TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, November 18, 2014

Rais Dk.Shein akutana na Uongozi wa Chama cha wapatholojia Tanzania

unnamed2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na ujumbe wa Chama cha Wapatholojia wa Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar  kwa ajili ya Kujitambulisha kwa Rais leo (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Chama hicho Dk. Charles Massambu,[Picha na Ikulu.]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na ujumbe wa Chama cha Wapatholojia wa Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar  kwa ajili ya Kujitambulisha kwa Rais leo (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Chama hicho Dk. Charles Massambu,[Picha na Ikulu.] unnamed 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na ujumbe wa Chama cha Wapatholojia wa Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar  kwa ajili ya Kujitambulisha kwa Rais leo (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Chama hicho Dk. Charles Massambu,[Picha na Ikulu.]

Bwawa la Mtera hatarini kutoweka

unnamed
Na  matukiodaimaBlogu
KINA  cha maji katika  Bwana  ambalo ni  moja kati ya  vyanzo vya  uzalishaji wa umeme  nchini  lina hali mbaya  baada ya maji  kukauka   na  sasa  kilomita  10  zaidi zageuka  ukame . Uchunguzi  uliofanywa na mtandao wa matukiodaima.co.tz   umebaini  kuwepo kwa kasi kubwa ya bwawa  hilo  kuendelea kupoteza sifa ya  kuendelea  kuitwa  bwawa  baada ya maji  kuendelea kukauka na  kulifanya sasa  bwawa  hilo kuwa na hadhi ya mto .
Mmoja kati ya  wavuvi  katika  bwawa  hilo Frank Mvili  alisema  kuwa   kupungua kwa  kina cha maji katika  bwawa  hilo  kumechangiwa  zaidi na uharibifu wa mazingira na baadhi ya  watu kulima kwa kutumia jembe la  kukokotwa na ng’ombe pia  uchungaji wa  mifugo katika kingo  za  bwawa  hilo na hatua ya Tanesco kuendelea  kulifungulia bwawa  hilo ni  sababu ya msingi
Kwani  alisema  kuwa  maji   katika bwawa  hilo kwa  miaka mitano  iliyopita  yalikuwa jirani na makazi ya  watu  ila kwa  sasa  maji hayo  yamejivuta  kutoka  eneo la awali umbali wa kilomita 10 na  kufanya  baadhi ya maeneo  kupoteza  sifa ya  bwawa na kuwa mfano  wa mto.
Alisema mbali ya mabadiliko  ya tabia nchi kuathiri  ila bado  serikali imeshindwa  kabisa  kuchukua hatua ya  kulinusuru  bwawa  hilo na uharibifu  unaoendelea kujitokeza .
Kuhusu  shughuli za  uvuvi ambazo zilikuwa  zikitegemewa  zaidi katika  bwawa  hilo Mvili alisema kwa sasa  shughuli  hizo  zimeanza  kupoteza sifa yake  baada ya  samaki kuanza  kuwa adimu  zaidi kupatikana na  waliopo ni  wale wadogo  wadogo na kuwa baadhi ya  wavuvi  wameanza  kufungasha vilango kwenda maeneo mengine ya nje ya mkoa wa Iringa  kwenda  kuendelea na shughuli za uvuvi .
Kwa  upande  wake  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Dr Leticia Warioba akielezea  kuhusu  bwawa  hilo alisema  kuwa mbali ya  sababu  nyingine  ila  hali ya  mvua  imechangia  maji kutojaa zaidi katika bwawa  hilo na kuwa  suala la uharibifu wa mazingira  umeendelea  kuliathiri  bwawa  hilo.
Hivyo  alisema amepanga  kufanya  ziara  katika maeneo ya  bwawa  hilo  ili  kupata uhalisia  wa bwawa  hilo kwa  sasa na kuweka mikakati mipya ya  kulinusuru.

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

unnamed
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Amina Makilagi (kulia) na Mary Chatanda kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 18, 2014. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed1 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Mary Nagu akiwasilisha  Muswada wa Marekebisho ya Sheria  ya Ubia Baina ya Sekta  ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2014, bungeni mjini Dodoma Novemba 18, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

FILAMU MPYA YA 990 WAMEKUFA IPO MBIONI KUZINDULIWA , WADAU WAOMBWA KUCHANGIA MILIONI 3 YA MAANDALIZI ,ASAS ,KISWAGA WAANZA

 Mkurugenzi mtendaji wa  Miale  sanaa Group Bw  Nurdin Khamis akihojiwa
Na  MatukiodaimaBlog
WASANII  wasanii wa   Miaele sanaa Group  wa mjini Iringa mkoani Iringa waanza kutembeza bakuli kuomba  kuchangia  kiasi cha Tsh milioni 3 kwa ajili ya kukamilisha uzinduzi  wa  filamu yao mpya  ya 990 wamekufa .
 
Akizungumza na mtandao  wa matukiodaima.co.tz   mkurugenzi  mtendaji  wa  kundi  hilo Nurdini Khamis alisema  kuwa   kundi hilo  limeendelea  kufanya vema katika  tasnia ya  filamu  nchini  kutokana na  wasanii  wake  kuifanya  kazi hiyo kwa  kutumia vipaji halisi vya  kuzaliwa na hivyo  kuwa  tofauti na  wasanii  wengine  ambao  wamekuwa  wakiifanya kazi  hiyo kwa  kutegemea elimu  ya  vyuo  vya  sanaa.
Alisema  kuwa kuanzishwa kwa  kundi hilo ni  jitihada  zake  binafsi  baada ya  kuona  mkoa wa Iringa una wasanii wenye uwezo wa  kuigiza  ila hakuna  sehemu ya kuonyesha  vipaji vyao na ndipo alipoanzisha  kundi  hilo mwaka 2009 kwa  kuwa na  wasanii 30  kabla ya  kufanyiwa mchujo .
Khamis  alisema  kuwa  mara  baada ya mazoezi  makali  zaidi  wale ambao  walifanyiwa mchujo  waliweza  kuonyesha  uwezo mkubwa katika  uigizaji na  hivyo kulazimika  kutoa kazi yao ya kwanza  iliyokwenda kwa  jina la  Zero Done kwa  kuwashirikisha  wasanii  wakubwa  nchini kama  Senga , Mwamba , Mzee Pembe , Patcho ,Halima Madiwa , Rado  na  wengine  wengi  wenye majina makubwa  kazi ambayo ilisambazwa  nchi nzima na  kuonyesha  kupendwa  zaidi.
Aidha  alisema  kutoka na ukata wa  fedha  wameendelea  kufanya kazi  hiyo kwa  kusua  sua  japo kwa  sasa  wanataraji  kuibuka na filamu kali kuliko ya 990  wamekufa ambayo  inategemewa  kuzinduliwa  wakati  wowote  kuanzia  sasa mara  baada ya maandalizi  kukamilika.
Mkurugenzi  huyo alisema  kuwa  kutokanana na uwezo mdogo  wa kipato na aina ya  wasanii  wanaounda kundi  hilo kutokuwa na kazi za kufanya kundi  hilo  limeendelea  kuwa  tegemezi zaidi kwa  kufanya kazi kwa migongo ya  wafadhili mbali mbali na kuwa  hata  filamu  hiyo  iliyopo jikoni  inategemea  kuzinduliwa kwa ufadhili wa    kamanda wa UVCCM mkoa  Salim Asas , Jackson Kiswaga ambae ni mkazi wa Iringa na mdau wa sanaa katika  mkoa wa Iringa aliyechangia kiasi cha Tsh 500,000
Pamoja na  kuwashukuru  wadau mbali mbali kwa  kuendelea  kujitolea kusaidia  ukuaji wa tasnia ya sanaa katika  mkoa  wa Iringa bado  alisema  kuwa ni mategemeo yao  kuwa wadau hao wataendelea  kutoa ushirikiano  zaidi kwao  ili  kufanikisha  kuutangaza  zaidi mkoa wa Iringa  kisanaa kutokana na  uwezo mkubwa  wa wasanii  wanaounda  kundi  hilo .
Kwani  alisema  mipango ya mbeleni  kwa  kupitia  kundi hilo kuanzisha utaratibu  wa kutengeneza  filamu  za kuelimisha  jamii  juu ya masuala mbali mbali ya kimaendeleo  katika  mkoa wa Iringa na Taifa  kwa  ujumla ikiwa ni  pamoja na kutoa  elimu ya kulinda hifadhi  zetu kutoingiliwa na majangili .
Hivyo  aliomba  wale  wote  wenye mapenzi ya  dhati na kundi hilo  kujitokeza  kuchangia  chochote kwa kupitia  huduma ya M- Pesa  kwa namba  0757 698 582 kwa madai kuwa  bila  kusaidiwa na  wadau  mbali mbali  uwezo  wao ni mdogo  zaidi kiuchumi ila  kisanaa wapo  juu ukilinganisha na makundi mengine makubwa  nchini.
” Uwezo wa  kucheza  filamu  zenye ubora  tunao na ndio maana vituo  mbali mbali vikubwa vya runinga  ikiwemo  Zuku swahili  wamekuwa wakirusha kazi  zetu baada ya  kuona ni bora zaidi”

TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI DAR KUTATULIWA

unnamed
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kulia),akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 7.5 litakaloanzia eneo la Aghakani na kuishia Coco beach, ujenzi huo unaotarajiwa kuanza mapema mwakani na unafadhiliwa na Serikali ya watu wa Korea Kusini ,lengo ni kupunguza msongamano wa magari katika daraja la Serender,kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. Juma Iyombe. (Picha Lorietha Laurence –Maelezo)
………………………………………………………………………………………..
 Na Beatrice Lyimo -Maelezo
Zaidi ya Bilioni 110 zinatarajia kutumika katika ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 7.5 ili kupunguza msongamano wa magari  jijini Dar es Salaam.  
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alisema daraja hilo litaanzia  eneo la Aghakani na kuishia Coco beach.
Waziri Dkt. Magufuli alisema daraja hilo litakalojengwa kwa msaada wa  Serikali ya Korea Kusini litakuwa  na njia nne na barabara mbili za huduma kwa kila upande lenye  uwezo wa kupitisha magari elfu 61 kwa siku .
“Serikali ya Korea Kusini imemaliza mradi wa ujenzi wa daraja la Kikwete pamoja na barabara ya Malagalasi Mkoani Kigoma na sasa tumewaomba waendelee kutoa  msaada kwa ajili ya ujenzi wa barabara mkoani Dar es Salaama ili kupunguza msongamano wa magari”, alisema Dkt. Magufuli.
Kwa upande wake  Mtendaji Mkuu kutoka TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale  amebainisha kuwa wataalamu kutoka Korea Kusini wameshafanya Upembuzi yakinifu uliomalizika hivi karibuni, hivyo ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao.
Aliongeza kuwa daraja hilo litakalofahamika kwa jina la  New Salender Bridge litaunganishwa na barabara ya Ally Hassan Mwinyi kutokea Aghakani na kwa upande mwingine litaunganishwa na barabara ya Chole iliyopo Masaki.
Serikali imeweka mikakati mingi ya kupunguza msongamano wa foleni za magari kwa kuanzisha ujenzi mbadala wa barabara za juu unaotarajiwa kujengwa maeneo ya TAZARA,Mbagala rangi tatu hadi gerezani, kuanzishwa kwa kivuko cha Dar es Salaam hadi  Bagamoyo.
Pia utafanyika utanuzi wa  barabara nyingine za Dar es salaam kwenda Morogoro kupitia Chalinze na ile ya  Morocco hadi Mwenge na  Bagamoyo hadi Msata.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE JIMBO LA MTAMA

 01
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Bernard Membe Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa wakati alipowasili katika Kiwalala Kituo cha Ufugaji cha Masister cha Narunyu ambapo ameshiriki kazi ya kukamua maziwa akiwa katika ziara yake ya kikazi ya mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali lakini pia  kuhimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi CCM, Katibu mkuu Kinana katika ziara hiyo anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi.3 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kukamua maziwa katika kituo cha uugaji cha Masister cha Narunyu Mtama mkoani Lindi wakati alipotembelea kituo hicho.02 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya Masister mara baada ya kuwasili katika kituo hicho katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.1 
Baadhi ya Ng’ombe wakiwa katika shamba hilo. 17 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa tanki la maji katika mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Nyangamara jimbo la Mtama.12 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kitabu kinachoelezea shughuli mbalimbali zilizotekelezwa na Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Bernard Membe alipotembelea ofisi ya mbunge huyo. 11 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli za kubangua korosho wakati alipotembelea kikundi cha akina mama cha kubangua korosho katika kata ya Nyegendi jimbo la Mtama. 9 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuchambua korosho kwa mashine katika kata ya Nyegendi wakati alipokitembelea kikundi cha kubangua korosho kinachoendeshwa na akina mama. 8
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Mtama wakiwa katika kikao cha ndani wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana . 7
Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Maifa Mh. Bernard Membe akizungumza na wajumbe wa mkutano huo huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikilizia wa pili kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.   18 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. kushoto na Mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Said Mtanda wakicheza ngoma za asili ya kabila la Kimakonde wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika kata ya Chiuta jimbo la Mtama mkoani Lindi19
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo. 24
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Chiuta leo. 23 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano huo. 22 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo. 21 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Bernard Membe wakati wa mkutano huo. 20 
Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Bernard Membe akizungumza na wananchi wa jimbo lake katika kata ya Chiuta leo.

MWANAMUME MMOJA AUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MTONI


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 18.11.2014.
  • MWANAMUME MMOJA AUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MTONI NA WATU WASIOFAHAMIKA WILAYANI KYELA.
MWANAMUME MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HENRY AMBAKISYE (60) MKAZI WA KIJIJI CHA KANDETE ALIKUTWA AMEUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MAJINI KATIKA MTO KANDETE NA WATU WAWILI AMBAO BADO HAWAJAFAHAMIKA MAJINA WALA MAKAZI YAO.
 MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KATIKA MTO HUO MNAMO TAREHE 17.11.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANDETE, KATA YA KAJUNJUMELE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
 AWALI MNAMO TAREHE 15.11.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU WAKATI MAREHEMU ANATOKA NGOMANI AKIWA NA MWANAMKE MMOJA AITWAYE KISA KIMA (48) MKAZI WA KAPWILI ALIVAMIWA  NA KISHA KUSHAMBULIWA NA WATU HAO. AIDHA MWANAMKE HUYO BAADA YA KUONA HALI HIYO ALIKIMBIA NA KUTOWEKA ENEO LA TUKIO.
 MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA YA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI UTOSINI.  CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI WA KUGOMBEA MWANAMKE.  KISA KIMA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO. AIDHA JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
 Imesainiwa na:
          [BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

IZUCHUKWU NDANI YA NYUMBA MSIMBAZI


MUDA wowote wiki hii Simba inaweza kumalizana na straika namba moja wa Elverum FC ya Norway, Minigeria Emeh Izuchukwu. Mchezaji huyo akiwa na mwenzake, Orji Obinna, waliwahi kutamba na Simba mwaka 2008 wakitokea Enyimba ya kwao Nigeria.
Wachezaji hao waliondoka nchini kwenda kusaka noti Ulaya, lakini sasa Emeh amefanya mazungumzo ya kina na Simba na wakati wowote wiki hii anaweza kumalizana nao na kutua nchini, Mwanaspoti limethibitishiwa.
Mbali ya hao, pia Simba imewapandisha ndege wachezaji watatu kutoka jijini Mbeya kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo na kuwasainisha mikataba. Wachezaji hao ni beki wa kati Nurdin Chona na beki wa kulia Salum Kimenya wote kutoka Prisons ambao walitua jijini Dar es Salaam Jumamosi wakati mshambuliaji wa Mbeya City, Deus Kaseke, aliingia jana Jumatatu.
Taarifa za kuaminika ambazo Mwanaspoti ilizipata jana Jumatatu ni kwamba vigogo wa Simba walikutana na mchezaji mmoja mmoja kwa nyakati tofauti ambapo ilielezwa kwamba Chona ametaka dau la Sh 30 milioni, Kimenya ameanzia Sh25 milioni huku Kaseke akitaka kupewa Sh40 milioni, hata hivyo vigogo hao wamesema kwamba kwao fedha sio tatizo.
Wachezaji hao ni mapendekezo ya viongozi baada ya kocha wao Patrick Phiri kutoa baraka kwa viongozi kumsaidia kusaka wachezaji wazuri kwa maelezo kwamba bado hawajui vizuri wachezaji wote wenye viwango vya juu vya kuichezea Simba huku wakipendekeza pia jina la Said Morad wa Azam FC.
Phiri yeye katika ripoti yake aliyoikabidhi alipendekeza majina ya wachezaji wa Mtibwa Sugar mshambuliaji Ame Ally na beki Hassan Kessy, Danny Mrwanda (Polisi Moro) na Dan Sserunkuma wa Gor Mahia ya Kenya ambaye tayari wameshaanza mazungumzo. Hata hivyo uwezekano wa kumpata Mrwanda ni mdogo kwani anarudi Vietnam alikokuwa akicheza soka la kulipwa.
Phiri alitaka pia atafutiwe wachezaji wa nafasi mbalimbali ikiwemo beki ya kulia na kushoto, beki ya kati, kiungo, straika na kipa ambapo imedaiwa kuwa Juma Kaseja atarejea Simba wakati wowote kwani tayari amevunja mkataba wake na Yanga.
Kwa upande wa viongozi wa Simba walisema wamezungumza na wachezaji wengi hasa nafasi ya straika na beki na wanaamini watafanikiwa kwa asilimia kubwa.
Simba ndiyo timu pekee inayoonekana kuhaha kwenye usajili wa dirisha dogo kuhakikisha inapata wachezaji wazuri kutokana na matokeo yao waliyoyapata katika mechi saba za kwanza za Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo ilitoka sare mechi sita na kushinda mechi moja tu. Ipo katika mpango wa kuwatema wachezaji wake kadhaa akiwemo Uhuru Seleman, Ivo Mapunda, Amri Kiemba ambaye Azam wanamhitaji.
Wengine ni Mrundi Pierre Kwizera anayedaiwa kupelekwa kwa mkopo Afrika Kusini pamoja na Joram Mgeveke anayetafutiwa timu ya mkopo, Nassoro Masoud ‘Chollo’ na Haruna Chanongo ambao wanatajwa kuachwa kutokana na madai ya kushuka kwa viwango vyao.
Chanzo: Mwanaspoti

FURAHIA KIBONZO NA NATHAN MPANGALA

kibonzo10 and 11 nov 2014

IGP MANGU AONGEZA ASKARI KITETO

E88A9486
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akimsikiliza Diwani wa Kata ya Matui Wilayani Kiteto Bw.Athuman Kidawa wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa  vifo.kushoto ni Afisa tarafa wa Matui Bw.Eliakimu Ndelekwa.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)E88A9514
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na wananchi  wa Kata ya Matui Wilayani Kiteto wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa  vifo. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)E88A9421
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na Mtendaji wa Kijiji cha Chekanao, Kata ya Kiperesa , Wilayani Kiteto Bw.Omar Ndee (kulia) wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa vifo.Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Deusdedit Nsimike pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Japhet Chafu (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Kiteto.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ameahidi kuongeza idadi ya Askari katika kijiji cha Chekanao, kata ya Kiperesa wilayani Kiteto Mkoani Manyara kufuatia wananchi katika kijiji hicho kujitolea nyumba kwa ajili ya kuishi Askari kwa lengo la kuimarisha usalama katika maeneo yao kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi inayosababisha kutokea kwa mauaji.
IGP Mangu aliyasema hayo jana wakati alipokuwa katika ziara Wilayani Kiteto ya kujionea uharibifu uliojitokeza pamoja na kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo iliyopelekea kutokea kwa vifo vya wakulima na wafugaji hivi karibuni katika wilaya hiyo ambapo watu kadhaa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na vurugu hizo.
Alisema kufuatia kuwepo kwa umbali mrefu wa kituo cha Polisi na kijiji hicho atahakikisha askari wa kudumu wanakuwepo ili kushirikiana na wananchi katika kuwabaini wahalifu wanaofanya vurugu na kuendeleza migogoro hiyo ambapo wananchi nao waliahidi kujenga kituo cha Polisi.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Chekanao Bw.Omar Ndee alisema wamekuwa wakipata shida kutokana na umbali mrefu wa kituo cha Polisi jambo ambalo limekuwa likifanya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu vinavyochangiwa na migogoro ya ardhi katika wilaya ya Kiteto.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho Japhet Chafu alilishukuru Jeshi la Polisi kwa kuimarisha usalama kijijini hapo tangu kutokea kwa mauji ya wakulima na wafungaji ambapo alibainisha kuwa bila kuwepo wao hali ingekuwa mbaya zaidi kutokana na kutokuwepo na muafaka baina ya wakulima na wafugaji.
“IGP hawa askari wako wasingekuwepo hapa usingekuta mtu lakini tunawashukuru sana hawa askari kwa kuwa hivi sasa hali ya usalama imerejea na hata shambani tumeanza kwenda” Alisema Bw.Chafu.
IGP Ernest Mangu alitumia ziara hiyo kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Wakaguzi wa Tarafa pamoja na Askari Kata ili kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama.

BASATA NA KITUO CHA UTAMADUNI CHA UJERUMAN (GOETH INSTITUT) WAENDESHA MAFUNZO KWA WASANII WA SANAA ZA MIKONO

???????????????????????????????
Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza (Kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa batiki yaliyoanza mapema wiki hii kwenye Ofisi za Baraza hilo zilizoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Leah Ruhimbi
???????????????????????????????
Sehemu ya Wasanii wa utengenezaji batiki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
Picha, habari na Aristide Kwizela-Afisa Habari BASATA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ujeruman maarufu kama Goeth Insitut wameendesha mafunzo ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za mikono yanayofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yanayotazamiwa kudumu kwa siku tano yaani kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa yanalenga kuongeza ubunifu na weledi miongoni mwa wasanii wa Sanaa za mikono ili kuongeza ubora na tija katika uzalishaji. 
Mapema akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Leah Ruhimbi alisema kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija kwa wasanii hao na kuwawezesha kubuni Sanaa zenye ubora zitakazopenya masoko mbalimbali ya Sanaa.
“Ni matarajio ya BASATA na wizara kwamba mafunzo haya yatakuwa yenye tija kwa wasanii na yatawawezesha kusambaza ubunifu na uzoefu kwa wasanii wengine nchini. Lengo ni kuwa na sanaa zenye ubunifu na ubora” alisisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Goeth Institut Bi. Eleonore Sylla alisema kwamba mafunzo hayo yanahusisha wasanii wenye uwezo wa kutengeneza batiki na lengo kuu ni kuwaweka pamoja ili wachangie uzoefu na baadaye kutengeneza batiki zenye ubora zaidi.
“Tunajua mnatoka sehemu mbalimbali nchini na wote mna uzoefu katika utengenezaji wa batiki lakini kuwa kwenu pamoja kwenye mafunzo haya kutawafanya mpate uzoefu zaidi na hatimaye kubuni batiki zenye ubora” aliongeza Sylla.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alisema kwamba BASATA kwa kushirikiana na Goeth Insitut wameona kwamba kuna haja ya mafunzo hayo ya wasanii na kwamba baraza litaendelea kuboresha ubora wa kazi za Wasanii kupitia kuwajengea uwezo.

CASILLAS AANZA KUPIGA ‘MATIZI’ MDOGO-MDOGO


MLINDA mlango namba mbili wa Simba sc, Hussein Sharrif ‘Casilas’ ameanza mazoezi leo baada ya kutoa nyuzi alizoshonwa kwenye ugoko kufuatia kuumia katika mazoezi ya Mnyama yaliyofanyika nchini Afrika kusini mwezi uliopita. Casillas ameanza mazoezi ya Gym na kukimbia mchangani baada ya kufungua nyuzi za chuma alizoshonwa. Kipa huyo bora wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita anaanza mazoezi ya peke yake na anaamini Mungu atamjaalia afya njema ili arudi uwanjani. Casillas aliumia Oktoba 11 mwaka huu, Simba ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Orland Pirates nchini Afrika kusini iliyomalizika kwa suluhu ya bila kufungana. Kipa huyo aligongwa ugoko kwa njuma za chuma na mshambuliaji wa miamba hiyo ya Afrika kusini. Kwasasa Simba inamtegemea zaidi kipa namba tatu, Peter Manyika Jr kwani hata kipa namba moja Ivo Mapunda hajawa fiti kwa asilimia 100. Wakati huo huo kuna taarifa kuwa Simba inataka kumrudisha kipa wake wa zamani anayecheza Yanga, Juma Kaseja katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili. Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema katikati ya wiki iliyopita kuwa Kaseja yuko huru kurudi Simba kwani ni sawa na nyumbani kwake.

FRIENDS RANGERS KUWASHIANA MOTO NA AFRICAN SPORTS MKWAKWANI


Na Mwandishi Wetu
KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, kesho kinajitupa  kwenye Uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga, kuvaana  na timu ya African Sports, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza.
Mchezo huo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa  ligi, ambapo kila timu inahitaji kupata pointi tatu iweze  kuanza vizuri mzunguko wa pili.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Asha Kigundula, alisema  kuwa tayari kikosi hicho kipo mkoani Tanga kwa ajili ya  mchezo huo.
Kigundula alisema kikosi chao kinaingia uwanjani  kikiwa na taadhari kubwa ya kutopoteza kwa sababu ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mechi zaidi ya kutoka sare.
Alisema kuwa ana amini kila kitu kinawezekana hata ushindi ni muhimu na ikipata ushindi inaweza kurudi katika nafasi ya kuongoza.
Kigundula alisema kuwa kikosi chao chini ya kocha wao  Ally Yusuph ‘Tigana, kina ari kuwa ya kupata ushindi, licha ya wachezaji wake wawili wa kikosi cha kwanza
kutoenda mkoani Tanga.Alisema wachezaji hao ambao ni Almas Mkinda, alipewa kadi nyekundu katika mchezo wao uliyopita dhidi ya Kimondo na Eliute Justine ni majeruhi.
Alisema kuwa kikosi kicho ambapo kimecheza mechi mbili za ugenini na kupata pointi nne katika mechi mbili, wana amini na huko kitafanya vizuri.
Kigundula alisema wanautambua ubora wa timu pinzani, lakini nao wamejipanga kufanya vizuri na kuibuka na ushindi ili waendelee na malengo yao ya kupanda ligi kuu msimu ujao.
Friends Rangers inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 20, huku Majimaji ikiongoza kwa kuwa na pointi 21, hivyo ikishinda itakuwa inaendelea vyema na safari yake ya kupanda daraja.

UNITY OF WOMEN FRIENDS (UWF) WAMKUMBUKA ALIYEKUWA MSHINDI WA SHINDANO LA MWANAMAKUKA 2013

Picha
ya pamoja, Baadhi ya wana kikundi cha UWF,
mwakilishi kutoka Tanzania Women Bank (TWB), Bi Khadija na Baadhi ya
washindi wa mradi huo wa Mwanamakuka tangu mwaka 2012 wakiwa katika
picha pamoja.
 Pichani
kulia ni Mwenyekiti wa UWF na Meneja Mradi wa Mwanamakuka,Bi.Maryam
Shamo, akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) Mikocheni jijini Dar,mwishoni mwa wiki,kuhusiana na hafla
fupi ya kumkumbuka Marehemu Aziza Mbogolume,ambaye alikuwa mshindi wa
kwanza wa shindano la MWANAMAKUKA 2013.

 
Shindano hilo huandaliwa na kikundi cha
UNITY OF WOMEN FRIENDS (UWF),kupitia mradi wao wa MWANAMAKUKA, hafla
hiyo pia iliwakutanisha wadau mbalimbali wa kikundi hicho wakiwemo na
washindi wa mradi huo ambao umekuwa ukifanya vyema kila mwaka,Anaefutia
pichani ni Bi Jane Magembe, , Mwate Madinda
na Martha Kalaghe. 

Mwenyekiti wa UWF na Meneja Mradi wa Mwanamakuka,Bi.Maryam Shamo,akionesha moja ya, kipaji cha marehemu Aziza, ambacho kilikuwa ni uchoraji.
 Baadhi ya washindi wa mradi huo wa Mwanamakuka tangu mwaka 2012 wakijadiliana jambo,ambapo walikukutana kwa madhumuni ya kumkumbuka Mwanamakuka mwenzao aliyefariki. 

SKYMOTO YAWABAMBA WAKAZI WA JIJINI MWANZA NDANI YA JEMBE BEACH

DSC_0206Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band Dkt. Sebastian Ndege a.k.a JembeniJembe akizungumza na wakazi wa Mwanza kuwakaribisha kwenye show ya SKYMOTO iliyofanyika kwenye hekalu la maraha la Jembe Beach lililopo Malimbe jijini Mwanza.
DSC_0209Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band Dkt. Sebastian Ndege a.k.a JembeniJembe akimtambulisha Mkurugenzi wa Yamoto Band Said Fella almaarufu kama Mkubwa na wanawe kwa wakazi wa jijini Mwanza waliotinga kwenye hekalu la maraha lililo Malimbe jijini Mwanza Jembe Beach.
DSC_0119 
Vijana wa Skylight Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza wakifungua burudani kwa kumpa sapoti Digna Mbepera (wa pili kulia) kutoa burudani kwa wakazi na mashabiki wa Skylight Band mwishoni mwa juma. Kutoka kushoto ni Sony Masamba, Aneth Kushaba AK47 pamoja na Hashim Donode (kulia).
DSC_0015 
Divas wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na Digna Mbepera wakionyesha ufundi wao ndani ya Jembe Beach.
DSC_0127 
Rapa mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower (kushoto) akiongoza kikosi cha Skylight Band kutoa burudani kwa wakazi wa jijini Mwanza kwenye show ya aina yake iliyopewa jina la SKYMOTO huku wakikolabo na Yamoto Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza.
DSC_0131 
Raia wa kigeni na couple yake wakiburudika na burudani kutoka vijana wa Skylight Band ndani ya Jembe Beach jijini Mwanza.
DSC_0098 
Kikosi kazi cha Skylight Band kikishambulia jukwaa kwa manjonjo ya aina yake.
DSC_0142 
Sam Mapenzi wa Skylight Band akiwa raha wakazi wa jijini Mwanza ndani ya Jembe Beach mwishoni mwa juma walipo kolabo na Yamoto Band.
DSC_0163Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na Skylight Band ndani ya Jembe Beach.
DSC_0175
DSC_0185
DSC_0187
DSC_0195
Aneth Kushaba AK47 akiwa chezesha ligwaride wakazi wa Mwanza ndani ya Jembe Beach.

MKOMBE CUP YAFANYIKA UWANJA WA BANDARI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mbunge wa Jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam , Abbas Mtemvu akiongea na wachezaji (pichani hawapo)  mara baada ya kukagua Timu hizo katika Fainali kati ya Timu 20  zilishiriki katika kumuenzi mwasisi wa Mashindano hayo marehemu Said Mkombe Cup. yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari Dar es Salaam (PICHA NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa UJIJIRAHAA.
 Wadau wa Timu shiriki wakifatilia kwaumakini mpambano huo .
Mashabiki wakifatilia kwa makini mpambano kati ya timu mbili zikichuana kati ya timu ya Kadiliya na Soweto , katika Fainali ya Mashindano ya Mkombe Cup 2014 katika kiwanja cha Bandari Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke  na Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam,Ababs Mtemvu, kati ya Timu 20 zimechuana katika kumuenzi mwanzilishi wa Mashindano hayo,  Said Mkombe  , ambapo  jumla ya Timu 20 zilishiriki na Alkadiria iliibuka mshindi   kwa kuifunga Soweto 2-0.
 Mbunge wa jimbo la Temeke Abass Mtemvu akikagua timu kabla ya mchezo huo kuanza.
  Mbunge wa jimbo la Temeke Abass Mtemvu akikagua timu kabla ya mchezo huo kuanza.
 Mchezo huo ukiendelea
Mbunge wa Jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu (kushoto), akimkabidhi   Laki 5 Nahodha wa Timu ya Alkadir. Juma Issa,(wakwanza kulia) baada ya kuibuka kidedea kwa kuifunga timu ya Soweto  kati ya Timu 20 zilipochuana katika kumuenzi mwanzilishi wa Mashindano hayo Said Mkombe Cup.  Soweto wamefungwa 2-O katika kiwanja cha Bandari Dar es Salaam  

MDAU ASIA KINJENGA APATA DIGRII YA ELIMU YA JAMII (SOSHOLOJIA) CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Asia Kinjenga kulia akiwa na nyuso ya furaha pamoja na mwenzie Felician Francis baada ya kumaliza digrii ya elimu ya jamii katika sosholojia wakati wa mahafali ya 48 ya chuo kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni
Asia Kinjenga wa pili kulia akiwa na wahitimu wenzie wa mahafali ya 48 katika chuo kikuu cha Dar es salaam
Asia Kinjenga
Asia Kinjenga akiwa na familia yake
Asia Kinjenga kulia akipongezwa kwa kuvalishwa shada la mauwa na mama yake mzazi Bi, Anchimole Lutengano wakati wa mahafali ya 48 ya chuo kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni ambapo alipata digrii ya elimu ya jamii katika soshiolojia
Asia Kinjenga katikati akiwa na mama yake mzazi Anchimole Lutengano kulia na bibi yake wakati wa mahafali ya 48 ya chuo kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni ambapo alipata digrii ya elimu ya jamii katika soshiolojia

MWANRI: ZUIENI UBADHIRIFU WA MIUNDOMBINU YA MAJI

SONY DSCKiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye koti jekundu) akihoji masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji kwenye manispaa ya Songea. SONY DSC
Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikishuka kutoka kwenye tanki la kuhifadhia maji ya Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani utakaohudumia zaidi ya wakazi 3000 wa kitongoji ya Kijiji cha Ruhuiko Kanisani na maeneo ya jirani. SONY DSCKiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza mara baada ya timu yake kukagua Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani. Wanaomsikiliza kutoka kulia ni Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara, anayemfuatia ni Msanifu wa Mradi huo Bw. Elezear Ndunguru na Mratibu wa ukaguzi huo Bw. Senya Tuni (Wapili kulia).
…………………………………………………………………
Na Saidi  Mkabakuli
Serikali imetoa wito kwa taasisi za umma kusimamia kwa umakini miundombinu ya miradi ya maji pindi inapokamilika ili kuweza kuwapatia wananchi huduma ya maji ya uhakika mara miradi hiyo inapokabidhiwa kwa kamati za usimamizi wa maji.
Wito huo umetolewa na kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati timu hiyo ilipokuwa ikifanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya maji ya utekelezaji wa program ya maji na usafi wa mazingira katika vijiji 10 vya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Bibi Mwanri ambaye pia ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu, alisema kuwa kwa miaka mingi kumekuwepo na ubadhirifu wa miundombinu ya miradi mingi ya maji hali inayorudisha nyuma juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wanafikiwa na maji safi na salama kote nchini.
“Kumekuwa na tabia mbaya ya ubadhirifu wa miundombinu hii, msikubali waiharibu ama kuiba vifaa vya ujenzi wa miradi yote 10 maana kama munavyoona serikali na wafadhili wamejitolea ili kuhakikisha munafikiwa na huduma hii muhimu,” alisema.
Akizungumza wakati timu hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ilipotembelea na kukagua Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani utakaohudumia zaidi ya wakazi 3000 wa kitongoji ya Kijiji cha Ruhuiko Kanisani na maeneo ya jirani, Msanifu wa mradi huo, Bw. Elezear Ndunguru alisema kuwa mpaka sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 55.
“Kasi ya utekelezaji wa mradi huu ni ya kuridhisha kwani mpaka sasa tumeweza kujenga vituo 12 vya kuchotea maji kati ya 15, kinachongojwa kwa sasa ni kukamilika kwa tanki la kuhifadhia maji,” alisema.
Msanifu huyo ameongeza kuwa hadi kukamilikwa miradi yote 10 jumla ya shilingi bilioni 2.77 zitatumika na kuweza kuwahudumia zaidi ya wakazi 9000 wa vijiji vitakavyopitiwa na miradi hiyo.
Kwa mujibu wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo, lengo kuu kwa upande wa maji ni kuongezeka kwa upatikanaji wa maji safi na salama ni mojawapo ya maeneo yanayotiliwa mkazo ili kuweza kuongeza kasi ya maendeleo na kupunguza umaskini miongoni mwa Watanzania.

TANZANIA yapata alama ya pointi tano katika masuala ya uongozi bora

4
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, akizungumza wakati akiifungua semina ya Kujadili masuala ya Uwajibikaji katika kuleta maendeleo kwa jamii nchini, Dar es Salaam jana. Semina hiyo iliyoandaliwa na wizara hiyo, imefadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB)(Picha na Magreth Kinabo)
3 Mwakilishi Mkazi wa ADB, Tonia   Kandiero  wakati  semina  ya Kujadili masuala ya Uwajibikaji katika kuleta maendeleo kwa jamii nchini, Dar es Salaam jana. Semina hiyo iliyoandaliwa na wizara hiyo, imefadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB).Picha namba 0635 ni Baadhi ya wadau wa semina hiyo .
 ………………………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo, MAELEZO
TANZANIA imepata alama ya pointi tano katika  masuala ya uongozi bora  kwenye ripoti ya  maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika(Afrika For Results) ya mwaka huu.
Hayo yalisemwa  leo na Waziri wa fedha,Adam Malima  wakati  akizungumza katika ufunguzi wa semina ya  siku nne wa  kutathimini  ripoti  hiyo kwa  nchi ya Tanzania ukilinganisha na tafiti za nchi zingine za Afrika unaoendelea kwenye hoteli ya Kunduchi Beach  jijini Dares Salaam.
“ Katika ripoti hii  kipimo cha alama  zilizotumika ni 0-5 , hivyo Tanzania imefanya vizuri katika masuala ya uongozi bora kwa kupata alama hiyo,” alisema Malima .
 Katika ripoti iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika(ABD) ikishirikiana na Serikali ya Tanzania ambayo imetaja maeneo sita ya kuzingatia katika kuhakikisha ukuaji wa uchumi unafika kwa wananchi wote  wakiwemo wa  kawaida kwa kuzingatia hilo na mengineo.
Aliyataja maeneo hayo   ambayo ni  uwajibikaji  kwa alama 4.1.  uwezo wa kitaasisi  alama 4, mikakati ya kibajeti  alama  2.9,  mipango yenye kuleta matokeo alama  4.5 na matumizi ya Tehama  alama 2.3.
Naibu Waziri huyo  alisema ili  kutengeneza fursa sawa katika ukuaji wa uchumi  ni muhimu kuboresha viashiria vya kukua kwa uchumi na kupunguza umaskini.
 “Wananchi wa kawaida  wanaambiwa kuwa uchumi umepanda kwa asilimia saba lakini, baadhi yao  hali yao kimaisha  bado ni duni na wanashindwa kuamini ukuaji huo hivyo  kwa kutumia viashilia hivyo tunaweza kugundua na kuboresha baadhi ya maeneo ambayo yameonekana kuwa chanzo cha kutowafikia wananchi wa kawaida,”alisema Malima.
Wadau hao  katika mkutano huo watajadili   njia ambazo zitakazo saidia kuwafikia wananchi wa kawaida kukua kiuchumi ili kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati.
Kwa  upande wake Mwakilishi Mkazi wa ADB, Tonia   Kandiero  alisema  wadau  hao  watajadili  ripoti  hiyo katika  mkutano  huo  wa  kutathimini  ripoti  hiyo kwa  nchi ya Tanzania  kwa siku nne ,  na kulinganisha na nchi zingine za Afrika unaoendelea kwenye hoteli ya Kunduchi Beach  jijini Dares Salaam.
 Akitoa uzoefu wake katika nchi ya Zimbabwe, Erick  Zinyengere, ambaye ni Meneja wa Ushauri alisema ili kuweza kuleta mafanikio ya kimaendeleo katika miradi mbalimbali ni vema kushirikisha wananchi  katika  hatua ya kwanza hadi ya mwisho.

MAHAKAMA YA ILALA YAFUTA AMRI YAKE YA KUWAKAMATA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WANAODAIWA KUKIFUNGA KITUO CHA TIBA ZA ASILI

 Wakili Lucas Kamanija (kulia), anayemtetea Dk. Juma Mwaka katika kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wanadaiwa kukifunga kwa makufuli  Kituo cha Tiba za Asili cha ForePlan Herbal Clinic kilichopo Ilala Bungoni, kinachomilikiwa na Dk.Mwaka, akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana, mara baada ya kusikiliza kesi hiyo ambapo Mahakama hiyo imefuta amri iliyotolewa awali ya kuwakamatwa  watuhumiwa tisa kutoka katika wizara hiyo. Kesi hiyo imeharishwa hadi Novemba 20. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
 Wanasheria wa Serikali wakibadilishana mawazo nje ya mahakama hiyo wakati wa kusikiliza kesi hiyo.
Wakili Lucas Kamanija (katikati), akizungumza na wanahabari
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo
 
Dotto Mwaibale
 
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imeifuta amri yake ya awali ya kuwataka wafanyakazi tisa wa Wizara ya Afya kufungua makufuli waliyoyafunga kwenye kituo cha  tiba za asili na mbadala cha Foreplan Herbal Clinic eneo la Ilala Bungoni.
 
Uamuzi huo umeleotolewa  na Hakimu Mkazi John Msafiri wa mahakama hiyo, Adolf Sachore. Kabla ya uamuzi huo kutolewa, Wakili  Charles Kamanija anayemtetea Dk. Juma Mwaka aliiomba mahakama hiyo isiusome kwa sababu hakimu aliyeuandaa Msafiri hakuwepo.
 
Hakimu Sachore aliyatupilia mbali maombi hayo na kuusoma uamuzi huo ambapo aliifuta amri ya awali iliyotolewa na mahakama hiyo ya kutaka wafanyakazi hao tisa kufungua makufuli kwenye kituo hicho na wasimuingilie katika biashara yake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.
 
Amri hiyo ya awali ilitolewa, baada ya Wakili  wa Serikali, Karim Rashid kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuiomba mahakama hiyo kuiondoa na kuruhusu wao kuunganishwa  na kuwa sehemu ya wadaiwa kwenye kesi hiyo.
 
Baada ya kutolewa kwa maombi hayo, Hakimu Sachore alikubaliana na maombi ya Karim na kuyatupilia mbali maombi ya Dk. Mwaka kwa maelezo kuwa hayana msingi.
Katika maombi ya Dk. Mwaka kupitia wakili wake, Charles waliwasilisha pia ombi la kuzuia maofisa hao kuingilia shughuli za mteja wake hadi kesi ya msingi waliyofungua mahakamani hapo itakapomalizika.
Kwa mujibu wa kesi hiyo ya madai namba 204 ya mwaka 2014, imepangwa kuendelea kusikilizwa kwa maombi ya zuio Novemba 20, 2014.
 
Dk. Mwaka vile vile anaiomba  mahakama iwaamuru washtakiwa wakafute maandishi waliyoyaandika kwenye kuta za kliniki hiyo yanasosomeka; ‘Kituo hiki kimefungwa na Wizara ya Afya leo 06/11/1914’ pamoja na kutomwingilia katika biashara yake mlalamikaji.
 
Kutokana na uamuzi huo, wakili wa mlalamikaji Charles Kamanija alidai nje ya eneo la  mahakamani kuwa viongozi wa  serikali wameshindwa kutii amri ya mahakama ya kuja mahakamani na kwamba wanapanga utaratibu wa kupinga umuzi huo. 

ABDULRAHMAN KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI NCHINGA, SAID MTANDA MAMBO YAKE SAFI

1 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Nchinga mkoani Lindi Mh. Said Mtanda wakati alipowasili katika Kitomanga kata ya Mkwajuni ambapo pia alishiriki katika shughuli za ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao linalojengwa katika kijiji hicho, Katibu Mkuu wa CCM yuko katika ziara ya siku 16 katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa pamoja na wananchi huku akihimiza uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.) 2 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea katika kata ya Mkwajuni jimbo la Nchinga leo. 3 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Lindi Dkt, Nassoro Ally Hamidi wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili katika jimbo la Nchinga. 4 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Said Mtanda wakati akizungumza na wananchi wa jimbo lake. 
 5 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akizungumza mara baada ya mapokezi hayo huku mbunge wa jimbo hilo Mh. Said Mtanda na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakifurahia jambo. 6 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki ujenzi wa ghala katika kata ya Mkwajuni huku mbunge wa jimbo hilo Mh Said Mtanda akishuhudia. 7
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi hayo. 8 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa matawi ya miti na wananchi wa Mipingo Namkongo katika jimbo la Nchinga. 9 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiagalia mashimo ambayo akina mama waliokuwa wakichimba ili kupata maji ya kutumia katika kijiji chao lakini kwa sasa tatizo hilo limeshakwisha baada ya mradi wa maji kukamilika katika kijiji hicho. 10 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi mifuko ya saruji Muhaji Mtondo Afisa Mtendaji wa kijiji cha Namkongo kwa ajili ya kusakafia soko katika kijiji hicho, katikati ni Mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Said Mtanda aliyetoa saruji hiyo.11 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji pamoja na Mbunge wa jimbo Nchinga Mh. Said Mtanda wakifugua maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji uliogharimu shilingi milioni 166 mpaka kukamilika katikati ni  Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndugu Magalula Said Magalula. 13
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza wakati Katibu Mkuu wa CCM alipowasili katika kata ya Kilangala jimbo la Nchinga. 15 
Mbunge wa jimbo Nchinga Mh. Said Mtanda  katikati Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika kata ya Kilangala. 16 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Nchinga kwa viongozi wa CCM wa kata kwa moja wa viongozi hao Bw.Samwel Kibena kutoka kata ya Kilangala. 19 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na watendaji wa halmashauri ya mkoa wa Lindi wakati alipotembelea ujenzi wa zahanati ya Nchinga II.



20 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka mara baada ya kukagua ujenzi wa zahanati ya Nchinga II mkoani Lindi. 21
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa kata ya Milola jimbo la Nchinga. 22 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Milola. 23 
Mbunge wa jimbo Nchinga Mh. Said Mtanda  akifafanua jambo kuhusu hatua zilizopigwa kwa maendeleo ya jimbo la Nchinga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Milola. 24
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo. 25 
Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mkoa wa Lindi Mh. Bernard Membe akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Milola jimbo la Nchinga mkoani Lindi leo.

WAZIRI MKUU PINDA NA MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI

PG4A0421 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Waziri wa Fedha,Saada Mkuya (kulia) na Naibu wake, Mwigulu Lameck Nchemba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 17, 2014. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
 PG4A0319
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akitoa kauli kuhusu mgogoro wa wakulima na wafugaji wilayani Kiteto , Bungeni mjini Dodoma Novembe 17, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A0476
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanafunzi wa shule ya rwekiza ya Bukoba Vijijini kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 17, 2014. Kulia kwake ni Mbunge wa Bukoba Vijijini na mmiliki wa Shule hiyo, Jasson Rwekiza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKUTANO WA MABALOZI WILAYA MJINI UNGUJA

IMG_0853
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine  wakiwa katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani  katika mkutano wa Mabalozi wa CCM Wilaya ya Mjini Unguja,alipofika kuzungumza nao akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi kwa Mikoa mitatu ya Unguja,[Picha na Ikulu.]  IMG_0855
Baadhi ya Viongozi na Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini wakiwa katika Mkutano uliohutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]IMG_1039
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini katika Ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Unguja leo  akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Mikoa ya Unguja  (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na (kushoto) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Juma Faki Chum,[Picha na Ikulu.]

TWIGA CEMENT YAMWAGA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA JESHI LA MAGEREZA KATIKA MRADI WA UJENZI WA MAKAZI YA ASKARI GEREZA WAZO JIJINI DAR ES SALAAM

PIX 1 (1)
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alphonso Rodrudges(suti ya bluu) akikabidhi mfano wa hundi yenye kiasi cha Tsh. Millioni Miamoja kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza zitakazotumika katika ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni (wa pili kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja. hafla hiyo imefanyika leo Novemba 17, 2014 katika viwanja vya Gereza Wazo, Jijini Dar es Salaam.
PIX 3 (1)
 Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi katika hafla ya kupokea vifaa vya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni, hafla hiyo imefanyika leo Novemba 17, 2014 katika viwanja vya Gereza Wazo, Jijini Dar es Salaam.
PIX 4 (1)
Sehemu ya Vifaa vya ujenzi vilivyokabidhi leo na Kampuni ya Twiga Cement. Kampuni hiyo imekabidhi mifuko 1200 ya saruji pamoja na fedha Tsh. Millioni Miamoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni.

WADAU WA FILAMU WAKUTANA NA KUJADILI MAENDELEO YA TASNIA YA FILAMU NCHINI

PIX 1. (1)
Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo (kulia) akieleza jambo wakati wa mkutano wa kujadili mambo yanayohusu tasnia ya filamu Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa wa Bodi hiyo, Bw. Benson Mkenda.
PIX 6.
Wadau kutoka Bodi ya Filamu Tanzania pamoja na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) wakimsikiliza Katibu wa TAFF (hayupo pichani) wakati alipokuwa akichangia mada kuhusu masuala ya filamu nchini wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Bodi ya Filamu jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO-DSM)

Acheni kuwabembeleza wawekezaji wasiozingatia sheria za mazingira- Kaimu Katibu Tawala Mbeya

Picha Na 3 (1)
Na Greyson Mwase, Mbeya
Maafisa Mazingira katika   wilaya zilizopo katika mikoa ya Iringa na Mbeya wametakiwa kuacha kuwabembeleza wawekezaji wasiozingatia sheria za uhifadhi wa mazingira.
Kauli hiyo imetolewa na  Kaimu Katibu  Tawala Mkoa wa Mbeya , Constantine Mushi wakati akifungua mafunzo  ya siku  tano yaliyoshirikisha maafisa mazingira kutoka katika wilaya  14 za mikoa ya Iringa na Mbeya ikiwa ni pamoja na  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)  na Ofisi ya  Mkemia Mkuu wa Serikali.
Mushi alisema kuwa   wapo baadhi ya wawekezaji katika sekta za madini na nishati wasiozingatia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 inayotaka shughuli yoyote ya maendeleo  kuendana na uhifadhi wa mazingira na hivyo kuchangia uharibifu mkubwa wa mazingira.
Alisema kuwa maafisa mazingira wanatakiwa kusimamia  sheria za mazingira kwa kuhakikisha kuwa zinafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali wawekezaji wasiozingatia sheria hizo.
Alisema kuwa katika sekta ya nishati kuna shughuli za utafutaji  wa mafuta na gesi unaoendelea sehemu mbalimbali nchini  katika  nchi kavu, kwenye  ukanda wa bahari, katika maji ya kina kirefu baharini (deep sea) na kwenye maziwa na kusisitiza kuwa hii ni  changamoto kwa maafisa mazingira katika kutoa ushauri na kuhakikisha kuwa binadamu  na viumbe wengine hai hawaathiriwi na uwekezaji huu.
Alieleza kuwa uwekezaji katika sekta ya nishati ni mkubwa sana kwani nishati ya umeme ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo suala la mazingira linatakiwa lizingatiwe ili kuhakikisha kuwa wananchi na  viumbe wengine hawaathiriwi na uwekezaji huu.
Aliongeza kuwa uwekezaji katika sekta ya madini  katika miaka ya karibuni  umekua kwa kasi kubwa sana lengo lake likiwa ni kuleta maendeleo na kusisitiza kuwa shughuli za uchimbaji madini zisipofuata kanuni na  sheria za mazingira zinaweza kuacha nchi ikiwa jangwa na kuathiri mabadiliko ya tabia nchi.
“Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa shughuli zote za maendeleo zinafanyika bila kuleta athari kubwa katika mazingira yetu kwa kusimamia sheria na kanuni za mazingira pasipokuwa na upendeleo,” alisisitiza Mushi.
Alisema kuwa kuzingatia hitaji  la sheria ya mazingira, Wizara ya Nishati na Madini  imeandaa mpango kazi wa mazingira wa sekta za nishati na madini (sector environmental action plan) ambao utekelezaji wake utaenda hadi katika ngazi ya wilaya.
Wakati huo huo Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara  ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege alisema lengo la mafunzo hayo  ni kuwashirikisha  maafisa mazingira mpango kazi wa mazingira  wa sekta za nishati na madini  wa Wizara,  kuwapa elimu ya mazingira  na kupata michango yao ili kuwa na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha kuwa sheria na kanuni za mazingira zinafuatwa.
Mhandisi Kasege alisema kuwa awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yalishirikisha mikoa ya Kanda ya Pwani kama vile Dar es Salaam, Tanga, Mtwara,  Morogoro na Kilimanjaro, awamu ya pili katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Simiyu,  Geita, Mara, Kigoma na  Tabora na kuongeza kuwa awamu ya tatu inahusisha mikoa ya Iringa na Mbeya.
Alisema kuwa mafunzo haya ni endelevu na kusisitiza kuwa mikoa iliyobaki kama Katavi,  Rukwa, Njombe, Ruvuma, Dodoma, Arusha ambayo bado haijafikiwa itashirikishwa katika awamu ya nne.
Alieleza kuwa mpango huo wa miaka mitano ulioanza mwaka 2011 unatarajiwa kukamilika mwaka 2016.
Naye Kamishna Msaidizi wa Madini  Kanda ya Kusini Magharibi  Wilfred Machumu alisema kuwa mafunzo hayo yatatumika kama fursa ya maafisa mazingira kubadilishana uzoefu na changamoto katika usimamizi wa mazingira na hatimaye kupata mkakati wa pamoja wa kuboresha usimamizi wa mazingira.

DKT. ADELHELM JAMES MERU AAPISHWA KUWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

 Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib Bilal (kushoto) akimuapisha Dkt. Adelhelm Meru kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akila kiapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.PIX 3
 Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akiweka saini katika Kitabu mara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib (kushoto) akiweka saini katika kitabu mara baada ya kumuapisha Dkt. Adelhelm Meru kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.PIX 5
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib (kushoto) akimkabidhi kitabu Dkt. Adelhelm Meru mara baada ya kumuapisha kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM)

Mkutano wa Mabalozi wa Nyumba kumi Wilaya ya Mjini Unguja

IMG_0843
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili viwanja vya Ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Unguja kuzungumza na Mabalozi wa Wilaya ya Mjini CCM katika kuimarisha Chama alipoanza ziara maalum kwa mikoa mitano ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]

KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA MBEYA CONSTANTINE MUSHI AFUNGUA RASMI SEMINA YA MAAFISA MAZINGIRA JIJINI MBEYA

Picha Na 2 (1)
Afisa Misitu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Theodore Silinge  akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayoPicha Na 1 (1)
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara  ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege (kulia) akitoa maelekezo kwa  baadhi ya wawasilishaji mada katika mafunzo yanayoshirikisha maafisa mazingira katika mikoa ya Iringa na Mbeya yanayofanyika jijini Mbeya leo.  Lengo   la mafunzo hayo ni kuwashirikisha mpango kazi wa Wizara  ya Nishati na Madini pamoja na kupata michango yao. Kushoto ni Meneja wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali  Nyanda za Juu Kusini David Elias. Katikati ni Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Abdullatif Nassor.
Picha Na 3 (1)
 Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara  ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege (kulia) akielezea shughuli za  Kitengo chake kabla ya kumkaribisha mgeni  rasmi, Kaimu Katibu  Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi ili aweze kufungua mafunzo hayo.
Picha Na 4
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa madini  hotuba iliyokuwa inawasilishwa na  mgeni rasmi Kaimu Katibu  Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi (hayupo pichani)

TFF YAIPONGEZA AFRIKA KUSINI KWA KUFUZU AFCON

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa pongezi kwa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kufuatia timu yake ya Taifa (Bafana Bafana) kufuzu kucheza fainali zijazo za AFCON nchini Equatorial Guinea.
 Afrika Kusini iliifunga Sudan mabao 2-1, hivyo kufuzu kabla ya kukamilisha michezo yote. Bafana Bafana bado imebakiza mchezo mmoja katika hatua hiyo.
 Wakati huo huo, TFF imeipeleka barua ya shukrani kwa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kwa kufanikisha kambi ya Taifa Stars nchini humo kabla ya kwenda kucheza Swaziland.
 SAFA ilitoa viwanja vya mazoezi kwa Taifa Stars na usafiri wa basi la kisasa kutoka Johannesburg kwenda Swaziland na kurudi, hivyo kuokoa zaidi ya dola 15,000 ambazo TFF ingetumia kama ingegharamia yenyewe safari hiyo au kuweka kambi ya timu hiyo nyumbani.
 Awali Benchi la Ufundi la Taifa Stars chini ya Kocha Mart Nooij lilipendekeza timu kufika Swaziland mapema au kuweka kambi nchini Afrika Kusini. SAFA ikajitolea kusaidia kambi hiyo.
 Pia TFF inakanusha madai ya gazeti moja la kila siku lililodai kuwa wakaguzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wamevamia/wamefanya ukaguzi wa siri kukagua fedha za udhamini wao kwa Taifa Stars.
 Ukaguzi wa hesabu ni utaratibu wa kawaida wa kila robo ya mwaka wa fedha. TFF ndiyo huwaalika TBL kutuma wakaguzi wao ili kuhakiki vitabu vya fedha. Uhusiano kati ya TFF na TBL ni mzuri, na kila kinachofanyika ni kwa nia njema kwa makubaliano ya pande zote mbili.
 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment