Balozi wa Tanzania nchini Austria
ambaye ana makazi mjini Berlin, Ujerumani Mhe. Philip S. Marmo; mapema
mwezi huu alikabidhi Hati za Utambulisho (Letter of Credence) kwa Mhe.
Dkt. Heinz Fischer, Rais wa Austria. Shughuli hizi zilifanyika katika
ukumbi maarufu wa Maria Teresa uliopo katika kasri ya wafalme wa zamani
wa “Austro-Hungarian Empire” mjini Vienna. Gwaride rasmi kwa ajili ya
Balozi mpya iliendeshwa katika viwanja vya Hofburg.
Balozi wa Tanzania nchini Austria
ambaye ana makazi mjini Berlin, Ujerumani Mhe. Philip S. Marmo akipokea
heshima kutoka Gwaride rasmi kwa ajili ya Balozi huyo ambalo katika
hafla ambayo iliendeshwa katika viwanja vya Hofburg.
No comments:
Post a Comment