Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet
ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi (kushoto)
akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.
Assah Mwambene wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuangalia
utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano.
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet
ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi akimueleza Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mikakati ya
ofisi hiyo ya kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma wakati wa ziara
ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika vitengo cha mawasiliano.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kushoto) akizungumza
na Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Bw. Exavier Daudi wakati alipotembelea ofisi hiyo ikiwa ni utekelezaji
wa mkakati wa Idara ya Habari kutembelea vitengo vya mawasiliano kwenye
taasisi za serikali ili kuangalia utendaji kazi wa vitengo hivyo.
Afisa
Habari wa Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Bw. Kassim Nyaki (kulia) akieleza kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mafanikio ya kitengo cha mawasiliano
cha ofisi hiyo katika kutoa taarifa kwa umma ambapo alisema hadi sasa
tovuti yao ina zaidi ya watu Elfu 8 wanaotembelea kwa siku.
Kaimu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila
(kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.
Assah Mwambene wakati alipotembelea Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali ili kujionea utendaji kazi wa kitengo cha
mawasiliano serikalini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu wa ofisi hiyo Bw. Gerard Mwanilwa.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia mwenye Kaunda
Suti) akiwaeleza baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika
kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma. Katikati ni Kaimu Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila.
No comments:
Post a Comment