Tarehe 17 Novemba, 2014 saa 4:00 asubuhi Jeshi la Magereza litapokea msaada
wa vifaa vya ujenzi na vitendea kazi vitakavyotumika katika ujenzi wa
makazi ya Maafisa na Askari wa Gereza Wazo. Tukio ambalo litafanyika
katika Viwanja vya Gereza Wazo, Wilayani Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi
iliyotolewa jana na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
Nchini msaada huo umetolewa na Kampuni ya Twiga Cement ya Jijini Dar es
Salaam kufuatia kusainiwa kwa Makubaliano ya kuiuzia Kampuni hiyo madini
ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo.
Mgeni rasmi katika tukio hilo
atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias M. Chikawe(Mb).
Aidha, Wadau mbalimbali toka nje ya Jeshi la Magereza watakuwepo katika
hafla hiyo.
Kuanza kwa mradi wa ujenzi wa
nyumba hizo utapunguza tatizo la muda mrefu la uhaba wa Nyumba zenye
hadhi kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Gereza hilo.
Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye shughuli hiyo katika muda ulioelezwa.
Imetolewa na;
Lucas A. Mboje, Mkaguzi wa Magereza;
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza;
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza;
DAR ES SALAAM.
14 Novemba, 2014.
No comments:
Post a Comment