Mkuu wa
Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala
(Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London
ikishirikiana na StraitsBridge
Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya
UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM).
Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw.
Maurice Kilavuka na Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
Mkuu
wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala
(watatu kulia) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw.
Maurice Kilavuka (wapili kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London
ikishirikiana na StraitsBridge
Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya
UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM).
Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
Mkuu
wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (kushoto) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw.
Maurice Kilavuka (kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London
ikishirikiana na StraitsBridge
Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya
UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM)
Mkuu
wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala
(Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London
ikishirikiana na StraitsBridge
Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya
UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM).
Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde, Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw.
Maurice Kilavuka (wapili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho (wakwanza kushoto) na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto)
BENKI ya Exim Tanzania imeingia ubia na kampuni ya StraitsBridge
Advisors (SBA) ya nchini Singapore, kampuni itoayo huduma za kifedha kwa ajili
ya kutoa huduma ya kitaalam katika masuala ya udhibiti wa majanga ijulikanayo
kama Enterprise – Wide Risk Management (ERM), itakayoiwezesha benki hiyo
kuongeza ufanisi katika udhibiti wa majanga.
Akizungumza katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam
jana, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala alisema,
ili Benki ya Exim iongeze ufanisi katika eneo la udhibiti wa majanga imesaini
makubaliano na kampuni ya SBA ambayo itashirikiana na kampuni ya Hymans
Robertson (H&R) ya London kuipa benki ujuzi mkubwa dhidi ya majanga
inayokutanayo na kutumia fursa mbali mbali zinazojitokeza kibiashara.
Alisema kuwa ikiwa inazaidi ya miaka 92 ya uzoefu katika utoaji huduma
hizo, Hymans Robertson ikishirikiana na SBA itaisaidia benki kuongeza ufanisi
wake katika eneo la udhibiti wa majanga yaani Enterprise-Wide Risk Management
(ERM).
“ERM inatoa muongozo katika masuala ya udhibiti wa majanga, ambayo
moja kwa moja inahusisha matukio yanayoiusisha benki (majanga na fursa),
kuyachunguza kwa kuyaangalia na kujua ukubwa wa athari zake na kufuatilia
uendeleaji wake.
“Kwa kutambua na kwa umakini kuangalia na kufanyia kazi majanga na
fursa, muongozo bora wa ERM utailinda benki na kuwajengea thamani wamiliki,
wafanyakazi, wateja na wadhibiti,” alisema Bw. Lusala.
Alibainisha kuwa, mafanikio ya benki yoyote yanatokana na uwezo wa
benki hiyo kuweza kufanya uwiano katika ya majanga yanayolandana na shughuli
zake za kibiashara dhidi ya gharama za kudhibiti majanga mbali mbali.
"Kwa hiyo, benki yetu inatarajiwa kuutekeleza
utaratibu huo wa ERM, ikiwa ni pamoja kuangalia maendeleo
yake na utumiaji wa profaili ya benki ya majanga ili iweze kutuongoza katika
ufanyaji wa maamuzi katika masuala yote ya kimkakati na yasiyokimakakati.
"ERM itahakikisha
kuwa matokeo yatokanayo na jitihada za benki hayapotei
kwa hasara zinazoweza epukika,
au majanga," aliongeza.
Kwa upande wake,
Mwakilishi kutoka Hymans & Robertson (H&R) Bw. Maurice Kilavuka alisema kampuni yake inafuraha
kupata fursa ya kufanyakazi na Benki ya Exim katika safari yake ya
kufikia ubora zaidi hususani katika masuala ya udhibiti
wa majanga.
"Tunayofuraha kubwa kupata fursa hii ya kufanyakazi
na Benki ya Exim ikiwa katika safari
yake ya kufikia ubora zaidi hususani
katika masuala ya udhibiti wa majanga. Ushirikiano huu unadhihirisha uelewa walionao Benki ya Exim juu utaalamu unaopatikana toka kwa wataalam wa
StraitsBridge & Hymans
Robertson. Tutafanya jitihada kubwa na kuiwezesha benki
kuwa na mfumo bora duniani katika masuala ya udhibiti wa
majanga yaani Enterprise Risk Management (ERM).
StraitsBridge Advisors pamoja
na Hymans Robertson,
imekuja mifumo mbali mbali madhubuti ya jinsi gani ya kudhibiti majanga ikiwa
ni pamoja na majanga katika masoko, majanga katika mikopo, ALM, uwekaji bei katika utumaji fedha, Usimamizi na
Upangaji wa Mtaji, na Usimamizi wa Fedha. Hii bila Bila ya shaka itakuwa ni nyenzo ya benki kuweza kujenga mfumo madhubuti wa udhibiti majanga,” Bw. Kilavuka
alisema.
No comments:
Post a Comment