Kulia
Mwanaisha Suleiman akiwa anafanya yake ndani ya studio za redio 5
mara Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh.
Juma Nkamia alipofanya ziara kituoni hapo
Waandishi wa habari pamoja na mkurugenzi wa kituo cha redio 5 Bw.Robert Francis katika
picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Mh. Juma Nkamia,kulia ni mmiliki wa mtandao wa Jamiiblog
Pamela Mollel
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni , Mbunge wa
Kondoa Kusini amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya
urais 2015 kama viongozi wengine wanavyotangaza nia huku akidai kuwa
kazi yake kubwa nikuhakikisha wananchi katika jimbo lake wanapata
maendeleo kupitia nafasi yake ya ubunge
Waziri
Nkamia aliyasema hayo leo mara baada ya kufanya ziara fupi katika
kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye
makao yake makuu jijini Arusha,ambapo alisema kuwa bado hajawa na ndoto
ya kuwa Rais 2015
Alisema
kuwa kiongozi anayestahili kuwa rais ni lazima awe na uwezo wa kuongoza
na anayekubalika na watanzania na vigezo isiwe umri wa mtu
”Pamoja
na umri nilionao 42 sina mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015
na umri usiwe kigezo cha kugombea uwezo wa kiongozi ni muhimu
sana”alisema Nkamia
Pia
Waziri huyo aliipongeza kituo hicho cha redio kwa kazi nzuri ya
kuburudisha na kuelimisha jamii kupitianvipindi vyake mbalimbali huku
akiwataka kuandaa vipindi ambavyo vitawashirikisha wachezaji wazamani
hali itakayosaidia kukuza na kuibua changamoto katika michezo
No comments:
Post a Comment