Liverpool
wakicheza ugenini wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya
Bournemouth katika michuano ya kombe la Capital Cup.
Majogoo hao
wa jiji la london walipata magoli yao kupitia kwa kwa winga Raheem
Sterling na Lazar Markovic akihitimisha ushindi uliompa faraja kocha
Brendan Rodgers. Bao la kufutia machozi kwa Bournemouth lilifugwa na
kiungo Dan Gosling.
Huku katika mchezo mwingine wa robo fainali
uliochezwa kwenye uwanja wa White Hart Lane Tottenham waliwachapa
Newcastle kwa goli 4-O,Kwa magoli ya Bentaleb, Chadli, Kane na
mshambuliaji Soldado.
Baada ya michezo ya robo fainali kukamilika
ratiba ya michezo ys nusu fainali ilijulikana kwa vigogo Chelsea
kuchuana na Liverpool huku Tottenham wakiwakabili Sheffield United.
No comments:
Post a Comment