Mkurugenzi wa
Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa Tigo Andrew Hodgson (wa pili kulia)
akipongezana na Mkurugenzi wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa
ZANTEL Hashim Mukudi mara baada ya kutangaza ushirikiano kati ya huduma
zao za TigoPesa na EzyPesa mapema leo Zanzibar. Kutoka kushoto ni Meneja
wa Biashara wa ZANTEL Zanzibar Mohamed Mussa, Meneja Miradi wa ZANTEL
Shinuna Kassim na Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga (kulia).
…………………………………………………………………………………………..
Kampuni za simu za mkononi za Tigo
na ZANTEL zamezindua rasmi huduma za kutumiana pesa miongoni mwa wateja
wake Tanzania. Mbali na huduma hiyo ya kutumiana pesa miongoni mwa
wateja wa mitandao hiyo, wateja wa EzyPesa na TigoPesa sasa wataweza
kutuma na kupokea pesa kwa marafiki na ndugu walio katika mitandao hiyo
popote pale nchini.
Kutekelezwa kwa mpango huo
kunazifanya Tigo na ZANTEL kuwa viongozi wa huduma kama hiyo Duniani.
Haya ni matokeo ya makubaliano yaliyotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu na
EzyPesa, TigoPesa na Airtel Money.
Jinsi Huduma hiyo inavyofanya kazi:
Wateja wa Zantel: Wateja wa Tigo:
1. Piga *150*02# 1. Piga *150*01#
2. Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa) 2. Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa)
3. Chagua: Chaguo la 2 (Tuma TigoPesa) 3. Chagua: Chaguo la 5 (Tuma EzyPesa)
3.1. Ingiza Namba ya TigoPesa 3.1. Ingiza Namba ya TigoPesa
3.2. Ingiza Kiwango 3.2. Ingiza Kiwango
3.3. Ingiza Neno la Siri 3.3. Ingiza Neno la Siri
3.4. Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno 3.4. Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno
Hakuna gharama za ziada mteja
anapotuma pesa kwa mtandao mwingine isipokuwa gharama zinakuwa sawa na
zile anapotuma kwenye mtandao wake. Wateja wanaopokea pesa kutoka
mtandao mwingine wanaweza kutoa pesa kwa wakala wa mtandao wao na
hapatakuwa tena na ulazima wa mteja kutafuta wakala wa mtandao wa mtu
aliyemtumia pesa.
Akizungumza kutoka Zanzibar, Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Andrew Hodgson alisema:
“Tunafuraha kupanua wigo kwa wateja wetu kwa ubia na Zantel. Hatua hii
ni muhimu hasa kwa Zanzibar ambapo fursa ya kukua kwa huduma za fedha
kwa mitandao ya simu bado ni kubwa.”
Anasema kama ilivyo kwa huduma nyingine za simu kama milio ya
sauti na ujumbe mfupi wa maneno, kuna fursa kubwa ya kuimarisha huduma
kwa wateja kwa kushirikiana badala ya kushindana baina ya wadau katika
sekta ya mawasiliano kwa kupanua huduma za kutuma na kupokea fedha kwa
kutumia mitandao Tanzania.
Anafafanua zaidi kuwa kwa kufanya kazi na wadau wengine,
kunawawezesha kupanua wigo wa wateja na hivyo kwa pamoja kutoa huduma
ambazo ni bora zaidi, salama, na za haraka kwa wateja wa pande zote.
“Ubia ambao tumeingia leo sio tu utaleta karibu kampuni zetu,
bali muhimu zaidi ni ukaribu wa wateja wetu kwa kuwapatia huduma za
fedha za kielektroniki bora zaidi ambazo hawakuweza kuzipata hapo
awali,” alisema Hodgson.
Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Mohamed Mussa, anasema Zantel
inaendelea kutimiza ahadi ya kuwarahisishia huduma za fedha wateja wake
kwa kufanya kazi pamoja na Tigopesa.
“Kwa kufanya hivi tunapanua wigo
kwa wateja wetu, huduma hii inawawezesha zaidi wateja kutuma na kupokea
fedha kwa urahisi zaidi,” anasema.
Anafafanua zaidi kuwa kwa huduma hii itasaidia kuimarisha huduma za fedha kati ya visiwa vya Zanzibar na Tanzania Bara.
“Zantel iko katika mstari wa mbele
kuhakikisha kuwa ushiriki wa wananchi wa Zanzibar katika sekta muhimu
ya fedha unaimarika na kukua. Tumehakikisha kuwa mtandao wa mawakala
wetu na watoa huduma wengine wako tayari kuwahudumia wateja wetu,”
anasema Bw. Mussa.
No comments:
Post a Comment