TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, November 13, 2014

HABARI ZILIZOTAWALA KWENYE VYOMBO VYA HABARI SIKU YA TAREHE 11/11/2014 HIZO HAPA

 Meneja wa Ghetto Radio ya Sibuka FM  94.5 Bw. Edward Rukaka  aliyeshika Mkasi ,akiizindua Rasmi Studio hiyo na kuitambulisha kwa wadau. kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Bahati nasibu Tanzania Bw. Abbas Tarimba akishuhudia uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Ghetto Radio Kenya Bw. Majimaji akizungumza wakati wa usiku wa kuzindua Rasmi Studio ya Kurushia matangazo ya Radio ya Ghetto Radio ya Sibuka FM Nchini Tanzania hivi karibuni
 Mkurugenzi wa Sibuka George Nangali kulia akiwa na
Mkurugenzi wa Ghetto Radio Matt Brouwer  wakati wa Sherehe Fupi za  uzinduzi wa Studio hiyo iliyopo mtaa wa Hananasifu Kinondoni.
Katikati ni Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka FM Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva Juma Nature wakati wa uzinduzi huo
 Mkurugenzi wa kituo cha afya cha Iran Nchini Tanzania Dkt. Farhad Arjomandi akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mtangazaji maarufu wa  Ghetto Radio ya Sibuka FM Basil Jonas Juu ya Studio hiyo
Dj Bling Kutoka Ghetto Radio ya Kenya akielezea uzoefu wake katika … Ku mix Mix  Ngoma mbalimbali ambazo zinagusa kila rika la wasikilizaji..
 Wadau mbalimbali wakiwa katika Sherehe hiyo ya Uzinduzi wa Studio za Ghetto Radio ya sibuka Fm.
 Kulia ni Bw. Kelvin Guninita mfanyakazi wa Sibuka Media akiwa katika sherehe hizo za uzinduzi  wa studio za Ghetto Radio ya  Sibuka Fm.
Meneja wa Ghetto radio Tanzania Bwana Edward Rukaka akiwaonesha wageni waalikwa sehemu mbalimbali za studio hiyo
Wadau mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Meneja wa kituo hicho cha Radio Bw. Edward Rukaka jinsi shughuli zinavyofanyika ndani ya studio hizo za Ghetto Radio.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa Bwana Abbas Tarimba akimsikiliza kwa makini Meneja wa Ghetto Radio Tanzania Bw. Rukaka
 Wakurugenzi wa Key Media nao walihudhuria sherehe hizo za uzinduzi wa studio ya Ghetto Radio Tanzania.
 Katika picha ya pamoja ni Balozi wa Ghetto radio Tanzania msanii wa mziki wa Bongo Fleva Juma Nature na Violeth Okina wa kwanza  kulia ambaye ni Meneja Mauzo wa Ghetto Radio Tanzania katika sherehe hizo.

SEMA KUTUMIA MILIONI 396/- KUWEKA SAWA MAZINGIRA MASHULENI IRAMBA

DSC02082Meneja wa shirika la SEMA, Ivo Manyanku, akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba. Kulia mwenye miwani ni mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda.
Na Nathaniel Limu, Iramba
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Sustainable Environment Management Action (SEMA),linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 396 milioni kugharamia utekelezaji wa mradi wa usafi mashuleni na mazingira kwa ujumla,katika shule saba ba kata saba za wilaya ya Iramba.
Fedha hizo ni ufadhili kutoka shirika la WaterAid Tanzania.
Hayo yamesemwa na meneja wa SEMA,Ivo Manyanku, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingirav nchini, iliyofanyika katika kijiji cha Tulya wilayani Iramba.
Alitaja baadhi ya malengo ya mradi huo, kuwa ni pamoja na kuhamasisha na kuelimisha wanafunzi na jamii kwa jumla namna bora ya kunawa mikono.
DSC02101Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo dunia na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika kimkoa katika kijiji cha Tulya wilayani humo.
“Pia kuwaelimisha wanafunzi wa kike waliopevuka (kuvunja ungo) njia bora zitakazowasaidia kuwa wasafi kipindi chote cha siku zao za hedhi”,alifafanua Ivo na kuongeza kwa kusema;
“Shughuli zingine ni ujenzi wa vyoo bora na kuwahamasisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kuvitumia kikamilifu.Tutawaelimisha na kuwaahamasisha kunawa mikono pindi wanapotoka chooni kujisaidia”.
Kwa upnde wake afisa afya wa wilaya ya Iramba,Yohana Dondi,alisema kuwa wilaya ya Iramba ina kaya zenye vyoo bora ni aslimia 42,vyoo kubalika 52,vyoo visivyokubalika asilimia 18 na bila vyoo,ni aslimia sita.
Kwa mujibu wa afisa huyo,nchi zinazoendelea,asilimia 70-80 ya maradhi yote,yanasababishwa na maambukizi yatokanayo na vinyesi,hivyo kuwa ni kisababishi namba moja cha vifo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu,ni Choo bora na mikono safi kwa afya bora,heshima na usawa”.
DSC02092Spider man kutoka Temeke jijini Dar-es-salaam akitoa burudani ya kutembea juu ya waya kwenye hafla ya uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini iliyofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.
DSC02060Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda (wa nne kutoka kushoto) akitoa maelekezo juu ya ujenzi wa choo bora cha shule ya msingi Tulya.Wa tatu kushoto ni meneja wa shirika la SEMA,Ivo Manyanku.
DSC02075Baadhi ya wakazi wa kata ya Tulya,waliohudhuria uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.(Picha zote na Nathaniel Limu).

Rais Kikwete aanza kazi nyepesi

unnamedRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea na kazi ndogo ndogo wakati akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore Maryland nchini Marekani leo(picha na Freddy Maro)

NHIF YAWAFANYIA UPIMAJI MAJAJI MKOANI MWANZA

1 
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Catherine Kameka akimpima urefu askari wa kituo cha Ilemela Pc Auson Pascal katika zoezi la upimaji afya linaloendeshwa na NHIF katika mkutano wa Majaji unaofanyika Mkoani Mwanza.
2Daktari Kevin Kanama akimpima kasi ya mapigo ya moyo Mkurugenzi wa Ukaguzi na Maadili wa Mahakama Kuu Mhe. Ilivin Mugeta katika zoezi la upimaji afya linaloendeshwa na NHIF katika mkutano wa Majaji unaofanyika Mkoani Mwanza.
3Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Moses Mzuna akipimwa kipimo cha sukari na Daktari Godliver Lwakatare katika zoezi la upimaji afya linaloendeshwa na NHIF katika mkutano wa Majaji unaofanyika Mkoani Mwanza.
4John Mgeta akipewa maelezo ya hali lishe na Daktari Kevin Kanama katika zoezi la upimaji afya linaloendeshwa na NHIF katika mkutano wa Majaji unaofanyika Mkoani Mwanza.

MZEE WA MATUKIODAIMA AWA MAKAMU MWENYEKITI WA WAMILIKI WA BLOGS TANZANIA

Mwandishi wa BBC nchini Aboubakar  Famau kulia akiwa katika picha ya pamoja na mmiliki wa mtandao  wa matukiodaima Bw  Francis Godwin mara baada ya  kuteuliwa kuwa makamu mwenyekiti wa wamiliki wa Blogs Tanzania 

 Mkurugenzi  mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma  akifungua  warsha  hiyo  leo 
……………………………………………………………………………………
MWANDISHI  wa gazeti la Jamboleo kutoka mkoani Iringa Bw Francis Godwin ameteuliwa kuwa makamu mwenyekiti  wa chama  cha   wamiliki  mitandao ya  kijamii (Blogs )Tanzania .
Godwin  ambae ni mmiliki  wa Blogs  hii ya  matukiodaima na Francisgodwinblog  ameteuliwa katika nafasi hiyo kama mwakilishi  wa  wamiliki  wote wa blogs za  mikoani  huku Joachimu  Mushi  akiteuliwa  kuwa mwenyekiti  wa  chama   hicho .
Uteuzi   huo umefanyika leo  katika ukumbi wa Mlimani City    baada ya  kumalizaka kwa warsha ya siku  moja  iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) 
Wengine   walioteuliwa nia pamoja na katibu  wa  chama   hicho Khadija  Kalili, wajumbe ni   Mdimu Henry , Wiliam Malecela,Othuman Maulid na Shamim Mwasha.
Akizungumza  mara  baada ya  uteuzi huo mwenyekiti wa chama  hicho Bw Mushi  alisema  kuwa  lengo  ni  kuhakikisha  katiba ya chama hicho inakamilika mapema  zaidi  ili chama  hicho  kiweze  kusajiliwa rasmi  .
 mkurugenzi  mkuu  wa TCRA Profesa  John Nkoma   alisema  kuwa  mamlaka  yake  itasaidia  kufanikisha  mchakato mzima  wa wamiliki  wote wa  Blogs nchini  kuwa na chama  chao na  kuwa  lengo ni  kuwawezesha  kufanya maamuzi  yao kwa  umoja na kuweza  kusimamiana wenyewe .
Profesa Nkoma  alisema  kuwa iwapo  wamiliki wa Blogs  nchini  wataanzisha  chama  chao  upo  uwezekano mkubwa  wa TCRA  kuwasaidia mchakato  huo na pia kuendelea  kuungana na chama  hicho  kwa kuendelea  kutoa elimu  zaidi.
Mbali ya  kuwataka  kuanzisha  chama  hicho  bado  aliwataka  wamiliki  wa blogs  nchini  kuendelea  kuifanya kazi  hiyo kwa  kuheshimu misingi ya maadili badala ya  kutumia  vyombo  hivyo  kuvuruga maadili .
 
Akielezea  kuhusu uwajibikaji wa  blogs nchini kuelekea  uchaguzi mkuu wa  mwaka 2015 alitaka   kuhakikisha  wanatoa nafasi  sawa  kwa vyama  na  wagombea  wote  bila  upendeleo.
Kwa  upande wake  mkurugenzi wa idara ya habari (Maelezo ) Assah Mwambene  aliwataka  wanahabari  nchini  na  walimiki wa  Blogs  kuendelea  kuutumia  vema  Uhuru  wa  vyombo  vya  habari na kuangalia  mambo ya msingi kwa jamii badala ya  kugeuza  mitandao hiyo kuvuruga amani ya nchi.

SERIKALI KUWALINDA WAHADZABE – WAZIRI MKUU

4Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea tuzo ya Uhamasishaji na Ufugaji bora wa nyuki  kutoka kwa Rais wa Chama cha Wafugaji Nyuki Duniani, Gilles  Ratia  katika kongamani la ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Novemba 11, 2014. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 5Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea tuzo ya Uhamasishaji na Ufugaji bora wa nyuki  kutoka kwa Rais wa Chama cha Wafugaji Nyuki Duniani, Gilles  Ratia  katika kongamani la ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Novemba 11, 2014. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 3Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaonyesha wazee wa kabila la Wahadzabe asali iliyofungashwa tayari kwa kuuzwa katika Kongamano la Ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika kwenye  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa chaArusha ( AICC)  Novemba 11, 2014. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Vincent Ole Kone, wapili kulia ni Maidona Wazael  na watatu kulia ni Jacob Edward. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akitazama mazao mbalimbali yanayotokana na nyuki katika maonyesho yaliyokwenda sambambamba na Kongamano la  Ufugaji Nyuki Afrika  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Novemba 11, 2014. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na kushoto kwake ni Mhamasishaji wa ufugaji nyuki na usindikaji asali  wilayani Loliondo, Krystern Erickson.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
1Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaonyesha wazee wa kabila la Wahadzabe asali iliyofungashwa tayari kwa kuuzwa katika Kongamano la Ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika kwenye  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa chaArusha ( AICC)  Novemba 11, 2014. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Vincent Ole Kone, wapili kulia ni Maidona Wazael  na watatu kulia ni Jacob Edward. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma kabla ya kufungua kongamno la ufugaji nyuki Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Novemba 11, 2014. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 6Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia  wakati alipofungua Kongamano la Ufugaji Nyuki Barani Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Novemba 11, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
7Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu vifaa vya kukamulia asali kutoka kwa watalaam wa Kichina, Huang Hejie (kushoto) na  Zhinyong Wang (watatu kushoto) katika kongamano la Ufugaji Nyuki Afrika  lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) Novemba 11, 2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itaendelea kuyalinda makabila madogo nchini yakiwemo ya Wahdazabe na Wasandawe ambayo yanategemea rasilmali misitu kwa maisha yao na ustawi wao.
 “Tutakuwa tunafanya makosa kama tutawanyang’anya rasilmali misitu makabila madogo hapa nchini kama vile Wahadzabe, Wandorobo na Wasandawe kwani ndiyo rasilami pekee inayowawezesha wapate chakula cha kutosha,” alisema.
 Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Novemba 11, 2014) wakati akifungua Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Barani Afrika la Mwaka 2014 lililoanza leo kwenye ukumbi wa AICC, jijini Arusha. Kongamano hilo linashirikisha wajumbe 590 kutoka ndani na nje ya nchi. Nchi za nje zinazoshiriki kongamano hilo ni 24, ambapo kati ya nchi hizo nchi 12 ni za bara la Afrika.
 Kongamano hilo la siku tatu limeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuwakutanisha wafugaji nyuki, wafanyabiashara, wataalamu na wawakilishi wa taasisi za ndani na nje ya nchi ili kujadili njia za kuboresha ufugaji nyuki na kukabiliana na changamoto za ufugaji nyuki hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla.
 Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa Halmashauri na watu wenye maamuzi wasiwasumbue kwa kuwalazimisha wabadili maisha yao na kutoka kwenye mfumo wa ikolojia (ecosystem) ambao wameuzoea. “Tusiwabugudhi, tusiwatoe kwenye mfumo wao wa ikolojia. Tuwasaidie kuwapa teknolojia mpya ili waweze kufuga kisasa na kupata faida huku wakiishi kwenye mazingira hayohayo waliyoyazoea mpaka hapo watakapozoea na kuamua kubadilika kwa kubaini kuwa njia zao za zamani haziwasaidii sana.”
 Akizungumzia kuhusu ufugaji nyuki barani Afrika, Waziri Mkuu alisema ufugaji nyuki umeegemea zaidi katika rasilimali misitu na kilimo ambapo Afrika kwa asilimia kubwa shughuli ya ufugaji nyuki hufanyika katika misitu.
 “Bara la Afrika lina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba milioni 30.2 na asilimia 20 ya eneo hilo ni misitu. Asilimia 40 ni misitu ya Savanna ambayo ni muhimu kwa ajili ya ufugaji nyuki. Mapori haya pamoja na maeneo ya kilimo yana uwezo mkubwa wa kuzalisha mazao ya nyuki kwa wingi,” alisema Waziri Mkuu.
 Akizungumzia kuhusu ufugaji nyuki nchini Tanzania, Waziri Mkuu alisema takwimu za Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) zinaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika inayozalisha asali kwa wingi (tani 34,000 kwa mwaka), ya kwanza ikiwa ni Ethiopia (tani 45,000 kwa mwaka).
 “Inakadiriwa kuwa Tanzania ina uwezo wa kuzalisha tani 140,000 za asali na tani 10,000 za nta kwa mwaka. Lakini ni asilimia saba tu ya uwezo huo ndio huzalishwa. Hii ni kwa sababu zao hilo limepuuzwa tangu siku nyingi na halijapewa msukumo unaostahili.”
 Alisema sekta ya ufugaji nyuki ina mchango mkubwa katika maisha ya mwanadamu kwa kumpatia chakula, ajira na kipato. “Wananchi hunufaika kutokana na mauzo ya asali, nta na mazao mengine ya nyuki, utengenezaji wa vifaa vya ufugaji nyuki, kusambaza malighafi za viwandani na huduma ya uchavushaji,” aliongeza.
“Wafugaji wa nyuki katika nchi zilizoendelea wanatumia teknolojia ya kuvuna sumu ya nyuki (bee venom), gundi ya nyuki (propolis), maziwa ya nyuki (royal jely) na chavua (pollen) ambavyo hutumiwa kama virutubisho na dawa. Tafiti zimethibitisha kuwa gundi ya nyuki hutibu maumivu ya meno, malaria na homa ya mifupa(arthritis) na kuongeza kinga mwilini. Sumu ya nyuki imekuwa ikitumiwa kuongeza nguvu za uzazi, kutibu uvimbe na homa ya mifupa,” alisema huku akishangiliwa.
 Waziri Mkuu aliitaka sekta  binafsi  na  taasisi  za utafiti barani Afrika zifanye tafiti zaidi katika eneo hili na kuwekeza katika teknolojia ambayo inaweza kuvuna na kuchakata mazao hayo ambayo yana soko kubwa katika viwanda vya kutengeneza madawa, virutubisho na vipodozi.
 Mapema, akielezea kuhusu kongamano hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Lazaro Nyalandu alisema Juni mwaka jana, Wizara hiyo ilisaini makubaliano na Shirikisho la Ufugaji Nyuki Duniani (Apimondia) ili waweze kuandaa kongamano la ufugaji nyuki barani Afrika mwaka 2014.
 Alisema kongamano hilo ambalo kaulimbiu yake ni: “Kufuga nyuki kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira na kukuza uchumi” yaani “African Bees for a Green and Golden Economy”  litahusisha mada 88 ambazo kati yake, 45 zitawasilishwa na watafiti wa kisayansi, 26 zitakuwa za majadiliano (roundtable) na 17 zitawasilishwa katika semina.
 Alisema kongamano hilo ni kwanza kwa sababu ni mara ya kwanza kwa kongamano kama kuandaliwa barani Afrika kwa kushirikiana na Apimondia kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu species za nyuki zilizopo Afrika na mazingira ya ufugaji nyuko barani humu.

Injinia Dkt Binilith Mahenge awataka watanzania kutumia teknolojia ya kisasa kuzalisha mazao

0Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge akifungua rasmi Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi  kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal,itakayofanyika kwa muda wa  siku mbili katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
1Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Ndg. Sazi Salula (katikati), akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (kulia), pamoja na Mkurugenzi Msaidizi – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt.Richard Muyungi katika Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi  iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
2Sehemu ya Washiriki kutoka Nje na ndani ya Nchi wakisikiliza kwa makini hotuba inayotolewa na mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani). unnamedMgeni Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki kutoka Ndani  na Nje ya Nchi waliohudhuria katika Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nch4Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ,kuhusu umuhimu wa Kongamano hilo lililoandaliwa na Benki Kuu ya Dunia kwa ushirikianao na Ofisi ya Makamu wa Rais. Anayefuatia wa pili kulia Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,maliasili na Mazingira  Mhe. James Lembeli, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. Philippe Dongier (kulia) pamoja na Bw.Vel Gnanendran Mkuu wa Ofisi ya DFID nchini Tanzania.
………………………………………………………………………….
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge amewasihi Watanzania kutumia teknolojia mpya  na za kisasa katika kuzalisha mazao na sekta nzima ya kilimo kwa ujumla ili kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo misitu. Aliyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Ukuaji wa Uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi. Lililofanyika jijini Dar Es Salaam. Alifungua Kongamano hilo kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Gharib Bilal.
Aliongeza kuwa Mikoa na Wilaya zote Tanzania  zinatakiwa kuweka sera endelevu ambazo zitaweza kuhakikisha kukabiliana na uharibifu wa Mazingira. Aidha alisema kuwa zipo juhudi ambazo Serikali imezichukua katika  kuhakikisha utunzaji wa  mazingira unatekelezwa na pia  kuzuia uharibifu wa mazingira kwa njia moja au nyingine.
Akiongea katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Philippe Dongier alisema Kongamano hilo ni fursa adhimu kwa ajili ya majadiliano kuhusu program za maendeleo ya Tanzania zinavyoweza kustawi licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia Nchi. Hivyo basi Watanzania hawana budi kuwa waangalifu sababu mabadiliko ya Tabia Nchi yana athari kubwa.
Mwisho Waziri Mahenge aliwashukuru Wadau mbalimbali ambao wamehudhuria kongamano hilo kutoka ndani na nje ya Nchi. Akiwasihi sana kuendelea kutunza mazingira na pia aliwaomba watembelee vyanzo mbalimbali vya Utalii vilivyopo Nchini Tanzania ili kukuza uchumi .
Kongamano hilo ni muendelezo ya Mkutano wa New York kuhusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu na limehudhuriwa na washiriki kutoka Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania.

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

index17
TAIFA STARS YAWASILI JOHANNESBURG
Kikosi cha wachezaji 23 wa Taifa Stars tayari kimewasili Johannesburg, Afrika Kusini tayari kwa maandalizi ya mechi dhidi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland.
 Mechi hiyo itafanyika Jumapili (Novemba 16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Swaziland. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwepo Johannesburg hadi Ijumaa itakapoondoka kwenda Mbabane.
 Wachezaji wote walioitwa na Kocha Mart Nooij wapo kwenye msafara huo isipokuwa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye amebaki Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kifamilia.
 Taifa Stars inatarajia kurejea nyumbani Jumatatu (Novemba 17 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
 Wakati huo huo, kikosi cha maboresho cha Taifa Stars kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 23. Mechi hiyo itachezwa Desemba 9 mwaka huu nchini Tanzania.
 Kikosi cha maboresho cha Taifa Stars kinachoundwa na wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 kitakuwa kinakutana mara moja kila mwezi hadi Mei mwakani kwa ajili ya mazoezi na kucheza mechi moja ya kirafiki.
 Kocha Mart Nooij atatangaza kikosi kwa ajili ya mechi hiyo na programu nzima mara atakaporejea kutoka Swaziland.
 WAAMUZI 23 KUSHIRIKI SEMINA DAR
Waamuzi 23 wa daraja la kwanza wakiwemo wenye beji la Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wameteuliwa kushiriki semina itakayofanyika Novemba 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wa semina hiyo ambayo pia itakuwa na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) wanatakiwa kuripoti Novemba 15 mwaka huu kwenye hosteli ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
 Wakufunzi wa semina hiyo wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Riziki Majala na Soud Abdi.
 Waamuzi watakaoshiriki semina hiyo ni Ahmed Juma Simba (Kagera), Arnold Bugado (Singida), Charles Peter Simon (Dodoma), Dalila Jafari Mtwana (Zanzibar), Ferdinand Chacha Baringenge (Mwanza), Florentina Zabron (Dodoma) na Frank John Komba (Pwani).
 Grace Wamara (Kagera), Hellen Joseph Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni Nkongo (Dar es Salaam), Issa Bilali Ali (Zanzibar), Issa Haji Vuai (Zanzibar), John Longido Kanyenye (Mbeya), Jonesia Rukyaa Kabakama (Kagera) na Josephat Deu Bulali (Tanga).
 Kudra Omary (Tanga), Martin Eliphas Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mfaume Ali Nassoro (Zanzibar), Mgaza Ali Kinduli (Zanzibar), Samwel Hudson Mpenzu (Arusha), Soud Iddi Lila (Dar es Salaam) na Waziri Sheha Waziri (Zanzibar).

Wadau mbalimbali sasa kupambana na ujangili

PG4A6421
Na Gladness Mushi Arusha
SERIKALI inatarajia kuhusisha wizara mbalimbali pamoja na wadau
mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya
ujangili ili kupunguza kasi ya mauji ya wanyama  hasa Tembo.
Hayo yamekuja mara baada ya wadau wa kupambana na ujangili katika nchi
za kusini mwa Afrika kuwekeana mikakati pamoja na maazimio 20 ya
kupambana na ujangili  mapema jana.
Akiongea mara baada ya kuwekeana maazimio hayo 20 waziri mkuu Mizengo
Pinda alisema kuwa  maazimio hayo ambayo ymelenga kupambana na
ujangili wa wanyama yataweza kusaidia sana nchi ya Tanzania endapo
kama wahusika wataweza kuyatekeleza.
Alidai kuwa maazimio hayo kwa hapa Tanzania hayataweza kwenda yenyewe
badala yake yataweza kuhusisha wizara na vyombo vingi vya habari
iwezekanavyo hivyo basi kuna umuhimu sasa wa wizara ya Mali asili na
utalii kuanza kuanda mikakati hiyo ya kuwajumuisha wadau hao
Alidai kwa kuwaunganisha watalamu kutoka katika Wizara na katika
vyombo vingine hapa nchini kutweza kusaidia Tanzania kupata vyanzo ,
mikakati, na hata njia ambazo wanatumia majangili  tofauti na sasa
ambapo wizara moja pekee ndiyo inayoshugulikia suala hilo la ujangili.
“Pamoja na kuwa Nyalandu anafanya kazi kubwa sana ya kupambana na
Ujangili lakini hataweza yeye kama yeye na maazimio haya yaliyowekwa
leo hayatafanikiwa ila kuanzia sasa vita vyaa ujangili vitapambanwa na
watu wengi zaidi na Serikali tupo tayari kuongeza Nguvu zaidi na
zaidi”aliongeza Pinda
Mbali na hayo Pinda alidai kuwa timu hiyo ambayo itaundwa itaweza
kutoa taarifa zake kila baada ya Miezi sita ambapo taarifa hizo pia
hazitaweza kuishia hapa hapa Tanzania bali zitaenda hadi nje ya Nchi
wanachama wa kupambana na ujangili huo
“ni aibu kila siku kusikia kuwa Tanzania vita vyake niMeno ya Tembo
wanatushangaa sana watu ni lazima tuamke kuanzia sasa na tupambane
wote na sio ofisi au wizara moja ili hili liweze kuondokana na sisi
kabisa kwani uwezo hatuna?alihoji Pinda.
Naye Waziri wa mali asili na Utalii Lazaro Nyalandu alisema kuwa ni
vyema kama Majangili wakaangalia namna na mbinu nyingine ya kuishi
kwani sasa Serikali ipo macho sana na nilazima majangili wote
wakamatwe kwani wanasababisha madhara makubwa sana kwenye maslahi ya
nchi.

MERU YAENDELEA KUSISITIZA UMUHIMU WA MAABARA, NA ADA KWA SHULE BINAFSI

index
Na Gladness Mushi, Arusha
HALMASHAURI ya Meru mkoani Arusha imeweka utaratibu wa kufuatlia
baadhi ya shule binafsi ambazo zinatoza kiwango kikubwa cha ada lakini
pia shule ambazo hazina maabara kwani vitu hivyo vinachangia sana
elimu kuwa hafifu kwenye shule hizo.
Kauli hiyo imetolewa wilayani humo na Afisa elimu Sekondari Zawadi
Mchome wakati akiongea kwenye maafali ya 13  ya kidato cha nne katika
shule ya sekondari ya Tanzania Adventist(TASS)mapema jana.
Mchome alidai kuwa Wilaya hiyo kupitia ofisi yake wameweka utaratibu
huo wa kufuatilia ada za shule binafsi lakini pia ujenzi wa maabara
kama agizo lilitolewa na Serikali linavyosema .
Alifafanua kuwa utaratibu huo wa kufuatilia shule binafsi utaweza
kuwafanya wazazi au wanafunzi ambao wamekosa nafasi katika shule za
serikali kuweza kusoma kwa amani kabisa tofauti na sasa ambapo
wanafunzi ambao wamekosa nafasi kwenye shule za serikali wakati
mwingine wanakuwa na wakati mgumu sana hasa wanapofikiria malipo
mbalimbali kwa ajili ya ada  ya shule.
Kutokana na hilo alisema kuwa tayari wakuu wa shule za sekondari za
binafsi wana miongozo  na jumla ya ada ambazo wanapaswa kuwatoza
watoto na endapo kama watakiuka basi Ofisi hiyo tayari wana adhabu za
kuwapa kwa kuwa lengo la shule zote ni kuwasaidia wanafunzi na wala
sio kuwafanya kama mitaji ya biashara .
Akiongelea suala zima la maabara alidai kuwa maabara nazo ni muhimu
sana kwa maendeleo ya Sayansi na ni lazima kwa kila shule kuwa na
maabara hata kama sio ya Serikali kwani bado lengo  ni lile lile la
kuwasaidia wanafunzi.
“Kwa mfano katika shule hii mara baada ya kukagua nimeona ina
maabara zote tatu za sayansi na zimekamilika vizuri sasa kwa hali hii
kwanini wanafunzi wasipende masomo ya Sayansi na shule nyingine za
binafsi zije hapa zione mfano wa kitu ambacho mimi afisa elimu
ninachokitaka lakini pia Serikali tunachokitaka”aliongeza Mchome
Katika hatua nyingine Mkuu wa shule hiyo Joseph Kehengu alisema pamoja
na kufanikisha ujenzi wa maabara zote ambazo zina vifaa vya kutosha
kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia masomo ya Sayansi bado wanakabiliwa
na changamoto ya ukosefu wa maktaba ya shule hivyo basi wadau wa
elimu, pamoja na wazazi wanatakiwa  kuliangalia suala hilo kwa
undani zaidi ili kuweza kuwafanya wanafunzi kuongeza bidii zaidi na
zaidi.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ASHIRIKI MKUTANO MKUU WA MWAKA WA MAJAJI WA MAHAKAMA TANZANIA


0Kamishna Jenerali wa Magereza bwana John C. Minja wa kwanza kushoto akiwa pamoja na Wadau Wengine Wakuu wa Mahakama kabla ya kuanza kutoa hotuba namna ya  Jeshi la Magereza linavyo shirikiana na Mahakama katika kutatua changamoto zinazozikabili ili kuboresha utoaji wa haki.Wa pili kushoto katika picha ni Inspekta Jenerali wa Polisi bwana Ernest Mangu.Na Watatu kutoka kulia katika picha ni Naibu Mwana Sheria Mkuu wa Serkali Mhe.George Masaju.Wadau Wakuu wa Mahakama ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serkali,Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mwendesha Mashtaka (DPP),Ofisi ya Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa. (TAKUKURU), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza,Chama cha Wanasheria ((TLS) 1Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Dr. Asha Rose Migiro wa pili kutoka kushoto akiwa pamoja na Jaji Mkuu wa Mahakama wa Tanzania Mhe. Othman Chande wa kwanza Kutoka kushoto walio kaa mstari wa mbele na Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Zanzibar Mh. Makungu Watatu kutoka kushoto mstari wa mbele,wakiwa pamoja na waheshimiwa Majaji Wengine wakiwasikiliza kwa makini Wakuu wa Taasisi za haki Jinai wakitoa hotuba zao namna Taasisi zao zinavyoshirikiana na Mahakama katika kutatua changamoto mbalimbali zinazo athiri utoaji haki na namna ya kutatua changamoto hizo. 2Waheshimiwa Majaji wakiwasikiliza kwa Makini Wadauu Wakuu wa  Taasisi za Haki Jinai (hawako pichani) wakati wa Mdahalo wa Kuibua Changamoto na Utatuzi wake Kati ya Mahakama na Mdau husika ili kuboresha utoaji wa haki.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Mkutano Mkuu wa Majaji wa Mahakama ya Tanzania unafanyika kwa siku tatu (3) kuanzia tarehe 10 Novemba ,2014 hadi tarehe 12 Novemba,2014. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dr.Asha Rose Migiro kwa niaba ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kauli Mbiu ya Mkutano wa Mwaka huu ni “KUJITATHMINI KAMA NJIA BORA YA KUIBORESHA MAHAKAMA”.Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Mwaka huu Wah. Majaji wamepata nafasi ya kujadili mambo yafuatayo na kuyatolea Maazimio:-Taarifa kuhusu Mashauri:Ahadi,Mikakati,Mafanikio na Changamoto,Kuendesha na Kusimamia Mashauri Mahakamani:Mtazamo na Wajibu wa Jaji.Hali ya Mashauri kwa baadhi ya Kanda za Mahakama Kuu,Hali ya Mashauri katika Mahakama ya Rufani:Mafanikio na Changamoto kwa 2012-2014.Mahakama inavyotazamwa na Wadau,Ukaguzi wa Mahakama na mnalalamika Yanayojirudi:Suluhisho la kudumu,Mfumo mpya wa usimamizi wa ubora wa kazi:Faida na Changamoto zake,Rushwa,Maadili na mienendo ya Watumishi wa Mahakama na Kesi za Uchaguzi na umuhimu wa Mahakama kujipanga mapema.
Picha zote na  Mpiga picha wa Magereza Makao Makuu ya Magereza.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA

index
MTU MMOJA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI, ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO KATIKA AJALI YA MAGARI MAWILI KUWAGONGA ENEO LA MBALIZI.
TUKIO HILO LIEMTOKEA TAREHE 10.11.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS KATIKA ENEO LA MBALIZI-KATA YA UTENGULE-USONGWE, TARAFA YA BONDE LA SONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA, BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA, KUFUATIA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MAWILI T.824 AUT/.T.935 AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA BRYSON HANS [26], MKAZI WA KIMARA-DSM NA GARI T.420 ANZ AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA TROMEO MWIHIHOLA[52],MKAZI WA SONGWE KISHA KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU HUYO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
HATA HIVYO MARA BAADA YA AJALI DEREVA WA GARI T.420 ANZ ALIKIMBIA NA GARI LAKE NA DEREVA WA GARI T.834 ATK AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEKIMBIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
TUKIO LA PILI
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA BAADA YA KUKUTWA MAHUTUTI KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KASSIM RASHID [55],MKAZI WA GHANA – MBEYA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA RUFAA JIJINI MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 10.11.2014 MAJIRA YA SAA 16:30HRS. AWALI MAJIRA YA SAA 09:30HRS MAREHEMU ALIFIKA KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO ATUKUZWE ILIYOPO ENEO LA SOKOMATOLA AKIWA AMEONGOZANA NA MWANAMKE MMOJA AMBAYE HATA HIVYO HAKUWEZA KUFAHAMIKA MARA MOJA JINA NA MAKAZI YAKE NA KUCHUKUA CHUMBA NAMBA 6. BAADA YA DAKIKA 20,MWANAMKE HUYO ALITOKA CHUMBANI HUMO NA KWENDA KUSIKOJULIKANA. HATA HIVYO MAJIRA YA SAA 12:00HRS MHUDUMU WA NYUMBA HIYO YA KULALA WAGENI NICKSON KAHANGA [24] WAKATI ANAPITA KUELEKEA UANI ALISIKIA KELELE ZA MTU KUKOROMA KATIKA CHUMBA NAMBA 6 NA ALIPOFUNGUA ALIMKUTA MAREHEMU AKIWA AMEJIFUNIKA BLANKETI MWILI MZIMA AKIWA MAHUTUTI ANAKOROMA HAJITAMBUI. AIDHA TAARIFA ZILIFIKISHWA POLISI KATI NA MHANGA ALIKIMBIZWA HOSPITALI NA MUDA MFUPI BAADAE ALIFARIKI DUNIA.
UCHUNGUZI ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO UNAENDELEA. IKIWA NI PAMOJA NA KUUFANYIA UCHUNGUZI WA KITABIBU WA MWILI WA MAREHEMU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MWANAMKE ALIYEKUWA NA MAREHEMU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

No comments:

Post a Comment