Kundi
la akina mama wa kilimani waliopo katika mtandao wa facebook nchini
Kenya limeapa kufanya maandamano katika bustani ya Uhuru Park tarehe 17
mwezi huu ili kuungana na mwanamke aliyevuliwa nguo hadharani siku ya
jumatano kwa kuvaa nusu uchi mbali na kupinga unyanyasaji wa kijinsia
dhidi ya wanawake.
Katika kisa hicho kilichofanyika katika kituo
cha kuegesha magari cha Embassava jijini nairobi,wanaume wanaodaiwa kuwa
makondakta wa matatu walimvua nguo mwanamke huyo na kusema kwamba
alikuwa anawasisimua kwa mavazi yake.Wanawaake hao wameapa kuelekea katika kituo hicho cha magari ya uchukuzi ili kuwaambia makondakta hao kwamba wanawake wana haki ya kuvaa wanavyotaka.
Kanda ya video ya kisa hicho ilichukuliwa na baadhi ya wasafiri na kuwekwa katika mtandao wa jambo net.
Wakenya pia wamepinga tukio hilo kupitia neno MyDressMyChoice katika mtandao wa twitter.
Wanaume wengi wamesema kuwa watajiunga na wake zao pamoja na wana wao wa kike kupinga uhalifu huo siku ya jumatatu.
No comments:
Post a Comment