Wananchi wa kijiji cha kerege
wamenufaika na huduma ya bure ya matibabu inayotolewa na klabu ya Rotary
ya Oster Bay ya jijini Dar es Salaam kila mwaka katika shule ya msingi
ya Kerege-Bagamoyo.
Akizungumza na wanahabari
waliofika kujionea aina ya huduma za matibau zinazotolewa na klabu hiyo,
Dk. Shukuru kawambwa,mbuge wa bagamoyo , Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
ufundi akiwa kama mgeni rasimi amesema kuwa amefurahishwa na kitendo
hicho cha wanachama wa Rotary klabu na kuwataka wananchi wa Kerege
wajitokeze kwa wingi siku nyingine kwani huduma hiyo ni bure.
“Ningependa kuwashukuru wanachama
wa Rotary kwa msaada huu wa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi wa
kerege na niwakuigwa katika jamii. Na pia ninawaomba wanakijiji wa
kerege mjitokeze kwa wingi kwani huduma hii ni ya bure, unapima afya
yako, unapata ushauri kutoka kwa madakitari bingwa mia moja”, Alisema
Dk.Shukuru.
Naye Bwana Thomas Scherer ambeye
ni raisi wa klabu hiyo amesema kuwa anajiskia furaha kuona wanachama wa
klabu hiyo wakiwa na moyo wakijitolea kwa ajiri ya jamii inayowazunguka.
“Tuna furaha na tunajivunia ya
kwamba kwa kupitia juhudi za pamoja za jamii, wanachama wa klabu za
Rotary nchini na nje ya nchi, serikali za mitaa na taasisi, mashirika
yasiyo ya kiserikali, jumuiya ya matabibu na sekta binafsi; tumeweza
kuandaa Kambi hii ya matibabu kwa mara ya nne,” alisema Thomas Scherer,
Rais wa mwaka 2014-2015 wa Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay
Kambi ya Matibabu, sehemu mojawapo
ya Miradi ya Afya ya Jamii, ambayo hufanyika kila mwaka toka
ilipozinduliwa mwaka 2011 katika kitongoji cha Chanika jijini Dar es
Salaam ambapo takribani wananchi 600 walijitokeza kupima malaria, VVU,
kisukari, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, macho na viashiria vya magonjwa
sugu.
Pia Dawa za bure na miwani
zilitolewa kwa watu waliokutwa na matatizo ya afya na macho. Mwaka 2012
tulitoa huduma kwa watu zaidi ya 700, na kutoa huduma kwa idadi kama
hiyo katika mwaka 2013. Mwaka huu, inatarajiwa kuwa idadi hiyo hiyo ya
watu watakaowahi kufika watasajiliwa ili kupata matibabu bure.
No comments:
Post a Comment