Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza
ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.
Mbali
na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete
pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani,
Washington, D.C.
Mjini
New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10
ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla (
General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba
29 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.
Rais
Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza hilo
mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu,
Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki ni
pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja
wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi
Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN),
Mheshimiwa Ban Ki Moon.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Septemba , 2014.
No comments:
Post a Comment