Mfalme
wa Muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuf (wa pili kushoto) akielezea kwa
wanahabari (hawapo pichani) alivyojipanga kuanguasha shoo ya nguvu
katika Tamasha la Wafalme Sikukuu ya Xmas Dar Live.
Meneja
wa Mashauzi Classic, Ismail Rashid ‘Suma Ragar’ akiongea na wanahabari
(hawapo pichani) jinsi walivyojipanga kutoa burudani katika msimu wa
Xmas Dar Live wakati wa mkutano na wanahabari hao uliofanyika leo kwenye
Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza-Afrikasana jijini Dar . Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Benjamin Mwanambuu, Mkurugenzi Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki (wa pili kushoto), Mzee Yusuf (wa pili kulia) na Damian Raphael ‘MC Dalada Kikombe’ kutoka Kundi la Masai Worriors (wa kw nza kulia).
Damian
Raphael ‘MC Dalada Kikombe’ kutoka Kundi la Masai Worriors (katikati)
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu makamuzi
watakayoyafanya Dar Live katika msimu huu wa sikukuu.
KAMPUNI ya Dar Live kwa mara
nyingine imetoa ratiba kamili ya burudani katika msimu huu wa kufungia
mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015.
Usiku wa Wafalme
Kwa mara nyingine shoo bab’kubwa ambayo ni habari ya mjini
kwa sasa ijulikanayo kama Usiku wa Wafalme itagongwa ndani ya ukumbi huo
pekee kwa burudani, Desemba 25 ‘Sikukuu ya Krismasi’ ambapo mkali wa
muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ atagonga nyimbo
zake zote kali siku hiyo.
Diamond ambaye ni mshindi wa tuzo
tatu kutoka Channel O zijulikanazo kama Channel O Africa Music Video
Awards (CHOAMVA), siku hiyo atatinga na tuzo zake zote hizo ikiwa ni
kuwapa shukrani mashabiki wake wote kwa sapoti waliyoitoa huku akipiga
nao picha kwenye ‘red carpet’ na kuongea nao mawili-matatu.
Mashabiki pia watapata nafasi ya
kumshuhudia Diamond kwa mara ya kwanza akipiga nyimbo zaidi ya 20
jukwaani pasipo kusimama huku akiwatambulisha madensa wapya sambamba na
kupiga pia na nyimbo zake zote ambazo zilishawahi kuachiwa na hazijawahi
kuisha mpaka mwisho.
Kwa upande wa muziki wa Pwani,
usiku huo utafunikwa pia na Mfalme Mzee Yusuf ambaye siku hiyo ataungana
na kundi lake la Jahazi Modern Taarab katika kuwaonjesha mashabiki
ngoma zao zote zilizopo katika albamu yao mpya ya Chozi la Mama huku
wakifunga mwaka na ngoma ambayo ni habari nyingine kwa sasa ya Mahaba
Niue.
Mashabiki watakaofika usiku huo
pia watapata bahati ya kushuhudia mshindi wa shindano la kumtafuta
mwanaume mwenye mvuto kutoka Gazeti la Ijumaa lijulikanalo kama Ijumaa
Sexiest Bachelor ambapo mpaka sasa wamebaki washiriki watatu, Yusuph
Mlela, Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba.
Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni
kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo watoto wote watakaofika watapata
bahati ya kucheza michezo kibao kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea
na mingine mingi huku kundi la sarakasi la Masai Worriors
likiwapagawisha kwa kutoa michezo kibao ya sarakasi , mazingaombwe
sambamba na kumwaga zawadi kwa kila mtoto.
No comments:
Post a Comment