Kamishna
Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally
Samaje, akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kuandaa miongozo ya
Ukaguzi wa Migodi kinachoendelea Jijini Mwanza.
Wakaguzi
wa Migodi kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiwa katika kazi za vikundi
kuandaa miongozo (checklist) itakazotumiwa na Wakaguzi wa migodi nchini
katika kikao kinachoendelea Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi akiwasilisha
kazi ya vikundi wakati wa kikao cha kuandaa miongozo ya Ukaguzi wa
Migodi
Sehemu ya Wakaguzi wa Migodi
waliohudhuria kikao kazi cha kundaa miongozo ya Ukaguzi wa Migodi nchini
wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika kikao hicho.
=====================================================
Na: Asteria Muhozya, Mwanza
Kamishna Msaidizi wa Madini
anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi Mhandisi, Ally Samaje, amesifu zoezi
la kuandaa miongozo (checklist) ya Ukaguzi wa Migodi na kueleza kuwa,
litaleta matokeo bora kutokana na kwamba shughuli hiyo imekuwa
shirikishi.
Kamishna Samaje ameyasema hayo
katika kikao kazi kinachoendelea Jijini Mwanza na kuwashirikisha
Wakaguzi wa migodi kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuandaa
miongozo itakayokuwa nyenzo muhimu kwa shughuli za ukaguzi wa migodi
nchini.
“ Kimekua ni kikao kizuri, kila
mmoja ameshariki kikamilifu jambo ambalo linaashiria kuwa, tutatoka hapa
tukiwa na kitu ambacho kitawezesha shughuli za ukaguzi migodini
kufanyika kwa utaalamu ,” amesema Samaje.
Ameongeza kuwa, miongozo hiyo
inatarajiwa kuleta mabadiliko katika shughuli za ukaguzi wa migodi,
vilevile shughuli nzima itafanyika katika muonekano unaofafana kutokana
na kwamba, miongozo hiyo inaandaliwa kwa ajili ya ukaguzi wa migodi yote
nchini , ikiwemo na migodi mikubwa na midogo.
“Tutatoka hapa na miongozo mizuri,
nina imani kwamba tutakuwa tofauti na miaka mingine. Tutaongea lugha
moja katika shughuli za ukaguzi, lakini zaidi tutajenga kikosi bora kwa
ajili ya shughuli za ukaguzi”, amesisitiza Samaje.
Aidha, ameongeza kuwa, uwepo kwa
miongozo hiyo, utawezesha shughuli za ukaguzi migodi kufanyika kitaalamu
zaidi na kuongeza kuwa, “suala jingine la kuzingatia ni kwamba uandaaji
wa miongozo hii unakwenda unazingatia hali halisi ya mazingira yetu.
Huku masuala ya afya,usalama na uhifadhi wa mazingira yakizingatiwa”,
ameongeza Mhandisi Samaje.
Kwa upande wake, mwezeshaji katika
kikao hicho, Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi,
Laurian Rwebembera , akifafanua masuala kadhaa katika kikao hicho,
ameeleza kuwa, miongozo hiyo inatarajiwa kuwa, shirikishi kutokana na
kwamba washiriki wote wameshiriki kikamilifu katika zoezi zima la
uandaaji miongozo hiyo.
“Kimekua ni kikao kazi kizuri,
kila mmoja ameshiriki kuonesha uzoefu na namna bora ya kufanya ili
kufikia lengo. Miongozo hii itakua nyenzo bora za kufanyia kazi, amesema
Mhandisi Rwebembera.
No comments:
Post a Comment