Wadau wa Windhoek ndani ya Villa Park Resort
katika promosheni hiyo.
Hapa shughuli imepamba moto waalikwa wakimsikiliza Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr.James Rugemalira.
Dotto Mwaibale
WAKAZI wa
jiji la Mwanza na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa, wamefurahishwa na
uwekezaji unaotarajiwa kufanywa na Kampuni ya Bia ya Mabibo (MBL) kwa
ajili ya kujenga kiwanda cha bia za Windhoek.
Wakizungumza
katika promosheni iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Mwanza juzi
katika ukumbi wa Villa Park Resort, wanachi hao walionesha kuguswa na
uwekezaji huo na kushauri kijengwe kiwanda hicho jijini Mwanza.
Walisema kujengwa kwa kiwanda hicho kutachochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kuongeza ajira kwa vijana wa Kanda ya Ziwa.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira alisema lengo la kufika Mwanza ni kupata mawazo mapya na ushauri wa nini kifanyike katika uwekezaji huo jijini humo.
“Tumeamua tuje Mwanza na kuomba ushirikiano wenu na rai yangu ni kupata
maoni yenu ili tukipata fursa tuwe na viwanda vidogo vidogo,lakini si
sawa na Tanzania Breweries (TBL),maana hatuwezi kushindana nao,” alisema
Rugemalira.
Alisema ushindani wa haki ni lazima kila
mtu apate haki ya kushinda,na wataka waweke misingi hiyo kwanza katika
mikoa ya Mwanza, Kagera, Mbeya na Mtwara kwa kuanzisha viwanda vidogo
vidogo.
Aliwataka wananchi wa kanda ya ziwa kuwaonesha na kuwaunga mkono ili wazalishe kinywaji cha windhoek Mwanza badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi kama ilivyo sasa,ambapo kinywaji hicho kinagizwa kutoka nchini Namibia.
“Mtu
anaweza kunipa ushauri au akaniamuru atakavyo ili nijitambue na ni vema
kukubaliana na ushindani bila hivyo hatuwezi kupata maendeleo na
malengo ya kampuni yetu ni kushirikiana na serikali kukabiliana na uhaba
wa ajira kwa Watanzania kwa kujenga viwanda hivyo ”alisema Rugemalira.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Mabibo Bia (MBL), Kanda ya Ziwa, Godfrey
Mwangungulu alisema Bia ya Windhoek imewahi kushinda medali za juu saba
kwa ubora Barani Afrika tangu ianze kuzalishwa mwaka 1920.
“Bia ya Windhoek ilishinda tuzo hizo mfufulizo kuanzia mwaka 2007, 2008, 2009,2010,2011,2012 na 2013.
No comments:
Post a Comment