VITUKO VYATAWALA MAZISHI YA MSANII MABOVU IRINGA , MLEVI AFANYA VURUGU KUBWA
Wasanii wakielezea kifo cha mabovu , Juu ni Msanii Mabovu enzi za uhai wake |
Waombolezaji wakiwa na jeneza la msanii Mabovu kutoka msikiti wa Mwangata kwenda makaburi ya Mlolo Iringa |
Baadhi ya wasanii wa kundi la Weusi ambao wamefika Iringa kumzika msanii Mabovu leo |
Makini akichangisha rambi rambi |
Msanii JOh Makini akiwa na michango ya msiba wa mwenzao Mabovu leo |
Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili makaburi ya Mlolo nje kidogo ya mji wa Iringa kwa mazishi.
Chapombe huyo ambae alifika makaburini hapo kwa kuchelewa alivamia eneo hilo la mazishi kwa kuanza kutoa lugha za matusi ya nguoni kwa wafiwa kwa madai wamewezaje kumzika marehemu huyo bila ya yeye kufika eneo hilo.
Kutokana na lugha hizo za matusi iliwalazimu Vijana waombolezaji kumtoa kwa nguvu eneo hilo na kwenda nae pembeni kidogo kumsihi asifanye vurugu kabla ya chapombe huyo kuanza kurusha Ngumi kwa wasanii.
Akizungumza mara baada ya
mazishi hayo mmoja kati ya wadau wa tasinia ya muziki nchini na
promota mkubwa wa mziki nyanda za juu kusini Edwin Bashir ambae ni
mtangazaji wa kituo cha Radio Ebony Fm alisema kuwa mbali ya umoja
ambao wasanii wameuonyesha katika msiba huo kwa kuja kushiriki
mazishi ila bado angeshauri wasanii kwa wakati mwingine kujenga
ushirikiano wa kumjulia hali mwenzao pindi anapoumwa.
” Sisemi kwa ubaya ila
kiukweli msanii Geez Mabovu ameumwa sana karibu mwaka mzima
anasumbuliwa na ugonjwa wake ila hakuna msanii ambae amefika kumjulia
hali ila leo wengi wamesafiri kuja kumzika….. inapendeza
kusaidiana wakati wa ugonjwa badala ya kusubiri mwenzenu afe “
Bashir alisema kuwa msanii
huyo ni miongoni mwa wasanii wa mwanzo zaidi kuutangaza mkoa wa
Iriga katika tasnia ya muziki na kuwa hata kabla ya vituo vya radio
kuanzishwa mkoani Iringa alikuwa akiutangaza mkoa na kusikika katika
radio mbali mbali za nje ya Iringa.
Alisema kuwa msanii huyo toka
amemaliza elimu yake kamwe hajapata kufanya shughuli nyingine nje
ya mziki na kuwa wakati wote alikuwa akijishughulisha na muziki
zaidi .
Hata hivyo alisema chanzo cha
Mabovu kuhama mkoa wa Iringa na kuhamishia makazi yake jijini Dar es
Salaam ni kuzidi kuutangaza muziki zaidi na mkoa wake wa Iringa
malengo ambayo alipata kufanikiwa kwa kiasi kikubwa .
” Utaona jinsi ambavyo msiba
wake leo ulivyowavuta watu wegi wapenzi na wadau wa muziki kutoka
mikoa mbali mbali ya nje ya Iringa ambao kimsingi baadhi yao imekuwa
ni mara yao ya kwanza kufika Iringa ….pamoja na kufarijika kwa umati
wa watu waliofika kumzika ila moyo umeniuma sana hasa ukizingatia
kuwa kifo chake hakikuwa na ghafla bali amekufa kwa mateso makubwa
kwa kuugua karibu mwaka mzima sasa hivyo kwa umoja huo
ningetegemea wangefika enzi za uhai wake kumuuguza mwenzao”
Kwa upande wake mwakilishi
kwa kundi la Weusi Bw Joh Makini alisema kuwa kifo cha Mabovu
kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya muziki hasa muziki wa hiphop
Tanzania,
Alisema kuwa Mabovu amepata
kuishinae Kinondoni Jijini Dar es Salaam mtaa mmoja ila pia
amepata kushirikiana kazi mbali mbali za kimzuki .
Hivyo alisema kuwa
ushirikiano huo ndio ambao umewasukuma kufika mkoani Iringa
kushiriki mazishi hayo baada ya pengo kubwa ambalo wamelipata .
Akizungumza kwa niaba ya wasanii wazawa na mkoa wa Iringa msanii Squza,alisema
kuwa Iringa imempoteza msanii mkongwe na kuwa kifo chake
kitaenziwa na wasanii wa mkoa wa Iringa pia ambao wapo nje ya mkoa
huo kwa kuangalia jambo la kufanya katika kuwanyanyua wasanii
chipukizi wa mkoa huo.
Alisema kuwa wapo wasanii
maarufu wengi kutoka mkoa wa Iringa ambao wana majina makubwa kama
Rehema Chalamila (RAY C} akina MiKe T na wengine wengi na kuwa
kama njia ya kumuenzi Mabovu watahakikisha wanaunganisha nguvu kwa
kushirikiana na vyombo vya habari kuona Iringa inampata mwakilishi
mwingine wa Mabovu kutoka kwa wasanii Chipukizi .
Msanii Mabovu alifariki dunia
jana majira ya saa 2 usiku nyumbani kwa wazazi wake eneo la Mwangata
mjini Iringa ambako alikuwa akiugulia na amezikwa leo katika makaburi
ya Mlolo nje kidogo na mji wa IringaTigo kusaidia mpango wa kujenga na kutoa vifaa kwa maabara ya shule za sekondari wilayani Mtwara
Mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini Bw. Wilman Ndile (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee inayojulikana kama Tigo Mtwara Benefit Gala kwaajili ya ujenzi wa maabara katika wilaya ya Mtwara, kulia kwake niMeneja wa Tigo kanda ya kusini, Bw.Daniel Mainoya na kushoto kwake mkurugenzi wa kampuni ya Proactive Solution, Nestory Phoye.
………………………………………………………………………………
Tigo Tanzania leo imetangaza
kwamba itasaidia kujenga na kuchangia vifaa katika maabara ya shule za
sekondari ambazo zimekwisha jengwa wilayani Mtwara. Mamlaka ya wilaya
yanaandaa harambee kubwa siku ya Ijumaa wiki hii kwa ajili kufanikisha
jambo hili.
Akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo katika
ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Meneja wa Kanda ya Mtwara kutoka Tigo
Daniel Mainoya alisema kwamba kampuni yake inaamini katika kuwapatia
watoto mazingira bora yakusomea, ili kuweza kuwajengea uwezo wa kuwa
wananchi wanaowajibika na kuzalisha ipasavyo.
“Hii ni muhimu sana hasa hasa katika kujifunza masomo ya
sayansi. Ni muhimu kwa watoto wetu kupewa vifaa vinavyotakiwa ili kuweza
kupata uelewa si wa kinadharia tu bali wakiuzoefu wa namna ya kujifunza
masomo ya sayansi kama Baiolojia, Kemia na Fizikia,” alisema Mainoya.
Wilaya ya Mtwara, ni moja kati ya wilaya sita zilizoko katika
halmashauri ya mkoa wa Mtwara, yenye jumla ya shule za sekondari 42
zinazoendeshwa chini ya serikali. Kati ya hizi asilimia 18 tu ya shule
hizi ndo zenye maabara ya kujifunza Fizikia, Kemia na Baiolojia,
kutokana na maelezo ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Kapenjama.
Akielezea kwamba hali kuwa ni “mbaya,” Kapenjama aliwaambia
waandishi wa habari kwamba kukosekana kwa maabara hizo ni kilema kikubwa
kwa wanafunzi wanaoazimia kuja kufanya kazi katika tasnia ya sayansi
kama madaktari, maenjenia na kadhalika. Kutokana na maelezo ya DC alama
ya wastani ya ufaulu kwa wilaya ya Mtwara katika masomo ya sayansi
kwenye shule za sekondari kwa sasa ni asilimia 35.
“Ni kwa sababu hii tuntoa rai kwa wadau wote kutoka katika sekta
binafsi na ya umma kuja kutuunga mkono katika kuchangisha fedha kujenga
maabara mapya na kuwapatia vifaa kwa maabara chache ambazo tayari
zilishajengwa ili kuweza kuwawezesha watoto wetu kufurahia masomo ya
sayansi na wakati huo huo kuweza kutimiza ndoto zao ya kuwa wanasayansi
bora duniani,” alisema
Harambee hiyo inayojulikana kama Tigo Mtwara Benefit Gala,
itafanyika Ijumaa hii na itajumuisha kampuni na watu binafsi, pia
kutakuwa kuna mnada wa bidhaa na vitu mbali mbali kama michoro ya
Kiafrika, Yakimakonde na mnada wa safari za kitalii nchini, yote haya ni
kwa ajili yakuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara 43 katika
sekondari mbali mbali hapa wilayani, alisema Kapenjama.PINDA AAGANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNIDO NCHINI
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa UNIDO nchini
aliyemaliza muda wake, Bw. Emmanuel Kalenzi ambaye alikwenda ofisini
kwa Waziri Mkuu kuaga Novemba 13, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago Mwakilishi Mkazi wa
UNIDO nchini aliyemaliza muda wake, Bw. Emmanuel Kalenzi ambaye
alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu kuaga Novemba 13, 2014. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu
==============================================================
==============================================================
TANZANIA KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA SEKTA YA NYUKI DODOMA
Mahmoud Ahmad Arusha
Tanzania inatarajia kujenga
kituo Kikubwa cha sekta ya nyuki ambacho kitatoa mafunzo juu ya
namna bora ya kufuga nyuki kisasa
Mtendaji Mkuu wa baraza la Taifa
la uwezeshaji wananchi Kiuchumi Dakta Anaclet Kashuliza ameeleza
hayo wakati wa kongamano la kwanza la ufugaji nyuki barani Afrika.
Kituo hicho kinatarajiwa
kujengwa MKoani Dodoma kwa msaada wa Kampuni moja kutoka Marekeni mbali
na kituo hicho kuhusika na utoaji mafunzo pia kitahusika na
uchakataji wa asali
Dakta Kashuliza amesema kuwa
kituo hicho kitahusika na utunzani wa kumbukumbu ya vitu vya asali
vya ufugaji nyuki hapa Tanzania na kinatarajia kuanza katika kipindi cha
miezi minne ijaayo
Dakta Kashuliza aidha amesema
mbali na kujengwa kwa kituo hicho kikubwa barani afrika pia Tanzania
inatarajia kujenga viwanda vidogo vidogo, vya kati na viwanda vikubwa
kwa ajili ya kusindika asali na nta
Viwanda hivyo vitatumika kwa
ajili ya watalii kutoka nje watakaopata fursa ya kutembelea viwanda
hivyo pamoja na kituo kikubwa cha Dodoma kujionea juu ya hali ya
raslimali asali ilivyo.
Wakati huo huo Serikali Mkoa wa Singida imesema kuwa ipo
tayari kuyaondoa makundi yote ya watu waliovamia maeneo ya wahadzabe
wakiwemo wakulima na wafugaji na hivyo kuwawezesha kumiliki maeneo hayo
kama zilivyo jamii nyingine nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Singida,Vicent Parseko Kone
Hatua hii inalenga kuwapa haki yao ya msingi ya kumiliki
ardhi jamii hiyo ya wahadzabe kama jamii nyingine ya watanzania hapa
nchini
Amewaambia washiriki wa kongamano la ufugaji nyuki barani
afrika kuwa asilimia 77 ya eneo linalokaliwa na jamii ya wahadzabe
tayari limevamiwa na wafugaji pamoja na wakulima jambo ambalo
linatishia maisha ya jamii hiyo ya wahadzabe ambao maisha yao yote
hutegemea sekta ya nyuki
Amesema katika mkakati huo wa kuwaondoa wavamizi wote pia
Serikali imefanikiwa kupeleka huduma mbambali za kijamii zikiwemo za
maji, miundo mbinu ya barabara, elimu na afya.
Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema Serikali Mkoani humo
imefanikiwa kuyapima maeneo yote wanamoishi wahadzabe ili kuwawezesha
kupata hati miliki
Pia amesema Serikali imesambaza mizinga zaidi ya 150
katika jamii hiyo ili kuiwezesha kuendeleza zaidi ufugaji wa nyuki
katika jamii hiyo pamoja na kuipatia mtama kwa ajili ya kuwawesha
kuendelezaa kilimo katika vijiji vyao
Mkoa huo hivi sasa una watu wapatao 1,300 wa jamii ya
wahadzabe ambapo 300 wanaishi katika wilaya ya Mkalama katika Kijiji
cha Munguli
Wakizungumza katika kongamano hilo mmoja wa jamii hiyo ya
wahadzabe amesema jamii hiyo inayo haki ya kumiliki ardhi kama jamii
nyingine ya kitanzania
Aidha ameitaka serikali kukomesha vitendo vya baadhi ya jamii kuvamia maeneo yao kwa kutumia nguvu za kiuchumi walizonazo
Hivyo ameitaka serikali kuhakikisha jamii ya wafugaji
na wakulima kufuata taratibu pale wanapoingia katika baadhi ya maeneo
Amekiri kuwa kwa asilimia kubwa jamii ya wahadzabe walikuwa hawajui haki haki zao pamoja na matumizi ya ardhi
==============================================================
Ugungaji wa Semina ya wakuu wa Mikoa na Wilaya Bara na Visiwani
Wakuu
wa Mikoa Bara na Visiwani wakiwa katika ugungaji wa semina yao ya siku
taku iliyozungumzia Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji
kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi
ya Tanzania bara iliyofungwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri katika
Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja,(Na Mpiga Picha Maalum)
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa Bara na Visiwani wakimsikiliza Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar
Kheri akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kuhusu
Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji kwa Wakuu wa
Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania
bara ufungaji huo ilifanyika jana Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji
wa Unguja,(Na Mpiga Picha Maalum)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ
Mhe,Haji Omar Kheri akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku
tatu kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na
Baadhi ya Tanzania Bara iliyohusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa
na Utendaji katika Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja,(Na
Mpiga Picha Maalum) Wakuu
wa Wilaya za Unguja na Pemba wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri
alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kwa
Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya
Tanzania Bara iliyohusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na
Utendaji katika Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja jana,(Na
Mpiga Picha Maalum)
Picha ya pamoja iliyowahusisha washiriki wa Semina ya siku tatu ya kwa
Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya
Tanzania Barabaada ya kufungwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri katikat, (Na Mpiga
Picha Maalum) Picha
ya pamoja iliyowahusisha washiriki wa Semina ya siku tatu ya kwa
Maafisa Tawala Mikoa na Wilaya za Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya
Tanzania Bara baada ya kufungwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri katikati, (Na
Mpiga Picha Maalum)
==========================================================
==========================================================
WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPIMA UGONJWA WA KISUKARI
Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Serikali imetoa wito kwa kila
mwananchi nchini kuhakikisha kwamba anapima afya yake mara kwa mara
kwa kuwa ugonjwa wa kisukari unaweza usionyeshe dalili yoyote mapema ili
kuweza kukabiliana na kupunguza athari za ugonjwa huo
Aidha Serikali imesisitiza kuwa
endapo mtu atatambulika kuwa ana ugonjwa huo, atumie huduma za afya
kulingana na ushauri wa atakaopewa na wataalam wa afya.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri
wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Stephen Kebwe leo alipokuwa
anatoa tamko kuhusu Siku ya Kisukari Duniani itakayoadhimishwa Novemba
14, mwaka huu duniani kote yenye kauli mbiu “Ulaji unaofaa, huanza na
mlo wa asubuhi”.
Siku ya kisukari duniani
ilianzishwa baada ya kuona ugonjwa wa kisukari unaongezeka sana duniani
kote na Tanzania kama nchi nyingine duniani huadhimisha siku hii kwa
kushirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania kutoa elimu ya
umuhimu wa kuzuia na kujikinga na madhara mbalimbali yatokanayo na
ugonjwa huu, alisema Naimu Waziri.
“Ugonjwa wa Kisukari ni hali
ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango
cha kawaida kwa muda mrefu” aliongeza Dkt Kebwe.
Amebainisha kuwa asilimia 80 ya
wagonjwa wa kisukari ulimwenguni wanaishi katika nchi zinazoendelea
ikiwemo Tanzania, na tafiti zinaonyseha kuwa mwaka 2007 kulikuwa na
wagonjwa 246 milioni duniani,mwaka 2012 wagonjwa milioni 371, mwaka 2013
wagonjwa milioni 382ulimwenguni kote na mwaka 2013 kulikuwa na
wagonjwa milioni 19.8 barani Afrika.
Aidha nchini Tanzania kwa mujibu
wa utafiti uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha wilaya 50 ulionyesha
kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana
ugonjwa wa kisukari.
Dk. Kebwe aliongeza kuwa
takwimu za watoto wenye kisukari mwaka huu ni kati ya asilimia 15
mpaka 20 ya wagonjwa wa kisukari ambao wanatibiwa kwenye kliniki za
hapa nchini.
“Lakini wapo wengine
hawajitokezi kwenye kliniki kwa sababu mbalimbali zikiwemo imani potofu,
gharama pamoja na umbali wa huduma za afya zilizopo” aliongeza Naibu
Waziri huyo.
Aidha Serikali kupitia Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii inaendelea na utekelezaji wa Sera ya Afya(2007)
inayolenga kutoa huduma kwa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani ya Nchi na wa kimataifa.
Tanzania inaungana na mataifa
yote duniani kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 2011 la
kuhakikisha magonjwa yasio ya kuambukiza yanapungua kwa asilimia 25
ifikapo mwaka 2025.
================================================================
BODI YA FILAMU TANZANIA YAZITAKA KAMPUNI ZA FILAMU KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA FILAMU.
Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo akiongea
na wahusijka wa Kampuni ya Kajala Entertainment wakati alipofanya nao
mkutano leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa
Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.
Mkurugenzi wa
Kampuni ya Kajala Entertainment, Kajala Masanja akiweka sahihi ya
kukubali kufanya marekebisho katika filamu yake pamoja na malipo ya
faini mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito
wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu
ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu yake ya Mbwa Mwitu.
Meneja ambaye pia
ni Mratibu wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Bi. Leah Mwendamseke
akiweka sahihi katika fomu maalum ya kukubali kufanya marekebisho katika
filamu iliyokaguliwa na Bodi hiyo mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu
Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika
filamu ya Mbwa Mwitu.
Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo akiagana
na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment wakati alipofanya naye
mkutano leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa
Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM)
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
BODI ya Filamu Tanzania
imezitaka Kampuni za filamu nchini kufuata Sheria na Kanuni mbalimbali
wakati wa kutengeneza filamu ili kuepusha ukiukwaji wa Sheria na Kununi.
Rai hiyo imetolewa leo na Katibu
wa Bodi hiyo, Bi Joyce Fissoo wakati alipofanya mkutano na Kampuni ya
Kajala Entertainment ambapo mnamo Septemba 22, mwaka huu ilikagua Filamu
fupi ya kampuni hiyo iliyopewa jina la Mbwa Mwitu yenye dakika 12 na
kubaini baadhi ya makosa.
Akiongea wakati wa mkutano na
wadau wa kampuni hiyo, Bi Fissoo alisema kuwa Bodi iliielekeza Kajala
Entertainment kuifanyia marekebisho filamu hiyo katika dakika ya 7
ambapo ilionekana wanawake wakidhalilishwa na kubakwa kinyama na pia
katika dakika ya 11 ambapo ilionyesha wizi na uvamizi.
Alisema kuwa, wahusika
walielekezwa kufanya marekebisho hayo kwa kuondoa vipande husika na
baada ya kufanya marekebisho hayo waliwasilisha Bodi ya Filamu nakala ya
filamu iliyokuwa imefanyiwa marekebisho yenye dakika 12 na kupewa
kibali namba 4261 ya tarehe 24 Septemba, 2014.
Bi Fisso aliongeza kuwa, mnamo
tarehe 25 Septemba, 2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
Salaam, filamu hiyo fupi ilionyeshwa bila ya kuzingatia marekebisho
yaliyokuwa yameelekezwa kwa mujibu wa Sheria kwa kuzingatia kifungu cha
Sheria cha 19 (2) (a).
“Baada ya ukiukwaji wa Sheria
katika kifungu cha 19 (2) (a) na kile cha 24 (i), (m) na (n) vya Kanuni
za Sheria ya Filamu husika, wahusika waliitwa mara mbili kufika Bodi ya
Filamu lakini hawakufanya hivyo, lakini baada ya kumbushio na kalipio
wahusika baadaye walifika Ofisi za Bodi katika kikao cha tarehe 13
Novemba mwaka huu”, alisema Bi. Fissoo.
Alieleza kwamba, wahusika
walikiri kuwa walipata ujumbe wa wito wao wa kuitwa na Bodi hiyo ambapo
Mratibu wa masuala yote ya Kampuni ya Kajala Entertainment, Bi. Leah
Mwendamseke aliieleza Bodi kuwa anaomba asamehewe kwa kuwa walikuwa na
shughuli nyingine mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo,
Kajala Massanja aliiomba radhi Bodi ya Filamu Tanzania huku akisema
kuwa mara nyingi yeye huwa amekuwa akiwaachia wsaidizi wake kutekeleza
majukumu ya kampuni yake ingawa yeye kama mmiliki wa kampuni hiyo
anawajibika moja kwa moja.
Aidha, Bodi iliitaka Kajala
Entertainment kueleza sababu ya kukiuka maelekezo ya Bodi ambayo
yalikuwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake licha ya mtunzi na
mwandishi wa musuada na muongozaji wa filamu hiyo, Bi. Leah Mwendamseke
alijitetea kuwa alifanya utafiti na kukutanana vijana mbalimbali
waliowahi kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Hata hivyo, Leah Mwendamseke
alishindwa kuoanisha uhalisia wa matokeo ya utafiti wake na ujenzi wa
visa vya hadithi ya filamu ambayo inaweza kupeleka ujumbe chanya kwa
jamii, huku wahusika wakieleza kwamba lengo lao kubwa lilikuwa ni
kuelimisha jamii kuhusu maovu yanayotokea na namna ya kuyaepuka ambapo
mtunzi huyo aliahidi kurekebisha vipengelee husika katika filamu hiyo
ili kuwa na filamu bora.
Kwa upande wake Mwakilishi toka
Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi Tanzania, Sylivester Mganga aliushauri
uongozi wa Kajala Entertainment kufuata maelekezo na kuzijua Sheria
mbalimbali zinazohusu mambo ya filamu kwa kuvishirikisha vyombo vya
ulinzi na usalama kabla ya kujichukulia maamuzi ya kutengeneza filamu
zenye kutishia amani ya nchi.
Bodi ya Filamu Tanzania imetoa
onyo kali kwa wahusika kwa kutengeenza filamu zenye kuonyesha ama kukuza
uhalifu na udhalilishaji bila kuainisha mkondo wa Sheria licha ya
msamaha kutokana na kosa hilo ambapo Bodi hiyo imeitaka kampuni hiyo
ilipe faini ya shilingi milioni moja kwa mujibu wa kifungu cha 47 (2)
(a) cha Kanuni za Sheria ya Filamu ambayo wahusika waliridhia adhabu
hiyo.
========================================================
WASIRA AKERWA NA MAKUNDI YA KUDUMU NDANI YA CHAMA
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais
,(Uhusiano na Uratibu ) , Stephen Wasira amesema kuwa yupo tayari
kuvunja makundi ya kudumu yanayoongozwa na Mbunge wa zamani wa Arusha
Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Felix Mrema pamoja na Batilda
Burian aliyekuwa mgombe wa ubunge na kushindwa kwa chama hicho kwenye
chaguzi mbali mbali.
Aidha amesema kuwa Arusha
inashindwa kwenye chaguzi mbalimbali kutokana na makundi yaliyopo ndani
ya chama hicho na si kwasababu ya vyama vya upinzani kuwa na nguvu ya
kuiangusha CCM.
Wasira aliyasema hayo jana
Jijini hapa kwenye kikao cha Halmashauri ya Wilaya kilichofanyika jana
ndani ya ukumbi wa CCM Mkoa na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa
chama hicho chenye lengo la kupitisha majina ya wagombea wa nafasi
mbalimbali za wenyeviti wa mitaa.
Alisema makundi ya Batilda na
Mrema ni lazima yamalizwe na kama mlezi yupo tayari kuyaita makundi hayo
ili kumaliza tofauti zilizopo ndani ya chama na kutoa rai kwa wagombea
wengine kuwa kama wameshindwa wakubali kushindwa na kumpa ushirikiano
mgombe aliyepitishwa kwa wakati huo ila si vyema kuweka makundi ndani ya
chama.
“Nakerwa sana na kushindwa kwetu
kwenye chaguzi ambao sisi wenyewe ndio tunaofanya tushindwe na kwanini
tunaendelea kushindwa kwenye chaguzi mbalimbali sisi tukishinda au
kushindwa tunapongezana hili ni tatizo hata kama tumeshindwa
tunapongezana haiwezekani lazima tufike mahali tuvunje makundi na
kuchagua kiongozi/mgombea aliyemteule na si kuongozi asiyetakiwa na
wananchi”.
Hata kamati za Siasa Mkoa wa
Arusha nazo pia zimegawanyika waandika maazimio na kamati nyinge
zinakaa na kuyakataa hapana tunachane na makundi na pia tunapoelekea
kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa lazima tuchague kiongozi mteule na
si kumchagua mjomba wala shangazi yako maana akishindwa tunashindwa
wote kama chama na si wewe uliyetaka awepo.
Alihoji suala la wananchi wa
Kijiji cha Nanja kilichopo Wilayani Monduli kuandamana hadi Ofisi za
Mkoa kutoa malalamiko yao kuwa mgombea waliyemtaka si yule aliyepitishwa
na kutoa tahadhari kwa wananachama na viongozi kuwa kwanini wanataka
kuwa wabinafsi na kuhoji kwanini mteule asipitishwe badala yake
apitishwe mgombea asiyetakiwa na wananchi wa eneo husika/.
Aliongeza asijidanganye mtu Rais
ajaye atatoka ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwani hata maandiko
yanasema kuwa wagombea ni wengi lakini wateule ni wachache .
Pia Wassira aliwasihi wanachama
wa CCM pamoja na wananchi kwa ujumla kujitokeza kupiga kura ya maoni
kwaajili ya katiba mpya pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu
la wapiga kura ili kuweza kutimiza wajibu wao.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Arusha, onesmo ole Nangole awali akikaribisha Wassira ambaye ni mlezi wa
chama hicho Mkoani hapa alisema kuwa kinachokiangusha CCM kwenye
chaguzi mbalimbali Mkoani hapa ni makundi ndani ya chama na kuyataja
makundi hayo kuwa yanaongozwa na Batilda pamoja na Mrema huku akimsihi
Wassira kuwaita kwa pamoja na kuwafungia ndani ili waweze kujadili kiini
cha makundi hayo na kuyavunja kabisa.
Nangole alihoji ni kwanini
wanaangusha wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama na kutoa rai kwa wanaccm
kuachana na majungu na kuacha watu kuamua nani wanayemtaka badala yake
wasipeleke wateule mizigo kwenye chaguzi halafu mwisho wa siku chama
kinashindwa kwenye chaguzi mbalimbali.uchaguzi unapofika tuweke nia ya
kushindwa na kupongezena
===========================================================
Tigo, Original Komedi,na Wasanii kibao kutikisa jiji la Mwanza kwenye tamasha la Welcome Pack jumamosi hii.
Kwaya
Master Mwana FA akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu
tamasha kubwa la Tigo welcome pack jijini Mwanza jumamosi wiki hii.
Meneja Bidhaa wa Tigo Bw.Edwin Mgoa alisema kwamba kampeni hiyo ya Welcome Pack inayoendelea kwa muda wa mwezi mmoja na zaidi sasa imekwisha fanyika kwa mafanikio makubwa katika mikoa mingine ikiwemo Kagera, Kilimanjaro, Arusha, Iringa, Dodoma na Mbeya ambapo imewapa fursa maelefu ya wananchi kupata huduma za Tigo kwa karibu ikiwemo kifurushi cha Welcome Pack.
Kifurushi cha Welcome Pack, kwa mujibu wa Mgoa, kinampa mteja anaenunua laini mpya ya Tigo dakika 20 za muda wa maongezi, MB 175 za intanet, kutuma ujumbe mfupi wa SMS bila kikomo, na kiasi cha shilingi 500 kama salio la Tigo Pesa kwa kila mteja atakaye nunua laini ya Tigo kwa kiasi cha shilingi 1000 tu.
“Tumeandaa matamasha haya kwa ajili ya kusherehekea huduma hii mpya mahususi kwa wateja wetu. Na kwa safari hii, Tigo imeamua kwenda kutikisa jiji la Mwanza na kikundi cha The Orijino Komedi na wasanii wengine wa Bongo fleva. Kwa hiyo tunapenda kuwasihi wateja wetu wote wa kanda hiyo ya ziwa kuchukua fursa hii kuja kujaribu hii huduma yetu mpya pamoja na kupata burudani isiyo na kifani kutoka kwa wasanii bora kabisa kutoka nchini Tanzania,” alisema Mgoa.
Mmoja wa wanakikundi kutoka Orijino Komedi, Lucas Mhavile almaarufu kama Joti alisema kwamba yeye binafsi pamoja na kikundi chake kizima wanafuraha kubwa sana kushiriki katika msafara wa tamasha la Tigo Welcome Pack na wapo tayari kwenda Mwanza kuwapatia zaidi ya burudani mashabiki wao.
“Napenda kutoa rai kwa watu wote wa Mwanza kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa CCM Kiruma siku ya Jumamosi kuanzia saa 6 mchana. Tamasha la Tigo Welcome Pack si jambo la kukosa! Njoo upate burudani, ucheze na ufurahi. Lakini usisahau pia kujipatia kifurushi cha Welcome Pack kutoka Tigo na uanze kuwasiliana na marafiki na familia yako kupitia ofa kabambe kabisa kutoka Tigo,” alisema Joti.
Akifafanua kuhusu kifurushi cha Welcome Pack, Mgoa alisema kwamba kifurushi hicho kinakuja na dakika 20 za muda wa maongezi, MB 175 za intanet, kutuma ujumbe mfupi wa SMS bila kikomo, na kiasi cha shilingi 500 kama salio la Tigo Pesa kwa kila mteja atakaye nunua laini ya Tigo kwa kiasi cha shilingi 1000 tu.
“Hii itawawezesha wateja wetu kuwasiliana zaidi na kwa gharama nafuu ambayo haijawahi kutokea,” alisema Mgoa.
Kampeni ya Welcome Pack itakuwepo kwa muda wa miezi mitatu, ambapo misafara zaidi ya 70 ikiwemo basi la Tigo la Kidijitali lenye malengo la kuwaelimisha wateja kuhusu huduma za Tigo za kidijitali litatembelea miji 70 na vijiji zaidi ya 100 ndani ya mikoa 10 tofauti ikiwemo Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Kigoma na Mtwara.
Wasanii maarufu wa Bongo fleva watakaotoa burudani ni pamoja na Profesa J, Joh Makini, Shah, Mheshimiwa Temba na Chege, Madee na Izzo Business. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisheni nyote,” alimalizia kwa kusema Mgoa.
No comments:
Post a Comment