Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI bw. Jumanne Sagini akikagua sehemu ya shehena ya vitabu vya
masomo ya sayansi vilivyotolewa na Serekali ya Marekani,vitabu hivyo
vimehifadhiwa katika bohari kuu ya Serikali ambapo mchakato wa
kuvipeleka mashuleni unatarajiwa kuanza hivi karibuni ili vianze
kutumika mapema mwakani katika shule za Sekondari.
……………………………………………………………………………………………….
Na: Frank Mvungi –Maelezo
Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa vitabu Milioni mbili na nusu vya masomo ya Sayansi ambavyo vitakavyotumika kukukuza kiwangob cha elimu hapa nchini.
Akikagua sehemu ya shehena ya vitabu hivyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) bw. Jumanne Sagini amesema msaada huo ni matokeo ya ziara ya Mh. Rais Dkt Jakaya Kikwete nchini Marekani.
Akifafanunua Sagini amesema Vitabu hivyo ni vya masomo ya Biolojia, fizikia,Hesabu,Kemia ambavyo vimeandaliwa kulingana na mahitaji ya nchi yetu na hivyo vitasaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa tatizo la vitabu katika shule za Sekondari hapa nchini.
Akitaja idadi ya vitabu hivyo kwa kila somo Sagini amesema kuwa vitabu vya fizikia ni 533,520,Kemia vitabu 533,520,Baolojia vitabu 666,480 na hisabati vitabu 766,480.
Akieleza kuhusu utaratibu wa kufikisha vitabu hivyo kwenye Mikoa na halmashauri zote hapa nchini Sagini amesema Serikali imeshaandaa utaratibu ambapo vitabu hivyo vitafikishwa katika Mikoa yote hapa nchini kabla ya Januari 10, 2015 ili wanafunzi waweze kuanza kuvitumia katika mwaka wa masomo ujao.
Kwa upande wa faida za msaada huo Sagini amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anakuwa na kitabu chake na kutoka katika uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi watano jambo ambalo kwa sasa litaanza kutekelezwa kwa kuzingatia juhudi zinazofanywa na Serikali.
Faida nyingine ni kuwapa wanafunzi uwezo mzuri wa kujifunza masomo ya Sayansi na hivyo Taifa litaweza kupata wataalamu katika Nyanja mbalimbali.
Pia Sagini alibainisha kuwa vitabu hivyo haviuzwi na yeyote atakayepatikana akifanya hivyo atachukuliwa hatua kali za Kisheria kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zilizopo.
Akitoa wito kwa wanafunzi wote Sagini amesema wanapaswa kutumia vyema msaada wa vitabu hivyo ili visaidie kukuza kiwango cha Elimu hapa nchini na kuondoa kabisa tatizo la vitabu.
Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali hapa nchini ikiwemo kujenga shule za Kata na maabara lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata elimu bora ambapo msaada wa vitabu vya Masomo ya Sayansi ni moja ya kielelezo cha juhudi za maksudi za kuinua Elimu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment