Waziri
wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akizindua rasmi Takwimu za
Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 leo jijini Dar
es salaam.
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha Dkt. Servicius Likwelile chapisho la lenye Takwimu za
Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakati wa
uzinduzi wa usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam. Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa(Kushoto) akitoa
ufafanuzi wa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa iliyofanywa na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliyotumia tafiti za taifa zilizofanyika kwa
kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.Kulia ni Waziri wa Fedha Mh. Saada
Salum Mkuya. Baadhi
ya viongozi na wageni waliohudhuria uzinduzi wa usambazaji wa Takwimu
za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007
wakimsikiliza Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Bw. Daniel Masolwa
wakati akiwasilisha mada kuhusu Pato la Taifa leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
. Dar es salaam.
Serikali imesema kuwa Pato la
Taifa kwa mwaka 2007 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 26.8
ikilinganishwa na trilioni 20.9 za mwaka 2001, ambapo wastani wa pato
la mwananchi mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi milioni1,186,200/=
mwaka 2001 hadi shilingi milioni 1, 561,050/= mwaka 2013.
Akizindua usambazaji wa takwimu
hizo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum
ameeleza kuwa matokeo hayo ni sawa na ongezeko la ukubwa wa Pato la
Taifa kwa asilimia 27.8.
Amesema ongezeko hilo ni matokeo
ya juhudi za Serikali kuweka mazingira mazuri na kutengeneza fursa za
kuwawezesha wananchi kufanya kazi za kujiajiri na hatimaye kupata kipato
halali kwa kazi wanazofanya.
Mh. Mkuya amesema kuwa kukua kwa
uchumi wa Tanzania kumechangiwa na kujumuishwa kwa shughuli mbalimbali
zikiwemo Sayansi na Teknolojia ambako kumetoa fursa kwa wananchi
kujiongezea kipato hususan matumizi ya simu za kiganjani ambazo
zimerahisisha mawasiliano na utafutaji wa masoko ya bidhaa ndani na nje
ya nchi.
Amezitaja shughuli nyingine kuwa
ni ukamilishaji wa miamala mbalimbali ya kibenki na mikopo ambazo
zimekuzwa na sekta ya mawasiliano , kuongeza ajira na kupunguza muda
wa kusubiri huduma za malipo katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, amefafanua kuwa
kuongezeka kwa thamani ya Pato la Taifa kunaiongezea Serikali uwezo
kimapato kupitia kodi na kuiwezesha kugharamia ujenzi wa miundombinu na
utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
“Serikali imeendelea kuimarisha
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, utafiti wa mapato na
matumizi ya Kaya Binafsi ya mwaka 2012 unaonyesha asilimia 60 ya kaya
zote nchini zinapata maji safi na salama hasa hususan maeneo ya
mijini,zaidi ya asilimia 20 ya kaya zote nchini zinatumia nishati umeme
haya ni mafanikio makubwa ya matokeo ya ukuaji wa uchumi nchini”
Amesisitiza Mh. Mkuya.
Akizungumzia mchango wa Sekta
Binafsi katika kukua kwa pato la taifa nchini amesema kuwa ajira
zipatazo laki nne kati ya laki sita katika sekta iliyo rasmi
zimepatikana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa
uzinduzi huo amesema kuwa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa
imetumia Tafiti za Taifa zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi
2007.
Amezitaja tafiti hizo kuwa ni
pamoja na utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya wa mwaka 2007, Sensa ya
Kilimo iliyofanyika mwaka 2008 na Takwimu nyingine za utawala kutoka
katika Wizara na Idara za Serikali.
Aidha, amefafanua kuwa
ukokotoaji wa takwimu hizo umefuata mfumo wa Umoja wa Mataifa wa
kutayarisha takwimu za Pato la Taifa wa mwaka 1993 na 2008 kwa lengo la
kuhakikisha kuwa takwimu hizo zinalinganishwa na takwimu nyingine
duniani.
No comments:
Post a Comment