BONDIA THOMAS MASHALI ASAINI KUZIPIGA NA ABDALLAH PAZI JANUAR MOSI 2015 FRENDS CORNER
Bondia Abbdallah Pazi kulia
akitia saini ya kupigana na Thomasi Mashali kushoto baada ya makubaliano
na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi
katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam
Bondia Thomasi Mashali kushoto
akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi ya
mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner
Manzese Dar es salaa
Promota Kassim Texas katikati
akiwainuwa mikono juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Abdallah Pazi
kuashilia makubaliano ya mpambano wao utakaofanyika january mosi katika
ukumbi wa frends corner manzese Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na SUPER D BLOG
===============================================================
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AFUNGUA KONGAMANO LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA
=====================================================================
SKYLIGHT BAND NI MOTO WA KUOTEA MBALI, WAZIDI KUWAPA RAHA MASHABIKI WAO KWA BURUDANI NZURI
Pichani Kutoka kushoto ni Bella Kombo akiongoza mashambulizi ya jukwaa
akipewa sapoti na Digna Mbepera(katikati) na kwa mbaliiiii ni Aneth
kushaba.
Kama kawaida yetu inapofika
mwishoni mwa juma yaani Ijumaa huwa inakuwa ni siku ya furaha na
kubadilishana mawazo, kupunguza stress za kazini…..paleee Thai Village
Masaki.Kwenye Jukwaa Bendi yako matata na inayotikisa Tanzania na Jiji
la Dar Skylight Band wanakuwa wanakupa burudani ya nguvu na iliyoenda
shule.Karibu leo kuanzia saa 3 kamili usiku upate zile Afropop, Zouk,
Lingala,Sebene, Reggae, Naija Flava na zingine kibao!
Aneth Kushaba AK 47 akizipiga vocal za kutoshaaaa ili kuwapa burudani wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Bella Kombo akitia madaha yake na swagga kibao ndani ya Thai Village.
Digna Mbepera (Mtoto Mzuri) akiimba kwa hisia kali kuwapa ladha wapenzi wa Skylight band ndani ya Thai Village
Anaitwa Hashimu Donode mkali wao akizipiga zile vocal kaliiii na tamuuu kuwapa raha mashabiki wake ndani ya Thai Village
Aneth Kushaba AK 47 akizipiga vocal za kutoshaaaa ili kuwapa burudani wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Bella Kombo akitia madaha yake na swagga kibao ndani ya Thai Village.
Digna Mbepera (Mtoto Mzuri) akiimba kwa hisia kali kuwapa ladha wapenzi wa Skylight band ndani ya Thai Village
Anaitwa Hashimu Donode mkali wao akizipiga zile vocal kaliiii na tamuuu kuwapa raha mashabiki wake ndani ya Thai Village
UNESCO, SAMSUNG KUJENGA KIJIJI CHA DIGITALI OLOLOSOKWAN
Pichani ni muonekano wa mchoro wa kijiji hicho utakavyokua.
Nyalandu amteua RC Singida Mwenyekiti wa Kikos kzi alichouunda jana.
Waziri
wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu amemteua Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt Paseko Kone kuwa Mwenyekiti wa Kikosi kazi kitachofuatilia uundwaji
wa chama cha wafuga nyuki hapa nchini.
Nyalandu alimteua Mkuu wa Mkoa
huo kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wafugaji wa nyuki
katika mkoa wake wa Singida bila kuchoka.
Waziri Nyalandu alitoa uamuzi huo wakati akifuga kongamano la ufugaji nyuki la Afrika lililomalizika Jijini Arusha jana.
Wajumbe Wengine walioteuliwa
katika kikosi kazi hicho ni Juma Shaban Mgoo ambaye atakuwa katibu wa
Kikosi kazi hicho na pia ni Mtendaji Mkuu,wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania na ambaye alikuwa mkamu mwenyekiti wa Kongamano atakuwa mjumbe
katika Kikosi kazi hicho,wengine ni Ester Mkwizu Mjumbe.
Wajumbe wengine ni mwakilishi wa
wafugaji nyuki ,mwakilishi wa wasomi na watafiti ili kikosi kazi kiwe
na mchanganyiko wa pande zote.
Walioteuliwa wote watapaa barua
jumatatu kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wao,ambapo waziri nyalandu
alieleza kuwa kuwa uteuzi huo wa wajumbe wanaounda kikosi kazi cha
kushughulikia uundwaji wa chama cha wafuga nyuki ni agizo lililotolewa
na Waziri Mkuu wakati wa ufuguzi wa Kongamano la nyuki kuwa ipo haja ya
kuundwa kwa chama cha wafugaji nyuki ili kiweze kuwaunganisha wafugaji
wote ndani ya nchi na kuwa na mtandao mmoja wenye nguvu na sauti.
Katika hotuba yake alieleza
jinsi Tanzania ilivyojithatitia kuhakikisha inainua ufugaji nyuki na
sekta ya nyuki ili kuwapita nchi ya Ethiopia ambayo ndiyo kinara cha
nyuki cha Ufugaji nyuki Afrika.
Akasema kongamano hili ni la
kwanza kufanyika katika ardhi ya Tanzania na limesaidia sana
katikakuwafumbua macho watanzania hasa wafugaji nyuki hasa katika
masuala muhimu yaliyosisitizwa katika mada zilizojadiliwa kwenye
kongamano hilo yatasaidia kukuza sekta ya ufungaji nyuki hapa nchini.
Kongamano hilo lililojumuisha
washiriki wapatao 550 kutoka katika mataifa ya Ghana,Ethiopia,Zimbabwe,
Afrika kusini,Camerun,Sudani,Kenya,Uganda na Rwanda.
Washiriki wengine walitoka
katika nchi ya Kanada,Marekani,Pakstan,Namibia,Misri,
Zambia,Ubelgiji,Uturuki na mengine.limekuwa la kufana sana,mada 88
zilikuwepo,mada 45 zilijadiliwa,katiyake mada 26 zilihusu tafiti za
nyuki,mada 17 zilijadiliwa kwa wafugaji nyuki.
Awali akimkaribisha waziri
Nyalandu Mwenyekiti wa Kongamano hilo SelestinKisimba alieleza kuwa
katika kongamano hilo wameondoka na mapendekezo sita mambyo wataenda
kuyafanyia kazi mara moja ili kuinua sekta ya nyuki.
Baadhi ya Mapendekzo hayo ni
kuwa ufugaji nyuki lazima uweb endevu kwa manufa ya wafugaji
wote,,umuhimu wa ufugaji nyuki na maendeleo,tatizo la ukosefu wa
mitaji,uendelezaji wa rasilimali zilizopo , kuongeza uzalishaji wa
thamani ya asali,ambapo mapendekezo hayo yatasaidia kuboresha ufugaji
nyuki.
Washiriki wamepata nafasi ya
kutembelea maeneo ya ufugaji nyuki katika mikoa ya Singida,Dodoma na
Ngorogoro Mkoani Arusha kuweza kujifunza na kuona hali halisi ya
mazingira yalivyo hasa katika maeneo yanayofugwa nyuki.
No comments:
Post a Comment