Mkurugenzi
wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga (kulia)
akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu safari ya
Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2013 kuelekea katika Mashindano ya Urembo wa
Dunia (Miss World 2014) nchini Uingereza.
Baadhi
ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kuhusu safari ya Miss
Tanzania 2013 nchini Uingereza kwenda kuiwakilisha Tanzania katika
Mashindano ya Urembo wa Dunia yatakayoanza mapema tarehe 14 Desemba,
2014.
…………………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
MREMBO wa Tanzania wa mwaka
2013, Happiness Watimanywa ameahidi kuing’arisha Tanzania katika
mashindano ya ulimbwende ya Dunia yatakayofanyika mapema mwezi ujao huko
nchini Uingereza.
Akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, mlimbwende huyo amewaeleza waadishi kuwa,
kutokana na uzoefu wa kazi zake alizokuwa akifanya kwa jamii kwa muda
kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo misaada ya hali na mali anayoipata toka
Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na wahisani wengine nchini amewaahidi
Watanzania kuibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho huko nchini
Uingereza ili kuitangaza Tanzania.
Alieleza kuwa, tayari Ubalozi wa
Tanzania nchini Uingereza utakuwa tayari kumpokea pindi atakapowasili
nchini humo kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya
ulimbwende yatakayowahusisha walimbwende toka Ulimwengu mzima.
“Nimejifunza mambo mengi hasa
kipindi wakati nasafiri sehemu mbalimbali nchini pamoja na kufanya kazi
za kusaidia jamii katika kipindi chote, hivyo nawaahidi watanzania
ushindi katika mashindano hayo yatakayofanyika huko Uingereza pia
mnipigie kura zenu za wingi”, alisema Watimanywa.
Naye Mkurugenzi wa Lino
International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga ambao ni waandaaji wa
Miss Tanzania, alisema kuwa mashindano ya Urembo wa Dunia ni mashindano
ya Kimataifa ambayo yanawakutanisha walimbwende toka nchi nyingi duniani
ikiwemo Tanzania, hivyo alitoa wito kwa watanzania wote kuunga mkono
kwa kumpigia kura nyingi mwakilishi ambaye ndiye mrembo wa Tanzania kwa
mwaka 2013, Hapinness Watimanywa ili ajinyakulie taji hilo la dunia ili
aweze kuipa sifa Tanzania kimataifa.
Mashindano ya Urembo ya Dunia
yanatarajiwa kufanyika mapema tarehe 14 Desemba, 2014 huko nchini
Uingereza ambapo mrembo huyo wa Tanzania anatarajia kuanza safari yake
ya kuelekea nchini humo tarehe 15 Novemba, 2014 tayari kwa ajili ya
mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment