Mkuu wa mkoa wa
Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akifuangua kikao cha Kamati ya Ushauri
ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando.
……………………………………………………………………………………………..
Aron Msigwa –MAELEZO
.Dar es salaam.
Jiji
la Dar es salaam linaangalia upya utaratibu wa kuwaondoa ombaomba na
wafanyabiashara ndogondogo(wamachinga) katika maeneo yasiyoruhusiwa
katika jiji la Dar es salaam kufuatia sheria na hatua zinazochukuliwa
ikiwemo kuwarudisha ombaomba hao katika mikoa wanayotoka kutokuzaa
matunda na kuwa endelevu kufuatia wengi wao kurudi katika maeneo ya
awali kila wanapoondolewa.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki wakati
akifuangua kikao cha wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es
salaam (RCC) kilichofanyika leo jijini Dar es salaam kujadili masuala
mbalimbali ya mendeleo katika jiji la Dar es salaam.
Amesema kuwa
kuendelea kuwepo kwa wafanyabiashara hao katika maeneo yasiyo rasmi ni
moja ya changamoto inayolikabili jiji la Dar es salaam kutokana na
biashara wanazozifanya kuchangia kuzuia maeneo ya barabara ya waenda kwa
miguu, kusababisha uchafuzi wa mazingira,kusabisha msongamano wa magari
kwa baadhi yao kuweka bidhaa barabarani.
Amesema kutokana
na hali hiyo baadhi ya wafanyabiashara walio na biashara rasmi ambao
hulipa kodi za Serikali wamekuwa wakilamikia hali ya ukwepaji wa kodi
inayofanywa na wafanyabiashara hao.
Bw. Sadiki
amesema mpango wa mkoa wa sasa ni kuendelea kuwatumia wafanyabiashara
hao kama fursa ya mtaji wa rasilimali watu ambayo itatumika kama chanzo
cha mapato katika kuleta maendeleo ya mkoa.
No comments:
Post a Comment