi na wadadisi kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar  watakaoendesha utafiti wa kufuatilia hali ya umasikini katika kaya nchini mwaka 2014/15 yanayofanyika mkoani Morogoro wakifuatilia masuala mbalimbali . 
==============================================
 
WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WATAALAM WA UTAFITI WA HALI YA UMASIKINI WA KAYA TANZANIA.
Na. Mwandishi wetu – Morogoro.
19/9/2014.

Serikali imewataka wananchi na viongozi wa maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano kwa wadadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu watakaoendesha  zoezi la utafiti wa ukusanyaji  wa takwimu za kufuatilia hali ya umasikini katika  kaya kwa mwaka 2014/2015, utaokaofanyika  kuanzia Oktoba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa jana mkoani Morogoro na Naibu Waziri wa Fedha –Sera, Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akifungua mafunzo ya wiki tatu ya wakufunzi, Wasimamizi na wadadisi watakaoendesha utafiti huo kutoka Tanzania Bara  na  Zanzibar.

Amesema serikali  kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa upande wa Bara na ile ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar  imeamua  kufanya utafiti huo ili kupata takwimu bora na sahihi zitakazoiwezesha kujitathmini na kupima juhudi zake katika kuwaletea wananchi maendeleo, kukuza uchumi na kupunguza umasikini wa kipato.

Amesema utafiti huo  pamoja na tafiti zilizopita utaiwezesha serikali kuchambua kiundani sababu zinazofanya kaya nyingi nchini kuendelea kubaki kwenye umasikini,  baadhi kutoka kwenye  umasikini na nyingine kuingia kwenye umasikini.

“Kufanyika kwa utafiti huu kutatuwezesha kufahamu namna na sababu zinazofanya kaya kuendelea kubakia kwenye umasikini , baadhi ya kaya kutoka kwenye umasikini na nyingine  kuingia kwenye umasikini” Amesema.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa utafiti huo kutaiwezesha serikali kuelewa kwa kina changamoto zinazoikabili katika utekelezaji wa Sera, mikakati na programu mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.

Mhe. Mwigulu amefafanua kuwa Serikali itaendelea kuiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuijengea uwezo ili iweze kukamilisha tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika nchini kwa kufikisha matokeo ya tafiti hizo katika ngazi zote za utawala.

“Nia yetu ni kuhakikisha kuwa mipango ya maendeleo ya wananchi inapangwa kwa kutumia takwimu rasmi, kwa upande wetu serikali takwimu rasmi ni masikio  na macho katika utendaji wa kazi za kilia siku” Amesisitiza Mh. Mwigulu.

Aidha, amewataka wakufunzi, wasimamizi na wadadisi watakaoendesha zoezi hilo walio kwenye mafunzo hayo kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yote watakayopita kuhusiana na umuhimu wa zoezi hilo kwa taifa  na kusisitiza kuwa serikali haitawavumilia wadadisi watakaokiuka maadili katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema  kuwa washiriki wa mafunzo hayo watakaofaulu wataruhusiwa kushiriki katika utafiti huo.

Amesema kuwa utafiti huo hufanyika  kila baada ya miaka 2  kwa kuzipitia kaya binafsi ambazo huhojiwa kwa vipindi tofafuti ili kupata ufahamu wa namna ambavyo kaya zinaingia na kutoka kwenye hali ya umasikini wa kipato na sababu zinazochangia hali hiyo.

Ameeleza kuwa kwa mwaka huu utafiti huo utakuwa wa nne  kufanyika hapa nchini ukitanguliwa na zile zilizofanyika mwaka 2008/09, 2010/11 na 2012/13.

Amefafanua kuwa madodoso ya utafiti huo yatafuatilia na kukusanya taarifa muhimu za sekta nyingine muhimu ambazo zinaweza kuchambuliwa kwa  kuhusishwa  na hali ya umasikini zikiwemo kilimo, uvuvi, mifugo, Afya, Ajira na Upatikanaji wa huduma za maji, umeme, afya na elimu.

Amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu itahakikisha  takwimu hizo zinasambazwa katika ngazi zote za utawala kwa ajili ya kutumika  kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera awali akizungumza wakati wa kuwakaribisha washiriki wa mafunzo hayo mkoani Morogoro amesema kuwa bila takwimu sahihi hakuna mipango ya maendeleo inayoweza kufanyika.

Amesema kuwa kukamilika kwa utafiti huo  kutatoa picha halisi ya nini kifanyike katika kuwaletea maendeleo wananchi.
 
 

PPF YAWANOA WAAJIRI KUHUSIANA NA HUDUMA ZAKE MPYA IKIWEMO PPF TAARIFA APP

Prof. Betria Mapunda ambae amemwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es salaam akifungua semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Waajiri kwa lengo la Kutoa elimu juu ya huduma zitolewazo na mfuko huo wa Pensheni wa PPF katika ukumbi wa Seaescape, Uliopo Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa akitoa mada wakati wa semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Penhsheni wa PPF kwaa Waajiri wa Makampuni na mashirika mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Seaescape, Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam leo.
Majaliwa E Mkinga, Mchambuzi na Mtengenezaji wa Mifumo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akielezea jinsi PPF ilivyotengeneza mfumo wa kupata taarifa za wanachama kupitia simu aina za Smartphone na kuutaja mfumo huo kuwa ni PPF TAARIFA App ambayo mteja ataweza kuiweka katika simu yake ya mkononi.
Baadhi ya waajiri wakielekeza kuhusu jinsi ya kuweka mfumo wa PPF Taarifa katika simu zao za Smartphone leo katika semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Seascape hotel Mbezi beach Jijini Dar Es Salaam.

MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMAJARO (KINAPA).

 Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 wametembelea hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) na kujifunza mambo mengi kuhusiana na hifadhi hiyo ya mlima kilamanjaro. Pichani ni warembo hao wakipiga picha na mdau mkubwa wa masuala ya urembo mkoani Kilimajaro, Athena Mawalla wa mgahawa wa Meku's Bistro wakati warembo hao walipomtembelea wakiwa njiani kwenda KINAPA.
 Warembo wakiwa katika gari njiani kuelekea KINAPA. 
 Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Hidan Rico (kulia) akitoa maelekezo baada ya kufika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimajaro.
 Warembo wakipanda kuelekea geti kuu la kupandia Mlima Kilimanjaro.
 Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.
 Eliud Bemba ambaye anaongoza timu ya utayarishaji Vipindi maalum vya warembo hao kutoka True Vision akichapa picha na walimbwende.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Erastus Lufungulo akitoa maelezo ya mlima huo kwa warembo wa Miss Tanzania.

Thursday, September 18, 2014

BASI LATUMBUKIA MTO PANGANI BAADA YA KUFELI BREKI

mwaka huu majanga basi lanusurika kuzama mto pangani Kwenye kivuko cha mv pangani baada ya kufeli break jana asubuhi majeruhi dereva peke yake

Wednesday, September 17, 2014

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WATIMIZA MIAKA 15 TOKEA KUANZISHWA KWAKE.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari- Maelezo, Bw Assah Mwambene akizungumza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na Viongozi wa Mfuko wa Hifadhi wa Pensheni wa PSPF mapema leo katika Ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa pensheni wa PSPF, Bw Adam Mayingu akizungumzia mafanikio ya mfuko wa PSPF katika kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa JB Belmonte Jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mh Adam Mayingu (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo, Mh Assah Mwambene leo katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo wakati Mkurugenzi mkuu wa PSPF alipokuwa akizungumzia mafanikio ya PSPF ndani ya miaka 15 tokea kuanzishwa Kwake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na wanahabari waliohudhuria mkutano kati ya Waandishi wa habari na Mfuko wa Pensheni wa PSPF uliolenga kuelezea mafanikio ya mfuko huo ndani ya Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake.
Mmoja wa Waandishi wa Habari akiuliza swali wakati wa Mkutano kati ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF na waandishi wa habari uliofanyika leo Katika ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es salaam, Mkutano huo ulilenga kueleza mafanikio yaliyopatikana kwa Kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwa mfuko huo wa PSPF.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

MJAMZITO AOKOLEWA KATIKA TUKIO LA WATU ZAIDI YA 600 KUHOFIWA KUZAMA NDANI YA MAJI. MASUALA YA KIJAMII.


Moja ya boti zilizowabeba wahamiaji haramu kutoka Afrika kuelekea Ulaya kupitia Bahari ya Mediterenia.

Muda mchache baada ya taarifa za kuzamishwa kwa boti iliyobeba zaidi ya wakimbizi 700 kwenye bahari ya Mediterania kuibuka, boti nyengine mbili zimezama Libya na kusababisha vifo vya watu 70.

Msemaji wa kikosi cha ulinzi wa pwani cha Libya, Qaasim Ayoub, ameliambia shirika la habari la AP kwamba waokoaji wanaendelea kuopoa miili inayosukumwa na mawimbi umbali wa kilomita 18 kutokea wilaya ya Tajoura mjini Tripoli. Aliongeza kwamba wahamiaji 36 wa Kiafrika, wakiwemo wanawake watatu - mmoja wao akiwa mjamzito wameokolewa.

Kamanda wa kikosi cha Walinzi wa Pwani cha Libya, Ali Sarti, amesema boti za doria zimewaokoa wahamiaji waliokuwa kwenye boti iliyokwishavunjika katikati ya bahari

"Vikosi vyetu vya doria vilikuwa baharini jana na kugundua boti iliyovunjika na kuharibika katikati ya bahari. Kulikuwa na wahamiaji wamelala kwenye boti hiyo baada ya kuzama na waliokolewa. Waliookolewa ni watu 36 miongoni mwa wahamiaji 97, kwa mujibu wa wahamiaji wengine, wakiwamo wanawake na watoto," alisema Sarti.

Miongoni mwa waliookolewa ni kijana mmoja wa kiume, ambaye licha ya kuwa na sura ya Kiafrika, anazungumza Kiarabu fasaha, na hivyo kuzua wasiwasi ikiwa kweli wahamiaji hao ni wale wanaootokea kusini mwa jangwa la Sahara pekee, au hata nchi za Kiarabu kaskazini mwa Afrika.

"Kulikuwa na matatizo kwenye boti, mulikuwa na watu 105, 36 tu ndio waliopona na 70 wamekufa. Kisha boti ya polisi ikaja kutoka baharini na kuwaokoa watu 36, wanawake watatu na mtoto mmoja walikufa," alisejma kijana huyo.
Watu 700 wahofiwa kufa maji
Boti za msako katika pwani ya Italia.

Taarifa ya maafa haya inakuja muda mchache baada ya kuibuka kwa habari za ajali nyengine mbaya kabisa kuwahi kutokea katika siku za karibuni, ambapo wahamiaji wanaokisiwa kufikia 700 wamekufa maji.

Shirika la Wahamiaji Duniani (IOM) limesema ikiwa ripoti zinazotolewa na manusura wa ajali hiyo iliyotokea Jumatano iliyopita karibu na Malta, zitakuwa za kweli, basi mkasa huu hautachukuliwa kama ajali, bali mauaji ya maangamizi yanayofanywa na wahalifu wanaoratibu safari hizo za hatari kwa wakimbizi wanaotaka kuingia barani Ulaya kwa njia ya bahari.

Manusura wawili wa Kipalestina ambao waliokolewa siku ya Alhamisi, wameliambia shirika hilo la wahamiaji kwamba kiasi cha abiria 500 walikuwa kwenye chombo kimoja ambacho kiliharibiwa kwa makusudi na wasafirishaji haramu.

Kwa mujibu wa manusura hao, wahamiaji kutoka Syria, Palestina, Misri na Sudan waling'oa nanga kutoka mji wa Damietta, Misri, tarehe 6 mwezi huu, na kulazimishwa kubadilisha boti mara kadhaa wakati wa safari yao kuelekea Ulaya.

Wasafirishaji hao haramu ambao walikuwa kwenye boti nyengine, waliwaamuru kuingia kwenye boti ndogo zaidi lakini walikataa kwa kuwa walihofia kuzama, na hapo ndipo wasafirishaji walipoitoboa boti kubwa waliyokuwamo hadi

Benki ya Exim yaingia ubia kuongeza ufanisi katika udhibiti wa majanga

 Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka na Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
 Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (watatu kulia) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (wapili kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
 Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (kushoto) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM)
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde, Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (wapili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho (wakwanza kushoto) na Mwakilishi toka Hymans Robertson  Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto)

BENKI ya Exim Tanzania imeingia ubia na kampuni ya StraitsBridge Advisors (SBA) ya nchini Singapore, kampuni itoayo huduma za kifedha kwa ajili ya kutoa huduma ya kitaalam katika masuala ya udhibiti wa majanga ijulikanayo kama Enterprise – Wide Risk Management (ERM), itakayoiwezesha benki hiyo kuongeza ufanisi katika udhibiti wa majanga. 

Akizungumza katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala alisema, ili Benki ya Exim iongeze ufanisi katika eneo la udhibiti wa majanga imesaini makubaliano na kampuni ya SBA ambayo itashirikiana na kampuni ya Hymans Robertson (H&R) ya London kuipa benki ujuzi mkubwa dhidi ya majanga inayokutanayo na kutumia fursa mbali mbali zinazojitokeza kibiashara.

Alisema kuwa ikiwa inazaidi ya miaka 92 ya uzoefu katika utoaji huduma hizo, Hymans Robertson ikishirikiana na SBA itaisaidia benki kuongeza ufanisi wake katika eneo la udhibiti wa majanga yaani Enterprise-Wide Risk Management (ERM).

“ERM inatoa muongozo katika masuala ya udhibiti wa majanga, ambayo moja kwa moja inahusisha matukio yanayoiusisha benki (majanga na fursa), kuyachunguza kwa kuyaangalia na kujua ukubwa wa athari zake na kufuatilia uendeleaji wake.

“Kwa kutambua na kwa umakini kuangalia na kufanyia kazi majanga na fursa, muongozo bora wa ERM utailinda benki na kuwajengea thamani wamiliki, wafanyakazi, wateja na wadhibiti,” alisema Bw. Lusala.

Alibainisha kuwa, mafanikio ya benki yoyote yanatokana na uwezo wa benki hiyo kuweza kufanya uwiano katika ya majanga yanayolandana na shughuli zake za kibiashara dhidi ya gharama za kudhibiti majanga mbali mbali.

"Kwa hiyo, benki yetu inatarajiwa kuutekeleza utaratibu huo wa ERM, ikiwa ni pamoja kuangalia maendeleo yake na utumiaji wa profaili ya benki ya majanga ili iweze kutuongoza katika ufanyaji wa maamuzi katika masuala yote ya kimkakati na yasiyokimakakati.

"ERM itahakikisha kuwa matokeo yatokanayo na jitihada za benki hayapotei kwa hasara zinazoweza epukika, au majanga," aliongeza.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Hymans & Robertson (H&R) Bw. Maurice Kilavuka alisema kampuni yake inafuraha kupata fursa ya kufanyakazi na Benki ya Exim katika safari yake ya kufikia ubora zaidi hususani katika masuala ya udhibiti wa majanga.

"Tunayofuraha kubwa kupata fursa hii ya kufanyakazi na Benki ya Exim ikiwa katika safari yake ya kufikia ubora zaidi hususani katika masuala ya udhibiti wa majanga. Ushirikiano huu unadhihirisha uelewa walionao Benki ya Exim juu utaalamu unaopatikana toka kwa wataalam wa StraitsBridge & Hymans Robertson. Tutafanya jitihada kubwa na kuiwezesha benki kuwa na mfumo bora duniani katika masuala ya udhibiti wa majanga yaani Enterprise Risk Management (ERM).

StraitsBridge Advisors pamoja na Hymans Robertson, imekuja mifumo mbali mbali madhubuti ya jinsi gani ya kudhibiti majanga ikiwa ni pamoja na majanga katika masoko, majanga katika mikopo, ALM, uwekaji bei katika utumaji fedha, Usimamizi na Upangaji wa Mtaji, na Usimamizi wa Fedha. Hii bila Bila ya shaka itakuwa ni nyenzo ya benki kuweza kujenga mfumo madhubuti wa udhibiti majanga,” Bw. Kilavuka alisema.

RAIS KIKWETE ZIARANI NCHINI MAREKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.

Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.

Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla ( General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.

Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu, Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Septemba , 2014.

TRAFIKI ALIYEGONGWA NA DALADALA JANA, AFARIKI DUNIA

WP 2806 CPL Riziki, akiwa chini baada ya kugongwa na daladala eneo la Mbagala Rangi 3 jana kabla ya kukimbizwa hospitali.

ASKARI wa usalama barabarani, aliyejulikana kwa jina moja la Riziki, WP 2806 CPL Riziki, aliyegongwa na daladala aina ya DCM wakati akiwa katika harakati za kutimiza majukumu ya kazi eneo la Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam jana asubuhi amefariki dunia jana.
Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikiuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
cdt:

MBUNGE WA JIMBO LA MKURANGA AZOMEWA MBELE YA KATIBU MKUU WA CCM, KISA AMESHINDWA KUTATUA KERO JIMBONI.


Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima

Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima, amejikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi wa jimbo lake kumshtaki kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kuwa hawatembelei jimboni.

Wananchi hao walimshtaki Malima ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha baada ya Kinana kuanzisha utaratibu mpya wa kuwataka wananchi waulize maswali magumu kwa viongozi wao ili wayajibu papo hapo aliouita ‘mahakama ya hadhara’.

Kinana alianzisha utaratibu huo juzi, katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kimanzichana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 10 katika mkoa wa Pwani wa kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2010/15.

“Hii ni mahakama ya hadhara, lazima kiongozi ajibu matatizo yanayolalamikiwa na wananchi, uongozi ni utumishi ya siyo utukufu, hivyo mnapaswa kuwatumikia wananchi waliowapatia fursa ya kuwa viongozi, lazima mjibu haya maswali ambayo wananchi wanayauliza. Kila mtu abebe msalaba wake,” alisema Kinana.

Mkazi wa kijiji hicho, Jamal Said, alisema kitendo cha Malima kutofika katika jimbo hilo kwa kipindi kirefu ndicho kinasababisha kero za wananchi zisitatuliwe.

“Katibu, Chama hiki ni kizuri ila watendaji wake ndiyo wanakiharibu, mbunge wetu hana utaratibu wa kuja huku mara kwa mara ndiyo maana unaona tunaeleza changamoto nyingi, hatuna pa kuzisema,” alisema.

Akijibu malalamiko hayo, Malima alikutana na zomea zomea ya wananchi, iliyoambatana na kauli za kebehi za ‘Utaachaje kuzomewa kama huji kutuona huku jimboni’, ‘huji jimboni mpaka udandie ziara ya wakubwa wako.’

Baada ya wananchi hao kuendelea kumzomea, Malima alidai kuwa anafahamu kuwa kelele hizo hazikukuwa za wana-CCM bali ni za vyama vya upinzani.

Aidha, alikiri kufahamu kero hizo zote na kusema kuwa zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi likiwamo la wananchi kurudishiwa eneo lao la bonde linalodaiwa kuuzwa.

Mbali na Malima, wengine waliokumbwa maswahiba hayo ya kujibu kero mbalimbali za wananchi walizouliza ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu na watendaji wenyeviti wa vijiji.

Akiuliza swali kwa niaba ya wanakijiji hao, Salum Lijonjo, mkulima wa mpunga, alisema viongozi wa serikali na chama walishirikiana kuuza eneo la kulima mpunga lililopo katika kijiji cha Lupondo na kijiji cha Mvule.

“Tunashukuru kwa ujio wako Katibu Mkuu kwa kuwa tunamini kilio chetu hiki kitapata majibu kwani tulikuwa tukilitegemea bonde hili kwa kilimo, lakini sasa limeuzwa hatuna pa kulima, tunaomba ubabaishaji huu uchukuliwe hatua,” alisema.

Akijibu malalamiko hayo, Katibu Tarafa ya Mkamba, Amini Mussa, alisema serikali imetoa agizo la kutotambua mauziano hayo na kwamba litaendelea kutumiwa wakulima.

“Wakulima endeleeni kulima kwa kuwa hatutambui kilichofanyika. Yeyote atakayedai kulinunua awabane waliomuuzia, kwa lugha rahisi imekula kwake aliyenunua,” alisema.

Jamal Said pia alimtaka Kinana awasaidie kuondokana na kero ya kulipa ushuru mkubwa katika vivuko vya mazao ya misitu.

Akijibu baadhi ya hoja hizo, Kinana aliahidi kulifikisha suala la ushuru wa mazao ya misitu kwa Waziri wa Maliasili na Utalii ili kupunguza ushuru huo ambao unawanyonya wananchi.

“Haiwezekani, ushuru wa serikali ni asilimia 18, lakini eti hapa , mnalipa asilimia 100,” alisema na kuongeza: “Nitazungumza na waziri ili tuone namna ya kupunguza ushuru huu.”

Wananchi hao wamekuwa wakilipa ushuru wa Sh. 120,000 kwa kitanda kimoja ambacho kinauzwa Sh. 120,000.

Kinana, ambaye amefuatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, yuko mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 30 katika mkoa huo, Tanga na Iringa ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2010/15 pamoja na kusikiliza kero za wananchi.